Somo la 6: Saa ya Hukumu Yake

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 14, Danieli 8 & 9, Waebrania 8 & 9
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
6

Somo la 6: Saa ya Hukumu Yake

(Ufunuo 14, Danieli 8 & 9, Waebrania 8 & 9)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Tulipoanza somo hili tulijifunza kutoka Ufunuo 1:1 kwamba lengo kuu la Ufunuo ni kuwaandaa Wakristo na mustakabali wao ujao. Mara zote Mungu amekuwa akijishughulisha kutuambia kile anachokiwazia. Tunaliona hilo katika Mwanzo 3:15 Mungu anapotuambia kuwa kwenye pambano kati ya wema na uovu “atakiponda kichwa” cha nyoka kilichotuingiza dhambini. Juma hili tunajifunza unabii unaotupatia taarifa mahsusi kuhusu kushindwa kwa dhambi. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Maswali, Maswali

A.  Soma Danieli 8:11-12. Danieli ameona maono ya wanyama wakipigana na pembe zao zikikua. Kisha anapokea taarifa hii kuhusu hekalu kuangushwa. Kama ungekuwa Danieli, ungefikiria nini? (Kumbuka kwamba Danieli alichukuliwa mateka baada ya kuharibiwa kwa hekalu Yerusalemu. Hii ingeonekana kama habari ya kizamani kwake.)

B.  Soma Danieli 8:13. Je, Danieli anasikiliza mazungumzo ya siri (yasiyomhusu)?

1.  Je, mazungumzo haya ni jambo linalomvutia Danieli? (Ni jambo la kuvutia sana kwa sababu linahusu kipindi cha uharibifu kitaendelea “hata lini.” Hilo liyanaathiri maisha ya Danieli moja kwa moja.)

C.  Soma Danieli 8:14. Sasa tunajua kama suala hili lilidhamiriwa kuwa mazungumzo ya siri. Jibu ni lipi? (Hayakuwa mazungumzo ya siri kwa sababu jibu linatolewa moja kwa moja kwa Danieli.)

1.  Je, hii ni habari njema? (Ni habari za kufurahisha kwa sababu zinamhabarisha Danieli kuwa hekalu (ambalo ataliamini ni hekalu lililopo Yerusalemu) litarejeshwa. Taifa lake litafanywa upya. Huenda ataweza kwenda nyumbani.)

D.  Soma Danieli 8:15-16. Je, Danieli anayaelewa maono haya? (Hapana. Anataka kuelewa lakini haelewi.)

1.  Nani anaombwa kumsaidia Danieli? (Malaika Gabrieli anaambia kumsaidia Danieli kuelewa.)

E.  Soma Danieli 8:17. Kuna tatizo gani kufundishwa na Gabrieli? (Ni mtu wa kuogofya. Utakumbuka majuma mawili yaliyopita tulijadili inamaanisha nini “kumcha Mungu.” Hoja mojawapo iliyo upande wa hofu halisi (kutetemeka) ni kwamba mwitiko kamili wa mwanadamu baada ya kumwona malaika ni kuogopa.)

1.  Licha ya woga huu, Danieli anaandika maelekezo ya Gabrieli. Ujumbe huu unahusu nini? Je, unahusu kujenga upya hekalu katika kipindi cha uhai wa Daneli? (Danieli hajui kuwa hekalu litaangamizwa mara mbili. Gabrieli anasema kuwa hii inahusu “wakati wa mwisho.” Isipokuwa kama dunia ingekoma mapema zaidi, Danieli asingeelewa ujumbe.)

F.  Soma Danieli 8:18-19. Jambo la kushangaza hili! Danieli analala wakati akiwa anaogopa? Unadhani kitu gani hasa kilitokea? (Danieli alizimia. Anazidiwa nguvu na ujumbe na uwapo wa Gabrieli.)

1.  Gabrieli ana nguvu kiasi gani? (Anaweza kukurejeshea uelewa kwa mguso tu.)

2.  Gabrieli anarudia ujumbe gani? (Kipindi fulani cha muda – hii inahusu mwisho wa dunia.)

G.  Soma Danieli 8:26-27. Je, Danieli anahitaji mguso mwingine kutoka kwa Gabrieli? (Anamakinika, lakini anaumwa.)

1.  Unadhani kwa nini Danieli anaumwa? (Ujumbe umemzidia nguvu. Hauelewi, licha ya juhudi bora kabisa za Gabrieli. Danieli anauona ujumbe huu kuwa ni wa kuogofya.)

a.  Unadhani Danieli anauona ujumbe huu kuwa wa kuogofya kwa sababu hekalu halitajengwa upya hadi wakati wa mwisho? (Bila shaka Danieli anaifikiria hali yake na kuangamizwa kwa hekalu lake. Nitaugua kama nikijua kuwa halitajengwa upya kwa kipindi kirefu, kimsingi, hadi mwisho wa dunia ufike.)

II  Majibu

A.  Soma Danieli 9:17-20. Danieli anaomba juu ya nini? (Mada ile ile. Anamwomba Mungu ajenge upya hekalu mapema. Hataki ucheleweshaji ambao Gabrieli alikuwa anamwambia.)

B.  Soma Danieli 9:20-21. Je, Gabrieli aliambiwa ajaribu tena? (Naam, kwa dhahiri kabisa!)

1.  Hebu tuingize jambo binafsi. Je, kuna nyakati ambazo huelewi Mungu anafanya nini? Pale unapodhani kuwa anatakiwa kuchukua hatua haraka na hafanyi hivyo? Je, huku kurejea kwa Gabrieli kunatufundisha nini? (Mungu anajali uelewa na mtazamo wetu. Anataka kutuhakikishia.)

C.  Soma Danieli 9:23. Kwa nini Gabrieli anakuja kwa ajili ya ufafanuzi? (Danieli “anapendwa sana” na mbingu.)

D.  Soma Danieli 9:24. Nini kinatokea katika kipindi hicho cha miaka sabini? (Mambo mengi. Ya muhimu sana ni upatanisho wa dhambi na kuleta haki ya milele.)

E.  Soma Danieli 9:25. Kipengele cha kwanza cha habari njema kwa Danieli ni kipi? (Kwamba hekalu lake litajengwa upya.)

1.  Je, haya ni maono yaliyopo kwenye jibu la anachokijali Danieli kuhusu hekalu lake kuwa chini ya maangamizi? (Huu ni ujumbe mkubwa zaidi. Hebu ngoja tujaribu kuuelewa.)

a.  Kitu gani kipo kwenye kiini cha ujumbe mkubwa? (Ujio wa “mtiwa mafuta,” “Mwana Mfalme.”)

III.  Ujumbe Mkubwa – Majuma 70

A.  Soma Danieli 9:26-27. Utaona kwamba zimetajwa nyakati tatu – majuma 62, majuma 7 na juma 1. Kwa pamoja jumla yake ni majuma 70.)

1.  Panaweza kuwepo kwa ukwepaji wa suala la msingi kuhusu tarehe sahihi, lakini kihistoria Wakristo waamini wa Biblia waliweka tangazo la kurejesha Hekalu alilojihusisha nalo Danieli katika kipindi kinachokadiriwa kuwa mwaka 457 K.K. Ukijumlisha majuma 62 na majuma 7 (majuma 69), na kuelewa kwamba siku moja ni sawa na mwaka mmoja, unafika mwaka 27 B.K. Huo ndio mwaka aliobatizwa Yesu na Yohana na kuanza kazi yake ya utume.)

a.  Hii inatufundisha nini kuhusu uaminikaji wa Biblia?  Hii inatufundisha nini kuhusu ukweli kwamba kitabu cha Ufunuo kiliandikwa ili kuwaambia wafuasi wa Mungu kile kitakachotokea?

B.  Angalia tena Danieli 9:26-27 na safari hii jikite kwenye juma moja na “nusu ya juma.” Hii inaendanaje na huduma ya Yesu hapa duniani? (Yesu alitoa huduma kwa muda wa miaka mitatu na nusu kabla hajasulubiwa. Angalia lugha ya “Mtiwa mafuta atakatiliwa mbali.” Katika hili tunaona kwamba kusulubiwa kwa Yesu pia ni mada ya maono haya yaliyotolewa kwa Danieli.)

1.  Vipi kuhusu kauli ya kuangamizwa kwa “mji na patakatifu?” (Hilo pia lilitokea baada ya kusulubiwa kwa Yesu.)

IV.  Ujumbe Mkubwa Zaidi wa Mbingu – Siku 2300

A.  Rejea nyuma na usome Danieli 8:14 na Danieli 8:17. Gabrieli anapokuja mara ya pili kufafanua kile tulichojifunza hivi punde, hatoi mapitio kuhusu “wakati wa mwiaho” na unabii mrefu wa siku 2,300. Kwa nini? (Danieli hakuuelewa na Danieli 8:26 inasema “kuyafunika maono.”)

1.  Jambo gani linatabiriwa kutokea mwisho wa siku 2,300? (“Ndipo patakatifu patakapotakaswa.”)

a.  Kihistoria Wakristo wameyaelewa majuma 70 (siku 490), lakini kuna kutokubaliana kwenye kipindi kirefu cha siku 2,300. Wengi wanadhani siku 2,300 ni siku halisi na zinahusiana na kiongozi wa kijeshi ambaye, muda mrefu kabla Yesu hajaja, alilinajisi hekalu la Kiyahudi kwa kutoa kafara ya nguruwe ndani yake. Je, muda unaobashiriwa uko sahihi kwa nadharia hiyo? (Hapana. Gabrieli alisema (Danieli 8:17) kwamba maono yalihusiana na wakati wa mwisho.)

b.  Hebu tuendelee na dhana ya kweli hadi kufikia hapa kwamba siku moja ni sawa na mwaka mmoja. Soma tena Danieli 9:26. Hii inatuambia kuwa miaka mingi kabla ya kipindi cha siku 2,300 hakijaisha hekalu litaangamizwa tena. Je, tunapaswa, kama ilivyokuwa kwa Danieli, tutangaze kuwa hatulielewi jambo hili? Kwamba hekalu lililoangamizwa haliwezi kurejeshwa, au linaweza kurejeshwa? Kama linaweza, kwa nini tulihitaji baada ya Yesu kufa kama sadaka yetu?

B.  Soma Waebrania 8:1-2, na Waebrania 8:5-6. Hii inatuambia nini kuhusu hekalu jingine? Na liko wapi? (Hekalu la duniani lilijengwa kwa mfano wa hekalu la mbingunu. Kitabu cha Waebrania kinatuambia kuwa baada ya hekalu la duniani kuangamizwa, Yesu anatoa huduma kwetu katika hekalu la mbinguni.)

C.  Soma Waebrania 9:8 na Waebrania 11-12. Waebrania inafunguaje maana ya unabii wa siku 2,300? (“Urejeshaji” huu upo mbinguni. Yesu anatoa huduma kwa ajili yetu katika hekalu la mbinguni.)

D.  Rafiki, hii ni habari njema! Biblia inaaminika katika kutuambia Yesu angekuja lini, kukaa duniani, na kufa kwa ajili yetu. Na inatupatia habari njema sana kwamba Mwokozi wetu anafanya kazi kwa niaba yetu mbinguni sasa hivi! Kwa nini usimwombe aingilie kati kwa niaba yako?

IV.  Juma lijalo: Kumwabudu Muumbaji.