Somo la 12: Wito wa Kusimama

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 6:10-20
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
12

Somo la 12: Wito wa Kusimama

Waefeso 6:10-20

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Hadi kufikia hapa unaweza kuyaelezeaje maelekezo ya Paulo katika kitabu cha Waefeso? Je, maelekezo mengi hayahusu mipangilio ya ndani? Hivyo ndivyo tunavyohusiana na wanafamilia wenzetu na washiriki wenzetu wa kanisa? Kwa kuwa sasa tuna uelewa wa pamoja kuhusu mipangilio yetu ya ndani, Paulo anazigeukia changamoto za nje. Isivyo bahati, kinachoendelea duniani ni vita, vita ya kiroho. Tunaitwa kuwa sehemu ya pambano hilo, hivyo hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone jinsi ya kuwa askari wazuri!

I.  Pambano Liko Tayari

A.  Soma Waefeso 6:10. Paulo anatupatia wito mara mbili kuwa hodari. Kama ungekuwa askari katika jeshi la kawaida ungefanya nini ili kuwa hodari?

1.  Paulo anatupendekezea njia tofauti kabisa. Tunapaswa kufanya nini ili kuwa hodari? (Tunamtegemea Mungu ili kuwa na nguvu.)

a.  Unafanyaje ili kuzipata? (Endelea kusoma!)

b.  Tusifanye nini? (Tusizitegemee nguvu zetu.)

c.  Haya yanaonekana kama maswali mepesi, lakini hebu jiulize, msukumo wako wa kwanza unakuwaje pale unapokabiliana na tatizo? Unamtegemea nani?

B.  Soma Waefeso 6:11. Mungu anatuambia tufanye nini ili kuwa imara katika Mungu? (Kuvaa silaha zinazotolewa na Mungu.)

1.  Angalia aina ya vita. Tunapaswa tuwe makini na jambo gani? (“Hila za Shetani.”)

a.  Hiyo ni vita ya namna gani? (Hii haionekani kuwa vita halisi ya kidunia bali vita ya kisaikolojia.)

C.  Soma Waefeso 6:12. Kama askari, ni muhimu kiasi gani kutambua kuwa nani ni adui na nani sio adui? (Kumwelewa yule unayepambana naye ni muhimu sana.)

1.  Kwa sasa ninasoma kitabu kizuri sana ninachokipendekeza kwa watu wote, kinaitwa “The War on the West,” kilichoandikwa na Douglas Kear Murray. Katika sehemu mojawapo ya kitabu anajenga hoja kuwa watu ambao kimsingi hawajafanikiwa chochote wanawashambulia wale waliofanikiwa mambo makubwa. Tatizo, kwa mujibu wa Murray, ni kwamba wanahodhi hisia za chuki na wivu, badala ya mtazamo wa shukrani. Ninapoendelea kukisoma kitabu ninadhani ya kwamba Murray hazingatii mtazamo mpana – pambano kuu kati ya Mungu na Shetani. Hii ni tamaa iliyopitwa na wakati – ambayo ni dhambi. Kuielewa taswira pana kunaathirije mtazamo wetu katika hii vita?

2.  Je, huwa unawakasirikia watu waliopo sehemu ya kurudisha vitu vilivyonunuliwa kwenye maduka makubwa? Je, sera ya maduka hayo ya kurudisha vitu vilivyonunuliwa ni kosa lao? (Tunatakiwa kuelewa nani anayepaswa kuwa mlengwa mkuu wa pambano letu. Paulo anasema hatupambani dhidi ya watu wengine.)

3.  Hebu subiri kidogo. Kwani hatuna mawakala wa kibinadamu wa Shetani ambao wamejitoa kikamilifu kwa upande wake? (Rejea ya Paulo ya “falme na mamlaka” ni rejea na mipangilio ya pepo wachafu wanaomtumikia Shetani. Ingawa Shetani ana mawakala wake miongoni mwa wanadamu, Paulo anatuambia kuwa pambano halisi ni dhidi ya Shetani na malaika wake wapotovu.)

II.  Mbinu za Pambano

A.  Soma Waefeso 6:13 na uangalie tena Waefeso 6:11. Jambo gani linakushangaza kama ushauri wa ajabu kwa askari? (Paulo anatuambia “kusimama.” Katika kifungu cha 11 anasema, “kusimama dhidi ya.” Katika kifungu cha 13 anasema “kusimama imara.”)

1.  Je, ulinzi imara sio kosa kubwa? Kwa nini tusiseme kuwa Wakristo wanapaswa kusonga mbele na pambano lao dhidi ya uovu wa kiroho? (Ni dhana ya majigambo kusema kuwa tunaweza kumshambulia Shetani kwa mafanikio. Ndio maana sisi ndio tunaoonekana kuwa uwanja wa pambano. Tunatakiwa kumtegemea Mungu, silaha zetu zinatoka kwa Mungu, na lengo letu ni kusimamia msimamo wetu wa kiroho.)

2.  “Tunazitwaaje” silaha hizi kiuhalisia? (Kwa njia ya maombi, kujifunza Neno, kuishi maisha ya haki, kupeleka injili kwa wengine, kuwa na imani, kuuelewa na kuushikilia wokovu wetu, na kuyatumia Maandiko.)

B.  Soma Waefeso 6:14. Kwa mara nyingine, tunaambiwa “kusimama.” Unapotafakari kuhusu pambano linalokuzunguka leo, ukweli ni wa muhimu kiasi gani? (Katika pambano, kusema uongo, hata katika ngazi za juu za serikali na utabibu, kunashangaza. Huu ni mfano mmoja wa dhahiri: madai kwamba mwanaume anaweza kuwa mwanamke na kinyume chake.)

1.  Utasema nini kama watu watakuambia kuwa waliamini walikuwa mazimwi wenye jicho moja na unapaswa kuchoma/kuchakura mojawapo ya macho yao?

2.  Nilisema kuwa walikuwa wanasema uongo. Je, hiyo inachukulia (assume) kwamba ninaujua ukweli? Je, kila mtu ana ukweli wake mwenyewe? (Hiyo inachukulia (assume) kwamba ninao ukweli. Ukweli ni ukweli wa Mungu – kinachofunuliwa kwenye Biblia. Hakuna ukweli ikiwa kila mtu ana ukweli wake mwenyewe.)

3.  Kwa ujumla ninadhani tunapaswa kusita kuwaita watu kuwa ni waongo. Ni nini matokeo ya wana wa uongo katika muktadha huu? (Matokeo ya uongo ni madhara yanayodumu maishani mwote. Ndio maana ushindi wa ukweli ni wa muhimu sana.)

4.  Unadhani inamaanishwa nini tunaposema “kuvaa dirii ya haki kifuani?” (Hii ni dirii inayoficha kiwiliwili.)

5.  Unaifanyaje dirii hii kuwa ya “haki?” (Utakumbuka kuwa silaha inatoka kwa Mungu. Kwanza tunatakiwa kuidai haki ya Mungu. Tunatakiwa kuutamani utakatifu, usafi, uaminifu maishani mwetu. Kunyooshea kidole tamaa, kutokuwa na uaminifu, na uchafu kwa watu wengine husababisha tatizo kama tutadhihirisha dhambi hizo maishani mwetu.)

C.  Soma Waefeso 6:15. Je, umewahi kujaribu kupigana ukiwa miguu mitupu (bila kuvaa viatu)? (Unakuwa kwenye mazingira hatarishi sana.)

1.  Viatu vinafananaje na “injili ya amani?” (Tunapokuwa na uweli wa Mungu na kutambua kuwa tuko upande wake tunakuwa na amani katika mapambano ya kiroho.)

D.  Soma Waefeso 6:16. Hii inaniambia kuwa nguvu za Shetani zinarusha mishale “yenye moto” kwako na kwangu. Tunapaswa kuhitimisha nini kutokana na ukweli inaitwa mishale “yenye moto?” (Inalenga kuleta madhara. Inalenga kuangamiza.)

1.  Imani yetu inatusaidiaje kwenye mashambulizi haya? (Tunajua tuko upande sahihi ikiwa tunamfuata Mungu. Habari njema sana ni kwamba mashambulio makali yanafeli. Yanazimwa moto.)

2.  Utagundua tena kwamba hiki ni kitendo cha kujilinda.

E.  Soma Waefeso 6:17. Ni kwa jinsi gani wokovu ni chapeo (helmeti)? Inakingaje kichwa chetu? (Imani yetu katika wokovu wetu inatufanya tuendelee kuwa imara. Shetani anataka kuangamiza imani yetu katika wokovu wetu na uhusiano wetu na Bwana wetu ambaye anatoa silaha hii.)

1.  Hebu tuangalie silaha pekee inayodhuru kwenye orodha – “upanga wa Roho.” Kwa tafsiri yangu neno “Roho” limeanza kuandikwa kwa herufi kubwa. Hiyo inaashiria uelewa wa kwamba huyu ni Roho Mtakatifu. Paulo anawezaje kumuita Roho Mtakatifu “neno la Mungu?” (Hii ni kweli angalao kwa namna mbili. Roho Mtakatifu aliwavuvia waandishi wa Biblia, kama Paulo (2 Petro 1:21). Roho Mtakatifu pia atakuvuvia wewe na mimi (Yohana 16:13). Silaha yetu inayodhuru inatakiwa kutumika kwa umakini. Inatakiwa kutumika kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu pekee.)

F.  Soma Waefeso 6:18-19. Kwa nini Paulo anasisitiza maombi baada ya kujadili silaha yetu? (Maombi ndio njia ambayo tunaamsha na kutwaa/kushika silaha. Ndio njia yetu ya mawasiliano na Kamanda na majeshi ya mbinguni!)

1.  Tunamwombea nani? (Sio tu kwamba tunajiombea wenyewe, bali pia tunawaombea waumini wenzetu na viongozi wetu.)

G.  Soma Waefeso 6:20. Swali la endapo pambano letu ni la kujilinda au la kushambulia ni suala muhimu. Paulo anaendeleaje na sehemu yake ya pambano? (Anaitangaza injili “kwa ujasiri.” Ufafahuzi huu wa kile ambacho amekuwa akikifundisha ni dhihirisho. Kuitangaza kweli kwa ujasiri kunaendana na pambano la shambulizi.)

H.  Rafiki, ujumbe mkuu ambao Paulo anatamani kutufundisha ni kwamba tuko kwenye vita ya kiroho, lakini Mungu anatupatia silaha na zana za kutusaidia kusimama imara na kuwa washindi. Je, utajitoa kila siku kuvaa silaha kamili za Mungu na kusimama imara katika kukabiliana na mapambano ya kiroho?

III.  Juma lijalo: Kuendeleza Amani.