Somo la 10: Waume na Wake : Pamoja Msalabani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 5:21-33
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Waume na Wake : Pamoja Msalabani

(Waefeso 5:21-33)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, ndoa za Kikristo ziko kwenye matatizo? Ninapohudhuria kwenye tukio la ndoa huwa ninasikia maoni ya kuhuzunisha kwamba mambo ni mazuri siku ya ndoa, lakini mwishowe ni huzuni. Mimi ni mtu mwenye msimamo wa kutegemea mazuri (optimist), hivyo huwa sisemi mambo kama hayo. Lakini takwimu kuhusiana na ndoa zinakatisha tamaa. Utakumbuka kwamba katika masomo machache yaliyopita kuhusiana na uhusiano ndani ya kanisa, tulisema kuwa dhana za umoja za kanisa zinaweza pia kutumika kwenye ndoa. Swali moja nililoliuliza ni kuwa “Je, ushirika pia ni wa muhimu katika ndoa?” Somo letu la leo linaelekea kutoa jibu la, “Ndiyo.” Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu ushirika katika ndoa – miongoni mwa mambo mengine!

I.  Unyenyekevu wa Pande Mbili (Mutual Submission)

A.  Soma Waefeso 5:21. Utakumbuka juma lililopita somo letu liliishia kwenye kifungu hicho. Je, unakumbuka baada ya tabia zote mbaya tulizojifunza juma lililopita, niliuliza jambo linalofanana na, “Kwa nini tuwanyenyekee wengine wakati watu wapumbavu wapo tele?”

1.  Tulihitimisha kuwa jibu ni lipi? (Maneno “hali mkinyenyekeana katika kicho cha Kristo” yanaelezea aina ya unyenyekevu tunaopaswa kuwa nao.)

2.  Unadhani Paulo anamaanisha nini anaposema “mkinyenyekeana?”

3.  Unadhani Paulo ana lengo gani kututaka tunyenyekeane?

B.  Soma Waefeso 5:22. Mimi ni mume. Je, inawezekana kwamba ninamchukulia mke wangu akininyenyekea tofauti na ninavyouchukulia wajibu wangu wa kuwanyenyekea watu wengine kanisani, hususani wapumbavu? (Kuna uwezekano mdogo kwa waume kujichukulia kama wapumbavu, hata kama ni kweli.)

1.  Kwa maneno mengine, je, mke kumnyenyekea mumewe ni tofauti na mume kuwanyenyekea washiriki wengine wa kanisa? (Utaona kuwa Waefeso 5:21 na waefeso 5:22 zina maneno yanayofanana mwishoni mwa kifungu. Kifungu cha 22 kinasema “kama kumtii Bwana.” Hii inatuambia kuwa asili ya unyenyekevu wa mke inathibitishwa.)

a.  Au sivyo? Kwani hatupaswi kumnyenyekea Mungu katika kila jambo?

C.  Tafakari tena kuhusu Waefeso 5:21 na Waefeso 5:22, kama mke pia ni mshiriki wa kanisa, je, hiyo inamaanisha tunaangalia unyenyekevu wa pande zote mbili?

1.  Je, uelewa wa sasa wa usawa wa kijinsia unapaswa kuathiri au kushawishi uelewa wetu wa vifungu hivi? (Tunawezaje kudhani kuwa uelewa wa sasa una thamani wakati nusu ya matokeo ya ndoa za sasa zinaonekana kuparanganyika?)

D.  Soma Waefeso 5:23-24. Hii inaashiria kuwa asili ya wajibu wa mume na mke ni ipi? (Hebu tutafakari kuhusu swali la ushirika. Ninadhani kwanza hii inatuambia kuwa katika kila taasisi hatimaye mtu fulani anapaswa kuwajibika, kuwa kiongozi. Kristo ndiye kichwa cha kanisa. Yeye ndiye kiongozi.)

1.  Vipi kama mke anadhani (au anajua) kuwa mume ni mpumbavu? (Ukiolewa na mpumbavu, unaweza kujikuta ukikabiliana na matatizo.)

2.  Je, ni muhimu kwamba katika ulinganifu huu kati ya waume na Kristo kifungu cha 23 kinasema Kristo ni “mwokozi wa mwili?”

II.  Waume na Upendo

A.  Soma Waefeso 5:25-27. Je, waume wanapaswa kutafakari kuwa katika matendo yao kama “kichwa” cha familia wanajipenda au wanawapenda wake wao?

1.  Kristo alilipenda kanisa kwa kiwango gani? (Alilifia.)

a.  Utalitumiaje hilo, waume, kwenye uhusiano na mke wako?

B.  Angalia tena Waefeso 5:26. Hapo awali niliuliza ni nini lengo la kunyenyekea huku. Hapa tunaona jibu gani? (“Kumtakasa” mke.)

1.  Hiyo inamaanisha nini?

2.  Hebu turejee kwenye suala la ulinganifu, ambalo ni ubatizo. Nini kinatutokea katika ubatizo? (Soma Wakolosai 2:12. Tunashiriki na Yesu katika kifo chake kwa ajili ya dhambi zetu.)

3.  Je, tunapaswa kuhitimisha kuwa waume wanatakiwa kunyenyekea ili kuwafanya wake zao kuwa watakatifu?

4.  Je, mume anatakiwa kujitoa sadaka ya upendo wake kwa mkewe?

C.  Soma Waefeso 5:28. Ilinganishe na Mathayo 7:12. Je, huu ni wito wa kumtendea mke sawa na unavyowatendea watu wengine? (Nadhani hiki ni kifungu cha muhimu kuliko vyote katika Biblia kuhusu ndoa. Unapaswa kumpenda mke wako kama unavyojipenda. Ukiangalia kwa kina, ukimpenda mke wako kama unavyojipenda mwenyewe, utapendwa na mke wako. Waume wanajitafutia mambo mazuri kama watawapenda wake zao. Na, hanapa, sidhani kama mke anapaswa kutendewa kama watendewavyo watu wengine. Kwa nini? Kwa sababu mjadala huu katika kitabu cha Waefeso hautakuwa na maana kama ulimaanisha tu kurudia maneno ya Mathayo 7:12.)

D.  Soma Waefeso 5:29-30. Paulo anajenga hoja gani ya kivitendo/kiuhalisia ya kumpenda mke wako?

III.  Siri/Fumbo

A.  Soma Waefeso 5:31-32. Ilinganishe na Mwanzo 2:24. Ni kwa jinsi gani hii ni siri kubwa? (Hapa ndipo mahala ambapo wanadamu wanafanana na Mungu kwa maana ya kwamba wanaweza kuumba uhai. Uwezo wetu wa uumbaji ni siri/fumbo.)

1.  Je, unadhani kuwa ukimwonesha mkeo upendo wa kujitoa kabisa naye atakupenda kwa siri zaidi? Kwa siri atakuwa mtu bora zaidi? (Nimeliona hilo. Wanandoa walioana baadaye sana maishani. Haikuwa ndoa ya kwanza kwa wote wawili. Mara moja mke alisikitishwa na ndoa hiyo na hasira zake (zilizoweza kuwa kubwa) zikamgeukia mumewe mpya. Mume akaamua tu kumpenda mkewe. Upendo huo ukambadilisha mke na kubadilisha ndoa yao.)

B.  Angalia tena Waefeso 5:31. Ni kwa jinsi gani “kumwacha baba yako na mama yako” kunaendana na dhana ya kuonesha upendo kwa mke wako? (Wote wawili, yaani mume na mke, anatakiwa kumpenda mwenzi wake kuliko wazazi wake. Mmoja kwa mmoja, mume mpya na mke mpya wanatakiwa kufikia makubaliano. Wazazi wakitakiwa kupiga kura, basi matokeo yake yatakuwa watatu kwa mmoja na hakuna maafikiano (compromise) yanayoweza kufikiwa.)

C.  Angalia tena Waefeso 5:32. Paulo pia anarejelea siri kwa kumrejelea Kristo na kanisa. Ni kwa jinsi gani hiyo ni siri? (Uhiari wa Yesu kuuchukua uanadamu, kuishi maisha makamilifu, kuteswa hadi kufa, na kufufuka ili kutupatia uzima wa milele ni fumbo/siri. Fumbo kwa maana ya kwamba ni vigumu sana kwetu sisi kuielewa.)

1.  Ni kwa jinsi gani siri hiyo inatumika kwenye ndoa? (Tunaweza kuwa na matokeo mazuri yasiyotarajiwa katika kupendana kwenye ndoa.)

IV.  Muhtasari

A.  Soma Waefeso 5:33. Je, utakubaliana kuwa huu ni muhtasari wa kile ambacho tumekuwa tukijifunza juma hili?

1.  Angalia maelekezo ya mke “kumtii” mume. Ni muhimu kiasi gani kwa mwanaume kuheshimiwa na mke wake?

2.  Ukiwasikiliza wake wakiongea miongoni mwao kuhusu waume wao, wangapi wanaonekana kuwatii waume wao?

3.  Hapo awali, niliwarejelea waume kuwa wapumbavu na nikauliza kuhusu kuwanyenyekea wanaume wapumbavu. Mjadala huo unaendanaje na mada hii hapa? (Hapo awali tulijadili kuhusu ukomo wa unyenyekevu. Kinachotakiwa hapa ni kuepuka kudhani kuwa mumeo ni mpumbavu. Hiyo inajumuisha kuzungumza na watu wengine kuhusu mume wako kuwa mpumbavu.)

B.  Rafiki, tumeona kwamba ushauri wa Paulo kwa ajili ya ndoa sio jambo linalokinzana na matamanio ya mke. Uelewa huo ni kinyume na maoni ya sasa ya Paulo kuhusiana na mada hii. Badala yake, kitabu cha Waefeso kinatoa wito wa kumtendea mke kama Yesu anavyotutendea. Siri hii kubwa kuhusu uhusiano wa ndoa itatupatia ndoa imara. Kwa nini mke na mume, msikubaliane sasa hivi kujiingiza kwenye majukumu yanayobainishwa na Waefeso?     

V.  Juma lijalo: Kujizoeza Uaminifu Mkuu kwa Kristo.