Somo la 2: Utume wa Mungu Kwetu: Sehemu ya 2

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yohana 20, Mathayo 28, Ufunuo 14
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
4
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Utume wa Mungu Kwetu: Sehemu ya 2

(Yohana 20, Mathayo 28, Ufunuo 14)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Mungu anatutarajia tufanye nini? Je, ni kuamini tu kwamba Yesu ni Mungu na kwamba alikuja ili kutuokoa? Au, ni suala gumu kuliko hivyo tunavyofikiria? Je, hiyo inahusisha sisi kuungana na Mungu katika kazi yake ya kuwaokoa wanadamu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze kuhusu utume wetu!

I.  Utume kwa Ajili ya Wanafunzi

A.  Soma Yohana 20:19-20. Wanafunzi wako katika hali gani kiakili? (Hali yao inatisha! Yesu amesulubiwa. Wana wasiwasi juu ya maisha yao. Lakini Mariamu (Yohana 20:18) anasema kuwa amemwona Yesu akiwa hai.)

1.  Hali yao ya kiakili inabadilikaje Yesu anapowatokea wanafunzi? (Kifungu kinasema kuwa “walifurahi.”)

a.  Je, hiyo inaonekana kama urahisishaji (understatement) wa dhahiri? (Soma Luka 24:41. Kifungu hiki kinasema kuwa wanafunzi walikuwa “hawajaamini kwa furaha.” Nadhani hii inafafanua kwa nini neno kama “furaha” linastahili hapa. Walikuwa na hofu juu ya usalama wao, na sasa Yesu anakuja kuonesha kuwa yu hai. Lilikuwa jambo la kushangaza na kufurahisha na wakati huo huo gumu kuliamini. “Jambo zuri mno kiasi cha kushindwa kuaminika kirahisi.”)

2.  Utaona katika Yohana 20:20 kwamba Yesu anawaonesha “mikono na ubavu” wake. Kwa nini alifanya hivyo? (Hii inasisitiza kwamba walihitaji uthibitisho kwamba kweli alikuwa hai.)

B.  Soma Yohana 20:21-22. Yesu alifanya nini kwanza? (Kwanza Yesu alishughulika na hali yao ya akili. Soma Warumi 5:1. Hitaji letu la msingi kabisa ni kuwa na amani na Mungu.)

1.  Yesu alifanya jambo gani la pili? (Aliwapatia kazi ya kufanya.)

2.  Yesu alifanya jambo gani la tatu? (Kumpokea Roho Mtakatifu ilikuwa muhimu katika kutimiza utume wao.)

a.  Je, kuna lolote la kujifunza katika hili kwa ajili yetu? Au maelekezo haya ni kwa ajili ya wanafunzi hawa pekee?

C.  Soma Yohana 20:23. Je, tuna uwezo wa kusamehe dhambi na kukataa kusamehe dhambi?

D.  Soma Marko 2:5-7 na Marko 2:10-11. Bila shaka yoyote Yesu ana uwezo wa kusamehe dhambi. Je, katika Yohana 20:23 aliwapa wanafunzi na sisi uwezo huo? (Je, Mungu atanipatia uwezo mkuu (extraordinary) wa kukataa kumsamehe mtu dhambi zake?)

1.  Soma Mathayo 6:14-15. Tukiyachukulia yote haya jinsi yalivyo (at face value), basi ninaweza kumzuia mtu mwingine asisamehewe kwa matokeo ya kwamba nami sitasamehewa. Je, hiyo inaleta mantiki yoyote kwako? (Haileti mantiki yoyote kwangu. Kwa nini? Kwa sababau tunao wanadamu wanaofanya uamuzi mkubwa ambao Mungu pekee ndiye anayepaswa kuuchukua uamuzi huo. Wanamaoni niliowapitia hawaamini kama Yesu anawapatia wanafunzi (au sisi) mamlaka ya kusamehe au kuzuia msamaha wa dhambi.)

E.  Angalia tena Yohana 20:23. Kama Yesu hazungumzii uwezo wa wanadamu kusamehe dhambi, atakuwa anazungumzia jambo gani? (Hebu tuangalie muktadha. Ni punde tu Yesu ameishinda dhambi. Anawapatia wanafunzi wake uwezo wa Roho Mtakatifu na anawatuma kwa niaba yake. Nadhani inaleta mantiki kuelewa kwamba hii inamaanisha kuwa kwa kupeleka injili kwa wengine tunawawezesha kuwa na msamaha wa dhambi. Ingawa sidhani kama Mungu ataniachia mimi peke yangu kazi ya kupeleka injili kwa mtu, nadhani jambo la msingi ni kwamba hatupaswi kumzuilia mtu yeyote injili.)

F.  Soma Mathayo 28:16-17. Baadhi waliona shaka? (Huu ni mwendelezo wa mjadala wetu wa awali. Bado wanafunzi wana wakati mgumu kufungamanisha mawazo yao na ukweli kwamba Yesu alisulubiwa na kisha akafufuka.)

G.  Soma Mathayo 28:18-20. Yesu amepewa “mamlaka yote mbinguni na duniani,” na kwa sababu hiyo anawaambia wanafunzi “kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi.” Agizo la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi linahusianaje na mamlaka ya Yesu? (Yesu anatuambia kuwa alishinda pambano kwa ajili ya ulimwengu. Alishinda na kurejesha mamlaka juu ya dunia kutoka kwa Shetani. Sasa anamiliki “mamlaka yote mbinguni na duniani.”)

1.  Mamlaka ya Yesu yanaongozaje utume wetu? (Ushindi wa Yesu dhidi ya dhambi ni kitovu cha ujumbe wetu. Katika kila mjadala juu ya kile kinachotokea maishani mwetu na katika dunia yetu, msingi ni kwamba Yesu alishinda!)

2.  Nani anayepaswa kuwa mlengwa wa ujumbe wetu wa utume? (Kila mtu. Mataifa yote. Hili ni jipya. Mungu hatumii taifa la Kiyahudi kama zingatio la msingi.)

3.  Kwa nini ubatizo ndilo lengo la kwanza la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi? (Soma 2:11-13. Mwanzo 17 inatuambia kuwa Mungu alimwambia Ibrahimu kwamba tohara ilipaswa kuwa ishara ya “agano la milele” kati ya Mungu na uzao wa Ibrahimu. Wakolosai 2:11-12 inatutaarifu kuwa ubatizo ndio tohara mpya. Hivi ndivyo tunavyoonesha kuwa tuko kwenye uhusiano wa pekee na Mungu. Ni kwa jinsi tunavyoshiriki katika kifo na ufufuo wa Yesu. Kwa dhahiri hii ni hatua ya kwanza yenye nguvu kubwa!)

H.  Angalia tena Mathayo 28:19. Unadhani kwa nini Yesu anautaja Utatu Mtakatifu kama rejea ya ubatizo? Kwa nini asiseme tu “kwa jina langu” kwa kuwa Yesu ndiye aliyekufa na kufufuka?

1.  Soma Matendo 2:38. Je, Petro anafuata mantiki ya swali langu la awali na kushindwa kufuata maelekezo ya Yesu? (Maoni ya Albert Barnes yanasema kuwa lugha ya Kiyunani iliyotumika hapa inamaanisha kubatizwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa Yesu. Yesu anamleta Mungu Baba kwenye uhusiano wa agano na sisi. Utaona kuwa mara moja Petro anamleta Roho Mtakatifu kwenye uhusiano huu.)

I.  Angalia tena Mathayo 28:20. Hatua inayofuata kwenye utume wetu ni ipi? (Baada ya ubatizo tunatakiwa kufundisha utii wa amri za Yesu.)

1.  Je, kanisa lako linatafuta mkokoteni kabla ya farasi? Je, unafanya hivi kinyumenyume, kwa kukiuka maelekezo ya Yesu? (Tatizo ya kutenda hili kinyumenyume sio tu suala la utii, tatizo halisi ni kwamba unamfundisha mtu ambaye kwanza hajaingia kwenye uhusiano na Roho Mtakatifu.)

2.  Yesu anawapatia wanafunzi wake ahadi gani nyingine? (Atakuwa pamoja nasi siku zote. Ninawasikia watu wakidai kuwa tunatakiwa kufikia hatua ya ukamilifu kwa sababu tunaweza kufikia kipindi ambacho Roho Mtakatifu ataondolewa na sisi kutakiwa kusimama uso kwa uso kwa Shetani na malaika wake wapotovu (demons). Fundisho hilo linakinzana na kifungu hiki.)

II.  Ujumbe wa Utume

A.  Soma Ufunuo 14:6. Je, malaika huyu anatoa ujumbe ule ule kama tulioambiwa kuutoa katika Mathayo 28? Kama jibu lako ni “ndiyo,” kwa nini malaika anatoa ujumbe huo? (Kwa kuwa hapo kabla tulipewa ujumbe huu, nadhani kinachomaanishwa ni kwamba mbingu zinaongezea mamlaka ya ziada kwenye ujumbe wetu. Huenda mojawapo ya sababu ni kwamba tumekuwa tukishindwa kufanya kazi yetu kikamilifu.)

B.  Soma Ufunuo 14:7. Je, ujumbe huu ni sawa na maelekezo ya Mathayo 28:20? (Kimsingi, huu ni ujumbe tofauti. Yesu katika Mathayo 28 anarejelea “ukamilifu wa dahari.” Ujumbe wa Ufunuo 14:7 ni kwamba “saa” ya mwisho ni sasa.)

1.  Unaweka kwenye kundi gani kile tunachoambiwa kukifundisha katika Ufunuo 14:7? (Hii ni kuhesabiwa haki kwa imani. Mungu Muumbaji wetu anatakiwa kuabudiwa, kumcha, na kutukuzwa kwa sababu hukumu ya mwisho imekaribia. Hii inaashiria kuwa jibu la hukumu ni kuyategemea maisha makamilifu ya Yesu, na kifo cha Yesu kwa ajili ya dhambi zetu.)

C.  Soma Ufunuo 14:8. Unaona mfanano gani na Mathayo 28:18? (Vifungu vyote viwili vinatangaza ushindi wa Yesu dhidi ya wapinzani wake.)

D.  Soma Ufunuo 14:9-10. Hapa ujumbe wetu wa utume ni upi? (Tunatakiwa kuchagua kati ya Yesu na Shetani.)

E.  Soma Ufunuo 14:12. Unakumbuka kwamba Mathayo 28:20 inatutaka tufundishe? Hii inatuelekeza tufundishe nini? (Ina mambo mawili. Jambo la kwanza ni “imani kwa Yesu,” ikimaanisha imani kwa Yesu kwa ajili ya wokovu wetu. Jambo jingine ni “kuzishika amri za Mungu.”)

1.  Unaweza kupatanishaje ujumbe wa pili na kuhesabiwa haki kwa imani pekee? (Ukitafakari “imani kwa Yesu” lazima utafakari kwamba ni kwa nini Yesu alijitoa sana kwa ajili yetu? Kwa nini usipindishe tu kanuni na kuepuka mambo yote hayo yasiyo mazuri (kwa kuliweka kiurahisi)? Jibu ni kwamba Yesu aliithamini sheria kwa kiasi kikubwa. Ninaamini kuwa utawala wa sheria ni kitovu cha ufalme wa Mungu wa upendo. Tunapotambua umuhimu mkubwa wa sheria, basi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, tutadhamiria “kuzishika amri za Mungu.”)

F.  Rafiki, Mungu ana matarajio gani na sisi? Tumejifunza kwamba matarajio hayo sio tu ya kumwamini Yesu, bali kupeleka habari hizi njema kwa watu wote wa ulimwengu. Malengo yetu ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi ni ubatizo, kufundisha, na utii kwa kuzingatia hukumu inayokuja. Je, utajiingiza kwenye utume huo sasa hivi?

III.  Juma lijalo: Wito wa Mungu Kwenye Utume.