Somo la 6: Toka Ufidhuli Hadi Uangamivu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Sura ya 5 ya kitabu cha Danieli ina maneno ya utangulizi mazuri sana. Mfalme Nebukadreza alifariki mwaka 563 K.K. Maelezo ya sura ya 5 yanajitokeza takriban miaka 25 baada ya kifo chake. Mfalme Nabonidus ndio sasa yuko madarakani, lakini anashiriki mamlaka yake na kijana wake mwovu, Belshaza. Waajemi, wakiongozwa na Mfalme Koreshi, wanaishambulia Babeli na wanayashinda majeshi yanayoongozwa na Mfalme Nabonidus. Mfalme Nabonidus analihamishia jeshi kuu la Babeli Borsippa, na Mfalme Koreshi anaelekea katika mji wa Babeli na kuuzunguka. Ubashiri wangu ni kwamba kabla Koreshi hajafika Babeli, maafisa wengi waliukimbilia mji kwa ajili ya usalama wao. Mji wa Babeli ulikuwa na ulinzi mkali kwa kuzungushiwa ukuta mnene na ulikuwa na chakula cha kutosha kwa miaka 20. Mazingira ya somo letu la leo ni kwamba Makamu wa Mfalme Belshaza yumo kwenye eneo la salama ndani ya kuta za Babeli, Mfalme Koreshi na Waajemi wanauzunguka mji, na jeshi kuu la Babeli linaelekea kulamba vidonda vyake. Hebu tuzame kwenye kitabu cha Danieli sura ya 5!
- Karamu
-
- Soma Danieli 5:1. Mfalme Belshaza alikuwa anafikiria nini? Mji umezungukwa na majeshi ya adui na yeye anafanya karamu? (Inawezekana ni mkakati wa kuwatia moyo viongozi wa mji – hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, maisha yataendelea kama kawaida, tuko salama ndani ya hizi kuta. Huenda kwa kujisikia kuwa salama ndani ya kuta za mji, na kwa kuwa ni “mtu wa karamu’ na aliye mnyonge, alidhani kuwa “kwa nini nisiandae karamu?”)
-
- Soma Danieli 5:2-3. Huu ni uchaguzi wa kufurahisha wa bilauri. Tulipomwona kwa mara ya mwisho “baba” Nebukadreza, alimkiri Mungu wa kweli wa mbinguni. Kwa nini mjukuu wake anavichagua vyombo hivi kwa ajili ya karamu? (Soma sehemu ya kwanza ya Danieli 5:23. Inatuhabarisha fikra ya Nebukadreza. Inasema kuwa Nebukadreza “alijiinua juu ya Bwana wa mbingu.” Haya ni makusudi. Huu ni uasi. Hakuchagua bilauri hizi za dhahabu kwa bahati.)
-
-
- Ikiwa hili si jambo la kupangwa, kwa nini kumwasi Mungu? (Nadhani inaenda mbali zaidi hadi kwenye unabii wa sanamu – Mungu alisema kwamba Babeli itashindwa na ufalme mwingine. Belshaza anaudharau unabii.)
-
-
- Soma Danieli 5:4. Jambo gani linadhihirishwa na uongozi wa Babeli? (Miungu yao ilimshinda “Mungu wa vyombo [bilauri]” – Mungu ambaye vyombo vya dhahabu vilimsherehekea.)
- Mharibifu wa Karamu
-
- Soma Danieli 5:5-6. Fikiria kwamba hujawahi kuangalia sinema. Ungekuwa na mwitiko gani baada ya kuona tukio kama hili? (Kwa Belshaza, lilikuwa jambo la kutisha sana.)
-
-
- Hii inazungumza nini kuhusu Belshaza? (Hakuwa mpiganaji, si mtu aliyekuwa na ujasiri mkubwa. Tunaelewa sababu ya Mfalme Nabonidus kuwa katika uwanja wa vita wakati Belshaza akiwa “salama” ndani ya kuta za mji.)
-
-
-
- Je, tabia ya uoga ya Belshaza inafanya kumwasi kwake Mungu kuwa jambo la kuchukiza zaidi?
-
-
- Soma Danieli 5:7-8. Utawapatia alama gani kiutendaji hawa wenye hekima? Mara tatu tumeliona kundi hili likipewa kazi ya kutafsiri jambo, na kamwe hawakuweza!
-
-
- Belshaza anatoa zawadi ya nafasi gani? (Nafasi inayofuata chini yake.)
-
-
-
- Utaona kifungu kinasema kuwa “wakaingia wenye hekima wote wa mfalme.” Je, hii inamaanisha kuwa Danieli si miongoni tena mwa wenye hekima? (Hicho ndicho kinachoashiriwa hapa. Ukweli kwamba Danieli alikuwa akishikilia nafasi “inayofuata baada ya mfalme” pia inaashiria kwamba hashikilii tena nafasi muhimu.)
-
-
- Soma Danieli 5:9. Kwa nini Belshaza aliogopa zaidi? (Kwa mara nyingine, hii inaonesha udhaifu wake. Anawategemea watu wengine. Washauri wake wanapokuwa hawafahamu jambo, anapata uoga zaidi. Unaweza kuwa na uhakika kwamba Nebukadreza asingejibu kwa namna hii.)
-
- Soma Danieli 5:10. Maoni ya watu mbalimbali wanaamini kuwa malkia huyu ni mjane wa Nebukadreza. Unadhani anamchukuliaje mjukuu wake kwa kumlinganisha na mumewe, Nebukadreza? (Huenda anafikiria kile tunachokifikiria – hana uti. Anakuja kuweka chuma cha pua kwenye uti wake.)
- Danieli Anaingia
-
- Soma Danieli 5:11-12. Je, hivi ndivyo ambavyo Danieli angependa kukumbukwa? (Hapana! Soma Danieli 4:8-9. Hivi ndivyo ambavyo Nebukadreza alimwelezea Danieli kabla hajakiri mamlaka ya juu kabisa ya Mungu wa mbinguni. Mjane wa Nebukadreza anamwelezea Danieli kwa namna iyo hiyo!)
-
-
- Je, ni jambo jema kwamba Mungu wa Mbinguni hajabainishwa? (Kama tuko sahihi kwenye nadharia yetu kwamba Belshaza anahusika kwenye tendo la uasi dhidi ya Mungu wa kweli, inaweza kuwa bora zaidi kwake kuchanganyikiwa kuhusu chanzo cha uwezo wa Danieli.)
-
-
- Soma Danieli 5:13 na uilinganishe na Danieli 5:11. Je, malkia alisema chochote kuhusu Danieli kuwa mtumwa? (Hapana. Malkia alisema kwamba Danieli alikuwa “mkuu wa wanajimu.”)
-
-
- Kwa nini Belshaza anamuuliza kwanza kama alikuwa mtumwa? (Ni mtu mbaya – na asiye mwerevu sana. Anamdhihaki mtu ambaye anahitaji sana msaada wake. Kuna uwezekano mkubwa kwamba sasa anatambua kuwa Danieli anamwabudu Mungu wa kweli wa Mbinguni.)
-
-
- Soma Danieli 5:14-16. Belshaza anahitaji taarifa hii kwa uchu mkubwa kiasi gani?
-
-
- Chukulia kwamba umepoteza kazi yako ya ngazi ya juu na sasa ulikuwa unarejeshewa kazi hiyo hapo baadaye. Ungesemaje? (Kuwa na cheo kinachofuata baada ya mfalme ndio iliyokuwa kazi ya zamani ya Danieli.)
-
-
- Soma Danieli 5:17. Je, Danieli anamdhihaki Belshaza? (Ndiyo! Aliyewahi kuwa mtumwa anamwambia “Huna chochote cha kunipatia ninachokithamini.”)
-
-
- Kwa nini hii ni kweli? (Danieli anafahamu ufalme unakoma sasa hivi.)
-
-
-
- Linganisha jibu la Danieli katika kifungu cha 17 na jibu lake katika Danieli 2:26-28. Kwa nini Danieli anashindwa kumpa Mungu utukufu kama alivyofanya kwa Nebukadreza? (Soma Mathayo 7:6. Belshaza alikuwa anakaribia kuuawa. Hakuwa na mustakabali. Danieli alimdharau. Babu yake aliushinda ulimwengu ambaye (hatimaye) alimkiri Mungu wa kweli. Belshaza hakufanya lolote, analewa wakati hatari inapokaribia, na anamdhihaki Mungu.)
-
-
- Soma Danieli 5:18-23. Je, hizi ni dhihaka zaidi? (Ndiyo!)
-
-
- Je, hii ni hatari? Mwanahistoria Xenophon aliandika kwamba Belshaza alimwua mmojawapo wa watu wake wenye cheo kikubwa “kwa sababu tu, katika mawindo, mtu huyo alimwua mnyama kabla yake.” Pia anaandika kwamba Belshaza alimhasi mmojawapo wa wafanyakazi wa mahakama kwa kuwa tu mmojawapo wa mahawara wake alisema kuwa mfanyakazi huyo ni mtanashati. Tukiachilia hayo, watu waliuawa na mwovu Belshaza kwa dhihaka (ambazo zilikuwa za kweli) ambazo Danieli alikuwa akizivurumisha sasa hivi.)
-
-
- Soma Danieli 5:24-28. Unakumbuka jinsi Danieli alivyoleta habari mbaya kwa Nebukadreza? (Soma Danieli 4:19. Hii inaendelea kuonesha dharau ya Danieli kwa Belshaza.)
-
-
- Nebukadreza alipewa nafasi kadhaa za upendeleo. Kwa nini Belshaza hapewi nafasi hata moja? (Soma tena Danieli 5:22. Danieli anasema kuwa Belshaza alifahamu historia ya babu yake na hakujifunza chochote.)
-
-
-
-
- Hiyo inatuambia nini sisi tulio na visa vyote hivi vya Biblia vya kuvitafakari?
-
-
-
- Soma Danieli 5:29. Je, huku ndiko kupandishwa cheo unakokutaka katika wakati kama huu?
-
-
- Kwa nini Belshaza anampandisha cheo Danieli licha ya dhihaka zote hizi? (Kwa sasa hata ana hofu zaidi. Ubashiri wangu ni kwamba anatumaini kuwa kwa namna fulani hivi Danieli au Mungu atamwokoa.)
-
-
- Soma Danieli 5:30-31 na Danieli 6:1-2. Linganisha matokeo kwa Belshaza na Danieli. Kwa nini Danieli, anayeshikilia nafasi ya juu kama hiyo, naye pia hafi usiku huo? (Nani anayeangalia mambo ya wanadamu? Hii inatuonesha kuwa tunatakiwa kujali zaidi mawazo ya Mungu juu yetu kuliko mawazo yetu juu ya wasimamizi wetu. Kwa kuwa Wamedi walichukua mamlaka usiku ule, inawezekana waliyaona maandishi yale na kubaini kuwa Danieli alibainisha kwamba Wamedi wangechukua mamlaka. Hiyo ilimfanya Danieli kuwa mshirika, na si adui.)
-
- Rafiki, inaonekana Danieli ameshushwa cheo katika uzee wake na anaonekana kutokuwa na umuhimu kwenye uongozi. Chochote kinachoweza kuwa kinatokea maisha ni mwako, bado Mungu yupo kwenye kiti chake cha enzi. Bado anadhibiti mambo ya wanadamu na anakujali. Je, utaukubali ukweli huu na kumtumaini Mungu bila kujali kitu chochote?
Juma lijalo: Toka Kwenye Tundu la Simba Hadi Tundu la Malaika.