Somo la 3: Sabato: Siku ya Uhuru

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Kutoka 16 & 20, Luka 13, Marko 2, Mathayo 12)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
3
Lesson Number: 
3

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Ninaipenda Sabato! Maisha yangu yana mifululizo ya masuala yenye ukomo wa muda (deadlines). Ninapokuwa nyumbani, huwa nina kazi ya kufanya ndani ya nyumba na nje bustanini. Nadhani unafahamu ninachokizungumzia. Nilipokuwa kijana, sufuria ya mvuke (pressure cooker), mali ya shule ya sheria iliniletea baraka ya Sabato kwa uzuri kabisa. Wakati wanafunzi wengine walipokuwa wakisoma, niliweza kuwa na uhuru wa muda bila kuwa na hatia yoyote kwa kwenda kanisani, kushiriki chakula na marafiki, na kusoma na kupumzika. Hebu tuzame kwenye Biblia zetu na tuone baraka nyingine tunazoweza kuzipata ndani ya Sabato!

 

  1.     Mpango wa Mana

 

    1.     Soma Kutoka 16:14-16 na Kutoka 16:21. Kwenye suala la kulishwa, watu walikuwa na wajibu gani? (Walitakiwa kuamka kutoka vitandani mwao na kuokota chakula. Wasingefanya hivyo, kingeyeyuka.)

 

    1.     Soma Kutoka 16:17-18. Kwa nini kila mmoja ana kiasi sahihi? (Mungu aliwaambia kiasi cha kuokota, walitii, na kila mmoja alipata kile alichokihitaji.)

 

      1.     Kitabu cha “The Bible Knowledge Commentary” kinafafanua kwamba “omer” (kipimo cha ujazo wa nafaka kavu na vitu vikavu) ni takriban lita (quarts) mbili. Vipi kuhusu walaji wenye nguvu na afya? Wale wanaohitaji kalori nyingi zaidi? (Vifungu hivi vinazungumzia juu ya kiasi ambacho kila mtu alikihitaji. Nadhani kilichokusudiwa kuhusu mambo yalivyofanyika ni kwamba Mungu aligawa kilichohitajika kwa kila mtu.)

 

      1.     Je, hii inatufundisha chochote kuhusu uchumi leo? (Ninahisi kwamba bila kujali vingi ulivyonavyo, mara zote unahitaji zaidi ya kile ulichonacho!)

 

    1.     Soma Kutoka 16:19-20. Kwa nini mtu anajaribu kutunza chakula kingi zaidi? (Hawakumwamini Mungu. Haikuwa na mantiki yoyote kujaribu kukitunza chakula ikiwa ulipokea chakula kipya kila asubuhi.)

 

    1.     Soma Kutoka 16:22-25. Hii inatufundisha nini kuhusu Sabato? (Mungu alikusudia tupumzike. Hakuna haja ya kudamka na kuokota chakula.)

 

      1.     Tunajifunza nini kivitendo leo? (Hatutapungukiwa kwa kupumzika siku ya Sabato. Hili ni fundisho nililojifunza mapema sana. Wale wanafunzi wenzangu wa sheria waliosoma kwa bidii siku ya Sabato hawakupata alama nzuri zaidi yangu.)

 

      1.     Hii inatufundisha nini kuhusu kuweka vipaumbele vya Mungu kwanza? (Ninakumbushwa siku tulipokuwa tunajenga kanisa letu. Nilikuwa nimetoka tu kununua gari la mtumba aina ya Mercedes Benz na nilifurahia kubadili mafuta yake. Badala yake, nilimweka Mungu kuwa wa kwanza na kufanyia kazi suala la ujenzi wa kanisa letu jipya. Nilipofika nyumbani mara moja nilianza kulishughulikia gari la Benz, na nikagundua kwamba lilikuwa na “oil drain plug’ isiyo ya kawaida. Ilihitaji kamba kubwa iliyosokotwa. Hakuna kamba yangu hata moja ambayo ingetosheleza na nilikuwa na mashaka kama kamba hiyo ilikuwa inauzwa maeneo yaliyokuwa yananizunguka. Kisha nikagundua kuwa aproni (nguo maalumu inayovaliwa hasa wakati wa shughuli za uchafu) niliyoitumia kazini ilikuwa na kifaa cha kung’olea msumari, huku ikiwa na mkono unaofanana na kamba kubwa ya msokoto. Inaendana kivipimo kabisa! Nisingeyapa kipaumbele masuala ya Mungu, ningepoteza muda wangu kufanya kazi kanisani kwa kutafuta kamba sahihi!)

 

  1.   Pumziko la Sabato

 

    1.     Soma Kutoka 20:8. Mungu anatuambia tufanye nini anaposema “ikumbuke?” (Anaweza kuwa anatuambia “tuizingatie,” lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba Mungu anatuambia tuikumbuke Mwanzo 2:2-3.)

 

    1.     Soma Mwanzo 2:2-3. Hii inatuambia nini kuhusu Sabato na pumziko? (Historia ya Sabato ni kwamba Mungu wetu Muumbaji alifanya kila kitu katika siku sita na kuikumbuka kazi yake kwa pumziko la Sabato.)

 

      1.     Unatoa alama ngapi katika dunia hii kwenye suala la kumkumbuka Mungu Muumbaji wetu? (Badala ya kukumbushwa kila Sabato kwamba Mungu ni Muumbaji wetu, utamaduni uliopo unatuambia kuwa Mungu hausiki kivyovyote vile na uumbaji. Uumbaji ulitokea kwa bahati na ushindani.)

 

    1.     Soma Kutoka 20:9-10. Ujumbe mkuu wa Sabato ni upi? (Mjadala uliopo ni kati ya “pumziko” na “kumkumbuka Mungu.” Nadhani vyote viwili ni muhimu.)

 

      1.     Unadhani kwa nini watumwa (watumishi), wanyama na wageni pia walipaswa kupumzika? (Hii inaonesha umuhimu wa kipengele cha pumziko la Sabato – kila mtu na kila mnyama alistahili pumziko.)

 

      1.     Kwa miaka mingi nimekuwa nikitafakari kinachostahili kufanyika siku ya Sabato. Nakumbuka siku moja kanisa langu liliamua kwamba siku ya Sabato litatenda jambo jema kwa kumsaidia mshiriki wa kanisa aliyekuwa maskini kuhama kwa kuhamisha vitu vyake kutoka nyumbani kwake. Tena tukizingatia kwamba, Yesu alisema kuwa tunaweza kumwopoa ng’ombe kisimani siku ya Sabato! Angalia Luka 14:5. Nina uhakika nami nilisaidia! Unalizungumziaje jambo hili? (Nadhani kitendo hiki kinapuuzia kipengele cha pumziko la Sabato. Ni vigumu kuwa na pumziko kwa kuhamisha samani. Tofauti na ilivyo kwa ng’ombe, haya si mazingira ambayo samani ilikuwa katika hali ya wasiwasi au hatarishi.)

 

    1.     Soma Kutoka 23:12. Nilisoma makala kumhusu mkulima ambaye hakutumia kifaa chake cha kumwagilia siku ya Sabato. Alitaarifu kwamba kilidumu zaidi kuliko vifaa vya washindani wake. Unalifikiriaje jambo hili? (Pampu si sawa na mwanadamu, ng’ombe, au punda. Hata hivyo, Kutoka 23:10-11 inasema kuwa hatupaswi kukwatua ardhi katika mwaka wa saba.)

 

    1.     Soma Luka 13:10-11. Je, hii ilikuwa hali ya dharura? Je, ilifanana na ng’ombe kutumbukia kisimani? (Hapana. Hali hiyo ilikuwepo kwa muda wa miaka kumi na minane.)

 

    1.     Soma Luka 13:12-14. Uponyaji ni sehemu ya kazi ya kawaida ya Yesu. Kwa nini hii inastahili kufanyika siku ya Sabato?

 

    1.     Soma Luka 13:15-16. Kwa ng’ombe au punda suala ni kumpatia maji ya kunywa, na sio kumfungua! Unaweza kutetea mantiki ya Yesu? (Ningejibu kwamba hii haikuwa kazi. Kwa kuzingatia mantiki aliyoitumia Yesu, mwanamke aliwekwa huru siku ya Sabato.)

 

    1.     Soma Marko 2:23-27. Yesu anasema kuwa Mfalme Daudi aliweka mfano wa kukiuka sheria. Daudi pia alifanya uzinzi na mauaji! Je, hilo pia linakubalika? Je, matendo ya Daudi ya ukiukwaji wa sheria yana utetezi kimantiki? (Sidhani kama Yesu anatuambia tuenende kama Mfalme Daudi. Badala yake, anajenga hoja ya kistaarabu zaidi. Anabainisha uwiano kati ya mahitaji ya mwanadamu na Sabato. “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu,” ikimaanisha kwamba ilifanyika ili kuboresha maisha yetu. Kuna mfumo, kushughulikia njaa ya mtu ni jambo la muhimu zaidi kuliko Sabato.)

 

      1.     Vipi kama wanafunzi wangeanza kupika supu jikoni siku ya Sabato?

 

      1.     Vipi kama wanafunzi wangeanza kufanya kazi kwenye mgahawa siku ya Sabato?

 

    1.     Soma Marko 2:28. Hapa Yesu anamaanisha nini? (Kwamba anasema kilicho sahihi siku ya Sabato!)

 

    1.     Mathayo inaandika kwa kina mazungumzo haya. Soma Mathayo 12:5-6. Kazi yangu ya kila siku ni kufundisha na kujaribu kushawishi. Ninafundisha takriban kila sabato na mara kadhaa huwa ninahubiri. Mara kwa mara nimefundisha na kisha kuhubiri katika Sabato hiyo hiyo – ambayo ni kazi kubwa sana kama ilivyo kwa kazi zangu za kila siku. Yesu anasema kuwa “sina hatia” kwa kuvunja Sabato. Kwa nini?

 

      1.     Je, ni kwa sababu sitozi gharama? Kulipia gharama za wachungaji. (Fikiria swali langu la kupika supu/kufanya kazi mgahawani.)

 

      1.     Je, ni kwa sababu ya suala lililopo? Ninafundisha katika shule ya kidini na mara kwa mara ninakwenda mahakamani kusimamia kesi zinazohusiana na uhuru wa dini.

 

      1.     Yesu anamaanisha nini anaposema “yupo aliye mkuu kuliko hekalu?” (Anajizungumzia yeye mwenyewe.)

 

        1.     Yesu anasema nini? (Kwamba wanafunzi wanamhudumia, na kwa hiyo kazi yao inafanana na ile ya makuhani hekaluni.)

 

          1.   Wanafunzi walikuwa tu na Yesu, walikuwa hawamkusanyii masuke ili ale. Shughuli gani nyingine ambazo wanafunzi wangeweza kujihusisha nazo mbele ya Yesu siku ya Sabato na bado wasiwe na hatia?

 

    1.     Soma Mathayo 12:7. Nimeuliza mfululizo wa maswali yanayoonesha ugumu wa kuchora mistari. Wengine wanaweza kusema kuwa kuchora mistari ni “ung’ang’anizi wa sheria,” lakini kamwe Yesu hakusema “sahauni mistari.” Badala yake, anaonekana kusema kuwa viongozi wa Kiyahudi walikuwa wanachora msitari mahali pasipo sahihi. Kifungu hiki kinatoa kipimo cha uchoraji wa msitari. Unakielezeaje kipimo hiki? (Haya ni maelezo yasizingatia utamaduni uliopo: kuwafanya wanafunzi wahisi njaa ni sehemu yao ya kujitoa nafsi. Yesu anasema kuwahurumia (kuwaonesha rehema) wanafunzi walio na njaa ni muhimu zaidi kuliko makusudi ya kuwafanya wawe na njaa. Yesu ananukuu Hosea 6:6, ambako muktadha ni tofauti. Hapo, Mungu anasema kuwa anapendelea tuwe na utii, badala ya kutoa kafara kwa kutokutii kwetu. Muktadha huo ni mgumu kuuelezea hapa, ndio maana ninapendekeza maelezo mapya.)

 

    1.     Rafiki, Sabato ni ya muhimu kwa afya yetu ya kimwili na kiroho. Unapofanya uamuzi juu ya kile kinachoendana na Sabato, je, utakumbuka kwamba Yesu alisema kuwa Sabato ilifanyika kwa ajili ya manufaa yako? Mwombe Roho Mtakatifu akufunulie utambuzi wa Mungu!

 

  1. Juma lijalo: Rehema na Haki Katika Zaburi na Mithali.