Somo la 1: Vita Inayosababisha Vita Vyote

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 12, Ezekieli 28, Mwanzo 1-3
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
1

Somo la 1: Vita Inayosababisha Vita Vyote

(Ufunuo 12, Ezekieli 28, Mwanzo 1-3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Watu wangapi wana tatizo la kumwamini Mungu mwema na mwenye uwezo mkubwa kwa sababu uovu wa kutisha upo? Watu wangapi wanamkataa Mungu kwa sababu ya jambo baya sana lililomtokea rafiki au mwanafamilia wake? Nilipotembelea kanisa moja kule California na kufundisha kipindi cha Shule ya Sabato, mshiriki wa kanisa hilo aliniomba kwenda kwenye chakula cha mchana pamoja naye ili nikazungumze habari za Mungu na marafiki wake waliokuwa na maswali. Kisa chao ni kwamba wazazi na watoto wao wote walifariki kwenye ajali ya gari. Nilitakiwa kusema nini kuhusiana na hilo? Hebu tuzame kwenye somo letu ili tuone kile Biblia inachotufundisha kuhusu chanzo cha uovu!

I.  Vita

A.  Soma Ufunuo 12:7-9. “Joka” ni nani? (Vifungu hivi vinambainisha kama Shetani.)

1.  Shetani alishindwa kabisa kwa kiasi gani? (Sio tu kwamba alishindwa pambano, bali yeye pamoja na malaika walio washirika wake walitupwa kutoka mbinguni.)

2.  Kwa nini hapakuwepo tena “mahali” pa Shetani na malaika wake mbinguni?

B.  Soma Ufunuo 12:3-4. Je, huyu ni joka yule yule ambaye anarejelewa katika Ufunuo 12:7? (Lazima atakuwa yeye kwa sababu ni joka “mkubwa.” Rangi nyekundu tu ndio inayoongezewa kwenye ufafanuzi.)

1.  Unadhani kwa nini Shetani anarejelewa kama “mwekundu?” (Soma Yohana 8:44. Shetani anarejelewa kama “mwuaji.” Rangi nyekundu ni rangi ya damu.)

2.  Asilimia ngapi ya malaika mbinguni ilishawishiwa na Shetani kuungana naye dhidi ya Mungu? (Theluthi.)

C.  Soma Zaburi 8:3-6. Je, hii inamaanisha kuwa sisi ni wa hadhi ya chini kuliko malaika? (Ndiyo.)

1.  Litafakari hili kidogo. Malaika wakamilifu, ambao katika uumbaji wana hadhi ya juu kuliko sisi, walishawishiwa kundi kubwa kumfuata Shetani. Una matumaini gani ya kusimama peke yako dhidi ya Shetani?

2.  Watu wengi wanaamini kwamba inakubalika kujihusisha kwenye mambo ya siri (occult) au kutazama sinema zinazohusu pepo wabaya (demons). Ushahidi huu wa mbinu za udanganyifu wa Shetani unatufundisha nini kuhusu kujiingiza kwenye mambo ya siri (occult)? (Tunapaswa kuyakimbia!)

II.  Kitu gani Kilisababisha Vita?

A.  Soma Ezekieli 28:13-16. Vifungu hivi vinaonekana kuwa na rejea ya aina mbili. Rejea ya kwanza ni ya mfalme wa duniani, na nyingine kwa mtu kama malaika aliyetiwa mafuta kama “kerubi mlinzi” aliyekuwa “juu ya mlima mtakatifu wa Mungu.” Mfalme gani wa duniani alikuwa pia malaika aliyeishi juu ya mlima mtakatifu mbinguni? (Hii isingeweza kumrejelea mwanadamu. Kwa upande mwingine, hii inaendana na maelezo ya Shetani aliyetupwa duniani.)

B.  Soma Ezekieli 28:17. Dhambi iliingiaje kwa kiumbe mkamilifu katika mazingira makamilifu? (Kiburi. Kiburi cha uzuri na ufahari wake. Shetani “aliiharibu hekima yake kwa sababu ya mwangaza wake.”)

1.  Kama wewe ni mzuri (handsome or beautiful), je, unalielewa hili? Je, unaelewa jaribu la kuwa na majivuno?

2.  Kama wewe sio mzuri (handsome or beautiful), je, unaona tabia hizi kwa watu wenye maumbo na sura nzuri? Je, wanatumia mionekano yao kuzidisha fahari zao?

a.  Je, kuna ubaya wowote kuzidisha fahari yako? Ili kuwa na mwonekano mzuri zaidi? (Ezekieli 28:16 inarejelea matumizi ya “vurugu” na Ezekieli 28:17 inarejelea “kuharibu” hekima ili kuongeza fahari. Tatizo sio fahari, tatizo ni njia alizozitumia Shetani ili kuongeza fahari yake.)

3.  Je, hii inaonesha jinsi “ukamilifu” unavyoweza kusababisha “kutokuwa na ukamilifu?”

C.  Soma Isaya 14:12-14. Ni nini lililokuwa lengo la fahari ya Shetani? (Kufanana na Mungu. Alitaka kuwa Mungu.)

D.  Soma Mwanzo 3:2-6. Zingatia kifungu cha tano kwa umakini. Ni nini msingi wa jaribu hili la kutokuwa watiifu kwa Mungu? (“Mtakuwa kama Mungu.”)

E.  Soma Mwanzo 1:31. Angalia mlinganisho. Mbingu ni kamilifu. Adamu na Eva wanaumbwa wakiwa wakamilifu katika dunia iliyo kamilifu. Kitu gani kilisababisha kuingia kwa dhambi katika maeneo yote mawili yaliyo makamilifu? (Tamaa ya kutaka kufanana na Mungu. Shetani alitumia uzuri na uwezo wake kuwashawishi wengine kuasi dhidi ya Mungu ili aweze kufanana na Mungu.)

1.  Unadhani Shetani na washirika wake wanatumia jaribu hilo hilo dhidi yako?

2.  Fikiria juu ya kigezo cha uabudu sanamu. Kitu kilichotengenezwa kwa mikono yako kinachukua tabia zinazofanana na tabia za Mungu. Je, uabudu sanamu (kuabudu kile ulichokitengeneza) ni tafsiri ya jaribu la asili?

III.  Miti Miwili

A.  Soma Mwanzo 2:15-17 na Mwanzo 3:3-4. Mti wa ujuzi wa mema na mabaya umewekwa wapi? (Upo “katikati” ya bustani ya Edeni. Nimeangalia jinsi maoni ya Strong yanavyosema kuhusu neno hili linavyopaswa kutafsiriwa na anatumia maneno yanayorejelea jiometri (geometry) – kitu kilicho katikati. Kitu kinachogawa kati msitari.)

B.  Soma Mwanzo 3:22-24. Tunaona mti gani mwingine maalumu katika bustani ya Edeni? (Mti wa uzima.)

C.  Tunayo miti miwili. Mmoja unaleta uzima na mwingine unaleta mauti. Kwa nini Mungu ana mti wa mauti katikati ya uumbaji wake mkamilifu?

1.  Kwa sababu ya umuhimu wa mti wa uzima, ninadhani kuna uwezekano kwamba miti miwili maalumu ilikaribiana katika eneo la katikati ya bustani. Kwa nini Mungu afanye hivyo? Kwa nini aruhusu hilo? (Masimulizi katika kitabu cha Mwanzo 1-3 ni kwamba Mungu aliumba dunia kamilifu ikiwa na watu wakamilifu. Sehemu ya ukamilifu huo ilikuwa ni kuwapa uhuru wa kuchagua. Kama wangekuwa roboti za kisasa, wasingekuwa wakamilifu na wasingeumbwa kwa mfano wa Mungu kama watawala. Angalia Mwanzo 1:27-28.)

2.  Kwa nini kwa umahsusi Mungu aliweka mazingira ya uwezekano wa uasi na dhambi?

a.  Je, hiki kinaonekana kama kipimo kilichokubalika kati ya Mungu na Shetani? (Hicho ndicho hasa ninachodhani kinaendelea.)

b.  Kwa nini Mungu akubaliane nacho? (Asingetaka Shetani aendelee kuwajaribu na kuwabughudhi Adamu na Eva mara kwa mara kwa namna ile ile aliyomshambulia Yesu.)

IV.  Hoja ya Upendo

A.  Fikiria kwamba wewe ni mwangalizi wa nje wa kile tulichojifunza hivi punde. Fikiria kwamba mara baada ya anguko la wanadamu unaulizwa kuhusu ugomvi kati ya Mungu na Shetani. Utatoa alama ngapi juu ya uwezo wa Mungu kushinda pambano kati ya wema na uovu? (Mungu alishinda hoja iliyokuwa ikiendelea mawazoni mwa malaika wengi. Alishindwa mdahalo kwa wanadamu – ingawa kinadharia Mungu alikuwa na uhusiano usio na kikomo na Adamu na Eva, na Shetani alikuwa na uhusiano ulioruhusiwa na kanuni za kiuhusiano pekee.)

B.  Soma 1 Petro 3:18-22 na Waebrania 2:9-10. Yesu aliturejeshaje? (Alikufa kwa ajili yetu! Njia ya ushindi haikuwa suala la mdahalo, sio nguvu ya hali ya juu, bali upendo wa kujitoa.)

C.  Unakumbuka sehemu ya utangulizi ambapo niliuliza kwa nini uovu upo wakati tunaye Mungu mwenye uwezo mkubwa? Unakumbuka changamoto yangu ya kuelezea jinsi Mungu mwenye upendo aruhusu wazazi na watoto wa wanandoa kufariki kwenye ajali ya gari? Jibu ni lipi? (Jibu ni kwamba Mungu alitupatia uhuru wa uchaguzi. Tulimchagua Shetani.)

1.  Kwa kadiri muda unavyoendelea kupita, je, uchaguzi kati ya Mungu na Shetani ni mwepesi kuufanya? (Msitari wa uovu sasa uko bayana. Tunaona matokeo ya dhambi. Mambo ya kutisha yanayotokea duniani yote ni matokeo ya kumchagua Shetani.)

2.  Ikiwa uchaguzi sasa uko dhahiri, kwa nini watu wengi sana wanaonekana kufanya uchaguzi mbaya? (Rejea kwenye jaribu lililomsababisha Shetani na Eva kushindwa. Kiburi. Kiburi cha mwonekano na uwezo.)

D.  Soma Waebrania 4:14-16 na Waebrania 7:24-28. Kutokana na kafara ya Yesu kwa ajili yetu, anafanya nini sasa hivi? (Anatenda kazi kama mwombezi wetu katika patakatifu pa mbinguni!)

E.  Rafiki, Yesu alimshinda Shetani kwa njia ya upendo! Alijitoa kwa ajili yetu. Aliteseka kiasi cha kutisha mikononi mwa Shetani. Hoja ya kuvutia kiasi gani ya kumchagua Mungu. Ukweli kwamba kafara ya Yesu inatufanya tuwe na uzima wa milele ni nzuri ajabu kiasi gani! Je, utauchagua wema dhidi ya uovu, Yesu dhidi ya Shetani? Kwa nini usifanye uchaguzi huo sasa hivi?

V.  Juma lijalo: Suala Kuu: Upendo au Ubinafsi?