Kujiandaa kwa Ajili ya Badiliko
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mojawapo ya visa vya familia ambavyo mke wangu anapenda kuvisimulia ni kwamba mama wake alimsisitizia kuwa alipenda “vitu vile vile.” Hakutaka mabadiliko yoyote maishani mwake. Majuma sita baadaye, aliolewa na kuhamia kwenye makazi mapya. “Mambo yale yale” kupita kiasi. Kwa ujumla, watu wanaogopa mabadiliko. Kama ilivyo kwa mama mkwe wangu, wanasema wanataka “mambo yaleyale.” Hebu tuchimbue somo letu la Biblia na tuone kile inachotufundisha kuhusu mabadiliko maishani na jinsi tunavyopaswa kuyatathmini!
- Mafundisho Yanayotokana na Historia
-
- Soma 1 Wakorintho 10:1. Unadhani Mungu anadhani kuwa tunapaswa kufahamu nini? (Historia! Tunapaswa kufahamu kilichowatokea “mababu (wahenga) wetu.”)
-
-
- Je, mababu hawa walikuwa katikati ya mabadiliko makubwa maishani mwao?
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:2-4. Biblia inazungumzia nini kuhusu historia ya pamoja ya watu hawa? (Kwamba wote walikuwa na msingi mzuri ajabu wa kiroho. Kristo aliwapatia chakula na maji na Musa aliwapatia uongozi wa kiroho.)
-
- Soma 1 Wakorintho 10:5. Kuna fundisho gani la kiroho? Tunapaswa kujifunza nini? (Kwamba kuwa na msingi mzuri wa kiroho na mafunzo haimaanishi kwamba maisha yetu yanampendeza Mungu. Tunaweza tusifanye vizuri kwenye badiliko.)
-
- Soma 1 Wakorintho 10:6. Mungu anazungumzia nini anapoyarejea mambo haya kama “mifano?” (Jambo la msingi ni kwamba historia ni ya muhimu sana katika kufanya uamuzi wa jinsi ya kuishi. Kuna mambo machache yanayonifadhaisha na kunifanya niwe na wasiwasi juu ya mustakabali wetu. Mojawapo ya mambo hayo ni mustakabali wa uhuru wa dini na uhuru wa kiuchumi. Uhuru huo uliifanya nchi yetu kuwa nzuri. Kwa kuwa mataifa ya dunia yanaugeukia uhuru wa dini na ule wa kiuchumi, idadi ya watu wanaoishi kwenye umaskini imepungua duniani kote. Pamoja na hayo, kizazi cha sasa nchini kwangu kinatilia shaka uhuru wa dini na ule wa kiuchumi.)
- Mabadiliko ya Maisha na Historia
-
- Soma tena 1 Wakorintho 10:6. Tunapaswa kuutumiaje uhuri tunapotafakari mabadiliko? (Historia inapaswa kuongoza fikra zetu. Mabadiliko gani yanatakiwa kufanywa, na mambo gani yanatakiwa kusalia vile vile? Historia ya Kibiblia inapaswa kutufanya “tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.”)
-
- Soma 1 Wakorintho 10:7 na Kutoka 32:5-6. Tunapaswa kuepuka dhambi gani inayotokana na historia? (“Ndama” ilikuwa ni sanamu iliyotengenezwa na Haruni. Ni punde tu watu wa Mungu walikuwa wameona uwezo wake wa kushangaza, na sasa wanataka kuabudu kitu kilichotengenezwa na Haruni. Wanaweza kuwa wapumbavu kiasi gani?
-
-
- Hakuna hata mmoja wa marafiki wangu wa Kikristo aliyetengeneza sanamu nyumbani kwake na kuiabudu (au kuitumainia). Je, hili ni somo la historia ambalo halina maana tena?
-
-
-
- Je, tunaabudu vitu tunavyovitengeneza au kuvinunua? (Wakati mwingine huwa ninasikia mambo ya kipuuzi. Mtu anapokuwa na gari au nyumba nzuri mtu mwingine mwenye wivu anaviita vitu hivyo kuwa ni “vijimungu.” Suala ni ibada: endapo tunavitumaini vitu hivyo. Ikiwa vitu hivyo vinaakisi utajiri, ni rahisi kuzitumaini mali.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:8 na Hesabu 25:1-3. Dhambi gani ilikuja kwanza: uabudu sanamu au uasherati? (Kujiingiza kwenye vitendo vya uasherati na wanawake wa Moabu. Hicho ndicho kilichowaingiza kutoa kafara mbele za miungu ya uongo.)
-
-
- Soma Hesabu 25:5. Dhambi gani inaonekana kumkera Mungu zaidi? (Ibada ya uongo.)
-
-
-
- Mara zote nimekuwa nikisema (kimsingi nimehubiri majuma mawili yaliyopita) kwamba “dhambi zote ni dhambi.” Hoja ni kwamba hatutakiwi kuchagua dhambi fulani na kuzishutumu kwa nguvu zote. Je, nimekosea? Au, je, historia inatufundisha jambo jingine? (Ninaweza kuwa nimekosea, na pia historia inatufundisha fundisho jingine. Nadhani somo la historia ni kwamba kitendo cha uasherati kinatuingiza kwenye dhambi nyingine. Kwa muktadha huu, Mungu anaichukulia ibada ya Baal-peori kama dhambi mbaya zaidi.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:9-10 na Hesabu 21:4-6. Dhambi gani mbili zinafunuliwa na historia hapa? (Kunung’unika na kumjaribu Mungu.)
-
-
- Kunung’unika kunaonekana kuwa dhahiri kabisa. “Kumjaribu” Mungu ndio kufanyaje? (Huku ni kuujaribu uvumilivu wa Mungu. Kufanya mambo yanayomhuzunisha Mungu.)
-
-
-
- Kama ulikuwa pamoja nasi tulipojifunza kitabu cha Ayubu, utakumbuka kwamba Ayubu alimlalamikia sana Mungu. Hata Ayubu aliomba kumshtaki Mungu (Ayubu 9:32-33), ili aweze kumpata mtu wa kusuluhisha mgogoro wao. Kwa nini hilo lionekane kuwa sawa, na kukinung’unikia chakula kunakufanya uuawe (1 Wakorintho 10:10)? (Tofauti ya dhahiri ni kwamba manung’uniko jangwani yalihusu Mungu kutowatunza watu vya kutosha. Watu waliendelea kusema kuwa mambo yalikuwa mazuri zaidi walipokuwa watumwa. Kitendo hicho kilimtukana Mungu. Ayubu, kwa upande mwingine, alijenga hoja kwamba Mungu alikuwa hamtendei haki. Ayubu hakuwa amefanya chochote kustahili adhabu iliyomsababishia mateso. Mungu alifahamu kwamba haya yalikuwa malalamiko yenye mantiki. Katika hali ya kawaida Ayubu hakupaswa kuwa anateseka. Somo la historia kuhusu badiliko ni kwamba Mungu anayashirikisha na kuyahusisha malalamiko yetu yenye mantiki. Hata hivyo, hatutakiwi kunung’unikia baraka zake.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:11-12. Tunaona onyo gani kwenye historia? (Kwamba wengine walianguka, hivyo nasi pia tunaweza kuanguka. Hatupaswi kujigamba na kujiamini kupita kiasi.
-
- Soma 1 Wakorintho 10:13. Mungu ametuahidi nini katika suala la majaribu?
-
-
- Hii inahusikaje na badiliko? (Tunaweza, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kustahimili jaribu. Badiliko la maisha yetu linaweza (na linapaswa) kuwa chanya na si hasi.)
-
- Badiliko la Malezi
-
- Soma Zaburi 127:3-5. Tunachukulia jambo gani kuhusu watoto na ulinzi? (Kama una watoto wa kiume wengi, utakuwa na maaskari wa kukulinda.)
-
-
- Je bado hili ni jambo la msingi? (Kujiingiza kwenye mapambano kwa niaba ya wazazi kunapaswa kuwa jambo hadimu, lakini kadri wazazi wanavyoendelea kuzeeka watoto wanaweza kusaidia kuwalinda kwa namna nyingine nyingi.)
-
-
- Soma tena Zaburi 127:3. Watoto ni thawabu na “urithi kutoka kwa Bwana.” Nadhani “heritage” inamaanisha “urithi” katika muktadha huu. Kama wewe ni mzazi, ni kwa namna gani umeliona jambo hili kuwa kweli? (Mimi na mke wangu tumejifunza kwamba watoto wetu wanatufundisha mambo makubwa kumhusu Mungu na wema wake kwetu. Watoto wetu walipokuwa waasi au kutokuwa watiifu, tuliufikiria uasi wetu wenyewe na kutokuwa kwetu watiifu kwa Mungu. Lilikuwa fundisho lisilo na kifani katika kuelewa neema ya Mungu.)
-
-
- Watoto wanayabadilishaje maisha yako? (Wanayabadilisha milele. Wanayafanya maisha yawe ya thamani na yenye kutatanisha zaidi.)
-
-
-
- Soma 1 Samweli 3:12-13. Wajibu wetu ni upi kwa watoto wetu? (Kuwarejesha kwenye msitari sahihi. Kwa dhahiri, katika kipindi fulani watoto wanafanya chaguzi zao wenyewe. Hata hivyo, kwa upande wa Eli, alikuwa na mamlaka juu ya wanaye zaidi ya yale ya kuwa baba.)
-
- Badiliko la Umri
-
- Katika sehemu iliyotangulia tumejadili idadi ya wana wanaoweza kukupatia ulizi katika uzee wako. Soma Zaburi 71:9. Tunakabiliana na tatizo gani uzeeni? (Nguvu kupungua.)
-
- Soma Zaburi 71:18. Tunapaswa kuwa na mtazamo gani tunapozeeka na kupungua nguvu? (Tunapaswa kufundisha kizazi kinachofuata kwamba uwezo uko mikononi mwa Mungu wetu. Tunaweza kuwa mashuhuda na mfano wa hilo.)
-
- Soma Zaburi 71:23-24. Mtazamo wetu unapaswa kuwaje tunapozidi kuongezeka umri? (Kuimba sifa kwa Mungu. Badala ya kunung’unika, tunapaswa “kusimulia matendo ya haki [ya Mungu] mchana kutwa.”)
-
-
- Zingatia kifungu cha 24. Tutarajie nini juu ya mustakabali wa wale wanaojitahidi kutudhuru? (Aibu na kutahayarika.”)
-
-
-
-
- Nina uzoefu na teolojia inayosema kwamba tunapaswa kuomba kwa ajili ya mkanganyiko na kushindwa kwa maadui wetu. Soma Ayubu 31:29-30 na Mathayo 5:43-44. Unavilinganishaje (unavipatanishaje) vifungu hivi?
-
-
-
-
-
- Hili ndilo fundisho langu la historia: Kipindi fulani niliamua kuwaombea mkanganyiko maadui wangu kwenye kesi ya uhuru wa dini niliyokuwa ninaitetea kwenye mahakama kuu. Mwanasheria aliyekuwa upande tofauti na mimi alipoingia mahakamani, aligonga kichwa chake kwenye chuma na kuanguka chini. Alipepesuka kwenye chumba cha mahakama! Alikuwa ameumia sana, kiasi kwamba hakimu hakumruhusu awasilishe hoja zake za utetezi. Lakini, hakimu aliona (hata kutoa) hoja bora zaidi dhidi yetu na kufuta kesi yetu!
-
-
-
- Rafiki, linapokuja suala la mabadiliko tunatakiwa kuangalia mafundisho ya jinsi ambavyo Mungu aliongoza katika siku za nyuma. Tunatakiwa kuyatafuta mapenzi yake na kumtumaini kwa moyo wa upendo. Je, utakubali kulifanya hilo kuwa lengo lako?
- Juma lijalo: Unapokuwa Peke Yako.