Somo la 11: Kumwonea Mungu Shauku Katika Sayuni

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 84, 122, 125, Ufunuo 21
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
1
Lesson Number: 
11

Somo la 11: Kumwonea Mungu Shauku Katika Sayuni

(Zaburi 84, 122, 125, Ufunuo 21)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: “Mwakani katika Yerusalemu” ndio maneno ya mwisho yaliyotolewa katika desturi ya chakula cha jioni baada ya Pasaka. Nilipotambua suala hili mara ya kwanza nilidhani ya kwamba, “Ombi zuri ajabu kwa Wakristo. Fikiria kwamba tumeomba kwa dhati kuwa mwaka ujao tuwe tunaishi katika Yerusalemu Mpya!” Somo letu la Zaburi juma hili linahusu maendeleo makubwa ya dhana hii. Zaburi hizi zinazungumzia hekalu la Kiyahudi, Mungu wetu mtukufu, kurejea kwa Sayuni, na jinsi suala hili linavyohusika kwetu leo na siku zijazo. Hebu tuzame kwenye somo hili la matumaini kwa ajili ya siku zijazo!

I.  Lengo letu

A.  Soma Zaburi 84:1-2. Utaona kwamba Zaburi hii inahusianishwa na “Wana wa Kora.” Je, unafahamu walikuwa akina nani? (Walikuwa walinzi malangoni na wanamuziki katika hekalu la Yerusalemu.)

1.  Unaweza kufikiria kwamba wale wanaofanya kazi hekaluni wanapenda kuelezea jinsi kazi hiyo ilivyo ya kupendeza? (Lazima ilikuwa kazi nzuri. Ukifanya kazi sehemu kubwa unaweza kuizoea na kuiona ya kawaida.)

B.  Soma Zaburi 84:3-4. Je, kila mtu anaweza kupata nafasi katika hekalu la Mungu? (Tunaambiwa kuwa ndege wanapata makazi pale – hata mashomoro wa hali ya chini. Kuna nafasi kwa ajili yetu.)

C.  Soma Zaburi 84:5-7. Mtazamo wa mwandishi umebadilikaje? Je, bado huu ni mtazamo wa mtu anayefanya kazi hekaluni? (Hapana. Vifungu hivi vinazungumzia safari ya kwenda hekaluni. Watu hawa wanaishi mahali kwingine.)

1.  Wana maoni wengi wanaamini kuwa “Bonde la Vilio” inarejelea bonde la kilio. Vilio kiasi gani vinaendelea? (Kifungu kinasema kuwa kilio “kinaifanya” kuwa mahali pa chemchemi. Hayo yatakuwa machozi mengi!

2.  Utaona kwamba kifungu cha saba kinasema kuwa “huendelea toka nguvu hata nguvu.” Hilo linawezekanaje? Kama unalia, je, uko imara? (Kifungu cha tano kinasema kuwa wale waliopo kwenye hii safari ya kwenda Yerusalemu nguvu zao zimejengwa juu ya Mungu. Kama katika safari ya maisha unakabiliana na masikitiko ya kutisha, kuuweka moyo wako kwenye safari ya kuelekea kwenye hekalu la Mungu katika Yerusalemu kunakufanya uishi maisha imara.)

D.  Soma Zaburi 84:8-9. Tuna mabadiliko mengine kwenye mtazamo wa mwandishi. Kipengele gani kipya kinaingia kwenye safari hii? (Sasa tuna “ngao,” lakini inaonekana kuwa dhidi ya Mungu.)

1.  Kwa nini tunatakiwa tuwekewe ngao na Mungu? (Ingawa tuko kwenye safari ya kwenda kwa Mungu, sisi ni wadhambi wa kutisha. Yeye ni Mungu mkamilifu. Hata kulia kilio kikubwa kunaonesha udhaifu. “Masihi” wetu (ambaye ana sura) ni Yesu. Anasimama mahala petu mbele ya Mungu. Anatukinga kwa ngao.)

E.  Soma Zaburi 84:10. Je, unaelewa hisia zilizo nyuma ya hii kauli? Kwani hatuzungumzii kuhusu (na sasa hivi) anasa za dhambi? (Hii inaonesha kuwa tunamhitaji Roho Mtakatifu ili kubadili mtazamo wetu. Kauli ni ya kweli, tunatakiwa kuwa na mawazo yanayoturuhusu kusema kuwa siku moja katika Yerusalemu ni bora kuliko siku elfu katika dhambi.)

1.  Je, kuielewa kauli ya “siku moja ni bora kuliko siku elfu” ni jambo ambalo tunaweza kulifahamu kiuhalisia tutakapokuwa katika Yerusalemu Mpya?

F.  Soma Zaburi 84:11-12. Tunapoingia kwenye uhusiano sahihi na Mungu tunaweza kutarajia nini? (Je, unapenda kusimama kwenye joto la jua? Je, unafurahia upendeleo na heshima? Hiki ndicho anachotutendea Mungu “tunapoenenda kwa ukamilifu.”)

II.  Amani Malangoni

A.  Soma Zaburi 122:1-4. Daudi amesimama wapi anapoandika Zaburi hii? (Amesimama “ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu!”)

1.  Kifungu cha nne kinatuambia nini kuhusu safari ya Yerusalemu? (Soma Kumbukumbu la Torati 16:16. Hii ni rejea ya sikukuu tatu za mwaka ambapo watu wa Mungu watasafiri kwenda Yerusalemu ili kutoa shukrani.) 

B.  Soma Zaburi 122:5-8. Utaona kwamba mara tatu kwenye hivi vifungu vinne tunaona neno “amani.” Hii inahusianaje na “viti vya hukumu?” (Je, unafikiria juu ya ukweli kwamba mahakama zetu zinatakiwa kuepuka mapigano? Badala ya kushinda kwa nguvu, mahakama zinatatua migogoro kutokana na makubaliano yaliyojengwa juu ya kanuni za kisheria.)

1.  Je, amani hii inahusu utatuzi wa migogoro miongoni mwa watu wa Mungu pekee? (Niliwahi kusoma kitabu kinachohusu historia ya Yerusalemu na kilifafanua makundi yote tofauti-tofauti yaliyopata ushindi. Amani dhidi ya nguvu za nje ni ya muhimu hata leo.)

2.  Unakumbuka hapo awali nilikuuliza kuhusu anasa za dhambi dhidi ya furaha ya siku moja katika Yerusalemu? Je, umewahi kuingia kwenye matatizo na ukatamani sana kama ungekuwa na amani badala ya matatizo?

3.  Kisa kinajidhihirisha ambapo kiongozi wa dini anakabiliwa na makosa ya jinai na huenda akafungwa jela. Unadhani kiongozi huyu wa dini atabadilishana siku ngapi za kutenda mabaya kwa ajili ya siku moja ya amani? (Ninahisi ataacha (yanayodaiwa kuwa) makossa yake yote ili kupata amani sasa hivi.)

4.  Tumia hili maishani mwako. Utabadilisha (trade) “anasa” gani kwa ajili ya uzima wa milele?

5.  Tumejadili dhana ya utendaji makosa kuingilia amani. Je, umejisikia kutokuwepo kwa amani pale ambapo hakuna kosa lililotendeka? (Mara nyingi uhusiano wa kifamilia unaiingilia amani. Kuonesha upendo wa Mungu, kama itakavyokuwa kwa watu wote katika Yerusalemu Mpya, hutupatia amani katika uhusiano baina ya watu wawili.)

III.  Mlima Jijini

A.  Soma Zaburi 99:9, Mika 4:1-2, na Isaya 2:2. Je, vifungu hivi vinaleta mantiki yoyote? Unadhani Yerusalemu Mpya utakuwaje mlima mrefu kuliko yote? Je, Mungu atauhamisha kutoka Yerusalemu ya sasa? Je, ardhi ambayo Yerusalemu ya sasa imejengwa kwa ghafla itainuka kama mlima mkubwa?

1.  Je, uligundua kwamba vifungu hivi havirejelei Yerusalemu kukaa juu ya mlima mrefu?  vinazungumzia nyumba ya Mungu kuwa mlima. Hilo linawezekanaje?

B.  Soma Ufunuo 21:15-17. Sura ya Yerusalemu Mpya inafananaje? (Haifanani na mji wowote wa sasa, sura yake inafanana na mchemraba. Inafanana na miliki kubwa (condominium)!)

1.  Kifungu hiki kinasema kuwa mchemraba wa Yerusalemu Mpya ni viwanja 12,000 kila upande. Hii inamaanisha nini kwa vipimo vya sasa? (Ukibadilisha kwa vipimo vya sasa hiyo ni sawa na maili 1,400 au kilomita 2,253, au futi 7,392,000.)

2.  Kwa kutumia urefu huo, je, kilele cha Yerusalemu Mpya kitakuwa juu ya mlima wowote mrefu wa sasa? (Ndege za biashara huruka umbali wa futi 33,000 juu ya usawa wa bahari. Anga la nje lipo umbali wa futi 380,000. Sehemu kubwa ya mchemraba wa Yerusalemu Mpya ipo katika anga la nje! Vifungu tulivyovisoma hivi punde havitupatii makisio ya umbali ambao Yerusalemu Mpya itajengwa juu ya vinara vinavyopatikana mahali popote hapa duniani.)

C.  Soma Zaburi 125:1-2. Kwa ukubwa wa Yerusalemu Mpya, unadhani inahamishika kiurahisi? (Mara Mungu atakapoisimika katika dunia mpya, haihamishwi na mtu yeyote. Badala yake, ukubwa wake unasababisha matatizo yote ya kinadharia: jengo kama hilo litahitaji msingi wa namna gani? Je, jengo hilo litaingiliana na mzunguko wa dunia? Litagandamizwa vipi kwa kuwa sehemu kubwa ya mji huo ipo katika anga la nje?)

IV.  Amani ya Milele

A.  Soma Zaburi 125:3-4. Je, umewahi kufikiria kama tatizo la dhambi linaweza kujitokeza tena mbinguni (katika nchi mpya?

1.  Kama jibu lako ni, “Ndiyo,” unadhani jambo gani litaepusha dhidi ya hilo? Je, Mungu ataweka ukomo wa uhuru wetu wa kuchagua? Je, ladha chungu ya dhambi itasalia kuwa imara kwa umilele, ili kwamba kamwe tusijaribiwe kugeuka nyuma?

2.  Je, mtunga Zaburi ana wasiwasi juu ya hili?

B.  Angalia tena Zaburi 125:3. Hii inatuambia kuwa kuna shaka kuhusu wenye haki kunyosha “mikono yao kwenye upotovu.” Unadhani inamaanisha nini kusema “fimbo ya udhalimu?” Ina nafasi gani kwenye utendaji makosa katika siku zijazo? (Nadhani fimbo inamaanisha kanuni au nguvu ya uovu. Mbinguni hatutakuwa na mvuto wa uovu kama tulio nao sasa. Tutakuwa na mawazo makamilifu na hisia kamilifu. Hatutajishawishi na kushawishiwa na nguvu za nje.)

1.  Tafakari jinsi Lusifa alivyoanguka dhambini katika mbingu kamilifu. Jambo gani linazuia hilo lisitokee tena? (Angalia tena Zaburi 125:2. Hii inatuambia kuwa “tumezungukwa” na Mungu. Tunayo historia ya uovu ya kutuzuia – na kama tutasahau nina uhakika Roho Mtakatifu atatukumbusha. Zaidi ya majibu haya, lazima tuamini hekima kubwa na akili ya Mungu. Nina uhakika ametafakari kwa umakini kuhusiana na tatizo hili linaloweza kujitokeza.)

C.  Rafiki, je, ungependa kuwa katika Yerusalemu Mpya mwakani? Kwa nini usiyaweke mawazo yako katika hilo? Kama hujampokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wako, kwa nini usifanye hivyo sasa hivi? Itakuweka katika njia ya amani sasa hivi na milele.

V.  Juma lijalo: Ibada Isiyokoma.