Uhuru Katika Kristo

(Wagalatia 4:1-15)
Swahili
Year: 
2011
Quarter: 
4
Lesson Number: 
11

Utangulizi: Uhuru ni kitu kizuri sana! Sote tunafahamu kuwa tunataka kuwa huru. Tunakuwa tunafahamu pale ambapo tunakuwa hatuna uhuru. Lakini je, hivi maana ya uhuru ni ipi hasa? Naweza kuwa na uhuru wa kumpiga ngumi puani jirani yangu. Lakini, hatadhani kwamba alikuwa huru kama angekuwa anapigwa ngumi na mimi mara kwa mara! Je, Paulo anamaanisha nini anapotuambia “kusimama imara” katika uhuru wetu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Wagalatia na kuona kile tunachoweza kujifunza!

  1. Simama Imara
    1. Soma Wagalatia 5:1. Je, ni nani aliyetupatia uhuru? (Yesu.)
      1. Unapomchukulia mwanzilishi wa uhuru wetu, je, hiyo inatuambia kitu fulani kuhusiana na asili ya uhuru wetu? Kwa mfano, je, Yesu angetupatia uhuru wa kuwadhuru wengine?
      2. Je, tuko huru na kitu gani? (Paulo anatuambia kuwa “mzigo” wa “kongwa la utumwa” umebebwa.)
    2. Soma Wagalatia 5:2-4. Je, hili kongwa la utumwa ni kitu gani? (Paulo anataja tohara, lakini pia anataja “torati yote.”)
      1. Kama sheria ni nakala ya tabia ya Mungu, kama ambavyo nimesikia mara kwa mara, je, yawezaje kuwa kongwa la utumwa? (Sidhani kama sheria/torati ndio “kongwa,” badala yake nadhani ni matakwa yanayotakiwa, kwamba tuitimize torati yote (tuishike sheria yote) ama tufe, hilo ndilo kongwa la utumwa. Ni kazi kubwa kutimiza kile kisichowezekana. Ni kama “Sisyphus” kusukuma mwamba kuelekea juu ya kilima.)Muhimu: “Sisyphus” ni mungu wa Kigiriki. Alihukumiwa kusukuma jiwe kubwa juu ya kilima maisha yake yote. Jiwe lenyewe ni kubwa kiasi kwamba hata haliwezi kuvingirika, lakini pamoja na yote hayo bado anapaswa kulisukuma ili liweze kwenda juu ya kilima.
      2. Paulo anaposema, “Sikilizeni maneno yangu,” je, unadhani anasema kitu gani? (Hili ni jambo la muhimu!)
      3. Je, kuhesabiwa haki kwa matendo ni “upinga Kristo?” (Ndiyo. Ndio maana mazungumzo haya ni ya muhimu sana. Kama unaamini kwamba matendo yako ni ya msingi sana kwa ajili ya wokovu wako, basi umemtupilia mbali Yesu na matendo yako yamechukua nafasi yake. Wewe ni mpinga Kristo.)
      4. Je, hakuna upande fulani hivi wa kati – kwamba ninaamini katika wokovu kwa imani lakini pia ninaamini kwamba matendo mema ni muhimu kwa ajili ya wokovu wangu? (Kama tunadhani kwamba matendo yetu yanatuhesabia haki, basi “tunatengwa” na Yesu. Hatuwezi kuidai neema kwa sababu “tumetanga mbali na neema.”)
  2. Utafakari Uhuru
    1. Soma Wagalatia 5:5-6. Kama kuhesabiwa haki kwa matendo kunapaswa kuepukwa, je, tunapaswa kutafuta kitu gani? (Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye wakala wa kutupatia haki.)
      1. Je, imani ni suala tu la utamkaji? (Paulo anarejea suala la “imani kujielezea yenyewe kupitia upendo.” Ni zaidi ya utamkaji tu.)
    2. Hili wazo la kuielezea imani yetu kupitia kwenye upendo linatuelekeza nyuma kwenye mjadala wetu kuhusu kile ambacho uhuru unamaanisha. Kama kweli ungekuwa huru, ungeweza kufanya jambo lolote, sawa? Hebu turukie mbele kidogo. Soma Wagalatia 5:19-21. Kama kweli ungekuwa huru, ungekuwa na uwezo wa kutenda mambo haya, sawa? (Paulo anatuambia kwamba hatuwezi kuyafanya mambo haya halafu tuurithi Ufalme wa Mungu. Lazima Paulo atakuwa na maana nyingine ya uhuru.)
    3. Fikiria maelezo fulani. Chukulia kwamba una mtoto mwenye umri wa miaka miwili. Halafu unamwambia mwanao, “ninakupa uhuru. Unaweza kufanya chochote utakacho. Lakini, kama unataka mwendelezo wa malezi na msaada wangu, basi unapaswa kushi nami na kufuata maelekezo yangu.” Kama wewe ndiye mtoto mwenye miaka miwili, njia yako ya uhuru itakuwa ipi? (Utakufa kama utachagua kuenenda njia zako mwenyewe. Kuwa mfu ndio mwisho wa uhuru wako wa kufanya uchaguzi. Njia pekee ya kuendelea kuishi ni kumchagua mzazi wako. Yesu alitupatia fursa ya uhuru wa mauti ya milele. Lakini, uhuru wa kweli unatutaka tutembee naye.)
    4. Hebu tuliangalie hili katika mtazamo mwingine. Je, ni uhuru wa aina gani unaotaka kuufurahia mbinguni? Je, ungependa wananchi wenzako kule mbinguni waweze kufurahia “chuki, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi na ulafi?” (Kama chanzo na mateso hapa duniani kitajipenyeza na kuingia kule mbinguni, basi hutaufurahia uhuru.)
    5. Mfano wa mwisho kabisa. Fikiria dhambi uliyoifanya ambayo unaijutia kabisa kuliko zote. Je, “ulifurahia” uhuru kwenye hiyo dhambi? (Kwa wazi kabisa, ulikuwa huru kuitenda dhambi, lakini kilichofuatia ni mateso! Rafiki, tunaweza kuangalia uzoefu wetu wenyewe ili tuweze kuelewa kwamba njia pekee ya kuufurahia uhuru wa uchaguzi ni kufanya maamuzi sahihi.)
  3. . Uhuru na Upendo
    1. Soma Wagalatia 5:13-14. Je, hilo umelisikia wapi hapo kabla? (Unaweza kushangazwa kwa kutambua kwamba umelisikia zaidi ya mara moja! Soma Mambo ya Walawi 19:18 na Mathayo 22:37-40.)
      1. Je, uhuru niliopewa na Yesu unamaanisha kuwa sina wajibu? (Hapana! Inamaanisha kuwa nina wajibu wa kuwapenda wengine kama ninavyojipenda mwenyewe na wajibu wa kuepuka kutosheleza matamanio ya asili yangu ya dhambi.
    2. Je, kauli ya Paulo inaendana na mjadala wetu wa kile tunachokidhani ni uhuru wa kweli? (Hatuambii kitu ambacho ni kipya kwenye uzoefu wetu wenyewe.)
      1. Je, tunakubaliana kuwa tunapomdhuru mtu mwingine basi tunajidhuru wenyewe? Na, tunapompenda mtu mwingine, basi tunajipenda wenyewe?
    3. Soma Wagalatia 5:15. Je, hii inatuambia nini ambacho tayari tunakijua kuhusu kuwadhuru watu wengine kwa “uhuru” wetu? (Wanalipiza kisasi! Watachukua kipande kutoka mafichoni mwako!)
  4. Wakili wa Upande wa Pili
    1. Tumekuwa tukirukia rukia mafungu kwenye Wagalatia 5, hebu turejee nyuma na kusoma mafungu tuliyoyaruka. Soma Wagalatia 5:7. Hii ni njia isiyo ya kawaida ya kuelezea kuhesabiwa haki kwa imani: kuuheshimu ukweli! Au, ndivyo hivyo? (Sio njia isiyo ya kawaida. Uamuzi wa kumwamini Mungu na kumtumainia Mungu (kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu) ni sawa kama vile uamuzi wa mtoto wa miaka miwili wa kuwatii na kuwatumainia wazazi wake. Ni uamuzi kuhusu kiapo cha utii.)
    2. Soma Wagalatia 5:8. Nani anayeweza kuondosha kama mwanzilishi wa kuhesabiwa haki kwa imani? (Yesu.)
    3. Soma Wagalatia 5:9. Je, ni vigumu kiasi gani kukabiliana na kosa/dosari? (Hii ni enye kudhuru kwa siri! Inajipenyeza na kuambukiza kanisa zima.)
    4. Soma Wagalatia 5:10. Je, tunaweza kukubaliana na Paulo? Kutokana na kile alichokiandika hadi hivi sasa, kwa nini awe jasiri kiasi hicho?
      1. Kama tuna aina fulani hivi ya wazo “jipya” la kulitikisa kanisa, je, tuchukulie jambo gani? (Kama wazo letu halina msingi wa Biblia, kama tunaleta mikanganyiko kanisani, basi tutalipa adhabu.)
        1. Je, tunamfahamu anayesababisha mikanganyiko? (Shetani. Paulo anatuambia kuwa hawezi kuwa Yesu. Kwa hiyo, lazima atakuwa ni –
        2. mpinzani wa Yesu (Shetani) na wafuasi wake wanaofanya mambo haya kanisani.)
    5. Hebu ruka mbele kidogo na usome Wagalatia 5:12. Kwa ulinganisho, soma tena Wagalatia 5:6. Je, unazilinganishaje hizi kauli mbili? (Kosa la msingi linahitaji jibu madhubuti.)
    6. Soma Wagalatia 5:11. Kwa nini kosa la kuhesabiwa haki kwa matendo ni “kosa la msingi?” (Linabatilisha msalaba. Mungu wetu alisulubiwa. Wazo la mungu kusulubiwa ni “kosa/hatia.” Nani ambaye atamfuata mungu aliyeuawa? Tunafanya hivyo! Wakristo wanaelewa kwamba maisha, kifo na ufufuo wa Mungu wetu ndio ufunguo wa uzima wetu wa milele. Kama hulipati suala hili kwa usawia, basi wewe sio Mkristo.)
    7. Rafiki, je, unaipata hoja ya Paulo inayosema kwamba njia ya Mungu ya kuuelekea uhuru wa kweli ni kuamini, kumtumaini na kumheshimu yeye. Tunaokolewa kwa neema, kwa kumchagua Yesu, lakini haya sio maneno tu, ni uchaguzi wa maisha. Ni uchaguzi wa kumpenda Mungu na watu wengine ili kwamba hatia, huzuni na pambano la ubinafsi liweze kuachwa nyuma. Tunaweza kusimama katika mwanga na furaha ya uhuru wa kweli. Je, utaufanya huo uchaguzi wa maisha hivi leo?
  5. Juma lijalo: Kuishi kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu.