Somo la 2: Mpango Mkuu wa Mungu Uliojikita kwa Kristo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 1
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Mpango Mkuu wa Mungu Uliojikita kwa Kristo

(Waefeso 1)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, shukrani ni sehemu ya mtazamo wako? Je, Umewaona watu wanaoongea kana kwamba wanastahili mambo fulani ambayo hawajafanya chochote kuyapata? Nafahamu huwa nina mjibizo chanya kwa watu walio na shukrani, na nina mjibizo hasi kwa wale wanaodai kile wasichokistahili. Vipi kuhusu wewe? Paulo anakianza kitabu cha Waefeso kwa shukrani. Anamshukuru Mungu Baba na anamshukuru Yesu kwa yote waliyotutendea. Kisha anaendelea kuwashukuru Waefeso kwa yote waliyoyafanya. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Shukrani kwa Mungu

A.  Soma Waefeso 1:3. Ni nini aina ya baraka ambazo kwazo Paulo anaelezea shukrani zake? (Baraka za kiroho.)

1.  Kwa nini baraka zetu za kiroho zinahusianishwa na mahala pa mbinguni? Jambo gani linazungumzwa kumhusu Paulo? (Hizi ni baraka ambazo ni za kwetu kule mbinguni.)

2.  Utazielezeaje baraka za kiroho tofauti na baraka za mali?

3.  Kwenye masomo haya mara kwa mara huwa ninaandika kuhusu baraka zinazotokana na utii wa sheria. Je, baraka hizo ni za kiroho au za mali? (Kimsingi huwa ninawaza baraka za mali.)

B.  Soma Waefeso 1:4. Hii ni baraka gani? (Tulichaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.)

1.  Je, hii ni baraka ya kiroho au baraka ya mali? (Kiroho)

2.  Inatolewa wapi? (Huu ndio mfano wa kwanza ambao Paulo anauzungumzia katika kifungu cha 3 – baraka ya kiroho tuliyopewa mbinguni.)

3.  Kwa nini hasa, baraka hii ya kiroho inapaswa kuwa takatifu isiyo na hatia? (Hii inaonekana kama kuhesabiwa haki kwa njia ya imani. Tatizo ni kwamba hatukuwa na imani kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu.)

a.  Inamaanisha nini kusema kuwa tuko “ndani yake?” (Tunakuwa “watakatifu watu wasio na hatia” kama matokeo ya kazi ya Yesu.)

4.  Fikiria kuhusu muda. Kwa nini tunapewa baraka kabla ulimwengu haujaumbwa na Mungu? (Yesu aliamua kuwaokoa wanadamu walioanguka kabla mwanadamu yeyote hajaumbwa.)

a.  Kwa nini Yesu alifanya hivyo? Kwa nini atuumbe wakati mustakabali wetu haukuwa wa uhakisa sana kiasi kwamba uliandaliwa mpango wa dharura?

II.  Mpango wa Familia

A.  Soma Waefeso 1:5. Unaweza kuelezea baraka hii mpya ya kiroho? (Tulichaguliwa ili tufanywe kuwa wana na binti wa Mungu!)

1.  Kama tulitarajiwa kuwa watu wenye matatizo, kwa nini kutufanya kuwa familia? (Utaona kuwa sehemu ya mwisho ya Waefeso 1:4 inasema “katika pendo” na kisha inanukuu kifungu cha 5.)

B.  Soma Waefeso 1:6. “Huyo mpendwa” ni nani? (Soma Mathayo 3:17. Yesu ndiye “huyo mpendwa.”)

1.  Tulifanyika wana na binti wa Mungu kwa baraka tulizopewa kwa njia ya “utukufu wa neema” ya Yesu. Hii inazungumzia nini kuhusu wale wanaodai kuwa matendo ni ya muhimu katika wokovu? (Matendo yanawezaje kuwa sehemu ya hili wakati tulichaguliwa kabla hatujaumbwa?)

C.  Soma Waefeso 1:7. Hapa tunaona baraka gani ya kiroho? (Ukombozi na msamaha.)

1.  Tunazipokeaje baraka hizi? (Kupitia kwa damu ya Yesu. Kwa sababu Yesu ni mwingi wa neema.)

a.  Fikiria kuhusu ambavyo neema hii kubwa ilivyomgharimu Yesu.

2.  Baadhi ya watu wanaamini kuwa damu ya Yesu inasamehe dhambi za nyuma pekee. Kuhusu dhambi zijazo, ni bora tukawa watiifu wa sheria. Neno “ukombozi” linamaanisha nini? (Inamaanisha kuwa tumeokolewa.)

D.  Soma Waebrania 10:14. Kifungu hiki kinatuambia kuwa Yesu alitukamilisha “hata milele” kwa kafara yake. Wakati huo huo kifungu kinatuambia tunatakaswa. Inawezekanaje vyote viwili vikawa kweli kwa wakati mmoja? (Tunatangazwa kuwa wakamilifu kutokana na kile ambacho Yesu alikitenda kwa ajili yetu kwa damu yake na neema yake. Wakati huo huo tunaichukulia kafara yake kwa dhati, tunauchukulia mpango wake kwa wanadamu kwa dhati, na tunafanya uamuzi wa kuishi maisha ya utii.)

E.  Soma Waefeso 1:8-9. Baadhi ya wanamaoni wanalielewa jambo hili kumaanisha kuwa Mungu alitupatia hekima na utambuzi kwenye programu yake. Kwa upande wangu inaonekana kana kwamba Mungu anatumia hekima na utambuzi katika kutukomboa. Chukulia kwamba niko sahihi. Ni nini hekima na utambuzi wa Yesu katika kutuokoa kwa neema? (Mungu alijua kuwa hatuiwezi kazi hiyo. Ukweli kwamba alikuwa na mpango wa kutukomboa tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu (Waefeso 1:4) inaonesha kile alichokitafakari kuhusu uwezo wetu wa kuishinda dhambi.)

F.  Angalia tena Waefeso 1:9 na usome Waefeso 1:10. Je, fumbo limefumbuliwa kwetu? (Hadi kufikia hapa kifungu kipo dhahiri kwamba Mungu alitubainishia kwa uwazi mpango wake kwa ajili ya wokovu wetu. Hata hivyo, sidhani kama hii inabadili kile tulichojadili katika swali lililotangulia.)

1.  Utaona kuwa Mungu ana lengo katika yote haya.  Ni lengo gani hilo?

2.  Waefeso 1:10 inasema kuwa lengo la Mungu linabainishwa kwenye mpango. Hatimaye mpango wa Mungu ni upi? (Umoja! Katika wakati sahihi Mungu “atavijumlisha vitu vyote katika Kristo.”)

3.  Tumekuwa tukitafakari baraka zetu za kiroho. Je, umoja ni miongoni mwa baraka hizo? Ikiwa ndivyo, umoja utayaboreshaje maisha yako sasa hivi?

G.  Soma Waefeso 1:11-12. Kwa mara nyingine tunaambiwa kuwa tunaandaliwa urithi wetu kama sehemu ya mpango wa Mungu. Mpango huu ni kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Lengo gani mahsusi linabainishwa katika kifungu cha 12? (Kwamba maisha yetu yanaweza kuwa “sifa ya utukufu wake.”)

1.  Inamaanisha nini kwa maisha yetu kumtukuza Mungu? (Hapa ndipo “matendo” yanapojitokeza. Maisha yetu yanapaswa kumtukuza Mungu.)

a.  Yatafakari maisha yako. Je, yanamtukuza Mungu?

III.  Roho Mtakatifu

A.  Soma Waefeso 1:13-14. “Mhuri” wa urithi wetu katika Yesu ni upi? (Kumpokea Roho Mtakatifu.)

1.  Kitu gani kinahamasisha huo utiaji mhuri?  (Tumeisikia na kuiamini injili. Tulimwamini Yesu Bwana wetu.)

2.  Kwa nini Roho Mtakatifu ndiye mhuri na dhamana ya mustakabali wetu na Mungu? (Roho Mtakatifu anapatikana kwa kila mmoja wetu sasa hivi. Mungu anaweza kuwa nasi sasa hivi tukimwomba.)

a.  Angalia rejea ya mwisho ya “milki” ya urithi wetu. Tutamiliki nini? (Tutakaa na Mungu! Roho Mtakatifu ni mtangulizi (preview) wa maisha yetu na Mungu katika dunia iliyofanywa upya.)

B.  Utaona kuwa Waefeso 1:12 na Waefeso 1:14 zinahitimisha kwa maneno, “kuwa sifa ya utukufu wake.” Waefeso 1:6 inasema jambo linalofanana – “utukufu wa neema yake.” Ni nini wajibu wa Roho Mtakatifu kwenye hii mada ya kumtukuza Mungu?

C.  Soma Waefeso 1:18. Tumekuwa tukijadili kuhusu urithi wetu – maisha katika dunia iliyofanywa upya na Bwana wetu. Zingatia lugha tofauti hapa. Inarejelea “utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu.” Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Sisi ni urithi wa Mungu. Sio tu kwamba tunao urithi katika dunia itakayofanywa upya, bali Mungu anao urithi na urithi huo ni sisi!)

1.  Je, Mungu anajivunia kuwa na wewe? Je, wewe ni urithi mzuri?

D.  Rafiki, Mungu amekuchagua ili upate urithi. Watu wengi wanafurahia pale wanapotambua kuwa wanarithi kitu fulani. Je, utaupokea urithi wako kutoka kwa Mungu? Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Uweza wa Yesu Aliyetukuzwa.