Somo la 5: Kilio cha Manabii
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Manabii katika Agano la Kale walikuwa na nafasi ya pekee ya matumaini. Leo tunayo Biblia, lakini maelekezo mengi ya Mungu kwa watu yaliletwa kwa njia ya manabii wake [Mungu]. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia na tuone kile inachotufundisha kuhusu mapenzi ya Mungu kwa miongoni mwa hawa walio wadogo!
- Tatizo la Kutumaini
-
- Soma 1 Samweli 8:5. Watu wa Israeli walidai nini? (Kuongozwa na mfalme.)
-
-
- Nani alikuwa anawaongoza? (Soma 1 Samweli 8:7. Mungu alikuwa akiwaongoza watu wake kupitia kwa nabii Samweli.)
-
-
-
- Watu walikuwa na masikitiko kuhusu wana wa Samweli. Walikuwa na tatizo gani? (Soma 1 Samweli 8:3. Hawakuwa waaminifu, walipokea rushwa, na kupotosha haki.)
-
-
- Soma 1 Samweli 8:11-12. Mfalme atafanya jambo gani? (Atakuwa na jeshi. Atawalazimisha watu kupambana.)
-
- Soma 1 Samweli 8:13-17. Mfalme atafanya nini kingine? (Atawatoza watu ushuru. Atachukua ardhi yenu, mavuno yenu na watu wenu.)
-
- Hebu turejee nyuma na tusome 1 Samweli 8:9. Samweli anatimiza hasa kile alichoambiwa na Mungu. Unapotafakari mambo yanayowahangaisha watu, je, hili linatimiza kinachowahangaisha? (Watu walikuwa na masikitiko kwamba wana wa Samweli wangewatawala. Vijana hawa walikuwa wamemomonyoka kimaadili na hawakuifuata sheria ya Mungu. Kwa dhahiri, hoja mbadala kwamba mfalme ataunda serikali kubwa itakayokuwa na gharama kubwa kuiendesha haitatui malalamiko ya watu.)
-
-
- Mjadala kuhusu matatizo ya serikali kubwa unazungumzia jambo gani? (Watu ndio sababu ya kutokuwepo kwa uhusiano kati ya malalamiko yao na jibu la Mungu. Tukichukulia kwamba wana wa Samweli walikuwa waovu, watu wangemwomba Mungu kurekebisha hali yao. Kuomba mfalme inamaanisha watamtumainia mtu asiye na jina kuliko wanavyomtumaini Mungu.)
-
-
- Soma 1 Samweli 8:21-22. Hii inatufundisha nini kuhusu Mungu? (Wakati mwingine atajibu maombi ya kipumbavu tutakaposhindwa kumtumainia.
-
-
- Kuna fundisho gani kwetu leo? (Kumgeukia Mungu katika kutatua matatizo yanayotukabili sasa hivi.)
-
- Tatizo la Sodoma
-
- Soma Mwanzo 18:17, Mwanzo 18:20-21, na Mwanzo 18:32-33. (Pia unakaribishwa kusoma “kwa undani zaidi.”) Vifungu hivi vinaelezea kwa ufupi kisa tangulizi kwa ajili ya kuangamizwa kwa mji wa Sodoma. Mungu anaamua kushiriki na Ibrahimu kile anachodhamiria kuitendea Sodoma. Ibrahimu anajaribu kuiokoa Sodoma. Mjadala wa mwisho kati ya Mungu na Ibrahimu unafunua habari gani kuhusu Sodoma? (Hawakuwepo watu kumi wenye haki kwenye mji wote!)
-
-
- Hii inatufundisha nini kuhusu rehema za Mungu?
-
-
-
- Huu ni mjadala unaohusu manabii, kwa nini mjadala wa Mungu kumtembelea Ibrahimu kuhusu mji wa Sodoma uwepo? (Badala ya kupitia kwa wanadamu, Mungu anazungumza na Ibrahimu moja kwa moja.)
-
-
- Soma Yuda 1:7. Dhambi ya Sodoma iliyo kinyume kabisa na maadili ni ipi? (Ngono na upotovu.)
-
- Baada ya Mungu kusema atabainisha kama Sodoma ni mji mbaya kama inavyodaiwa, malaika wawili walijitokeza kama watu na kuutembelea. Hebu tusome kile kinachotokea pale Lutu anapowachukua ili wasidhuriwe na watu wa mji. Soma Mwanzo 19:4-5. Hii inakuambia nini kuhusu asili ya dhambi ya ngono ya watu wa Sodoma? (Kifungu kinasema “watu wa mji,” “vijana kwa wazee” wakaizunguka nyumba ya Lutu kwa lengo la kuwabaka hawa malaika wawili.)
-
-
- Je, ni kweli kwamba watu wote katika mji ule walikuwa wasenge wenye vurugu nyingi? Au, je, walikuwa radhi kulazimisha ngono na mtu yeyote wa jinsia yoyote? (Soma Mwanzo 19:8-9. Lutu anajitolea bintize walio mabikra ili wafanye nao ngono – na watu hawa wanakataa ofa hiyo. Hii inaashiria kwamba Lutu anategemea mbinu zake mwenyewe badala ya kumtegemea Mungu, lakini pia inaonesha kwamba Lutu anabainisha kwa usahihi kuwa wanaume hawa wa Sodoma hawakuwa na haja na wanawake.)
-
-
- Soma Ezekieli 16:49. Licha ya haya maelezo ya kutisha juu ya kile kinachowatokea wageni kule Sodoma, na kauli ya dhahiri ya Yuda kwamba ngono na upotovu ndizo zilizokuwa dhambi za mji ule, watu wengi leo wanarejea kifungu hiki cha Ezekieli kwamba kinajenga hoja kuwa Sodoma haikuunguzwa kutokana na dhambi ya ngono. Dhambi halisi ya Sodoma ilikuwa ni kushindwa kuwasaidia maskini. Una maoni gani?
-
-
- Soma Ezekieli 16:50. Hiyo inatuambia nini kuhusu dhambi ya wale walioishi Sodoma? (Walikuwa na kiburi, ufidhuli na kutenda mambo ya kuchukiza sana. Nani angeweza kuhitimisha kwa mantiki kwamba wale walioishi Sodoma walikuwa na dhambi moja pekee?
-
-
-
- Soma Isaya 3:9. Hii inatuambia nini kuhusu dhambi ya Sodoma? (Hii inaziunganisha pamojakiburi na upotovu. Kifungu kinasema kuwa “wamefunua dhambi yao.”)
-
-
-
-
- Umewahi kusikia “Gay Pride Parade?”
-
-
-
- Kuuangalia ushoga kwa undani ni muhimu kwa sababu ya kukua kwa mgongano wa uhuru wa dini kati ya watetezi wake na Wakristo wanaoiamini Biblia. Soma warumi 1:20. Kwa nini Mungu anasema kuwa watu wote wanapaswa kumjua?
-
- Soma Warumi 1:21-23. Paulo anafundisha kwamba dhambi inaongezeka hatua kwa hatua. Baada ya kupuuzia uthibitisho wa Mungu, nini kinafuatia kwa wadhambi? (Mchakato wa fikra yao unapungua, mioyo yao inatiwa giza, na wanaabudu vitu vinavyofanana na wanadamu na wanyama.)
-
- Soma Warumi 1:24-27. Nini kinafuatia baada ya ibada ya sanamu? (Wanauamini uongo na kujiingiza kwenye vitendo vya ubasha.)
-
- Soma Warumi 1:28-31. Nini kinachofuatia uovuni? (Wanamchukia Mungu, wenye jeuri, wenye majivuno, na wenye kukashifu. Hawana uelewa, upendo, au rehema.)
-
-
- Hatua gani inayofuatia dhambini baada ya ubasha? (Kumchukia Mungu na kupungukiwa uelewa, upendo, na rehema.)
-
-
-
- Je, ubasha ni dhambi ya “hali ya chini” kuliko dhambi zilizoorodheshwa katika Warumi 1:29?
-
-
-
- Kwenye mijadala juu ya athari ambazo vuguvugu la wasenge inazo kwenye uhuru wa dini, maoni yanayojirudiarudia ni kwamba uvumilivu wa vitendo vya ubasha dhidi ya Wakrisho unatokana na vitendo visivyovumilika vilivyopita vya Wakristo dhidi ya wasenge. Je, vifungu tulivyovisoma hivi punde vinaunga mkono hii nadharia ya “malipo?” (Hapana. Chuki, ufidhuli/ujeuri, kutokuwepo kwa upendo na rehema ni vitu vya asili vinavyojiingiza kwenye hii dhambi. Hivyo ni vitu vya asili vinavyojielekeza kwenye dhambi zote.)
-
-
- Soma Warumi 1:32. Je, mapenzi ya Mungu ni fumbo kwa wadhambi? (Hapana. Sio tu kwamba wamehafifisha ukweli kuwa dhambi huleta mauti, bali pia wanaithibitisha, kuitangaza na kuiendeleza dhambi.)
- Sodoma Kanisani
-
- Soma Isaya 1:9-11. Je, ni kweli kwamba Mungu anazungumza na viongozi wa mji wa Sodoma na Gomora? (Hapana. Ukiuangalia muktadha, Isaya anaizungumzia Israeli!)
-
-
- Je, hawa ndio watu wanaomchukia Mungu? (Hivyo sivyo wanavyoonekana. Wanatoa kafara kwa Mungu wa kweli na si kwa sanamu.)
-
-
-
-
- Tatizo ni lipi? (Hawana utii, wanaendelea tu kutoa kafara! Hawalichukulii kwa dhati suala la dhambi.)
-
-
-
- Soma Isaya 1:12-15. Kwa nini Mungu anachukia ibada ya watu wake? (Hawana nia ya kutii.)
-
- Soma Isaya 1:16. Mungu anataka watu wake wafanye nini? (Waache kutenda mabaya.)
-
-
- Ninaamini kwamba mfumo wa kafara unaelezea suala la haki kwa imani. Watu “hawakuupata” wokovu. Adhabu ya dhambi zao ililipwa kwa mnyama wa kafara. Isaya 1:16 inatufundisha nini sisi tunaoamini katika neema? (Matendo ni ya muhimu! Lengo letu ni kuacha kutenda makosa.)
-
-
- Soma Isaya 1:17. Mungu anasema kipi kilicho sahihi kukitenda? (Kutafuta haki!)
-
-
- Chini ya mwavuli wa haki tunaambiwa “kuwatetea wanaoonewa,” kuwapatia haki “yatima” na “kuwatetea wajane.” Hapa lengo ni lipi? (Hukumu sawa na y haki.)
-
-
-
- Kwa sasa hapa nchini Marekani vyombo vya habari vinashadadia sana suala la uhamiaji. Tuna wahamiaji (na wahamiaji watarajiwa) wanaofuata utawala wa sheria, wanatuma maombi kuingia nchini, na wanakuwa raia. Pia tuna wahamiaji wanaoingia kinyume na utaratibu na kukaa nchini kinyume cha sheria. Wengine wanaingia kwa mujibu wa sheria, lakini wanakaa nchini kinyume cha sheria. Isaya 1:17 inafundisha nini kuhusu hii hali? (Isaya inafundisha kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa upande wa hukumu ya haki na usawa. Utawala wa sheria unapaswa kufuatwa isipokuwa kama sheria yenyewe si ya haki.)
-
-
- Rafiki, tumegusia masuala yenye kuleta mabishano makubwa sana. Ikiwa lengo letu ni kuyafuata mapenzi ya Mungu, je, tunapaswa kutumia mafundisho ya Mungu kwenye masuala yanayoleta ubishani mkubwa kabisa katika zama za leo? Au, je, tunapaswa kutumia mafundisho ya manabii kwenye mambo yasiyo ya msingi? Omba kwamba Roho Mtakatifu auguse moyo wako ili uweze kutenda yaliyo sahihi.
- Juma lijalo: Mwabudu Muumba.