Somo la 13: Kuteketezwa na Utukufu wa Mungu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
1 Wathesalonike 5, Yohana 7, Ufunuo 18 & 21
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Kuteketezwa na Utukufu wa Mungu

(1 Wathesalonike 5, Yohana 7, Ufunuo 18 & 21)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kijana wangu aliniambia habari za mizunguko yake ya kikazi kama daktari. Alipokuwa akiwashauri wagonjwa wenye kisukari, hali inayoweza kuwaingiza kwenye matatizo ya moyo, au tatizo lolote la kiafya linaloweza kujidhihirisha kwao muda wowote katika siku za usoni, wagonjwa wake walionekana kutozingatia sana ushauri wake. Alipokuwa katika kitengo cha saratani wagonjwa wote wazingatia ushauri wake kwa ukaribu. Kwa nini? Kwa sababu wagonjwa wa saratani walijua kuwa kifo kinaweza kuwa karibu nao zaidi. Kwa magonjwa mengine, walidhani walikuwa na muda zaidi kabla hawajawa wazingativu zaidi kuhusu matatizo yao ya kiafya. Tumesikiliza ujumbe wa Malaika Watatu, tumejifunza kuhusu mgawanyiko kati ya waliookolewa na wasiookolewa, na tunadhani wakati wa mwisho unaweza kuwa karibu zaidi. Swali ni kama tutakuwa werevu kwa kujiandaa muda wote. Je, tutalichukulia suala hili kwa umakini? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Jitayarishe

A.  Soma 1 Wathesalonike 5:1-2. Kwa nini Paulo anawaandikia Wathesalonike anaposema kuwa hana haja ya kuwaandikia? (Anachokimaanisha hasa ni kwamba sina haja ya kuwaandikia, lakini ninadhani nina haja ya kufanya hivyo.)

1.  Anamaanisha nini kuhusu mwivi aibaye usiku? (Watu wengi hawatarajii mwivi awatembelee katika usiku wowote mahsusi. Kwa kawaida watu hulala usiku. Paulo anaonya kuwa mwivi anakuja.)

B.  Soma 1 Wathesalonike 5:3. Matukio ya siku za mwisho yatatujiaje? (Dunia inapojihakikishia kuwa hiki ni kipindi cha amani na usalama, kinyume chake ndicho hutokea – uangamivu.)

1.  Kwa nini Paulo amchague mjamzito kufafanua matukio ya siku za mwisho? (Mwanamke anajua kuwa atajifungua mtoto. Tukio linalokuja sio la kushtukiza. Kinachoshtukiza ni pale ambapo kimsingi mtoto anaanza kuja. Tunajua Yesu anakuja tena, tunajua kuhusu mwisho wa dunia, lakini bado tutashtukizwa mwisho unapokuja.)

C.  Soma 1 Wathesalonike 5:4-6. Paulo anaonekana kusema mambo mawili yanayokinzana kwa kiasi fulani. Anasema kuwa Wakristo wa Thesalonike ni wana wa mchana, hawako gizani. Wakati huo huo anasema kuwa wanatakiwa kukesha (wasilale usingizi) na kuwa na kiasi. Kwa nini? (Kuwa macho wakati wa mchana sio sawa na kuwa na tahadhari.)

D.  Soma 1 Wathesalonike 5:7-8. Paulo anafafanua kuwa kulala usingizi au kulewa sio njia ya kuwa na tahadhari. Kitu gani kitatufanya tuwe macho? (Kujivika silaha ya kiroho ya imani, upendo, na tumaini la wokovu.)

1.  Kwa nini hilo litufanye tuwe macho? (Tunazingatia masuala ya kiroho. Tunajihusisha kwenye vitendo vya kiroho.)

E.  Soma 1 Wathesalonike 5:9-11. Wanamaoni wanaelewa kauli ya “kwamba twakesha au kwamba twalala” kumaanisha kuwa tu hai au tumekufa wakati wa ujio wa Mara ya Pili. Kinachonishumbua kuhusu tafsiri hii ni kwamba hapo kabla Paulo alitumia kauli hii kumaanisha kama tu macho. Je, tunapaswa kuwa macho ili kuokolewa? (Ninadhani wanamaoni wanakosea jambo la msingi. Wokovu wetu haugeukii kwenye uelewa wetu sahihi wa matukio ya wakati wa mwisho.)

1.  Kwa nini uelewa wa matukio ya wakati wa mwisho, na kuwa macho, ni jambo la muhimu? (Kama utii kwa Mungu unavyoyaboresha maisha yetu, vivyo hivyo uelewa wa kile kinachoendelea wakati wa mwisho utatupatia ujasiri na amani.)

F.  Angalia tena 1 Wathesalonike 5:8. Je, hii inaashiria kuwa kuzielewa nyakati za mwisho na kuwa tayari ni sawa na kuwa vitani? (Ni vita ya kiroho.)

1.  Itafakari mitazamo ya wafuasi wa Mungu juu ya Ujio wa Yesu Mara ya Kwanza. Wangapi waliupatia? (Wachache sana, ikiwa wapo. Utaona kuwa wanafunzi wa Yesu, hata baada ya kufundishwa na Yesu kwa muda wa miaka mitatu, hawakuupatia. Matendo 1:6.)

2.  Kanisa langu linafundisha kuwa miongoni mwa masuala ya utii yanayohusika katika kipindi cha mwisho, Sabato ndio ya muhimu kuliko yote. Ni nini hatari ya uhakika kamili katika uelewa wetu wa matukio na changamoto za siku za mwisho? (Kasoro juu ya ujio wa Yesu Mara ya Kwanza zilijengwa juu ya uelewa wa manabii wa Agano la Kale na kutoelewa kile ambacho Yesu alikifundisha. Kwa kuwa tunatakiwa kujiandaa kwa ajili ya vita, sidhani kama tunapaswa kuhafifisha uwezo wetu wa kukosea mambo. Tunapaswa pia kujiandaa kwa mambo yasiyotarajiwa.)

G.  Soma Yohana 7:17-18. Yesu anasema kuwa tunapaswa kujenga uelewa wetu wa matukio ya wakati wa mwisho juu ya msingi gani? (Yesu anarejelea juu ya kuyategemea mafundisho kutoka kwa Mungu.) anapendekeza kuwa tunaweza, ikiwa tu radhi, kutenganisha ukweli kutoka kwenye kasoro.)

1.  Ni nini msingi wa kuwa na uelewa wa aina hii? (Soma Yohana 16:13. Uongozi wa Roho Mtakatifu unatufanya tuwe na utambuzi huu. Hii ndio sababu Waefeso 1:13-14 inamrejelea Roho Mtakatifu kama mhuri kwa waliookolewa.)

II.  Kiangaza cha Nyakati za Mwisho

A.  Soma Ufunuo 18:1-2. Unadhani inamaanisha nini kusema nchi “ikaangazwa kwa utukufu wake?” (Miongoni mwa giza na wasiwasi wote wakati wa pambano la mwisho, kuna nuru ya ukweli.)

B.  Soma Ufunuo 4:4-5. Unadhani kwa nini roho wa Mungu anawakilishwa na moto? (Soma Matendo 2:1-3. Moto ni uwakilishi wa kawaida wa Roho Mtakatifu. Katika Matendo 2 Roho Mtakatifu alikuja kwa uwezo mkubwa ili kuwafundisha watu kuhusu habari za Yesu.)

1.  Kuna jambo gani kubwa kuhusu mgongano kati ya Joka na wafuasi wa Mungu katika kipindi cha mwisho? (Mgongano huu husaidia kuleta usikivu wa masuala mbalimbali. Giza hupenda kujificha gizani. Kuwasha taa huwafanya watu wawe macho na masuala mbalimbali na kuwasaidia kufanya uchaguzi.)

C.  Soma Ufunuo 5:6. Huenda umegundua rejea ya ajabu ya “Roho saba” katika Ufunuo 4:5. Tunaiona hapa tena. Unadhani hii inamaanisha nini?

1.  Soma Waefeso 4:4-6. Tuna Roho Watatatifu wangapi? (Tunaye Roho Mtakatifu mmoja pekee.)

2.  Rejea hii ya “Roho saba” inamaanisha nini basi? (Saba ni namba kamili. Inamaanisha kuwa Roho amtakatifu anafanya kazi duniani kwa uwezo wake wote. Nuru ya Mungu inaangaza kikamilifu.)

D.  Soma Ufunuo 21:8 na ujikite kwenye fafanuzi mbili za awali: waoga na wasioamini. Katikati ya kiangaza cha ukweli wa Mungu dhidi ya giza la joka, tunaitwa kufanya nini? (Kumtumaini Mungu! Tunatakiwa kumtumaini Mungu na uwezo wa Roho wake Mtakatifu katika wakati huu mgumu. Hatutakiwi kuwa waoga kwa kunywea mbele ya uovu. Tunatakiwa kuing’ang’ania imani. Tunatakiwa kuwa imara!)

III.  Mbingu Mpya na Nchi Mpya

A.  Soma Ufunuo 21:1. Kitu gani kimeitokea nchi (dunia) na pambano kati ya wema na uovu? (Mungu ameshinda. Anafanya kila kitu kuwa kipya.)

1.  Kwa nini Mungu ahitaji mbingu mpya? (Baadhi ya watu wanasema hii inarejelea tu mazingira mapya. Nina mashaka juu ya tafsiri hiyo.)

B.  Soma Ufunuo 21:2-3. Tunafahamu kuwa jambo gani limeitokea nchi ya kale? (Mungu amehamishia makao yake ya msingi kwenye nchi mpya. Ameishusha Yerusalemu Mpya katika nchi mpya. Ninadhani matukio hayo mawili yanatosha kuelezea mabadiliko makubwa katika mbingu ya kale.)

C.  Soma Ufunuo 21:4. Ni kitu gani usichokipenda sana kuhusu dunia yetu ya sasa? (Kifo? Ugonjwa? Maumivu? Masikitiko? Yote haya yametoweka milele.)

D.  Soma Ufunuo 21:7. Je, wewe ni mshindi? Je, umefanya uchaguzi wa kumtegemea Mungu badala ya kuitegemea falsafa ya mwanadamu? (Ikiwa ndivyo, nchi mpya ndio urithi wako na Mungu ndiye Baba yako!)

E.  Rafiki, je, umejiandaa kwa pambano la mwisho kati ya wema na uovu? Je, umezama kwenye neno la Mungu kiasi kwamba utayaelewa kwa usahihi masuala ya wakati wa mwisho? Je, utaongozwa na Roho Mtakatifu kuwa mwaminifu na thabiti dhidi ya uovu? Kuelewa kilicho sahihi? Ikiwa ndivyo, kuna mustakabali mzuri ajabu unaokusubiria. Utakaa pamoja na Mungu! Je, utadhamiria, sasa hivi, kujitayarisha?

IV.  Juma lijalo tunaanza somo la kitabu cha Agano Jipya cha Waefeso.