Somo la 2: Kutoka Yerusalemu Hadi Babeli
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, wakati fulani maishani mwako maisha yamewahi kukubadilikia? Je, uliyachukuliaje mabadiliko hayo? Mwaka jana gari langu liligongwagongwa kwenye ajali kadhaa. Dereva ambaye hakuwa mwangalifu alinigonga, na mgongano ukasababisha mwendelezo wa mgongano na magari mengine. Ninamshukuru Mungu kwa kuwa nilitoka salama katika uharibifu uliosababishwa na ajali hiyo. Ajali hiyo ingeweza kusababisha matokeo tofauti na kubadili maisha yangu yote yaliyosalia. Somo letu juma hili linahusu tukio linalobadilisha kabisa maisha. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!
- Kutokutii
-
- Soma Danieli 1:1-2. Lengo muhimu kabisa la mji wa Yerusalemu ni lipi? (Ni kiini cha ibada ya Mungu wa kweli. Ndani ya mji huo kuna hekalu la Mungu lililoandaliwa na Mfalme Daudi na kujengwa na Mfalme Sulemani. Ndani ya hekalu mlikuwa na vyombo vya thamani vya ibada vilivyokuwepo tangu kipindi cha safari ya wana wa Israeli kutoka Misri.)
-
-
- Ungejisikiaje kama ungekuwa mfuasi wa Mungu wa kweli?
-
-
-
- Nani anayewajibika na janga hili? (Kifungu cha pili kinatuambia kuwa Mungu “aliingilia kati na kuokoa” hali hii.)
-
-
- Soma Yeremia 25:6-9. Kwa nini Mungu alichukua uamuzi huu? (Watu wake waliabudu miungu mingine. Walikataa kumsikiliza alipowaambia hasa kile kitakachotokea.)
- Majuto
-
- Soma Danieli 1:3-4. Hawa walikuwa ni vijana wa namna gani? (Wenye werevu mkubwa. Wale ambao mustakabali wao ulikuwa mzuri. Walitoka katika uzao wa uungwana, hadhi ya juu kabisa katika jamii.)
-
-
- Fikiria kwamba ulikuwa mmojawapo wa vijana hawa. Fikiria maeneo yote mazuri na ya kufurahisha uliyopendelea kwenda pale Yerusalemu. Matukio yote makubwa na tamaduni za kifamilia. Migahawa yote mizuri uipendayo na matukio yote mazuri ya michezo. Matumaini yako yote na njozi kwa ajili ya mustakabali wako. Sasa ungejisikiaje kutokana na ukweli kwamba yote hayo yametoweka na unakabiliana na mustakabali wako kama mtumwa kwa Mfalme wa Babeli? (Mambo yangeweza kuwa mabaya sana. Wanachaguliwa ili kushindania huduma ya kipekee sana.)
-
-
- Soma Danieli 1:5-7. Unaona matatizo gani kwa Danieli na marafiki wake kwenye hivi vifungu? (Wayahudi walikuwa na masharti maalum ya ulaji. Inawezekana chakula hiki kilitolewa kwa miungu. Badiliko la jina lilimaanisha uaminifu na utiifu mpya.)
-
-
- Tuchukulie kwamba taifa lako limechukuliwa na taifa jingine unalolichukia. Ungejisikiaje kwa jina lako kubadilishwa ili kuakisi taifa lililokuchukua utumwani?
-
-
- Hebu tujikite kwenye Danieli 1:7 na ufikirie badiliko la majina kwa undani zaidi. Hebu niambie ikiwa utapinga kuitwa kwa majina haya mapya:
-
-
- Danieli “Mungu mwamuzi wangu,” lilibadilishwa na kuwa Belteshaza “Mwana mfalme wa Beli.” Beli akiwa mungu mkuu wa Babeli.
-
-
-
- Hanania “ambaye Yehova amempa upendeleo,” lilibadilishwa na kuwa Shadraka “aliyeangaziwa na mungu Jua.”
-
-
-
- Mishaeli “anayelinganishwa na Mungu,” lilibadilishwa na kuwa Meshaki “Mnyenyekevu mbele za mungu wangu.”
-
-
-
- Azaria “Yehova amesaidia,” lilibadilishwa na kuwa Abednego “Mtumishi wa Nebo.” Nebo alikuwa mwana wa Beli.
-
-
-
- Unadhani lengo la badiliko la majina haya ni lipi?
-
- Changamoto
-
- Soma Danieli 1:8. Utakumbuka hapo awali tulikisia matatizo yaliyotokana na ulaji wa chakula cha kifalme. Danieli anaona tatizo gani? (Anasema kuwa “kitawanajisi.” Wanajali sana suala la kula nyama isiyo safi (Mambo ya Walawi 11), na nyama isiyoandaliwa vizuri (Mambo ya Walawi 17:10-14), na chakula na kinywaji kilichotolewa kwa ajili ya miungu ya kipagani. (Kutoka 34:15).)
-
-
- Je, hili lilipaswa kuwa suala zito? Je, Yesu hasemi (Mathayo 15:11) kwamba kitokacho kinywani mwa mtu ndicho kinachomnajisi, na si kiingiacho kinywani? (Soma Ezekieli 4:13. Mungu alitabiri kwamba sehemu ya hukumu yake dhidi ya watu wake itakuwa hivyo kwa kuwa kama wakimbizi watakula chakula kilicho najisi. Danieli aliamini kuwa hili lilikuwa jaribu la uaminifu wake kwa Mungu.)
-
-
- Soma Danieli 1:9-10. Afisa mwenye jukumu la kuwapa chakula Danieli na marafiki wake ana wasiwasi gani? (Hana wasiwasi juu ya suala la kidini linalomhangaisha Danieli, bali ana wasiwasi kuhusu kupoteza kichwa chake ikiwa Danieli na marafiki wake wataonekana kuwa na afya mbaya.)
-
- Soma Danieli 1:11-13. Tafakari jinsi Danieli anavyojishughulisha na suala hili. Hajengi hoja juu ya suala la dhamiri: kwamba ulaji wa nyama utakiuka imani zao za kidini. Badala yake, anazungumzia wasiwasi wa yule afisa kwa kuandaa jaribio. Chukulia kwamba unakabiliana na changamoto kwenye imani zako za kidini kazini kwako. Tunajifunza nini kivitendo kutoka kwa Danieli? (Danieli hadai kwa nguvu au kwa uchokozi. Badala yake, anapendekeza jaribio la msingi ambalo halitaathiri lengo la afisa. Katika suala la biashara au la kikazi, unapaswa kubainisha imani zako za kidini, lakini pia unapaswa kupendekeza suluhisho.)
-
- Soma Danieli 1:14-16. Je, hii inaelezea faida ya kuwa mla mbogamboga (vegetarian)? (Nimekuwa mla mbogamboga kwa miaka 57. Ikiwa siku kumi zileleta tofauti kama hiyo, ningepaswa kuwa mtu mwenye uwezo kupita kiasi (superman) kwa sasa! Kura yangu inaegemea kwenye ukweli kwamba jambo hili lilihusisha mpango wa Mungu.)
-
- Soma Danieli 1:17. Kumbuka kwamba Danieli na marafiki wake hawakuwa wasomi pekee wa jamii ya Kiyahudi waliochukuliwa mateka. Hii inatupa fundisho gani? (Mungu anatutunuku kwa kuwa waaminifu.)
-
- Soma Danieli 10:2-3. Hii inatuambia nini kuhusu ulaji wa Danieli baadaye maishani mwake? (Anakula “chakula kitamu,” “nyama,” na anakunywa “divai.” Ukisoma sura yote (hususani Danieli 10:11) utaona kwamba Danieli bado unafurahia upendeleo wa Mungu.)
-
-
- Hii inawekaje bayana kile ambacho tumekuwa tukikijadili? (Ikiwa chakula si jambo linalohusika hapa, basi lazina itakuwa ni jinsi chakula kinavyoandaliwa na kukitoa kwa miungu ya kipagani. Hii inaweka bayana kwamba Mungu anatenda muujiza katika maisha ya hawa vijana wanne kutokana na uaminifu wao katika kumtumikia. Kwa umahsusi kabisa Mungu anayaingilia kati maisha yao.)
-
-
- Soma Danieli 1:18. Unadhani sasa afisa huyu anajisikiaje juu ya uhusiano wake na Danieli kwenye ombi lake la chakula? (Baraka za Mungu kwa Danieli zinabadilika na kuwa baraka kwa afisa huyu pia.)
- Mtihani wa Mwisho
-
- Soma Danieli 1:19. Kuna fundisho gani katika jambo hili kwa wale wanaotaka kufanikiwa katika taaluma zao?
-
-
- Mungu anabadilishaje msiba wa maisha ya Danieli na kuwa jambo chanya?
-
-
- Soma Danieli 1:20. Ni muhimu kiasi gani kwamba Danieli na marafiki wake waliwashinda wenye hekima wote wa Babeli?
-
-
- Tafakari kwa mapana yake. Taifa la Mungu limeshindwa na Babeli ya Kipagani. Hekalu la Mungu limeporwa na kuangamizwa. Ni kwa jinsi gani kwamba Mungu anamsaidia Danieli na marafiki wake kwenye hili jambo dogo kwenye huu mtihani wa mwisho wa kuhitimu kwa ajili ya huduma ya mfalme? (Mungu anawatafuta mashujaa. Anawatafuta wale walio waaminifu kwa kile kinachoweza kuonekana kuwa ni mambo madogo. Mungu ataonesha kwamba njia yake ni bora kwa kuwabariki wale walio waaminifu.)
-
-
- Soma Danieli 1:21. Kauli hii fupi inatuambia nini kuhusu taaluma ya Danieli alipokuwa Babeli? Ingawa Danieli aliendelea kuishi miongoni mwa Wapagani, ninahisi Babeli palikuwa mahali pazuri na pa kufurahisha kwa mtu kuishi.)
-
- Rafiki, je, ungependa kubarikiwa na Mungu? Je, ungependa kuwa bora mara kumi zaidi kuliko washindani wako? Kwa nini usidhamirie sasa hivi, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuwa mwaminifu kwa Mungu katika mambo yote?
- Juma lijalo: Kutoka Fumbo Hadi Ufunuo.