Somo la 11: Kuchukuliwa na Kushtakiwa
Somo la 11: Kuchukuliwa na Kushtakiwa
(Marko 14)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, huwa unakuwa na mwitiko/mjibizo gani kwenye msongo wa mawazo? Kwa ujumla sijawahi kuwa na msongo wa mawazo uliohatarisha maisha yangu. Msongo niliowahi kuupitia unahusiana na masuala ya kimahakama na unenaji mbele ya hadhara. Kiwango kidogo cha msogo wa mawazo ni kizuri kwa ajili ya kufanya mawasilisho mbele ya hadhara. Kiwango kikubwa cha msongo kinaweza kuleta mfadhaiko. Katika somo letu juma hili, wanafunzi wa Yesu wanatoka katika hali ya kufurahia chakula cha jioni hadi kuingia kwenye msongo wa kudhani kuwa wanaweza kuuawa. Yesu anajua kuwa atauawa, licha ya hayo anakabiliana na msongo kwa ujasiri. Hebu tuzame kwenye somo letu la Marko na tujifunze zaidi!
- Maadui na rafiki
-
- Soma Marko 14:1-2. Kwa nini viongozi wa Kiyahudi wanataka “kumkamata [Yesu] kwa hila na kumwua?” (Soma Yohana 11:47-48. Nia yao ya kuua inatokana na ukweli kwamba wanaamini Yesu atawatoa maanani. Yesu ni tishio kwa mfumo wa kisiasa. Nia yao ya kufanya hila ni kwa sababu wanaenenda kinyume na matakwa ya umma. Kutumia mfumo wa “kimahakama” dhidi ya adui nje ya mtazamo wa umma ndio asili ya wadhalimu na madikteta.)
-
- Soma Marko 14:3. Mwanamke huyu anafanya nini kilicho kinyume na viongozi wa Kiyahudi? (Anamheshimu Yesu kwa kumimina marhamu ya gharama kubwa kichwani pake.)
-
-
- Je, hili ni jambo jema?
-
-
- Soma Marko 14:4-6. Yesu anasema ni “kazi njema” ambayo ameitenda. Ni kwa msingi gani watu wengine wanamkaripia mwanamke huyu? (Fedha wangeweza kupewa maskini.)
-
-
- Je, unawafahamu “wakaripiaji” leo wanaotoa mashtaka kama hayo kuhusu jinsi ambavyo watu wengine wanatumia fedha zao?
-
-
- Soma Marko 14:7-9. Yesu anawaambia nini “wakaripiaji” na anamwambia nini mwanamke? (Anawaambia wakaripiaji kuwa wanaweza kuchangia fedha zao kwa maskini muda wowote wanaotaka. Kwa mwanamke anasema kuwa amempaka marhamu kwa ajili ya maziko na tendo lake litakuwa maarufu.)
- Meza ya Bwana/Pasaka (Last Supper)
-
- Ruka hadi mbele na usome Marko 14:12-13, Marko 14:16-17, na Marko 14:22-24. Yesu anafafanua nini kuhusu Pasaka? (Yeye ni kondoo wa Pasaka. Wanachokula ni ishara ya mwili na damu yake.)
-
-
- Kwa nini Yesu anatoa ufafanuzi huu sasa hivi? (Anataka wanafunzi wake waelewe kwa nini anakaribia kufa. Anawataka waelewe jinsi anavyotimiza ishara ya Pasaka. Wamekataa kuamini kuwa Yesu atakufa.)
-
-
- Soma Marko 14:25. Kwa nini hili? (Miongoni mwa mambo mengine, ni ahadi ya mbingu. Kinachodokezwa ni uelewa kwamba watakuwepo ili kunywa na Yesu mbinguni.)
- Usaliti
-
- Soma Marko 14:10-11 na Marko 14:43-46. Tutaona kwamba wengi wa wanafunzi sio waaminifu kwa Yesu. Je, kitendo cha Yuda kinaleta mantiki yoyote kwako? Ikiwa Yuda aliamini, kama ambavyo wanafunzi wengine waliamini (angalia Matendo 1:6), kwamba Yesu atauandaa ufalme, kwa nini auuze mustakabali huu uliojaa utajiri kwa kiwango kidogo cha fedha? (Ninaamini Yuda alimsaliti Yesu ili apate fedha, lakini si kwa fedha alizopewa na makuhani wakuu. Alikuwa ameuona uwezo wa Yesu, na alidhani alikuwa akimlazimisha Yesu kuchukua mamlaka sasa hivi. Yesu atamshukuru baadaye.)
-
- Soma Marko 14:18-21. Kwa nini Yesu anambainisha msaliti wake? (Anampatia Yuda nafasi ya mwisho. Nadhani Yesu anamwambia Yuda kwamba hausaidii ufalme wa Yesu, bali anamsaliti Yesu.)
-
- Soma Marko 14:26-28. Je, wanafunzi wa Yesu waliosalia pia hawatakuwa waaminifu kwake?
-
-
- Ungejisikiaje kama ungekuwa Yesu?
-
-
-
- Je, usaliti wa wanafunzi wengine unatofautiana na ule wa Yuda?
-
-
- Soma Marko 14:29. Kwa nini Petro anadhani kuwa yeye peke yake ndiye hatamsaliti Yesu? Hii inazungumzia nini kumhusu?
-
- Soma Marko 14:30-31. Utaona kwamba wanafunzi waliosalia wote wanasikiliza. Je, hii inamwaibisha Petro?
-
- Soma Marko 14:32-37. Kwa jinsi gani mtu ambaye yuko radhi kufa kwa ajili ya Yesu asiweze kuwa macho na kumwombea? (Soma Marko 14:38. Jibu la Yesu ni kwamba Petro ni mwanadamu. Yesu ni mkarimu kwa Petro.)
-
-
- Je, umewahi kuangushwa (let down) na “mwili dhaifu?”
-
-
-
- Ni nini tiba ya “mwili dhaifu?” (Yesu anamwambia Petro “akeshe na kuomba.” Tunatakiwa kumtegemea Mungu na tunatakiwa tuwe wasikivu kwa kilicho muhimu.)
-
-
- Soma Marko 14:39-42. Jiweke kwenye nafasi ya Yesu. Mara tatu wanafunzi wake wa karibu kabisa wamemwangusha kwenye suala jepesi sana – kumwombea. Ungejisikiaje pale unapoingia kwenye kipindi kigumu kabisa maishani mwako? (Fundisho ni kwamba tunaweza kumtumaini Mungu peke yake. Watu wengine watatuangusha na inaweza isiwe kwa kudhamiria.)
-
- Hebu turikie mbele na tusome Marko 14:46-47 na tusome Yohana 18:10-11. Yesu anapochukuliwa mara ya kwanza, Petro anatoa upanga wake na anajaribu kukata kichwa cha mtumwa wa Kuhani Mkuu. Je, Petro alimaanisha kwa dhati aliposema kuwa atakufa kwa ajili ya Yesu? (Alimaanisha kwa dhati kabisa. Kwa kutoa kwake upanga kungeweza kusababisha auawe.)
-
- Hebu tuendelee na Petro. Soma Marko 14:53-54 na Marko 14:66-72. Unaielezeaje safari ya Petro tangu kuchomoa upanga wake hadi kuapa kuwa hamjui Yesu? (Petro alimaanisha kile alichokisema. Alitoa upanga wake, aliyapuuza maisha yake ili kumtetea Yesu. Lakini Yesu hakujiunga kwenye pambano. Petro alipata mshtuko kwamba Yesu, ambaye alikuwa na uwezo wa kuwadhibiti, hakujibu mapigo na kuuchukua ufalme wake. Petro alikuwa radhi kufa kwa ajili ya ushindi. Hakuwa tayari kufa kwa sababu ambayo ingemfanya awe na mashaka na mustakabali wa siku zijazo.)
-
-
- Unadhani kwa nini Petro alilia? (Alikuwa amemwangusha Yesu. Asingeweza kujiamini na hakuweza kuutumaini mustakabali wake unaokuja. Maisha yake yalikuwa yameyoyoma.)
-
-
- Hebu tumwangalie mtoro mwingine. Soma Marko 14:51-52. Je, huyu ni mwanafunzi? (Hapana. Vinginevyo jina lake lingebainishwa.)
-
-
- Kwa nini amevaa nguo ya kitani pekee? (Hii inaashiria alikuwa amelala, akasikia kuwa Yesu anakaribia kukamatwa, na akakimbia kuelekea kwenye tukio bila kuvaa kikamilifu.)
-
-
-
- Je, mtu huyu anamuunga mkono Yesu? (Watu wanaokuja kumkamata Yesu wanadhani hivyo.)
-
-
-
- Kwa nini tukio hili linajumuishwa kwenye kitabu cha Marko? (Watu wengi wanadhani Marko anaandika habari zake mwenyewe. Inaweza kuwa toba yake kwamba yeye pia alimtelekeza Yesu. Kama huyu hakuwa Marko, isingekuwa na maana kulijumuisha tukio hili. Dhana iliyopo ni kwamba Yesu aliangushwa na wafuasi wake wote.)
-
- Yesu Mwamba Wetu
-
- Soma Marko 14:43-46 na Marko 14:48-49. Ni nini jibu la Yesu kwenye swali la kwa nini hawakumkamata wakati wa mchana hekaluni? (Tunafahamu jibu kutoka Marko 14:2. Waliwaogopa watu.)
-
- Soma Marko 14:53 na Marko 14:55-59. Kesi inawaendeaje viongozi wa dini? (Inawaendea vibaya sana. Mashahidi wa uongo hawakubaliani kwenye visa vyao.)
-
- Soma Marko 14:60-61. Kuhani Mkuu ana hali gani pale anapomtaka Yesu ajihukumu mwenyewe? (Soma Kumbukumbu la Torati 17:6 na Kumbukumbu la Torati 19:15. Walikuwa na kanuni ya utoaji ushuhuda kwamba mtu asingeweza kutiwa hatiani kwa ushuhuda wake mwenyewe. Yesu alikuwa na haki ya kukaa kimya.)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 19:18-20. Kuhani Mkuu alipaswa kufanya nini? (Alipaswa kuwachunguza kwa makini mashuhuda wa uongo. Unabashiri kuwa nani aliwatafuta mashuhuda wa uongo?)
-
- Soma Marko 14:61-64. Je, baraza zima limeamua kupuuzia kanuni ya ushuhudiaji? Je, Yesu amenyimwa taratibu kamili za kufuatwa? (Hapana. Sasa tunao mashuhuda wengi. Mashtaka mapya ni kufuru ambayo msingi wake ni Yesu kusema kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu. Wote walisikia kauli hiyo.)
-
-
- Unadhani Yesu alikuwa na wajibu wa kimaadili kutoa jibu ambalo alilitoa?
-
-
- Soma Marko 14:65. Je, kwa upande wako hii inaonekana kuwa njia ya kawaida ya kesi inavyopaswa kuwa? (Kwa dhati walimchukia Yesu!)
-
- Rafiki, si watu wengi wanaosoma somo hili wamepitia uzoefu wa kuchukiwa kweli kweli na watu kwa sababu ya injili. Hilo linabadilika katika ulimwengu wa Magharibi. Chuki inaongezeka. Utafanya nini utakapokabiliana na watu watakaouchukua uhuru wako au kuyachukua maisha yako? Mwombe Roho Mtakatifu akupatie ujasiri wa unyenyekevu kusalia kuwa mwaminifu kwa Yesu.
- Juma lililopita: Kushtakiwa na Kusulubiwa.