Somo la 6: Mashahidi Wawili

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 11, Zekaria 4
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
6

Somo la 6: Mashahidi Wawili

(Ufunuo 11, Zekaria 4)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Mojawapo ya unabii usio wa kawaida kabisa katika Biblia ni utabiri wa Ufunuo 11 kuhusu “mashahidi wawili” wanaohusika katika kudhihirisha nguvu za ajabu. Ufunuo 11 inatuambia, “Moto unatoka vinywani mwao” ili kuwaangamiza wapinzani. “Wana nguvu za kulifunga anga,” kubadili maji kuwa damu, na kusababisha kila aina ya msiba! Kisha wanauawa. Lakini, hebu subiri, wanafufuka tena! Ni jamaa (guys) gani hawa? Tunaanza kupata ufumbuzi kwamba wanaweza wasiwe “jamaa” au watu kabisa kwa sababu wanashuhudia kwa zaidi ya miaka elfu moja! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuvumbue kile ninachodhani kuwa ni uelewa wenye mantiki kubwa juu ya mashahidi wawili wa Ufunuo 11!

I.  Miti ya Mizeituni na Vinara vya Taa

A.  Soma Ufunuo 11:1-4. Mashahidi wawili wanalinganishwa na vitu viwili visivyokuwa na uhai, miti na vinara vya taa. Unapovifikiria vinara vya taa, rejea gani ya awali katika kitabu cha Ufunuo inakujia akilini? (Soma Ufunuo 1:12-13 na Ufunuo 1:20. Tunaona mwanzoni mwa kitabu cha Ufunuo kwamba vinara vya taa vinarejelea makanisa.)

1.  Kwa nini “kinara cha taa” ndio kiwe ishara ya kanisa na sio taa yenyewe?

B.  Soma Zekaria 4:1-3. Tunaona tena miti ya mizeituni, kinara cha taa, na taa. Unadhani mitu ya mizeituni inahusianaje na taa kwenye vifungu hivi? (Soma Zekaria 4:12. Miti ya mizeituni inatoa “mafuta ya dhahabu” ambayo yanawasha taa.)

1.  Taa ngapi zipo kwenye hiki kinara cha taa? (Saba. Utaona kwamba idadi hiyo inalingana kabisa na idadi ya makanisa katika Ufunuo 1.)

C.  Ufunuo 11:3-4 inawalinganisha mashahidi wawili na miti na vinara vya taa. Kama ningekuwa nimekupatia taarifa ambazo tumejadiliana hadi kufikia hapa kuhusu mashahidi wawili, ungehitimisha nini kuwahusu? Dhana gani inaunganisha kanisa na taa inayowashwa kwa kutumia mafuta? (Mwongozo wa injili. Lakini hebu tuendelee kuchunguza dhana hii. Inaonekana kama tunajishughulisha na vipande vya fumbo.)

D.  Soma Matendo 10:38 na Luka 4:18. Unadhani inamaanisha nini “kutiwa mafuta?” (Soma Kutoka 30:22-25 inayotupatia maelekezo ya kupata “mafuta matakatifu kwa ajili ya kumtia mtu mafuta.” Uelewa wa jumla wa Biblia ni kwamba kutiwa mafuta inamaanisha kuwekewa mafuta.)

1.  Vifungu katika vitabu cha Matendo na Luka vinahusianaje na kitendo cha kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu? (Kutia mafuta kwa kutumia mafuta kunalinganishwa na kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu.)

E.  Soma 2 Petro 1:21. Taa gani inawashwa na Roho Mtakatifu? (Biblia! Tunapounganisha vipande vya fumbo vya miti ya mizeituni, mafuta, taa, na vinara vya taa, taswira inayoibuka inaashiria kuwa mashahidi ni neno la Mungu, Biblia.)

1.  Je, Mungu ana Biblia mbili? (Nadhani Agano la Kale na Agano Jipya zinajibu swali hilo.)

II.  Umri wa Mashahidi

A.  Bado tuna viashiria vya kuchungunza kuhusu asili ya mashahidi wawili. Hebu tuchunguze kiashiria kingine. Soma tena Ufunuo 11:3. Je, hapo kabla umeona rejea ya siku 1,260 kwenye Biblia? (Fungu la awali, Ufunuo 11:2 linarejelea miezi arobaini na miwili ambayo ni sawa na siku 1,260. Danieli 7:25 inarejelea “wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.” Hii ni sawa na 3.5, ambayo inarejelea miaka, sawa na siku 1,260. Kisha Ufunuo 12:6 na Ufunuo 13:5 zinarejelea kipindi kile kile.)

1.  Unadhani inamaanisha nini kwa mashahidi wawili kutoa unabii “wakiwa wamevikwa magunia?” (Unavaa gunia unapokuwa kwenye masikitiko au unapokuwa na huzuni.)

a.  Kama hitimisho letu la awali kwamba mashahidi wa kwenye Biblia ni sahihi, unadhani inamaanisha nini kutoa unabii ukiwa umevaa magunia? (Biblia imepitia uzoefu mbaya wa mabadiliko ya matokeo.)

2.  Unadhani rejea zote hizi kwenye Biblia kuhusu siku 1,260 zinarejelea kipindi kimoja? Je, ni suala la upatanifu (coincidence) kwamba kipindi hiki kimoja kinaelezewa katika maeneo kadhaa tofauti kwenye Biblia?

B.  Soma Danieli 7:23-26. Je, inaonekana kama matukio haya yanaweza kutokea katika miaka 3.5? (Maoni ya Adam Clark yanasema kuwa hii ni miaka ya “kinabii” “na mwaka wa kinabii una mwaka mmoja kwa kila siku moja.” Kama yuko sahihi, na ninadhani muktadha unamuunga mkono, basi tunazungumzia kuhusu miaka 1,260, na sio siku 1,260. Ikiwa rejea hizi kadhaa za siku 1,260 ni za kipindi kimoja, basi lazima tuhitimishe kwamba mara zote inarejelea miaka 1,260. Kwa kuzingatia miktadha mingine, hiyo inaleta mantiki.)

1.  Je, mwanadamu atakuwa shahidi kwa zaidi ya miaka elfu moja? (Kwa dhahiri jibu ni, “hapana,” na hiyo inatoa kiashiria cha ziada kwamba mashahidi wawili sio wanadamu.)

III.  Uwezo wa Mashahidi Wawili

A.  Soma Ufunuo 11:5-6. Je, unaweza kukumbuka jambo lolote kati ya haya likiarifiwa kwenye Biblia?

1.  Soma 2 Wafalme 1:9-10. Je, moto ulishuka kutoka mbinguni kwa neno la Eliya?

2.  Soma 1 Wafalme 17:1. Je, anga lilifungwa kwa neno la Eliya?

3.  Soma Kutoka 7:20. Je, maji yalibadilika kuwa damu kwa neno la Musa?

4.  Ukiweza kupitia kwa haraka haraka kitabu cha Kutoka sura za 7-11 utaona mapigo kadhaa yaliyokuja juu ya Misri Musa alipojitokeza mbele ya Farao. Kwa kuwa sasa umeshaona kilichotokea Eliya na Musa waliponena, je, inawezekana kuwa hawa ndio mashahidi wawili?

a.  Je, wanatatua tatizo la wanadamu kutoishi kwa miaka elfu moja? (Soma Mathayo 17:1-3. Tunaona kwamba Musa na Eliya walikuja duniani kutoka mbinguni! Unaweza kuona kwa nini baadhi ya watu wanaamini kuwa mashahidi wawili ni Eliya na Musa.)

B.  Hebu tuzame kwa kina zaidi. Je, kuna chanzo kimoja cha nguvu kilicho nyuma ya maneno ya Eliya, Musa, na Biblia? (Ndiyo! Roho Mtakatifu. Tunaweza kuona kwa nini utambulisho wa mashahidi wawili unazua mjadala, lakini ninaamini Biblia, ikiwa na maagano yake mawili, ndio inayofaa zaidi.)

IV.  Kifo cha Mashahidi Wawili

A.  Soma Ufunuo 11:7-10. Mashahidi wawili wanawezaje kuuawa ikiwa hawako hai? Hii ni dalili kuwa pendekezo langu la kwamba mashshidi wawili ni Biblia haliko sahihi!

B.  Jikite kwenye Ufunuo 11:7. “Ushuhuda” wa mashahidi “umemalizika” na “mnyama” “anafanya vita nao” na kisha anawaua. Je, Biblia ni ushuhuda? Je, vita imetangazwa juu ya Biblia? Hebu tuchunguze nukuu za nyuma:

1.  Papa Leo XII alitangaza, “Kama ilivyodhihirishwa kutokana na uzoefu kwamba, ikiwa Biblia takatifu kwa lugha ya wenyeji kwa ujumla inaruhusiwa bila tofauti yoyote, madhara yanasababishwa zaidi kuliko manufaa.” Great Encyclical of Letters of Leo XIII, pp. 412-413.

2.  Papa Pius IV aliandika: “Biblia sio kwa ajili ya watu: yeyote atakayeokolewa lazima aikanushe. Ni kitabu kilichopigwa marufuku. Jamii za Biblia ni hila za kishetani.” Catholic Church Council of Trent, Rule III.

3.  Kwa nini viongozi wa dini watoe kauli kama hizi? (Kilichopo ni kwamba watu wasio na elimu hawataweza kuielewa Biblia kwa usahihi.)

a.  Una maoni gani juu ya mzatamo huo?

C.  Chukulia kwamba katika zama za kati, kwa kuzingatia kauli za Mapapa hawa, Kanisa Katoliki lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumfanya mtu wa kawaida asiweze kusoma Biblia. Soma Ufunuo 11:11. Je, Biblia inaweza kufufuka? (Uchapishaji ulipovumbuliwa, watu wengi waliweza kusoma na kujifunza Biblia wao wenyewe. Ilikuwa zama mpya ya kujua kuandika na kusoma Biblia!)

D.  Hebu tuangalie tena katika Ufunuo 11:10. Je, umewasikia watu wanaoiona Biblia kuwa ni mateso? Je, kuna mtu yeyote wa zama za sasa anayeichoma Biblia?

E.  Soma Ufunuo 11:12. Hii inatuambia nini kuhusu pambano dhidi ya Biblia? (Biblia inashinda. Kama ambavyo Yesu kupaa kwenda mbinguni kunavyoonesha kuwa alishinda, kiishara Biblia inashinda na kusababisha “hofu kuu” kwa wale wanaopinga mafundisho ya Biblia.)

F.  Umejiuliza kwa nini tunajifunza Mashahidi Wawili? Kuna umuhimu gani, zaidi ya kutatua siri nyingine katika kitabu cha Ufunuo? (Mada yetu kwenye somo hili ni pambano kuu kati ya wema na uovu. Biblia ndio kinga, ukweli ulioshinda, kwenye pambano dhidi ya uovu.)

G.  Rafiki, je, utaithibitisha tena imani yako kwa Biblia? Je, unakubaliana kwamba kinachosemwa na Biblia ni kweli, na kuachana na dhana zako?

V.  Juma lijalo: Kuhamasishwa na Tumaini.