Nyakati Ndogo za Taabu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, wewe ni mkali kwa wale wanaokupenda? Mke wangu, mwalimu mstaafu wa shule ya kanisa, alikuwa akiniambia mara kadhaa wazazi wangetoa taarifa ya jinsi gani watoto wao ni wenye tabia njema na wema wawapo shuleni, lakini walikuwa kitu tofauti wawapo nyumbani. Je, wahusika wa familia yako ni wapole, wakarimu na wavumilivu kwa wageni kuliko kwa wale wanaowapenda? Kwa nini ipo hivyo? Je, hivyo ndivyo jinsi inavyopaswa kuwa? Hebu tuzame kwenye Biblia yetu ili tuone inatufundisha nini kuhusu ukarimu kwa wengine!
- Bwawa
- Soma Mithali 17:14. Umewahi kuona sinema ya bwawa likipasuka? Kama umewahi, huwa linaanzaje? (Huanza kwa kuvuja sehemu ndogo.)
-
- Nini hutokea mwisho wa kupasuka kwa bwawa? (Uharibifu kamili.)
-
- Je, unaweza kudhibiti upasukaji wa bwawa? (Hii ndio hoja ya mithali hii, zuia mgogoro wako kabla haujakosa udhibiti.)
- Hebu tizama wahusika wa familia yako. Je, unafahamu kitu kinachosababisha mgogoro kwa mwanafamilia fulani? Kama ndiyo, je, unaweza kuepuka mijadala hiyo?
- Maisha ya Kipagani
- Soma Waefeso 4:17. Je, Wakristo wanapaswa kuishi tofauti na dunia (Ndiyo.)
-
- Kwa nini andiko linasema tunapaswa kuwa tofauti? (Kufikiria kwetu ni bora. Fikra za Wapagani ni “batili.”)
-
-
- Kuwa na fikra “batili” humaanisha nini? (Hebu tuendelee kusoma.)
-
- Soma Waefeso 4:18-19. Sasa hebu nieleze namna unavyoelewa fikra “batili?” (Hawaelewi mapenzi ya Mungu. Ni wajinga na hii hufanya mioyo yao kuwa migumu. Badala ya kuwa waelewa, wao wana tamaa za mwili, si safi na ni wenye tamaa.)
-
- Ni kwa jinsi gani fikra batili huweza kusababisha mgogoro baina ya mfanyakazi mwenza au mwanafamilia?
- Maisha ya Kikristo
- Soma Waefeso 4:20-21. Kwa nini hii inazungumzia sisi kujifunza namna mpya ya maisha? (Katika madarasa yangu ninafundisha juu ya kutawala hisia kwa kutumia misingi ya Biblia. Utawalaji wa hisia ni jambo linalofundishika, tofauti na akili za asili. Uboreshaji huu wa sehemu ya maisha yako kama mkristo ni suala la kujifunza. Inapatikana kwa wote.)
-
- Roho Mtakatifu ana jukumu gani katika kujifunza huku? (Soma Yohana 14:26. Roho Mtakatifu si tu kwamba anatufundisha jinsi gani tuishi, bali pia hutukumbusha kile ambacho tumejifunza.)
- Soma Waefeso 4:22-24. Nini kiini cha namna hii mpya ya kufikiri? (Una mtizamo mpya.)
-
- Tazama tena Waefeso 4:22. Sehemu gani ya utu wetu wa zamani inapingana na sisi? (“Tamaa zenye kudanganya.” Tutatamani kufanya mambo ambayo hatupaswi. Tamaa hizi ni za kudanganya kwa jinsi yakufikiri kuwa zitatupa furaha, lakini hazitotupatia.)
- Soma Waefeso 4:25. Ni kwa jinsi gani kukosa uaminifu huibua matatizo kwetu? (Tusipokuwa waaminifu, tunatoa taarifa mbaya. Andiko hili linatuambia kuwa sisi ni “viungo vya mwili mmoja.” Familia zetu haziwezi kutusaidia kama tunazipa taarifa mbaya. Familia zetu huweza kuathirika na taarifa zetu mbaya.
- Soma Waefso 4:26. Ni kwa muda mrefu kiasi gani kwa kawaida huwa unakuwa na hasira? Je, huwa unakuwa na kinyongo na mwanafamilia kwa siku kadhaa?
-
- Kwa nini hii inatupatia muda wa ukomo wa kuwa na hasira?
-
- Nini maana ya kuwa na hasira, lakini “kutotenda dhambi?” (Ni dhahiri kugadhabika si tatizo. Hatupaswi tu kufanya ikose udhibiti.)
- Soma Waefeso 4:27. Kwa nini Biblia inazungumzia kumpa “ibilisi nafasi” baada tu ya kututahadharisha kuhusu hasira? (Hasira hutufanya tutende mambo ambayo baadaye huwa tunayajutia. Hii ndio sababu inatupasa tujifunze kudhibiti hasira zetu.)
- Soma Waefeso 4:28. Hivi karibuni nilikuwa naongea na mtu aliyesema baadhi ya watu wanapaswa kuiba ili waweze kula. Biblia inasema nini kuhusu hili? (Inatupasa tufanye kazi, sio tuibe.)
-
- Kwa nini kazi ni baraka? (Inatupatia kitu cha maana kufanya kwa mikono yetu. Hatupaswi kupuuza umuhimu wa kazi.)
-
- Jambo gani jingine kazi inaturuhusu kufanya? (Kushiriki na wengine walio wahitaji.)
- Hebu tupitie tabia ambazo Biblia inasema tunapaswa kujifunza: mtazamo chanya, uaminifu, kudhibiti hasira na uchapaji kazi. Ni kwa jinsi gani mitazamo hii inaboresha hali ya familia yako? Ni kwa jinsi gani inaboresha maisha ya watoto wako?
-
- Je, unapenyeza tabia hizi kwa watoto wako?
-
- Hivi karibuni nilikuwa nikiongea na mwanangu na kumwambia ni baraka ilioje kuwa na akili. Nilipendekeza kwake kuwa bidii inaweza kuwa jambo ambalo unarithi. Alidhani kuwa bidii ilikuwa inapasishwa kwa watoto kwa wao kuona wazazi wenye bidii. Wewe unadhanije? (Biblia inatufundisha kuwa, angalau kwa sehemu, ni tabia inayoweza kufundishika.)
- Soma Waefeso 4:29. Tafsiri ya Biblia ya NIV inatafsiri neno hilo kuwa “isiyo kamilika” na tafsiri ya KJV inalitafsiri kuwa “ovu.” Sehemu iliyobaki ya kifungu inaonesha tafsiri ipi kuwa bora? (Mazungumzo yetu yanapaswa “kuwajenga” wengine “kulingana na mahitaji yao.” Mazungumzo yetu yanapaswa “yawanufaishe” au “kuwainua” wale wanaoyasikiliza. Hivyo tafsiri ya “ovu” inaonekana kufaa zaidi kwa sehemu inayosalia ya kifungu.)
-
- Ni kwa jinsi gani utatumia uzungumzaji huu kwa watoto wako?
-
- Watoto, ni kwa jinsi gani utatumia hii katika kuzungumza na wazazi wako? (Kihistoria, nimekuwa nikidhani kuwa kifungu hiki kimekuwa kikihusu maongezi yasiyofaa yahusuyo ngono. Lakini, nadhani inazungumzia maongezi yaliyokusudia kuwainua wale wanaotuzunguka. Usiwavunje moyo wale unaowapenda.)
- Soma Waefeso 4:30. Ni kwa jinsi gani tunaweza “tukamhuzunisha” Roho Mtakatifu? (Kutenda jambo lisilo sahihi bila shaka humhuzunisha Roho Mtakatifu. Hata hivyo, nafikiri kifungu hiki kinazungumzia kutomsikiliza Roho Mtakatifu. Kumpuuza Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni kiini kwetu katika kujifunza masomo tuliyokuwa tukijadili.)
- Soma Waefeso 4:31-32. Hii inawekaje masuala yetu ya familia? Maisha yetu ya kazi?
-
- Kifungu kinaposema “yaondoke kwenu,” je, hii huashiria kuwepo kwa sehemu ambayo inatakiwa sisi tufanye katika badiliko hili?
-
- Tazama tabia zilizoorodheshwa, zote nzuri na mbaya. Unaweza kuzielezea kwa jinsi gani? (Kwa ujumla ni mitazamo.)
-
-
- Je, unaweza kubadili mtazamo wako? (Kama haikuwa dhahiri hapo awali, inapaswa kuwa sasa. Roho Mtakatifu ana sehemu muhimu katika badiliko hili. Tunapaswa kumwomba Roho Mtakatifu kuingilia kubadili mitazamo yetu.)
-
- Kufikiri taratibu
- Soma Yakobo 1:19. Hii inaonekana zaidi kama matendo au mwitikio. Je unaweza ukajituliza kiasi na kwa kudhamiria ukawa na mwitikio wa jinsi hii?
- Soma Mithali 19:11. Ni kwa jinsi gani huwa unapokea matusi?
-
- Unadhani unatunza “heshima” yako kwa kujibu kila tusi?
-
- Je, unapaswa uanze tabia ya kutokuwa unajibu matusi papo kwa papo?
- Soma Wafilipi 2:3-7. Je, kufanya hivi itakuwa ngumu kwako?
-
- Ni kwa jinsi gani itabadilisha wale wanaokuzunguka?
- Soma Wafilipi 2:9-11. Je, kwa kudumu umepangwa kuwa mtumwa? (Yesu anatuonesha kuwa mtazamo huu utalipwa kwa heshima na mamlaka.)
- Rafiki, endapo unatamani uhusiano ulioboreka katika familia yako na kazini, kwa nini usizifanyie majaribio kanuni hizi za Biblia? Kwa nini isiwe, kwa njia ya Roho Mtakatifu, ujifunze kuzifanya kuwa sehemu ya maisha yako?
- Juma lijalo: Familia za Imani.