Somo la 3: Nuru Hung’aa Gizani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 14, Kumbukumbu la Torati 4, Matendo 20, Luka 9
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Nuru Hung’aa Gizani

(Yohana 14, Kumbukumbu la Torati 4, Matendo 20, Luka 9)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Unakumbuka kusikia visa vya mashujaa wa Kikristo walioambiwa kumkana Kristo au vinginevyo wafe? Je, umejiweka kwenye kisa hicho? Kuuawa ni suala la kutisha sana. Lakini huu ni uchaguzi mzuri, wa dhahiri – si ndio? Hakuna mjadala juu ya jambo sahihi la kulitenda. Ni suala tu la kama unajitoa au la. Wakati ninakumbuka chaguzi ngumu nilizozifanya wakati mibadala ilikuwa dhahiri, sehemu kubwa ya maisha inanijia ikiwa na rangi za kijivu. Swali ni endapo kweli kuna jambo ambalo lina makosa? Je, ni dhambi? Tunachokihitaji ni nuru zaidi. Tunachokihitaji ni utayari wa kupiga hatua kuingia nuruni. Hilo ndilo somo letu juma hili. Hebu tuzame kwenye uchunguzi wetu wa Biblia!

I.  Njia

A.  Soma Yohana 14:1-4. Je, unaona ukinzani wowote kati ya anachokisema Yesu katika vifungu vya tatu na nne? (Katika kifungu cha tatu Yesu anawaambia wanafunzi kwamba “niwakaribishe kwangu.” Lakini katika kifungu cha nne Yesu anawaambia kwamba “wanaijua njia.”)

B.  Soma Yohana 14:5. Kama mwalimu wa muda mrefu ninafahamu kwamba mwanafunzi anayeonekana kuuliza “swali la kipumbavu” huwa anaonyesha tu ujasiri. Wanafunzi wengine wengi wana swali hilo hilo. Je, unaijua njia ya kwenda mbinguni?

C.  Soma Yohana 14:6. Jiweke kwenye nafasi ya Tomaso. Je, hilo linajibu swali lako? (Tomaso anauliza uelekeo. Anauliza kuhusu jiografia. Yesu anajibu kwa muktadha wa teolojia!)

D.  Kwa kuwa sasa tunajua kuwa hatuzungumzii maelekezo ya matembezi, soma Yohana 14:7-10. Yesu anataka wanafunzi wake waelewe nini? (Asili ya Mungu. Yesu anawaambia jambo la kustaajabisha sana: wanachokijua kumhusu Yesu kinawafundisha kuhusu asili ya Mungu Baba.)

1.  Je, uelewa mwingine wowote ule kuhusu asili ya Mungu Baba ni sahihi? (Soma tena Yohana 14:6. Hii ndio njia pekee ya kumwelewa Mungu.)

E.  Soma Yohana 14:11-13. Sasa Yesu anageukia kwenye suala la matendo. Utakumbuka tulianza kwa kuangalia maelekezo ya matembezi kuelekea mbinguni. Je, haya ni maelekezo ya matembezi?

1.  Matendo gani ya Yesu ambayo ungependa kuyafanya?

2.  Matendo gani ya Yesu ambayo unapaswa kuwa unayatenda?

3.  Kazi kuu ya Yesu kupita zote ilikuwa ni ipi? (Kuishi kwa ajili yetu, kufa kwa ajili yetu, na kuibuka mshindi dhidi ya dhambi.)

II.  Matendo

A.  Soma Kumbukumbu la Torati 4:2. Je, kuna tatizo kubwa kwa kuwaambia watu kuwa lazima watende kazi ambayo Mungu haihitahji? (Ndiyo. Imekatazwa kama ambavyo imezuiliwa kuwaambia watu kwamba hawahitaji kufanya mambo ambayo Mungu anayahitaji.)

1.  Mara kwa mara huwa tunajadili ukweli mkuu wa kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Hatutavipitia vifungu hivyo. Ukweli huu unaendanaje na maelekezo ya kuacha kuwaambia watu kutenda mambo yasiyohitajika? (Msingi wa mjadala wetu wa matendo ni ukweli kwamba hayatuokoi. Badala yake yanaakisi maisha ya yule ambaye ameokolewa.)

B.  Soma Mithali 23:23. Unadhani inamaanisha nini “kuuza” ukweli? (Kiuhalisia, inamaanisha usiuache ukweli kwa ajili ya fedha. Usifanye maafikiano (compromise) ili kuongeza utajiri wako.)

1.  Unaweza kuunganisha Kumbukumbu la Torati 4:2 na Mithali 23:23 ili kufikia hitimisho la jumla? (“Inunue” kweli. Jifunze ili kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Kisha usiongezee kile unachodhani kuwa ni wazo zuri. Kama una mawazo mazuri, yachukulie hivyo na si kama matakwa ya Mungu.)

C.  Soma Matendo 20:27-28. Tunapaswa kuwa na kiwango gani cha kujali kuhusu hali ya maisha yetu na wale wanaotuzunguka kanisani? (Kama Yesu alikufa kwa ajili yetu, basi tunatakiwa kulichukulia suala hili kwa dhati.)

1.  Maelekezo haya yanahusika kwa nani? (Sio kwa wakosoaji kanisani. Bali, yanahusika kwa wale waliochaguliwa na Roho Mtakatifu ili kuwa “waangalizi.”)

D.  Soma Matendo 20:29-30. Hapa tunaona kazi gani ya muhimu? (Kuwakanusha wale wasiofundisha ukweli.)

III.  Ukweli

A.  Soma Mithali 16:25. Je, watenda maovu wote ni watu wabaya? (Hii inatuambia kuwa watu wenye dhamira njema wanaweza kufanya makosa ya kutisha.)

B.  Soma Isaya 53:6. Je, tumejumuishwa kwa hao watenda maovu? (Ndiyo. Tumezigeukia “njia zetu wenyewe.” Habari njema ni kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi “zetu wenyewe.”)

C.  Soma Kutoka 20:3-5. Katika sheria huwa tunarejelea “vipengele vinavyoonesha kuwapo kwa ushahidi kwenye kesi (elements of a prima facie case).” Vipengele hivi ndivyo ambavyo lazima uvithibitishe ili kushinda kesi yako. Vipengele vya uabudu sanamu ni vipi? (1. Umetengeneza kitu. 2. Kwamba “unakisujudia” au “kukiabudu.”)

1.  Unadhani kitu ulichokitengeneza kinatakiwa “kufanana” na kitu chochote? (Amri inabainisha kuwa ni mfano wa kitu.)

2.  Je, kitu hicho kinaweza kuwa kitabu, makala, au kitu chochote kinachoakisiwa kwenye ukurasa uliochapishwa? (Hicho kinajumuishwa kwenye “mfano wa kitu.”)

3.  Kwa kuzingatia mjadala huu, je, tamaduni za kisasa zinaweza kujumuishwa kwenye uabudu sanamu kwa kutangaza dhana ambazo hazijajengwa kwenye Biblia?

D.  Soma Yohana 17:14-17. Mitazamo gani miwili inakinzana ambayo tunatakiwa kuibainisha? (“Ulimwengu,” ambao unatuchukia, na “ukweli” unaopatikana “ulimwenguni.” Ukweli huu unatutakasa!)

1.  Je, unaweza kuibainisha mitazamo hii miwili inayokinzana maishani mwako leo? Je, unaweza kuitaja? (Biblia ndio neno. Ulimwengu ni mtazamo wa kipagani wa maisha.)

E.  Soma Waefeso 6:10-13. Adui wetu wa kweli ni nani? (Shetani na washirika wake.)

F.  Soma Luka 9:49-50. Akina nani si maadui wetu? (Wakristo wenzetu ambao wanaweza wasione mambo kama tuyaonavyo, lakini hawako kinyume nasi.)

1.  Yesu anawatazamaje wale wanaojaribu kuitangaza injili kwa namna ambayo “haiko kinyume na upande wetu?” (Yesu anasema kuwa wako “upande wetu.” Angalia jinsi Yesu anavyobadili kijivu kuwa nyeusi na nyeupe.)

G.  Nilipokuwa nikiandika somo hili kiongozi mmoja muhimu nchini Marekani alinipigia simu kutaka kujua kwa nini jarida la uhuru wa dini la kanisa langu lilikuwa likishambulia “Wazalendo wa Kikristo” (Christian Nationalists) au “Wazalendo Weupe wa Kikristo.” Yeye si mshiriki wa kanisa. Nilimwambia kuwa mabadiliko yaliyotokea ni madogo isipokuwa msamiati. Miongo kadhaa iliyopita jarida hilo hilo lilikuwa linashambulia “Haki ya Dini.” Miaka michache iliyopita msamiati huo ulibadilishwa ili kuwalenga “Wazalendo wa Kikristo.” Sasa mbari (race) imekuwa sehemu ya shambulio. Unadhani dhana hizi zimetokea wapi? (Haya ni mashambulizi kwa Wakristo wenzetu na chanzo chake ni dunia ya kipagani na kiongozi wake.)

1.  Unaweza kufikiria sababu moja kwa nini Mkristo awe na ushirika na wapagani ili kuwashambulia Wakristo wenzake?

2.  Kama ukweli wa Biblia unakinzana na “ukweli” wa ulimwengu, hiyo inaashiria nini juu ya shambulio hili?

3.  Je, unakifahamu kifungu chochote cha Biblia kinachotuambia tuwashambulie Wakristo wenzetu kwa sababu wao ni Wakristo? (Biblia inalaani mambo mengi, lakini kuwa mfuasi wa Yesu sio miongoni mwa mambo hayo. Kama Mkristo haufuati ukweli wa Biblia, basi matendo mabaya, mawazo mabaya, na sio uamuzi wa kumfuata Kristo, ndivyo vinavyopaswa kuwa kitovu cha ukosoaji.)

IV.  Akili

A.  Soma Warumi 1:21-23. Tatizo la mawazo ya watu hawa wanaoamini kuwa Mungu yupo lakini hawamtii ni lipi? (Mawazo yao yanakuwa “hayana maana.”)

B.  Soma 2 Wakorintho 4:4-6. Tatizo la watu wasiomwamini Mungu ni lipi? (Shetani amepofusha mawazo yao.)

1.  Tunapaswa kuhitimisha nini kuhusu aina hizi mbili za watu – wale wanaoamini, lakini hawatii, na wale wasioamini? (Kumheshimu Mungu kwa kuigeukia Biblia ili kupata nuru ndio kiini cha fikra sahihi. Tusipoitumia Biblia kama msingi wa kufanya uamuzi wa aina zote wa kipi ni sahihi na kipi si sahihi, tutadanganyika.)

C.  Rafiki, tumeishia mahali pale pale tulipoanzia – Yesu anatupatia njia moja na pekee ya uzima wa milele. Sauti nyingine zote hapa duniani ni kelele tu. Je, utachukua uamuzi leo kuifanya Biblia, na Biblia pekee, kuwa kipimo chako cha hukumu?

V.  Juma lijalo: Kuusimamia Ukweli.