Somo la 7: Kuwafundisha Wanafunzi: Sehemu ya 1
Somo la 7: Kuwafundisha Wanafunzi: Sehemu ya 1
(Marko 8 & 9)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Marko anatupatia uthibitisho baada ya uthibitisho kwamba Yesu ni Masihi. Yesu ni Mungu. Sasa Marko anabadili mwelekeo. Lengo lake sasa ni kutufundisha kuwa Mungu alikuja ili afe. Hilo linaonekana jambo la kufedhehesha sana kiasi kwamba wanafunzi hawakuweza kuliamini. Tuna msemo wa Kiingereza usemao, “He could not wrap his mind around it” (Mawazo yake hayakuweza kulielewa). Hicho ndicho kinachoendelea hapa: wanafunzi hawakuweza kuelewa suala la Yesu kufa. Je, nasi tunafanana na wanafunzi? Je, kuna vipengele vya uelewa wetu wa Kikristo vinavyohitajika kubadilika kwa namna ambayo ni vigumu kwetu kuamini? Ikiwa ndivyo, tunatakiwa kutembea na wanafunzi wanapotambua jambo hili lisiloeleweka. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!
- Usipofanikiwa Mara ya Kwanza, Jaribu Tena
-
- Soma Marko 8:22. Nani anayeomba uponyaji? (“Watu” waliomleta kipofu kwa Yesu.)
-
- Soma Marko 8:23-24. Yesu anampeleka kipofu nje ya kijiji. Kwa nini? (Huenda hili linahitaji kipofu kuwa na kiasi fulani cha imani. Utakumbuka kwamba ni watu waliomzunguka ndio waliotoa wito wa uponyaji, na si kipofu.)
-
-
- Kwa nini Yesu anamtemea mate machoni na kumwekea mikono? Hatujaona muujiza ambao Yesu anamtemea mtu mate.
-
-
- Soma 2 Wafalme 5:9-11. Naamani alitarajia nini kwa ajili ya uponyaji wake? (Alitaka mtu aonekane.)
-
-
- Unadhani kwa nini alitarajia mtu ajitokeze? (Sababu yoyote utakayoitoa, ndio sababu ya kwa nini Yesu alikuwa anampatia kipofu huyu aina fulani hivi ya kujionesha.)
-
-
- Angalia tena Marko 8:24. Nani anayeelewa anachokielezea kipofu? (Niliwahi kuwa na uoni hafifu. Mtu yeyote mwenye shida ya kuona mbali analielewa hili – watu wanaonekana kama miti inayotembea kwa mbali. Hii inatuambia kuwa upofu wa mtu huyu bado haujaponywa kikamilifu.)
-
- Soma Marko 8:25. Kwa nini Yesu alishindwa kutenda muujiza kwa usahihi mara ya kwanza? Je, ni kwa kuwa hakuwa na uwezo? (Yesu alikuwa na uwezo. Marko hatupatii jibu. Huenda Yesu anajenga imani ya kipofu.)
-
- Soma Marko 8:26. Je, tunafahamu sababu ya Yesu kumwongoza mtu huyu kwenda nje ya kijiji? (Hapo kabla tulijadili suala hili la Yesu kuwaambia wale aliowaponya kufanya uponyaji huo kuwa siri. Kifungu hiki kinatupatia jibu la kwa nini Yesu alimpeleka nje ya kijiji. Yesu alitaka kuepuka kuwaamsha na kuwakereketa watu katika kijiji kile.)
- Toba
-
- Soma Marko 8:27-28. Mawazo ya watu wengine yanayaongozaje mawazo yako?
-
-
- Je, huwa unaona kuwa hakuna unayemfahamu aliye na mawazo sawa na yako? (Hilo litakuwa jambo lisilokuwa la kawaida kabisa.)
-
-
-
- Kwa kuzingatia majibu haya, je, inashangaza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja anayemfahamu mtu nje ya kundi lao aliyedhani kuwa Yesu ni Masihi?
-
-
- Soma Marko 8:29-30. Je, unadhani Petro anawajibia wanafunzi wengine, au anajijibia mwenyewe? (Kama Petro hawajibii wenzake, ukweli kwamba Yesu anawaelekeza wasiseme inadhihirisha kuwa Yesu anaidhinisha jibu la Petro kwamba Yeye ni Mungu.)
-
-
- Mojawapo ya mambo ya msingi kabisa ambayo nimejifunza kutokana na kujifunza Biblia ni kwamba Roho Mtakatifu hatii msukumo wa visa na kauli za aina mbalimbali. Muktadha ni msaada mkubwa katika uelewa. Je, uponyaji uliozingatia hatua mbili ni wa muhimu kwenye mjadala huu wa Yesu ni nani? (Ni kioo. Maoni ya wengine yalionesha kuwa Yesu alichukuliwa kuwa mtu wa muhimu. Lakini kama ilivyo kwa watu wanaoonekana kama miti, hii haikuwa sahihi. Yesu anapouliza wanafunzi wana maoni gani, swali hili la hatua ya pili linajibiwa kwa usahihi. Kama ilivyokuwa kwa hatua ya pili ya uponyaji wa kipofu.)
-
- Jambo Gumu Kueleweka
-
- Soma Marko 8:31-33. Hebu tujadili hili kifungu kwa kifungu. Je, ungechukulia ujumbe wa kifungu cha 31 kuwa tatizo kama ungekuwa mwanafunzi? Yesu atarudi ndani ya siku tatu! Mgogoro wake na viongozi wa Kiyahudi sio habari za kushangaza.
-
-
- Unadhani kwa nini Petro alidhani kuwa ana mamlaka ya kumkemea Yesu? (Bado alikuwa anajihisi mwenye nguvu kwa kumtambulisha Yesu kama Kristo.)
-
-
-
- Utaona kwamba Marko 8:33 inasema “akawatazama wanafunzi wake.” Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Inawezekana Petro alimchukua Yesu pembeni, lakini wanafunzi walikuwa wanasikiliza. Hii, hata hivyo, ilikuwa habari ya kushangaza.)
-
-
-
- Tafakari shtaka la Yesu kwamba Petro alikuwa anayawaza yaliyo ya wanadamu na si mambo ya Mungu. Hii si ni kinyume na kile ambacho Petro alidhani alikuwa anakitenda? Masihi anawezaje kufa?
-
-
-
-
- Kama hili ni “jambo la kibinadamu,” je, upendo sio jambo bora kabisa la hisia za mwanadamu? Petro alimpenda Yesu!
-
-
-
-
-
- Kuna uwezekano kuwa Petro aliwazia “jambo gani la kibinadamu” lililoweza kuwa la Kishetani? (Tutajadili hili kwa kulihusianisha na vifungu vinavyofuata.)
-
-
-
-
- Kabla hatujaachana na kifungu cha 33, je, mtu anaweza kuzungumza kwa niaba ya Mungu dakika moja na kwa niaba na Shetani dakika inayofuata? (Soma Yakobo 3:10-12. Yakobo anasema halipaswi kutokea.)
-
-
- Soma Marko 8:34. Hili linahusianaje na Yesu kumwambia Petro kuwa anawaza mambo ya kibinadamu? (Soma Matendo 1:6. Bila shaka Petro alimpenda Yesu, lakini pia alipenda wajibu wake ujao katika ufalme mpya wa Masihi hapa duniani. Yesu kuuawa, na kufufuka baada ya siku tatu, hakukuendana na mtazamo wa Petro juu ya siku zijazo.)
-
-
- Hili ni suala ambalo kila Mkristo anapaswa kulitafakari. “Je, ninatenda mambo mema ili kujitukuza, au kumtukuza Mungu?” (Katika 1 Timotheo 5:17 tunaambiwa kuwa wale wanaofundisha na kuhubiri wanapaswa kuheshimiwa. Lakini kuuchukua msalaba inamaanisha kuwa majukumu na wajibu huja kabla ya heshima.)
-
-
- Soma Marko 8:35-37. Yesu anajenga hoja gani ya kiuhalisia? (Sote tutakufa. Tutakuwa na busara kufa kwa namna ambayo inatupatia uzima tena.)
-
- Soma Marko 8:38. Tunapaswa kufanya nini katikati ya ulimwengu mwovu? (Kusimama imara!)
- Ni Vigumu Kuwa Mnyenyekevu
-
- Hebu turukie mbele na tusome Marko 9:30-32. Katika sura iliyotangulia Yesu aliwaambia “wazi” kuwa atakufa na kufufuka. Petro “akamkemea” Yesu kwa kulisema hili. Sasa Yesu analisema hili tena na wanafunzi hawaelewi na wanaogopa kuuliza. Je, umewahi kuona jambo kama hili? Watu hawawezi kuelewa taarifa mbaya? (Nimewahi kuona kwenye masuala ya kitabibu.)
-
- Soma Marko 9:33-34. Wanafunzi wanaelewa nini? (Hatima yao ni ukubwa!)
-
-
- Je, hii ndio sababu kwa nini hawawezi kuielewa kauli ya Yesu kwamba atakufa?
-
-
-
- Vipengele gani vingine vya maisha ya Kikristo vinaangukia kwenye kundi hili? Ukweli unakinzana sana na mipango na matarajio yetu kiasi kwamba hatuwezi kuelewa na hatutaki kuuliza?
-
-
- Soma Marko 9:35. Je, Yesu anawakemea kwa kutaka kuwa wakubwa? (Hapana. Badala yake, anawaambia jinsi unavyotendeka.)
-
-
- Kama mtu anaupata ukubwa kwa njia hii, je, anajisikia vizuri? (Hilo ndilo suala. Mtu anataka kuwa mkuu/mkubwa ili atumikiwe. Yesu anaondoa majivuno nje ya ukuu.)
-
-
- Soma Marko 9:36-37. Ni kwa jinsi gani “kumpokea” mtoto ni mfano wa kutumikia? (Sidhani kama hili linahusiana kivyovyote vile na hulka ya watoto, bali hili linahusiana na endapo mtoto anaweza kuendeleza bahati zako. Ukimsaidia mtu ambaye hawezi kukulipa kwa kukusaidia, hiyo ndio huduma ya kweli.)
-
- Soma Marko 9:38-40. Je, hili ni tatizo la majivuno? Je, Marko anasalia kwenye mada hiyo? (Ndiyo. Wanafunzi wanadhani kuwa wana haki miliki ya kipekee ya kusambaza injili.)
-
-
- Je, hili ni tatizo katika zama za leo? (Ndiyo. Nilipokuwa mtu mzima na kuanza kupeleka injili kwa washiriki wa makanisa mengine, nilitambua kuwa wao pia walidhani kuwa walipokuwa wakikua kanisa lao ndilo lililokuwa kanisa pekee “la kweli.” Masalia katika kitabu cha Ufunuo linafafanuliwa kwa kile ambacho watu walikiamini na kukitenda, na si kwa jina la madhehebu. “Asiye kinyume chetu, yu upande wetu.”
-
-
- Soma Marko 9:41. Hapo kabla suala lilikuwa kuondoa pepo wachafu, hii ni kutoa kikombe cha maji ya kunywa. Yesu anamaanisha nini? (Chochote kinachofanyika ili kuutangaza Ukristo, hata kama ni kidogo kiasi gani, kitapewa thawabu.)
-
- Rafiki, je, majivuno yako yanaingilia kati uelewa wako kamili wa injili? Injili inahusiana na huduma, na hata huduma ya msingi kabisa inapewa thawabu. Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, akupatie uwezo wa kuyashinda majivuno?
- Juma lijalo: Kuwafundisha Wanafunzi: Sehemu ya II.