Somo la 7: Tumaini Lisilotetereka 

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ayubu 1, 31, 38 & 40, Habakuki, Waebrania 12
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
7

Somo la 7: Tumaini Lisilotetereka 

(Ayubu 1, 31, 38 & 40, Habakuki, Waebrania 12) 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza. 

Utangulizi: Je, unapata ugumu kumwelewa Mungu? Tumejifunza katika masomo yaliyopita kwenye mfululizo wa masomo haya kwamba sababu ya msingi ya sisi kupitia mateso ni kwamba Shetani anatuletea matatizo maishani mwetu kwa matumaini kwamba tutamkataa Mungu. Shetani anataka kusababisha utengano na Mungu. Kama humfahamu mtu, je, hiyo haikufanyi umwamini kidogo? Uwezekano mkubwa kwa watu wengi ni jibu la “ndiyo.” Kama hilo ni kweli, je, Mungu anatutaka tumwelewe? Mungu anajilinganisha na baba mwenye upendo. Kama una baba mwenye upendo, je, hiyo inakusaidia kumwelewa Mungu vizuri zaidi? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi! 

I.  Ayubu 

A.  Soma Ayubu 1:1 na Ayubu 1:8-11. Tulijifunza vifungu hivi katika siku za hivi karibuni, kwa hiyo haya ni mapitio. Kwa nini Ayubu alipitia uzoefu mbaya kabisa wa mateso uliofuatia? (Sio kwa sababu ya kasoro yoyote ya kitabia. Ayubu alikuwa mfano wa mtumishi mwaminifu wa Mungu. Shetani alitaka kumtenganisha Ayubu na Mungu.) 

B.  Soma Ayubu 31:35-37. Ayubu anamwomba Mungu ampatie nini? (Mashtaka yanayoonesha kitu gani amekosea.) 

1.  Ayubu atafanya nini na kauli hiyo ya mashtaka? (“Angeelezea hesabu” ya matendo yake. Angejitetea kwa msingi kwamba hajafanya jambo lolote baya ambalo lingestahili aina hii ya mateso.) 

a.  Je, Ayubu anadai kuwa Mungu hatendi haki? Kwamba hakutendewa haki? (Nadhani hilo ndilo hitimisho lenye mantiki. Ayubu anataka mashtaka ambapo ataweza kujitetea mwenyewe.) 

C.  Soma Ayubu 38:1-3. Je, Mungu ameamua kumpa Ayubu kesi ambayo anaitaka sana? (Kama ningekuwa Ayubu ningeyafurahia maneno haya kutoka kwa Mungu. Utakumbuka kwamba hapo kabla hakuweza hata kumpata Mungu ili aweze kudai mashtaka yake.) 

D.  Soma Ayubu 38:4-11. Hii ni kesi ya namna gani? Je, Ayubu anaulizwa juu ya matendo yake? 

1.  Kwa nini matendo ya Mungu ni ya msingi? Je, Mungu ameshtakiwa? 

E.  Mungu anaendelea na mfululizo wa maswali yake hadi sura ya 40 ya kitabu cha Ayubu. Soma Ayubu 40:1-2. Mungu anapouliza hili swali, je, anamuita Ayubu kuwa ni “mtafuta kasoro?” (Ndiyo. Mungu analiangalia jambo hili wakati Ayubu anapompa Mungu changamoto.) 

F.  Soma Ayubu 40:3-5. Ayubu anakuwa na mwitikio gani kwa Mungu anapobainisha kuwa Ayubu anampa changamoto? (Ayubu anasema kuwa atafunga kinywa chake! Hatampa tena Mungu changamoto.) 

G.  Kuanzia hapa Mungu anaendelea kuuliza mfululizo wa maswali lengo likiwa ni kuonesha kuwa Mungu ni Mungu na Ayubu si Mungu. Soma Ayubu 42:1-6. Unaweza kuelezeaje kwa ufupi jibu la Ayubu kwa Mungu? (Anakiri kwamba yeye ni mjinga. Hana uelewa. Ayubu anajichukia na kutubu.) 

H.  Soma Ayubu 42:10-11. Mungu anamfanyia Ayubu urejeshaji. Baada ya hapo marafiki wa Ayubu waliosema kuwa Ayubu alikuwa anateseka kwa sababu alikuwa mdhambi walimpa fedha. Je, hiyo ni ishara kwamba walitubu shutuma zao? (Ninadhani walikuwa wanaomba radhi kwa kutomsaidia Ayubu alipokuwa anateseka.) 

1.  Jiweke kwenye nafasi ya Ayubu. Unaelezeaje yale yaliyokutokea? (Ayubu hana cha kuelezea. Alichojifunza kutoka kwa Mungu ni kwamba Mungu ni Mungu na yeye si Mungu.) 

2.  Je, utahitimisha kutokana na jambo hili kwamba Mungu haeleweki wala hatabiriki? Kama tunadhani tunapaswa kumwelewa tutavunjwa matumaini? (Fungua macho yako! Kamwe Ayubu hakuona “taswira pana.” Kamwe hakujua kwa nini aliteseka. Lakini Mungu alitupatia kitabu cha Ayubu. Kinadhaniwa kuwa mojawapo ya vitabu vya zamani kabisa vya Biblia. Mungu anataka kila mmoja wetu kuona hasa kwa nini Ayubu aliteseka.) 

a.  Macho yako yakiwa yamefumbuliwa, unapaswa kuhitimisha nini kuhusu endapo Mungu anaeleweka na kutabirika? (Tunatakiwa kukubaliana kwenye msingi wa kwamba sisi ni wajinga tusio na ufahamu wa taswira pana. Tunatakiwa kumtumaini Mungu kwa sababu yeye ni Mungu na sisi si Mungu. Lakini, badala ya kufikiria kwamba Mungu ni fumbo la namna fulani kwamba kamwe hatuwezi kumwelewa wala kumtabiri, Mungu anatupatia kisa hiki ili kutufafanulia kile ninachokiona kama sababu kuu ya mateso – Shetani alitaka kumtenganisha Ayubu na Mungu. Ayubu alisalia kuwa mwaminifu, jambo lililomruhusu Mungu kutumia hali ya Ayubu kujipatia utukufu na uelewa kwa kila mfuasi wa Mungu kuanzia kipindi hicho.) 

II.  Habakuki  

A.  Soma Habakuki 1:1-2. Lalamiko la kwanza la Habakuki kwa Mungu ni lipi? (Kwamba Mungu hamsikilizi.) 

B.  Angalia nusu ya mwisho ya Habakuki 1:2. Malalamiko yake yamebadilikaje? (Sasa anaamini kuwa Mungu anasikiliza, tatizo ni kwamba Mungu hamwokoi.) 

C.  Soma Habakuki 1:3-4. Habakuki anaelezea kwa nini anahitaji Mungu aingilie kati. Sababu hiyo ni ipi? (Sheria ya nchi haifanyi kazi. Haki haiwezi kupatikana katika mahakama za nyumbani. Anahitaji haki ya mbinguni. Tatizo ni kwamba Mungu anafahamu juu ya uangamivu na machafuko lakini hafanyi chochote.) 

D.  Soma Habakuki 1:5. Je, Mungu anasikiliza? Je, Mungu hafanyi jambo lolote? 

1.  Kwa nini Mungu anasema kuwa hajamshirikisha Habakuki kile anachokifanya? (Habakuki hataamini mpango kazi wa Mungu.) 

2.  Je, unaona mfanano katika mazingira ya Ayubu? 

E.  Soma Habakuki 1:6-7. Hawa Wakaldayo waletao haki ni akina nani? (Ni watu wabaya. Wao si watu wa Mungu. Wao ni watu wa Babeli.) 

F.  Soma Habakuki 1:12. Je, hii ndio sababu Mungu anasema kuwa Habakuki hatauamini mpango wa Mungu? (Watu wabaya wataivamia Yuda.) 

1.  Kwa nini Habakuki anayaelezea mateso ya Yuda yajayo? (Anaiita “hukumu” na “kuadhibisha.”) 

a.  Je, Mungu anawatakasa watu wake kwa mateso? 

G.  Soma Habakuki 1:13. Je, Mungu alikuwa sahihi kusema kwamba Habakuki asingeamini mpango wa Mungu? (Ndiyo.  Habakuki anataka kujua ni kwa jinsi gani Mungu mkamilifu atawatumia watu waovu kuwaadhibu watu wa Yuda. Watu wa Babeli ni wabaya zaidi kuliko mambo yanayoendelea katika Yuda! Habakuki anauliza, “hili linafaaje?) 

H.  Soma Habakuki 2:2-4. Mungu anamwambia Habakuki aandike kile ambacho Mungu amesema kitakuwa suluhisho kwa vitendo visivyo vya haki katika nchi. Mungu anataka watu wake wafanye nini? (Katika nyakati za mateso tunapaswa kuishi kwa imani kwa Mungu. Tunapaswa kumtumaini Mungu.) 

1.  Hilo linaendanaje na mijadala yetu ya nyuma kuhusu mateso? (Shetani huleta mateso ili kututenganisha na Mungu. Mungu anasema “ishike imani.” Usijiingize kwenye malengo ya Shetani.) 

I.  Hebu twende mwishoni mwa kitabu cha Habakuki na tuone jinsi mambo yote haya yanavyotendeka. Soma Habakuki 3:17-19. Utakumbuka Hababuki alianza kwa kumuuliza Mungu maswali. Hatimaye mtazamo wake ni upi? (Licha ya mambo kwenda mrama, Habakuki anaishika imani kwa kumtumaini na kumsifu Mungu.) 

III.  Nidhamu 

A.  Soma Waebrania 12:1-2. Hili wingu kubwa la mashahidi ni nani? (Hii inafuatia baada ya Waebrania 11, sura ya imani. Inawaelezea wafuasi wa Mungu ambao hawakuzipokea ahadi za Mungu kikamilifu wakingali hai. Waliitazamia mbingu. Wao ni mashahidi wetu.) 

B.  Soma Waebrania 12:3-4. Tunatakiwa tumfikirie nani tunapopitia mateso? (Yesu. Mwandishi wa Waebrania anatuambia kuwa tofauti na Yesu, hatujafa kifo kichungu kutokana na mateso yetu.) 

1.  Utaona kwamba kifungu kinasema kuwa tunapambana dhidi ya dhambi. Kifungu kinatuambia kuwa nani anayeleta mateso? (Shetani.) 

C.  Soma Waebrania 12:5-6. Inaonekana kama hatimaye tumefikia ile dhana ambayo nimekuwa nikiikana – kwamba mateso hutoka kwa Mungu ili kututakasa. Je, hivyo ndivyo unavyoelewa vifungu vya 5-6? 

1.  Utaona kwamba mwandishi wa Waebrania ameyalinganisha mateso yetu na yale ya Yesu. Je, Yesu alitakaswa kwa mateso? 

D.  Soma Ayubu 5:17. Je, hii pia inatuambia kuwa tunaadhibiwa na Mungu ili kuturekebisha mwenendo? 

1.  Nani anayezungumza katika Ayubu 5:17? (Ni Elifazi (angalia Ayubu 4:1), mmojawapo wa “marafiki” wa Ayubu ambaye anajenga hoja kwamba Ayubu anatakiwa kutubu.)  

a.  Je, Elifazi alikuwa sahihi? (Tunafahamu tangu mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu kwamba hakuwa na haja ya kutubu.) 

E.  Soma Ayubu 42:7. Hebu subiri kidogo! Mungu anasema nini juu ya kile alichokisema Elifazi kwa Ayubu? (Mungu anamshutumu Elifazi kwa kuwa “humkunena yaliyo sawa katika habari zangu.”) 

1.  Unaweza kuelezea kwa nini Elifazi anaonywa kwa kunena jambo lile lile ambalo mwandishi wa Waebrania anatuambia – kwamba mateso huja ili kututakasa? 

F.  Kwa dhahiri, tunatakiwa kulichimbua jambo hili zaidi. Soma Mithali 3:11-12. Hiki ndicho chanzo cha Waebrania 12:5-6. Tunalifahamu hilo kwa sababu Waebrania 12:5 kwa umahsusi inarejelea “ushawishi” wa awali. Unadhani wazazi wenye upendo watawasababishia mateso watoto wao? (Kwa kuwa Waebrania 12 inanukuu Mithali 3, kimantiki kauli ya msingi inatoa ukomo kwa Waebrania 12 (it is logically limited by the original statement.) Hakuna baba au mama mwenye upendo atakayetekeleza kwa mtoto wake kile kilichomtokea Ayubu au Yesu. Waebrania haiwezi kuwa inazungumzia aina hiyo ya mateso au baadhi ya mateso yaliyoelezewa katika Waebrania 11. Badala yake, tunaangalia namna Amri Kumi zinavyofanya kazi. Mungu anasema “Usifanye hivi,” ili maisha yetu yawe mazuri. Tukipuuzia kile anachokisema Mungu, basi tunaingia kwenye matatizo na tunateseka. Hiyo inaendana na jinsi baba zetu wenye upendo wanavyoenenda.) 

G.  Soma Waebrania 12:11-13. Je, umewahi kuwa na tatizo katika utembeaji wako? Usipoutibu mguu wako, hali inakuwa mbaya zaidi, sawa? Na, mguu huo huathiri viungo vingine vya mwili. Hii inatuambia nini kuhusu lengo la Mungu kwetu? (Mungu anasema kuwa tembea kwa usahihi ili hali yako isiwe mbaya. Usiongezee na kukuza tatizo.) 

H.  Rafiki, ni matumaini yangu unakubaliana kwamba Biblia inafundisha kuwa mateso hutokana na Shetani na dhambi. Lengo lake ni kudhuru, sio kuboresha, uhusiano wetu na Mungu. Hata hivyo, kuna fundisho la asili linalotokana na kutomtii Mungu. Tunatakaswa (natumaini hivyo) ili kuelewa kwamba tusingependa kutenda kosa hilo tena. Je, utauchukua huu mtazamo chanya wa Mungu? 

IV.  Juma lijalo: Kumwona Yeye Asiyeonekana.