Somo la 2: Nehemia
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unakabiliana na changamoto? Je, kuna jambo maishani mwako linalotakiwa kubadilishwa au kutatuliwa? Somo letu la leo linazungumzia juu ya Nehemia kupokea habari mbaya, anamgeukia Mungu kwa ajili ya msaada, na kisha kwa umahiri mkubwa anafanya kazi pamoja na Mungu katika kila hatua ili kutatua tatizo. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze mambo halisi kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku!
- Habari Mbaya
-
- Soma Nehemia 1:1. Hii inatupatia taarifa gani? (Tunapata kumfahamu mwandishi, na muda na mahali halisi ujumbe ulipoandikwa. Inaonekana ni mwezi Novemba-Desemba wa mwaka 444 K.K.)
-
- Soma Nehemia 1:2. Nani anayempelekea Nehemia taarifa? (Kaka yake na wengineo wanaokuja kutoka Yuda.)
-
-
- Je, utaiamini taarifa hii? (Hawa ni mashahidi na Nehemia yuko sahihi kabisa katika kutenga muda na mahali wa kunakili kwake. Hii ina alama za kuaminika.)
-
-
- Soma Nehemia 1:3. Masalia walioponea kwenda uhamishoni ni akina nani? (Utakumbuka juma lililopita kwamba waliokwenda uhamishoni walikaa huko kwa miaka 70. Hawa ni Wayahudi waliokuwa uhamishoni na ambao wamerejea Yerusalemu.)
-
-
- Habari ni ipi? (Ulinzi wa Yerusalemu upo kwenye maangamizi. Watu wapo kwenye “dhiki nyingi” na mashutumu.)
-
-
-
- Kwa nini hivyo? (Kwa sababu hawawezi kulinda hekalu – ambalo limejengwa upya. Bado mji wao upo kwenye uharibifu. Kuna jambo linalotakiwa kubadilishwa!)
-
- Kuzikabili Habari Mbaya
-
- Soma Nehemia 1:4. Unaichukuliaje (unaonyesha hisia gani) habari mbaya? Mwitiko wako wa kwanza ni upi? Unalinganishaje mwitiko huo na Nehemia?
-
- Soma Nehemia 1:5. Nehemia analiwekaje ombi (sala) lake? (Anaanza kwa kusifu.)
-
-
- Linganisha na Luka 11:1-2. Tunapaswa kuanzaje maombi yetu?
-
-
-
- Angalia tena Nehemia 1:5. Nehemia anabainisha jambo gani jingine mwanzoni mwa ombi lake? (Mungu anatunza ahadi zake kwa wale wanaompenda na kumtii.)
-
-
- Soma Nehemia 1:6-9. Nehemia anaonekana kama vile ni mwanasheria wa mkataba. Vigezo vya mkataba wake ni vipi? Nani aliyeuvunja mkataba?
-
-
- Ungejibuje ombi hilo kama ungekuwa Mungu?
-
-
- Soma Nehemia 1:10-11. Nehemia anampendekezea nini Mungu kuhusu mustakabali wa makubaliano haya?
-
-
- Sehemu ya mwisho kabisa ya kifungu hiki inatuambia nini? (Kwamba Nehemia alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Mfalme Artashasta. Hakuwa mtumishi, alikuwa “mtu mwenye hadhi na mtu muhimu” kwa mujibu wa maoni ya Jamieson-Fausset-Brown. Maoni ya watu wengi yanabainisha kwamba mnyweshaji wa mfalme aliaminika sana kwani sio tu kwamba alimwepusha mfalme kupewa sumu, bali pia alisikiliza masuala binafsi ya mfalme yakijadiliwa.)
-
- Ujasiri
-
- Soma Nehemia 2:1-2. Hii inatuambia nini kuhusu Mfalme Artashasta? (Sio mbinafsi sana kiasi cha kushindwa kuwazingatia wale wanaomzunguka. Mwitiko wake unaonesha kwamba ni mtu mwenye huruma – angalao kwa Nehemia.)
-
-
- Nehemia anaogopa nini?
-
-
-
- Soma Ufunuo 21:8. Kati ya hii orodha ya dhambi za kutisha, kwa nini “uoga” umeorodheshwa wa kwanza? Kwa nini hata ipo kwenye orodha ya dhambi?
-
-
- Soma Nehemia 2:3. Unaona mambo gani mawili kwenye jibu hili ambayo yanawasilisha jambo tunaloweza kujifunza tunapokuwa na uoga? (Kwanza, Nehemia, kama ilivyo kwa mfalme, hajizingatii mwenyewe. Jambo la kwanza analolisema ni jambo chanya kwa mfalme, hata kama ameambiwa kutoa taarifa inayomhusu. Pili, Nehemia anaonesha ujasiri, hata kama ana hofu. Anajitokeza mbele kwa kile anachoamini Mungu amekifunua kwa ajili yake.)
-
- Soma Nehemia 2:4. Nehemia anadhibitije hofu yake? (Ombi. Angalia tena Ufunuo 21:8. Mara baada ya “uoga” kuorodheshwa unafuatiwa na “wasioamini.” Tunakuwa waoga tunaposhindwa kumtumaini Mungu. Nehemia anamgeukia Mungu mara moja katika maombi kwa ajili ya hekima ya jinsi anavyopaswa kumjibu mfalme.)
-
- Soma Nehemia 2:5. Ombi la Nehemia ni refu kiasi gani? (Kwa dhahiri hili ni ombi la haraka kiakili. Tunapaswa kujifunza tabia ya kupeleka maombi kwa Mungu pale tunapohitaji msaada.)
-
-
- Hii inahusianaje na ombi la awali la Nehemia? (Kumbuka Nehemia 1:4-10 wakati alipojihusisha kwa kina na Mungu kuhusu mahitaji ya Yerusalemu. Soma Nehemia 1:11. Kwa umahsusi Nehemia aliomba kwa ajili ya kipindi hiki, kwa fursa hii. Sasa kwa kuwa ombi lake limejibiwa, Nehemia anapeleka ombi la haraka. Ninahisi sehemu ya ombi hilo ilikuwa ni “Asante Mungu! Tafadhali naomba unipatie hekima.”)
-
-
-
- Kwa nini Nehemia alijitolea kuongoza jambo hili? Mnyweshaji wa mfalme ana ujuzi gani kwa ajili ya mradi huo? (Huu ni uthibitisho wa ziada kwamba Nehemia hakuwa mtumishi tu. Alikuwa mtu mwenye hadhi ya juu kimamlaka.)
-
-
- Soma Nehemia 2:6. Jambo gani linabainishwa kwa kuzingatia uwepo wa malkia? (Maoni ya “The Bible Knowledge Commentary” yanabainisha kwamba haikuwa kawaida kwa malkia kujitokeza kwenye dhifa rasmi. Hiyo inaashiria kwamba Mungu alipangilia hivyo ili kwamba Nehemia awe na mazungumzo ya faragha na mfalme.)
-
-
- Umegundua kwamba Nehemia hakutaja mji mahsusi unaohusika? Kwa nini? (Utakumbuka kwamba hapo kabla Mfalme Artashasta aliamuru kusitishwa kwa ujenzi upya wa Yerusalemu. Nehemia hataki jibu la kwanza la mfalme liwe “Kwani sikuamuru kusitishwa kwa kazi pale?”)
-
-
-
- Swali la mfalme kuhusu hili litachukua muda gani linatuambia nini? (Kwamba anamthamini Nehemia na anataka kujua kuwa hatakuwepo kwa muda gani.)
-
-
- Soma Nehemia 2:7-8. Nehemia anatoa sifa kwa nani kutokana na mafanikio yake? (Mungu! Nehemia anamhusisha Mungu katika kila hatua.)
- Akili
-
- Nehemia 2:9-10 inatuambia kuwa maafisa wa mahali pale alipopita Nehemia “walihuzunika sana” kwamba mtu fulani alikuwa amekuja kuwasaidia Waisraeli. Soma Nehemia 2:11-15. Nehemia anafanya nini tunachopaswa kukitumia katika utatuzi wetu wa matatizo? (Anaweka mipango yake moyoni mwake hadi pale anapolielewa tatizo kwa ukamilifu. Tunapaswa kuepuka kutoa ahadi au kupendekeza suluhisho hadi pale tunapokuwa na uelewa kamili wa tatizo.)
-
-
- Unatabiri kwamba nini kingetokea endapo mara moja Nehemia angewaambia wale watu wenye uhasama kwamba alikwenda mahali pale kuujenga upya mji?
-
-
-
- Kuifanya mipango yake kuwa siri kwa kipindi fulani kulimruhusu kufanya nini? (Anaruhusiwa kubainisha kwa uhuru chanzo kamili cha tatizo.)
-
-
- Soma Nehemia 2:16-17. Fedheha ni ipi? (Mji wao umeharibiwa.)
-
- Soma Nehemia 2:18. Je, hivi ndivyo ambavyo ungedhihirisha mipango yako kwa watu wa Mungu? (Kwanza anaelezea baraka za Mungu, na kisha anaongezea kwamba mfalme anawaunga mkono.)
-
-
- Watu wanajibuje? (Wako pamoja!)
-
-
- Soma Nehemia 2:19. Kwa nini viongozi mahalia wanauliza kama huu ni uasi? (Hawamwamini Nehemia. Hii inathibitisha tatizo ambalo lingetokea endapo Nehemia angewaambia mpango wake mara moja.)
-
- Soma Nehemia 2:20. Je, hili ni jibu linalostahili kwa swali la endapo Nehemia anafanya uasi dhidi ya mfalme? (Hatimaye Nehemia anamtegemea Mungu!)
-
- Rafiki, unapokabiliana na matatizo makubwa, je, utafuata mfano wa Nehemia? Anaomba msaada wa Mungu. Fursa inapojitokeza, anajitokeza mbele kwa imani hata kama ana hofu. Kila hatua anayoichukua inahanikizwa na ombi. Nehemia pia anatumia akili yake. Yuko makini kwa jinsi anavyowasilisha tatizo kwa mfalme na jinsi anavyowasilisha suluhisho kwa watu wake. Kwa nini usimwombe Mungu, sasa hivi, kwa ajili ya imani na busara ya kufuata mfano wa Nehemia?
- Juma lijalo: Wito wa Mungu.