Somo la 2: Ishara za Uungu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 6, 9 & 11
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
4
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Ishara za Uungu

(Yohana 6, 9 & 11)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Umekutana na watu wangapi wanaokiri kwamba Yesu ni “mtu mzuri,” “rabi wa muhimu,” au “nabii?” Wanakiri kuwa Yesu ni mtu wa muhimu kihistoria, lakini kwamba Yesu si Mungu. Je, miujiza ya Yesu inathibitisha kuwa yeye ni Mungu? Hebu tuzame kwenye somo letu na tujifunze miujiza iliyopo katika kitabu cha Yohana, visa vinavyojielekeza kwenye uungu wa Yesu!

  1.    Muujiza wa Mkate
    1.    Soma Yohana 6:1-3. Unadhani Yesu na wanafunzi wake walikuwa na lengo linalofanana na watu waliowafuata? (Soma Marko 6:31-32. Tulipojifunza kitabu cha Marko hivi karibuni tuliona kwamba Yesu na wanafunzi wake walihitaji pumziko kwa kuachana na watu. Walihitaji kupumzika hivyo walikwenda “mahali pasipokuwa na watu.”)
    1.    Soma Yohana 6:4-5. Ungesema nini kama ungeona kundi hili kubwa la watu likikujia? (Ningejiuliza kwa nini hawatupi nafasi kwa kutuacha? Kwa nini wasitupatie muda wa kupumzika japo kidogo?)
      1.    Jambo gani lilihamasisha kundi la watu kumsumbua Yesu? (Soma tena Yohana 6:2. Waliona kwamba Yesu alikuwa anawaponya watu na walitaka uponyaji.)
        1.    Je, hiyo ni nia ya ubinafsi kabisa?
      1.    Je, swali la Yesu linaonesha ubinafsi? (Hapana. Anawatafuta, na si kwa ajili yake.)
    1.    Soma Yohana 6:6. Swali la Yesu katika kitabu cha Yohana 6:5 ni jaribu kwa Filipo. Hili ni jaribu la namna gani? Jaribio la hisabati? Jaribio la kuoka mkate? Jaribio la masuala ya fedha?
    1.    Soma Yohana 6:7. Filipo anafanya uamuzi kuwa hili ni jaribu la namna gani? (Jaribu la masuala ya fedha.)
    1.    Soma Yohana 6:8-9. Andrea anafanya uamuzi kuwa hili ni jaribu la namna gani? (Kipimo halisi cha kutafuta chakula.)
    1.    Soma tena Yohana 6:6. Yesu anatafakari mwenyewe, “Ninajua nitakalolitenda.” Tunaona kidokezo gani kuhusu aina/asili ya jaribu? (Jaribu ni endapo Filipo atamtazamia Yesu kutenda muujiza ili kutatua hili tatizo halisi. Kwa dhahiri, Andrea hakufanya juhudi zozote kulielewa jaribu.)
    1.    Soma Yohana 6:10-13. Kama ungekuwa mmojawapo wa watu katika kundi hili kubwa ambaye umekuja kuona uponyaji au kuponywa, ungehitimisha nini? (Hili linaonekana tofauti. Ni tofauti hata kuliko kubadili maji kuwa divai. Yesu anatengeneza chakula- tena chakula kingi kabisa.)
      1.    Je, kuna umuhimu kwenye ukweli kwamba Yesu alichagua kutengeneza divai na mkate, vitu ambavyo ni vya msingi kwenye Pasaka (Meza ya Bwana)? (Soma tena Yohana 6:4. Hii inaashiria kuwa vinahusiana.)
      1.    Ngoja tukujaribu. Unadhani muujiza huu unathibitisha nini? (Ni ishara kwamba Yesu ni Mungu kwa sababu tunafahamu kwamba Mungu alitengeneza chakula kwa ajili ya watu wake walipoutoroka utumwa nchini Misri.)
    1.    Soma Yohana 6:14-15. Watu wanajibuje jaribu hili? (Wanahitimisha kwamba Yesu ni “Nabii” atakayewaangusha Warumi.)
    1.    Soma Matendo 3:22-23 na Yohana 1:19-21. (Mfanano kati ya Musa na Yesu uko dhahiri kwenye utengenezaji wa chakula. Musa alitabiri kuwa “nabii” atainuka ambaye anafanana naye. Yohana Mbatizaji alikana kuwa yeye si nabii aliyezungumziwa na Musa. Maoni ya Adam Clarke yanafafanua kuwa Wayahudi walimwelewa visivyo (misunderstood) Musa kwenye jambo hili. Walidhani kuwa Musa alikuwa anazungumzia juu ya marejeo ya mmojawapo wa manabii wakuu, yumkini Yeremia. Lakini Musa alikuwa anamtabiri Masihi, Yesu.)
    1.    Hebu turuke vifungu kadhaa chini na tusome Yohana 6:25-27. Sasa tunalo jibu la Yesu kwenye jaribu.  Yesu anasema kuwa wanapaswa kuhitimisha nini kutokana na muujiza huu? (Yesu anawaambia kuwa jibu si baraka za kidunia, kama vile kupewa chakula au kuwa huru. Anatoa uzima wa milele. Muujiza huu ni “Mhuri” wa Mungu kwamba yeye ni “Mwana wa Adamu.”)
    1.    Kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, hatutajadili Yohana 6:28-40. Lakini unapaswa kusoma vifungu hivyo ili kuona jibu la Yesu lisiloelezeka kwa urahisi (complex).
  1.   Muujiza wa Uoni
    1.    Soma Yohana 9:1-2. Jibu kwa swali la wanafunzi ni la muhimu kiasi gani? (Ingejalisha nini? Kwa dhahiri ingekuwa jambo la ajabu kudai kuwa mtu yule alitenda dhambi kabla ya kuzaliwa kwake.)
    1.    Soma Yohana 9:3. Je, mtu yule alizaliwa kipofu ili kumpa Mungu utukufu? (Lengo la kila mwanadamu ni kumtukuza Mungu. Sidhani kama Yesu anasema kuwa mtu yule alizaliwa kipofu ili kukidhi lengo la kumtukuza Mungu. Chanzo cha upofu ni dhambi duniani. Yesu anasema tu kwamba janga hili litatumika katika kumtukuza Mungu.)
    1.    Soma Yohana 9:6-7. Unadhani ni jambo la upatanifu (coincidence) kwamba Yesu anamponya kipofu, tofauti na aina nyingine yoyote ile ya uponyaji? (Soma Yohana 9:4-5. Yesu anasema kuwa Yeye ni nuru ya ulimwengu, na hii ni sehemu ya kazi ya “nuru” yake. Usiku waja (giza linakuja).)
    1.    Ruka vifungu kadhaa chini na usome Yohana 9:15-17. Je, kipofu anaitimiza Yohana 9:3?
    1.    Soma Yohana 9:18-21. Je, wazazi wanaulizwa maswali yenye mantiki? (Swali kuhusu jinsi gani kijana wao sasa anaweza kuona halina mantiki.)
    1.    Soma Yohana 9:22. Je, viongozi wa Kiyahudi wanatafuta majibu nyofu (ya kweli)?
    1.    Soma Yohana 9:24-27 na Yohana 9:30-33. Ninakuuliza tena, je, mtu yule anaitimiza Yohana 9:3? (Ndiyo. Hii ni hoja nzuri sana na yenye nguvu kubwa kuhusu uungu wa Yesu.)
    1.    Soma Yohana 9:34. Hii ni hoja ya namna gani? (Wanamshambulia kipofu, hawazungumzii hoja zake zenye mantiki.)
    1.    Soma Yohana 9:35-39. Je, Yesu anadai kuwa yeye ndiye Masihi?
  1.      Lazaro
    1.    Soma Yohana 11:1-3. Unadhani Lazaro, Mariamu, na Martha walitarajia nini kutoka kwa Yesu? (Yesu alikuwa anawaponya watu wengine, ama kwa hakika atamponya mtu aliyempenda.)
      1.    Kwa nini akina dada wale waliandika kuwa Yesu “alimpenda” Lazaro? Je, alihitaji kukumbushwa? Je, akina dada hawa hawakuwa na uhakika kama Yesu angekuja na hivyo jambo hili kuongeza dukuduku?
    1.    Soma Yohana 11:4-6. Je, hili ni jambo la dharura? (Yesu anasema kuwa halitaishia kwenye kifo.)
      1.    Kwa nini Yohana anaandika kuwa Yesu alimpenda Lazaro? (Matendo ya Yesu yanaashiria kuwa hampendi Lazaro. Yesu anachelewesha msaada wake.)
    1.    Soma Yohana 11:7-8. Wanafunzi wana maoni gani kuhusu Yesu kwenda kumsaidia Lazaro? (Kura yao ni, “hapana.” Maisha ya Yesu yako hatarini.)
    1.    Soma Yohana 11:9-10. Je, kuna mtu yeyote aliyependekeza kwamba wafanye safari hii wakati wa usiku? Ikiwa sivyo, Yesu anazungumzia jambo gani? (Sote tuna kiasi fulani cha muda tulichopewa. Bado Yesu amebakiwa na muda mchache wa kuishi duniani, na hivyo ataendelea kufanya kazi za mchana. Atakuwa salama.)
    1.    Soma Yohana 11:11-16. Je, sasa wanafunzi wameshawishika kwamba ni wazo jema kwenda kwa Lazaro? (Huu ni mzaha mkubwa kabisa. Sasa kila mtu atakufa.)
    1.    Hebu turuke vifungu kadhaa chini hadi Yohana 11:20-21. Martha anaamini kuwa chanzo cha kifo cha Lazaro ni kipi? (Kutokuja kwa Yesu wakati alipoitwa.)
      1.    Kwa nini Martha peke yake ndiye aliyemlaki Yesu? (Kinachoonekana ni kwamba Mariamu amemkasirikia Yesu.)
    1.    Soma Yohana 11:22-27. Martha anasema kuwa imani yake kumhusu Yesu ni ipi? (Yesu ni Masihi, Mwana wa Mungu. Ameshuka kutoka mbinguni.)
      1.    Je, ni muhimu kuwa na imani ya Martha ili kukubali/kukiri kwamba Yesu atamponya Lazaro? (Tunaona kwamba Yohana anauandika muujiza huu ili kuthibitisha kuwa Yesu ni Mungu.)
    1.    Soma Yohana 11:32-35. Mariamu pia anamlaumu Yesu kwa kifo cha Lazaro. Kwa nini Yesu analia wakati mashtaka haya yalipoibuliwa dhidi yake? (Mashtaka ni ya kweli. Hata hivyo, Yesu anampenda Martha, Mariamu, na Lazaro. Yesu Analia wakati akijua kile atakachokitenda.)
    1.    Soma Yohana 11:36-37. Je, hiki ndicho hasa ambacho Maratha na Mariamu wanakifikiria?
    1.    Soma Yohana 11:38-40 na usome tena Yohana 11:4. Ukweli kwamba mwili wa Lazaro umeanza kuoza ni wa muhimu kwa jinsi gani kwenye utukufu wa Mungu?
    1.    Soma Yohana 11:41-44. Yesu anamfufuaje Lazaro? (Kwa kunena tu. Huu ni uwezo ule ule ulionena na Uumbaji ukafanyika.)
      1.  Hebu tusome tena Yohana 11:24-25. Kuna tofauti gani kati ya ufufuo huu na ule wa siku ya mwisho
    2.    Soma Yohana 11:45-47. Ungejibuje swali lililoibuliwa na viongozi wa Kiyahudi?
    3.    Soma Yohana 11:53. Je, jibu lao linaleta mantiki yoyote?
    1.    Rafiki, jibu sahihi la swali ni kwamba “Amini Yesu ana uwezo juu ya mauti.” Yeye aliyetengeneza mkate, kumponya kipofu na kumfufua Lazaro anaweza kukupatia uzima wa milele ili uweze kuishi milele. Kwa nini usichague kumwamini Yesu sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Kisa Usuli: Utangulizi.