Somo la 1: Mwanzo wa Injili

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Matendo 12-13, Marko 1
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
3
Lesson Number: 
1

Somo la 1: Mwanzo wa Injili

(Matendo 12-13, Marko 1)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umewahi kupitia uzoefu wa vipingamizi maishani mwako? Vipingamizi hivyo vilikusababishia nini? Somo letu katika robo hii limejengwa juu ya Injili ya Marko. Mwanzoni kabisa maishani mwake Marko alipitia uzoefu wa kipingamizi kikubwa. Aliendelea kuwa imara na kuishia katika kitovu cha kazi ya kanisa la awali. Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu aliandika Injili ya Marko. Kurejea kwa kishindo kikubwa namna gani! Hebu tuzame kwenye kisa cha Marko na tuone jinsi maisha yake yalivyorejea katika mstari na jinsi gani anavyoanzisha injili yake!

I.  Mwana wa Petro?

A.  Soma 1 Petro 5:13. Je, ulifahamu kuwa Petro alikuwa na mwana aliyeitwa Marko? (Kama tutakavyoona, Petro na Marko walifanya kazi pamoja. Petro anatumia msamiati wa upendo/huba, hasemi kuwa Marko ni mwanaye halisi.)

1.  Je, huyu Marko, mfanyakazi mwenza wa Petro, ndiye mwandishi wa Injili ya Marko? (Papias, mwandishi wa awali wa Kikristo, anatuambia kuwa Marko alikuwa mshirika wa karibu wa Petro. Hii inafafanua kwa nini Petro anamrejelea Marko kama “mwanangu.” Kwa mujibu wa the Bible Exposition Commentary, utamaduni wa kanisa unamrejelea Marko kama “mkalimani wa Petro.” Inaonekana kwamba Petro alihubiri kuhusu kazi yake na Yesu, Marko akayaandika na kuyapangilia. Hii imenukuliwa kutoka NIV Study Bible, Introduction to Mark.)

2.  Unapowafikiria wanafunzi wa Yesu, ungependa kufanya kazi na nani? (Petro ni mtu wa vitendo. Kitabu cha Marko kimejaa matendo – haishangazi kama alichukua vyanzo vyake vya taarifa kutoka kwa Petro.)

B.  Soma Matendo 12:1-2 na Matendo 12:6. Unadhani maneno “Wakati Petro alipotaka kumtoa [Petro]” yanamaanisha nini? (Kutokana na ukweli kwamba Herode alikuwa ametoka kumwua Yakobo, alikuwa anataka kumtoa Petro ili amwue.)

C.  Soma Matendo 12:7 na Matendo 12:11-12. Tunajifunza nini kuwahusu Yohana Marko na Petro? (Petro alijua kuwa watakuwa wakimwombea nyumbani kwa mama wa Yohana Marko.)

II.  Yohana, Marko, Paulo, Barnaba

A.  Soma Matendo 13:2-5. Sasa tunamwona Yohana Marko akiwa wapi? (Anawasaidia Paulo na Barnaba!)

1.  Hiyo inakwambia nini kumhusu Yohana Marko? (Alikuwa kiini cha tukio.)

B.  Soma Matendo 13:13 na Matendo 15:36-39. Litafakari hili. Kwa nini Barnaba hakukubaliana tu na Paulo? Roho Mtakatifu aliwaita Paulo na Barnaba ili wafanye kazi pamoja! Kifungu cha 39 kinarejelea kutokubaliana “kwa kiwango kikubwa.” Lazima Barnaba alimchukulia Yohana Marko kwa upekee mkubwa na lazima alidhani kwamba Paulo hakutafakari kwa umakini. Lazima itakuwa kwamna Paulo alikuwa mkosoaji mkubwa wa Yohana Marko.)

C.  Soma Wakolosai 4:10. Hapa tunaona kiashiria gani kuhusu sababu ya Barnaba kuwa muungaji mkono mkubwa wa Yohana Marko? (Wana uhusiano!)

D.  Soma 2 Timotheo 4:11 na Wakolosai 4:10-11. Tunajifunza nini kuhusu uhusiano kati ya Paulo na Yohana Marko baadaye kabisa maishani mwa Paulo? (Wamepatana na Yohana Marko ni msaada muhimu kwa Paulo.)

1.  Sasa tunafahamu kuwa Yohana Marko hatimaye ni mshirika wa karibu wa Paulo na pia ni mshirika wa karibu wa Petro. Hiyo inakwambia nini kuhusu kurejea kwa Marko kama mtendakazi wa injili? (Anafanya kazi na viongozi wakuu wa kanisa la awali. Marko amerekebisha mambo yake kutokana na kufeli kwake kwa awali.)

a.  Kutokana na vifungu tulivyojifunza, unadhani Marko alifanikiwaje kurejea kwa kishindo? (Ilikuwa jambo la msaada kwa Marko kuhusiana na Barnaba. Lakini muktadha unaashiria kwamba Marko alifanya kazi kwa bidi akiwa na viongozi wa juu. Ingawa Paulo alikuwa kinyume naye, alifanya kazi na Paulo ili kubadili mtazamo wake. Hakumwepuka/hakumkwepa Paulo.)

III.  Marko Anamtambulisha Yesu

A.  Soma Marko 1:1. Je, unapendelea urahisi au ugumu? Marko anaanzaje injili yake? (Kiurahisi, moja kwa moja, na bila kuzungukazunguka.)

1.  Je, unaweza kumwona Petro akizungumza kwa namna hii?

B.  Soma Waefeso 6:18-19. Paulo anaandika kuhusu “ile siri ya injili.” Je, Marko anaanza vibaya kwa kufanya mambo yaonekane marahisi? Je, Marko anaelekea kubaya kwa sababu ya ushawishi wa Petro tofauti na Paulo?

C.  Hebu tusimame kando kidogo. Jiweke katika kipindi cha kanisa la awali. Ingekuwa changamoto kiasi gani kujenga hoja kwamba Yesu alikuwa “Mwana wa Mungu?”

1.  Je, kuna siri kwenye dhana ya kwamba Mwana wa Mariamu pia ni Mwana wa Mungu?

D.  Soma Marko 1:2-3. Marko anajenga hoja gani kwamba Yesu ni Mungu? (Soma Malaki 3:1 na Isaya 40:3. Vifungu vyote hivi vinatabiri kwamba mjumbe ataandaa njia kwa ajili ya ujio wa Bwana.)

E.  Soma Marko 1:4-7. Je, Yesu alitanguliwa na mjumbe? (Ndiyo! Yohana Mbatizaji aliandaa njia kwa ajili ya Yesu. Yohana mbatizaji pia anasema kuwa hicho ndicho anachokifanya.)

1.  Kama ungekuwa unasoma Injili ya Marko, je, hili lingesaidia kukushawishi kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu? (Marko ananukuu Biblia na matukio ya hivi karibuni yakionesha utimilifu wa unabii kuhusu ujio wa Bwana. Je, hiki sicho tunachoelekea kukitenda? Tunaangalia katika mazingira yetu, na kuona kile kinachotendeka, na kisha kukilinganisha na unabii wa Biblia.)

F.  Soma Marko 1:8. Ubatizo wa Yesu unatofautianaje na ubatizo wa Yohana?

G.  Soma Yohana 4:1-2. Unafafanuaje Marko 1:8 ambapo Yohana Mbatizaji anatabiri kuwa Yesu atabatiza kwa Roho Mtakatifu? (Kifungu hiki kinaendana kwa maana ya kwamba Yesu habatizi kwa maji. Lazima Yohana Mbatizaji atakuwa anamaanisha kwamba Yesu atawafanya watu waje “chini” ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Ninaweza kuona ishara kati ya kuzikwa majini na kufunikwa na Roho Mtakatifu. Linganisha na Mathayo 28:19.)

H.  Soma Marko 1:9. Kwa nini Yesu ahitajike kubatizwa? Je, alikuwa mdhambi aliyehitaji kutubu na kubatizwa? 

I.  Soma Mathayo 3:13-15. Hili ni jibu la Yesu kwa swali la kwa nini anapaswa kubatizwa na Yohana. Yesu anamaanisha nini kwamba anabatizwa ili “kuitimiza haki yote?” (Ubatizo ni agizo ambalo tunalipitia ili kuonesha kwamba tulikufa katika maisha yetu ya kale na sasa sisi ni wenye haki kwa njia ya imani katika Yesu. Warumi 6:4-5. Yesu anakuwa mfano kwetu. Anatuonesha jinsi ya kutimiza haki.)

J.  Soma Marko 1:10-11. Marko anatoa uthibitisho gani wa ziada kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? (Mungu alitangaza kuwa Yesu ni Mwanaye wakati wa ubatizo wa Yesu.)

1.  Angalia nani aliyemshukia Yesu. Je, huu ni uthibitisho zaidi kwamba nyongeza ya Yesu kwenye ubatizo wa Yohana ni ubatizo wa Roho Mtakatifu?

2.  Je, umebatizwa kwa maji na Roho Mtakatifu?

IV.  Ujumbe

A.  Soma Marko 1:14-15. Marko anatufundisha kuwa “injili ya Mungu” ni ipi? (Wakati umetimia. Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini injili. Hebu tuangalie kila kimoja kati ya hivi vilivyobainishwa.)

1.  “Wakati umetimia.” Soma Yohana 3:30. Je, Yesu alisubiria kuanza utume wake kwa uaminifu hadi baada ya Yohana kutiwa gerezani? (Huduma hizi mbili zilitofautiana. Utume wa Yohana ulikoma wakati huduma ya Yesu ilipokua. Yohana aliandaa njia. Sasa ulikuwa wakati wa Yohana kupungua na Yesu kuzidi.)

2.  “Ufalme wa Mungu umekaribia.” Je, Yesu ndiye Ufalme wa Mungu? (Ndiyo. Mfalme yupo. Njia ambayo Ufalme wa Mungu duniani utarejeshwa sasa inafanya kazi.)

3.  Tubuni na kuiamini injili.” Nilidhani kwamba Yohana alihubiri toba. Je, bado watu wana uhitaji wa kutubu dhambi? (Sidhani kama hicho ndicho kinachomaanishwa na toba hapa. Kimsingi watu walikuwa na dhambi. Lakini hapa toba inafungamanishwa na injili. Watu walihitajika kubadilika kutoka katika mtazamo wao wa kale wa kukabiliana na dhambi, na kuingia kwenye mtazamo mpya wa Yesu kuwa mbebaji dhambi wao na Roho Mtakatifu kuyaongoza maisha yao katika njia sahihi.)

B.  Rafiki, je, umempokea Yesu kama Mungu aliyekuja duniani? Je, umetubu na kuiamini injili ya Yesu Kristo? Kama jibu ni hapana, kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

V.  Juma lijalo: Siku Moja Katika Huduma ya Yesu.