Somo la 4: Kushiriki na Wengine Utume wa Mungu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 18-19
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
4
Lesson Number: 
4

Somo la 4: Kushiriki na Wengine Utume wa Mungu

(Mwanzo 18-19)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Masomo yaliyopita katika mfululizo wa masomo haya yalijadili suala la Roho Mtakatifu kutenda kazi pamoja nasi ili kutimiza utume wa Mungu hapa duniani. Je, umetafakari suala la Mungu kufanya kazi pamoja nawe katika umbo la mwanadamu? Je, umewafikiria malaika wanaofanana na watu wakiwa wamesimama pembeni yako? Hilo lilimtokea Ibrahimu! Juma hili tunajifunza mwendelezo wa kisa juu ya Mungu na malaika kuja duniani katika umbo la mwanadamu na kumpa Ibrahimu thawabu kwa kumbariki na kuilinda familia yake. Pia tunaangalia hadithi za sasa. Hebu tuzame kwenye kisa chake cha kupendeza kuhusu kazi yake ya utume pamoja na Mungu katika umbo la mwanadamu!

I. Ugeni

A. Soma Mwanzo 18:1. Kama ingekuwa ni uchaguzi wako, ungekuwa umekaa wapi wakati wa mchana wa jua kali? (Habari njema ya kwanza ni kwamba Ibrahimu amepumzika badala ya kufanya kazi katika mchana wa joto kali. Habari njema ya pili ni kwamba yupo mlangoni pa hema yake ambapo palikuwa na kivuli na huenda upepo mwanana. Habari njema kupita zote ni kwamba Mungu anakuja kumtembelea.)

B.Soma Mwanzo 18:2-3. Tunaambiwa kuwa Mungu alisimama mbele ya Ibrahimu katika umbo la mwanadamu. Unadhani Ibrahimu alitambua kuwa huyu ni Mungu?

1. Ukikichukulia kifungu hiki kiuhalisia, Ibrahimu anaangalia juu na kuwaona watu watatu wakiwa wamesimama mbele yake. Chukulia kwamba Ibrahimu hakuwa amelala, inawezekanaje watu watatu wajitokeze ghafla bila Ibrahimu kuwaona wakitembea kuelekea upande wake? (Nadhani hii ndio sababu ya Ibrahimu kumtaja mgeni kama “Bwana wangu.” Kifungu kinasema kuwa Ibrahimu “alipiga mbio kuwalaki,” hivyo hawakuwa wamesimama moja kwa moja mbele ya Ibrahimu.)

C. Katika Mwanzo 18:4-8 Ibrahimu anaagiza kuwa miguu ya watu hawa ioshwe, mikate iandaliwe kwa ajili yao, ndama achinjwe kwa ajili yao, na wapewe maziwa na siagi. Unadhani hivi ndivyo Adamu alivyowapokea watu wote waliopita karibu na hema yake? (Baadhi ya wanamaoni wanarejelea kitendo hiki kama ukarimu wa kawaida wa watu kama Ibrahimu. Nina mashaka kama Ibrahimu atamtaja mgeni yeyote kama “Bwana,” ambayo ndio salamu yake ya awali katika Mwanzo 18:3. Kamusi ya Strong inasema kuwa hili neno lilikuwa jina sahihi lililotumika kwa ajili ya Mungu pekee.)

D. Soma Mwanzo 18:13-14 na Mwanzo 19:1. Hii inaongezea nuru gani ya ziada kwa “watu” watatu? (Mmoja ni Mungu na wengine wawili ni malaika. Sidhani kama kisa hiki kinahusu ukarimu wa kawaida, nadhani hiki ni kisa cha mtu aliye makini na uwepo wa Mungu maishani mwake.)

E. Soma Mwanzo 18:9-10. Unadhani kwa nini Mungu aliamua kufikisha ujumbe huu yeye mwenyewe? Kwa nini hakutumia maono au njozi? Kwa nini sio ujumbe wa malaika? (Hii inatufikisha kwenye kiini cha ugeni. Mungu amemuahidi Ibrahimu kuwa atakuwa taifa kubwa. Utimilifu wa ahadi hiyo umecheleweshwa. Mungu anataka kufikisha habari hizi njema yeye mwenyewe.)

1. Hii inatufundisha nini kumhusu Mungu? (Kadiri kisa hiki kinavyoendelea kujidhihirisha tutaona jinsi upendo wa Mungu kwa Ibrahimu ulivyo mkuu.)

2. Kuna mafunzo gani kuhusu jinsi tunavyopaswa kumtendea Mungu kwa namna ambavyo Ibrahimu alimpokea? (Tunapaswa kufanya yote tuyawezayo ili kumfanya Mungu akaribie nyumbani kwetu.)

F. Soma Mwanzo 18:11-14. Tunajifunza nini katika mwitikio wa Sarah? (Hakuna kilicho kigumu kwa Mungu. Hakuna kinachoweza kusimama kati yetu na upendo wake.)

II. Safari Kuelekea Sodoma

A. Soma Mwanzo 18:16-19. Tafakari fikra ya Mungu kwa nini ashiriki aina ya safari yake kuelekea Sodoma. Kwa nini ashiriki habari hizi na Ibrahimu? (Mungu anatoa sababu mbili. Kwanza, kwamba Ibrahimu ni mtu wa muhimu sana kwa ajili ya mustakabali wa kazi ya Mungu duniani. Pili, kwamba Ibrahimu atakuwa kiongozi katika kutenda kilicho sahihi kwa “kuwaamuru wanawe na nyumba yake.”)

1. Kadiri kisa hiki kinavyoendelea kujidhihirisha, tunaona kwamba kinashughulika na pambano la sasa. Je, kisa hiki kinapaswa kuongoza jinsi tunavyowaamuru watoto wetu? Au, hilo lilikuwa jambo kwa ajili ya Ibrahimu pekee?

B. Soma Mwanzo 18:20-21. Kuna nini kingine cha kujifunza hapa kwa Ibrahimu na kwetu? (Inaonesha hali ya Mungu ya kutenda haki. Hatatoa hukumu bila yeye mwenyewe kuthibitisha ukweli wa mambo.)

C. Soma Mwanzo 18:22-23. Tunaambiwa kuwa Ibrahimu “akamkaribia” Mungu ili kuwa na mazungumzo haya. Tunaweza kuhitimisha nini kutokana na hili? (Hii inatoa taswira ya mjadala binafsi sana. Yanaonekana kama mazungumzo muhimu na ya siri.)

D. Soma Mwanzo 18:24-26. Hivi punde nimetoka kusoma madai ya kwamba Ibrahimu alitoa pendekezo hili kwa Mungu kwa sababu ya upendo wake kwa watu wote wa Sodoma. Je, hicho ndicho Biblia inachokisema? (Haisemi chochote kinachofanana na hicho. Ibrahimu anajenga hoja kwamba kuwaadhibu wadhambi katika mji hakupaswi kusababisha kifo kwa wenye haki.)

E. Soma Mwanzo 18:32-33. Ibrahimu “anamshusha” Mungu kiasi cha kufikia kuwalinda watu kumi wenye haki. Tunapata fundisho gani la muhimu katika hili? (Kama u mwenye haki, unaweza kuulinda mji wako na familia yako. Inaonesha umuhimu wa neema ya Mungu na utii wetu.)

F. Ninataka kumalizia kisa kuhusu hukumu ya Mungu kwa Sodoma, hivyo hebu turuke vifungu kadhaa na tusome Mwanzo 19:12-13 na Mwanzo 19:15-16. Mungu alikuwa tayari kiasi gani kuwalinda wenye haki kwa uchache kabisa? (Ibrahimu alimshusha Mungu hadi kufikia watu kumi wenye haki, lakini hapa tunamwona Mungu akiingilia kati kuwaokoa watu wanne wenye haki wanaoitasita. Mungu hakuwa tayari kwa mtu yeyote mwenye haki kuathirika kwenye hukumu hii. Hata “wenye haki” wanaopaswa kuburuzwa nje ya mji wanaokolewa.)

G. Tutasoma sehemu tu, na sio kisa chote cha Lutu na familia yake.  Mkewe anakufa mara moja baada ya tukio lile (Mwanzo 19:26) kwa sababu ya kutokutii, na Lutu na mabinti wake wanajiingiza kwenye dhambi ya kutisha (Mwanzo 19:30-38). Je, hawa ni watu “wenye haki?” (Soma Mwanzo 19:29. Kisa hiki hakihusu upendo wa Mungu kwa waovu, kisa hiki kinahusu upendo wa Mungu kwa Ibrahimu. Ni kisa kinachohusu, kama wewe ni mwenye haki, jinsi unavyoweza kuikinga familia yako dhidi ya madhara.)

III. Kisa cha Dhambi ya Sodoma

A. Soma Mwanzo 19:1-2. Je, Lutu anafuata nyayo za Ibrahimu anapowapatia malaika wawili (wanaotokea kama watu), mahali pa kulala usiku? (Ndiyo. Lutu pia anawaita “bwana,” lakini maoni ya Strong ni kwamba hii inaweza kumrejelea kiongozi wa kibinadamu. Katika sehemu inayofuata tutaona kuwa Lutu ana sababu ya msingi zaidi ya kuwahurumia wageni hawa.)

B. Soma Mwanzo 19:3-5. Sodoma ni ovu kiasi gani? (Kifungu hiki kinasema kuwa watu wote wa Sodoma walisisitiza juu ya kuwabaka/kuwalawiti watu hawa.)

C. Soma Mwanzo 19:6-8. Je, Lutu ni baba mbaya? Anawalinda wageni badala ya binti zake kwa kuzingatia wajibu wake wa ukarimu?

D. Soma Mwanzo 19:9-11. Watu wa Sodoma wanawakataa mabinti wa Lutu na sasa wanataka kumtendea Lutu vibaya kuliko wageni. Je, Lutu alitarajia kwa usahihi kwamba watu hawa watawakataa mabinti wake bikira? Je, Lutu alikuwa anajaribu kuwachezea akili, huku akijua kwamba mabinti wake hawatakuwa hatarini kwa wasenge/mabasha hawa? (Ushahidi uliopo kwenye kisa ni kwamba watu hawa walisisitiza juu ya kufanya ngono na Lutu badala ya kukubali kufanya ngono na mabinti wa Lutu. Hiyo inatuambia kuwa hawakuwa na haja na wanawake.)

E. Watetezi wa ushoga katika zama za leo wanajenga hoja kwamba kiburi na kutokuwa na ukarimu ndivyo vilivyokuwa sababu ya kuangamizwa kwa Sodoma. Hebu tusome Ezekieli 16:49-50 na Yuda 1:7. Ezekieli anasema kuwa kiburi na kutowajali maskini na wahitaji ndilo lililokuwa tatizo la Sodoma. Yuda anasema uasherati na “tamaa ya mambo ya mwili yasiyo ya asili” ndio iliyokuwaa sababu ya adhabu. Je, katika zama za leo, kiburi na ushoga (homosexuality) vinahusiana? (Je, umewahi kusikia magwaride ya “Kiburi?”)

F. Baadhi ya wasomaji wanaweza kudhani, “Bruce ana tatizo gani, kwa nini anajikita kwenye dhambi hii wakati sisi sote ni wadhambi? Kwa nini anazungumzia suala hili wakati mwanangu (au mwanafamilia mwingine) ni shoga na anahangaika na kupambana ili kusalia kanisani?” (Jibu ni kwamba ingawa sote tunahangaika na dhambi, na dhambi zote husababisha mauti, dhambi hii mahsusi inapigiwa chapuo na washawishi ambao lengo lao ni kuvunjavunja taasisi ambazo hazitaidhinisha dhambi hii. Ndio maana ncha ya mkuki kwa uhuru wa kuabudu siku hizi ni utetezi dhidi ya watetezi wa ushoga na usenge. Hakuna hata shule moja ya sheria ya Kikristo nchini Canada kwa sababu ya nguvu ya ushawishi huu. Nani anayetetea uhuru wa watu?)

G. Watu wa nchi za magharibi wanaposimama katikati ya pambano hili la kiroho, kuna nini cha kujifunza kutoka kwenye sura hizi za kitabu cha Mwanzo? (Waaminifu wa Mungu wanaikinga jamii ovu dhidi ya hukumu za Mungu. Mungu anawapenda watu wake. Hatatufagia pamoja na waovu. Bado kuna muda na tumaini la kuwaongoa wasio na haki.)

H. Rafiki, je, utaendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu? Je, utailinda familia yako kwa kumtii Mungu? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, kukupatia roho ya uaminifu?

IV. Juma lijalo: Visingizio vya Kuukwepa Utume.