Somo la 8: Miongoni Mwa Walio Wadogo
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Tunao msemo nchini Marekani kuhusu majibu “yanayobandikwa nyuma ya vyombo vya usafiri” (Bumper Sticker), ukizungumzia wito wa aina mbalimbali ambao mtu anaweza kuubandika kwenye bamba la gari. Unamuuliza mtu swali, na anakupa jibu la “bumper sticker.” Kauli ya “Miongoni mwa hawa” inafananishwa na “bumper sticker.” Je, inamaanisha nini? Mungu anampenda kila mtu, hivyo tunawezaje kumpachika mtu “udogo?” Yesu anatuambia kuwa “mdogo” kati yetu “ndiye mkubwa” (Luka 9:48). Wakati huo huo, mara mbili Yesu anazungumzia umuhimu wa kumsaidia “mmojawapo wa hao walio wadogo” (Mathayo 25:40 & 45). Tunatakiwa kuchimbua zaidi na kuyaelewa mapenzi ya Mungu, hivyo hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!
- Kulielewa Hubiri la Yesu
-
- Soma Mathayo 5:3. Inamaanisha nini kuwa “maskini” inapokuja kwenye suala la roho zetu? Je, huo ni “udogo?”
-
- Soma Warumi 8:13-14. Hatupaswi kuwa na “Roho” mwenye nguvu? (Ulinganifu upo kati ya “roho” yetu wenyewe na “Roho Mtakatifu.” Ikiwa tunajisifu na kuridhishwa na matakwa yetu wenyewe, basi tupo kwenye matatizo. Lakini, tukisalimisha roho yetu “maskini” kwa Roho Mtakatifu, basi tunaurithi Ufalme wa Mbingu.)
-
- Soma Mathayo 5:4. Je, kuhuzunika ndilo lengo? (Soma Warumi 15:13. Hapana, lengo ni furaha.)
-
-
- Ikiwa lengo letu ni furaha, Yesu anamaanisha nini? (Yesu anafundisha kwamba ikiwa tunahuzunika, atatufariji. Sidhani kama huzuni ndilo lengo.)
-
-
- Soma Mathayo 5:5. Tafsiri yako ya “upole” ni ipi? Je, mtu mpole ni “mdogo?”
-
-
- Soma Yohana 18:22-23. Je, hii inaendana na tafsiri yako ya upole?
-
-
-
- Soma Matendo 16:36-37. Je, hii inaendana na tafsiri yako ya upole? (Kukubali matokeo yasiyo ya haki si ambacho Yesu alikimaanisha, ikiwa Yesu na Paulo wanaenenda sawa sawa na fundisho la Yesu. Nadhani wema ndio uelewa mzuri wa jambo hili, na sio mtazamo wa ubinafsi wenye kujikweza.)
-
-
- Soma Mathayo 5:6. Unapofikiria suala la kuhisi njaa na kiu, unakuwa na wasiwasi kiasi gani kutatua matatizo hayo?
-
-
- Je, una njaa ya kiwango hicho hicho ya kuyajua mapenzi ya Mungu?
-
-
-
- Nini kitatokea ikiwa tuna hamu kubwa ya kumjua Mungu? (Hamu zetu “zitatimizwa.”)
-
-
- Hatutapitia hubiri (fundisho) lote la Yesu, lakini tumelianza kwa kuwa baadhi ya watu wanajenga hoja kwamba Yesu anazungumzia “umaskini uliopo ndani yetu na duniani mwetu.” Je, Yesu anatangaza au anapendekeza “umaskini?” (Hapana. Watu wengi maskini wana nia kubwa na kushawishika kwamba hali yao ya kiroho iko juu kuliko ya matajiri. Hii ni sababu mojawapo ambapo watu wanajenga hoja kwamba serikali inapaswa kuchukua fedha kutoka kwa matajiri na kuwapatia maskini. Wakati huo huo, kuna matajiri wengi ambao wanadhani kwamba wao ni bora zaidi ya wengine kwa kuwa wao ni matajiri. Yesu anawasifia wale wanaomtegemea, wale wanaomtumainia, na wale ambao hadhi yao inatoka kwake.)
-
- Soma Mathayo 5:38-42. Soma tena Yohana 18:22-23. Nitachukulia kwamba Mathayo 5:39 na Yohana 18:23 havikinzani. Unatatuaje huu mgogoro wa dhahiri?
-
-
- Ili kufanya mambo kuwa magumu zaidi, soma Luka 22:36-38 na Matendo 23:1-4. Kwa nini Yesu anapendekeza ununuzi wa upanga kwa wale wanaopaswa kugeuza shavu jingine?
-
-
- Soma tena Mathayo 5:38. Yesu anaposema, “mmesikia kwamba imenenwa,” hiyo inaonekana kama aina fulani hivi ya hekaya (kauli za uwongo). Je, huu ni msemo tu usiothibitika? (Soma Kutoka 21:24, kumbukumbu la Torati 19:21 na Mambo ya Walawi 24:20. Hii ni torati ya Agano la Kale iliyotolewa na Mungu.)
-
- Sasa hebu tusome muktadha katika Kumbukumbu la Torati. Soma Kumbukumbu la Torati 19:18-21. Nia ya adhabu kama hii ni ipi? (Hii ni njia ya Mungu ya kukomesha uovu. Watu wataogopa kutenda uovu.)
-
- Kwa mara nyingine, unaelewaje jinsi Mungu wetu wa Agano la Kale anavyokinzana na Mungu wetu wa Agano Jipya? (Nadhani Yesu anatoa fundisho kwamba tunatakiwa kusisitiza juu ya haki zetu. Tunaweza kutoa msisitizo – kama Yesu na Paulo walivyosisitiza juu ya haki zao. Tunatakiwa kuonesha busara na unyenyekevu katika kufanya uamuzi kuwa ni wakati gani wa kudai haki zetu.)
-
-
- Je, kuna tofauti kati ya serikali kukabiliana na uovu na mtu kulipiza kisasi? (Lengo la haki katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati lilikuwa ni kwa serikali kukabiliana na uovu. Hata hivyo, wakati Yesu na Paulo waliposimama kutetea haki zao walifanya hivyo dhidi ya mawakala wa serikali.)
-
-
-
- Je, kuna tofauti kati ya kuwaita polisi na kuwataka wasimamie utekelezaji wa sheria, na wewe kumpiga risasi mvamizi nyumbani kwako anayejaribu kukudhuru? (Sidhani kama hiyo ni tofauti sahihi. Mathayo 5:39 inasema “msishindane na mtu mwovu.” Lakini, “uovu” unaonekana kuwa mdogo – kofi, shati na koti lako, au kutembea umbali wa maili ya ziada. Hii ni njia moja ya kupatanisha mgogoro wa dhahiri. Tunapozungumzia kuhusu kanuni za msingi, basi tunaweza kutoa upinzani. Tunapozungumzia usumbufu mdogo, ni bora zaidi tusipojaribu kulazimisha haki zetu.)
-
- Hubiri la Paulo
-
- Soma Warumi 12:9. Paulo anasema kuwa mtazamo wetu dhidi ya uovu unapaswa kuwaje? (Tunapaswa kuuchukia.)
-
- Soma Warumi 12:13. Paulo anawekaje ukomo wa kuwasaidia wahitaji? (Anawazungumzia “watu wa Bwana.”)
-
-
- Ilinganishe na Mathayo 25:35. Je, “mgeni” ni sehemu ya “watu wa Bwana?”
-
-
- Soma Warumi 12:14-16. Hii inatoa mwanga gani kwenye fundisho la Yesu kuhusu kutopingana na mtu mwovu?
-
- Soma Warumi 12:17. Tulizungumzia ulipizaji kisasi. Hii inatufundisha nini? (Hatutakiwi kumtendea uovu mtu yeyote. Tukilipa uovu kwa uovu, ulimwengu unaweza tu kuona uovu tunaoutenda!)
-
-
- Hebu turukie mbele na tusome Warumi 12:19. Jambo gani litatufariji tunapodhuriwa na watu waovu? (Mungu anaahidi kwamba atalipiza kisasi.)
-
-
- Soma Warumi 12:18. Mambo gani mawili ya msingi yanapatikana kwenye kifungu hiki? (Kwanza, Mungu anatutaka tuishi kwa amani. Hilo ndilo lengo. Ikiwa itahusisha maumivu kidogo ili kupata amani, hicho ndicho anachokitamani Mungu. Pili, hii inakiri kwamba inawezekana amani isiwepo.)
-
- Soma Warumi 12:20-21. Eneo lote hili linahitaji hekima iliyovuviwa na Roho Mtakatifu. Ninafahamu si mara zote ninakuwa na hekima hii, lakini fanya uamuzi. Kazi yangu ni kuwafungulia mashtaka “watu wabaya” ili kuwafanya waheshimu dhamiri za kidini na za kisiasa za wateja wangu. Ninatumia mahakama kuupinga uovu unaofanywa kwa watu wengine. Lakini, katika kesi hizi, ninakuwa na mazingira rafiki na kujaribu kuwa mwema kwa wakili/mwanasheria ninayepingana naye. Je, hii inaendana au haiendani na maneno ya Yesu na Paulo?
- Matumizi Maishani
-
- Hebu tusome sehemu ya hivi visa viwili. Soma Luka 16:19-23 na Mathayo 25:33-36 na Mathayo 25:41-43. Hitimisho gani la dhahiri linapaswa kuhitimishwa kutoka kwenye hivi visa viwili? (Matajiri ni wabaya na maskini ni wema. Ukiwasaidia walio wahitaji unakwenda mbinguni.)
-
-
- Je, Biblia inaendana na hitimisho hili? Hadhi yako maishani au matendo yako yanabainisha wokovu wako?
-
-
-
- Soma Warumi 8:1-4. Hii inasema kuwa tunaokolewaje?
-
-
-
- Soma Ayubu 1:1-3. Hii inazungumzia nini kuhusu mwenendo wa Ayubu kwa Mungu, hata kama alikuwa tajiri sana?
-
-
- Hebu tuangalie visa vyetu vilivyotangulia kwa ukamilifu. Soma Luka 16:24 na Luka 16:27-29. Hii inatufundisha kwamba waliopotea wanapata maumivu makali ya moto wakati wote, na wanawaona na kuzungumza na watu waliopo mbinguni. Na kwa kuongezea, wafu wanaweza kututembelea. Je, hizi ni kweli zilizojengwa juu ya Biblia? (Hizo zimetolewa uamuzi, kama inavyomaanisha kwenye hali ya kuwa tajiri kwamba umepotea.)
-
- Soma Luka 16:30-31. Ni nani atakayefufuka kutoka katika wafu? (Yesu! “Kweli” hizi zimetungwa ili ziendane na hitimisho kwamba kufufuka kwa Yesu kusiko na faida kutoka kaburini hakutawashawishi wale wanaokataa kufuata maelekezo ya Mungu yaliyopo.)
-
-
- Je, kweli zinakusudia kutufundisha kanuni za Kibiblia? (Hapana, hususan pale zinapokinzana na vifungu vingine vya Biblia. Kweli zinaweka tu hitimisho kwamba baadhi ya watu watapinga uthibitisho wenye ushawishi mkubwa kuhusu Yesu.)
-
-
- Soma Mathayo 25:37-40. Unazielewaje kauli za Yesu ikiwa hatuokolewi kwa matendo yetu? (Hitimisho lenye mantiki ni kwamba uhusiano wa imani kwa Yesu hutufanya tuwasaidie walio wahitaji. Hubadilisha mioyo yetu.)
-
-
- Kuna watu wengi wanaotaka kutenganisha serikali na dini, lakini kwa ukinzani wanadhani serikali ina wajibu wa kimaadili kuchukua fedha kutoka kwa baadhi ya wananchi na kuwapatia wengine ili wawe na usawa zaidi. Vifungu hivi vinatufundisha nini kuhusiana na jambo hilo? (Yesu anatusifia kwa kile tunachokitenda binafsi, sio kile tunachowalazimisha wengine wakitende.)
-
-
- Rafiki, tunaokolewa kwa neema pekee, na si kwa matendo yetu. Lakini, moyo ulioongoka ni moyo unaowapenda na kuwajali wengine. Je, utamwomba Roho Mtakatifu aendelee kuulainisha moyo wako na kuinoa akili yako?
- Juma lijalo: Huduma Katika Kanisa la Agano Jipya.