Somo la 5: Mihuri Saba

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ufunuo 4:6)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
1
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Juma lililopita tulijifunza jambo lenye utukufu mkubwa: Yesu alifungua kitabu ambacho hakuna mtu mwingine yeyote yule (akiwemo Baba wetu wa mbinguni) “alistahili” kukifungua. Dhana ya kwamba Mungu Baba hakustahili ilionekana kuwa la kidhihaka (kimzaha), hadi tulipolitafakari kwa kina zaidi. Yesu alituokoa milele kwa maisha yake makamilifu, kafara yake msalabani, na kufufuka kwake kwa ajili yetu. Yesu aliufungua mustakabali wetu! Juma hili tunajifunza zaidi juu ya kitabu hiki na mustakabali wetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Ufunuo na tujifunze zaidi!

 

  1.     Kufungua Kitabu

 

    1.     Hebu tupitie tena Ufunuo 5:3 kwa kusoma kifungu hicho. Inamaanisha nini “kukifungua” hicho kitabu? (Somo letu juma hili linahusisha kutazama ndani ya kitabu. Tunajifunza mustakabali wetu uliowezeshwa na kile alichotutendea Yesu.)

 

      1.     Hii inazungumzia nini juu ya uelewa wa mbingu kwa kuzingatia matokeo ya utume wa Yesu hapa duniani? (Kwa kulichukulia kiuhalisia, inamaanisha kwamba mbingu hazikujua kama Yesu atafanikiwa. Mustakabali ulikuwa umefungwa na Yesu pekee ndiye angeweza kuufungua mustakabali wa mafanikio.)

 

        1.     Je, hiyo inamaanisha kwamba Mungu Baba hakujua kama Yesu atafanikiwa? (Jibu la swali hili li zaidi ya uelewa wangu. Hii inaibua maswali juu ya ujuzi wote wa Mungu (uelewa wa Mungu juu ya mambo yote) pamoja na asili ya Utatu Mtakatifu.)

 

        1.     Je, unadhani Shetani alitumia kila alichonacho katika jitihada za kumshinda Yesu msalabani? (Bila shaka uelewa wa Shetani wa mazingira na hali halisi ni mzuri zaidi kuliko uelewa wetu. Kama alifanya kila awezalo ili kumfanya Yesu atende dhambi, hiyo inatuambia kwamba alidhani angeweza kushinda.)

 

    1.     Soma Ufunuo 5:5. Mzee anatuambia kwamba ushindi wa Yesu unafungua kitabu na mihuri saba. Kwa nini hilo ni kweli? (Kwa ushindi wa Yesu, mustakabali wetu uko wazi. Tafsiri ya Mungu ya mustakabali, badala ya tafsiri ya Shetani, sasa ndiyo inayoshika hatamu. Hebu tugeukie jambo hilo katika sehemu inayofuata.)

 

  1.   Mhuri wa Kwanza

 

    1.     Soma Ufunuo 6:1-2 na ulinganishe na Ufunuo 6:15-16. Je, ulinganisho huu mfupi wa muhuri wa kwanza na wa sita unafunua jambo gani kuhusu asili ya mihuri? (Hizi ni alama muhimu katika historia kuanzia kwenye ushindi wa Yesu msalabani na ujio wake wa Mara ya Pili.)

 

      1.     Unalinganishaje jambo hili na somo letu la makanisa saba? (Makanisa saba yalifunua historia ya kanisa la Kikristo. Mihuri ni mfano: inaakisi mgongano uliopo kati ya wema na uovu.)

 

    1.     Angalia tena Ufunuo 6:1-2. Huyu mpanda farasi ni nani? (Soma Ufunuo 19:11-13. Huyu ni Yesu mshindi.)

 

      1.     Ushindi huu ni upi? (Ushindi wa Yesu msalabani. Taswira ya baadaye ya Yesu ndani ya vazi jeupe katika Ufunuo 19 ni taswira ya ujio wake wa Mara ya Pili.)

 

      1.     Yesu anatimiza “ushindi” gani katika Ufunuo 6:2? (Kuwaongoa wanadamu na kuwaleta upande wake. Yesu alishinda vita dhidi ya dhambi na Shetani, pambano linaendelea kwa ajili ya mioyo na akili za wanadamu.)

 

    1.     Soma Matendo 2:1-3 na Matendo 2:40-41. Kitu gani kiliifanya hii siku kubwa iwezekane? (Roho Mtakatifu.)

 

      1.     Unadhani “sauti ya ngurumo” iliyoelezewa kwenye Ufunuo 6:1 ni kitu gani? (Nikiilinganisha na Matendo 2 inanifanya nitafakari kwamba huyo ni Roho Mtakatifu. Upinde, kama ilivyo kwa “upinde na mshale,” unaweza kuonesha nguvu na uwezo wake kupitia hewani. Hiyo ni sehemu ya uwezo wa Roho Mtakatifu.)

 

  1. Mhuri wa Pili

 

    1.     Soma Ufunuo 6:3-4. Unadhani rangi “nyekundu” kiishara inamaanisha jambo zuri au baya? (Soma Ufunuo 12:3-4. Joka jekundu linamwakilisha Shetani, hivyo ninahitimisha kwamba hii si rangi nzuri.)

 

    1.     Soma Matendo 12:1-3. Tunaona jambo gani limeandikwa baada ya wanafunzi kuanza kazi yao ya injili? (Mateso yamekuja. Kakaye Yohana, Yakobo, alikuwa mmojawapo wa waathirika wa mwanzo. Wakristo wengine walipoteza maisha yao kutokana na kazi zao za injili.)

 

  1.   Mhuri wa Tatu

 

    1.     Soma Ufunuo 6:5-6. Rangi nyeusi inatuambia nini? (Soma Yeremia 4:27-28. Weusi ni ishara ya maombolezo. Hata leo tunavaa mavazi meusi kwenye misiba.)

 

    1.     Angalia tena Ufunuo 6:6. Gharama hizi zinaakisi nini? (Watoa maoni wanaashiria kwamba hizi ni gharama za juu sana, hivyo zinaashiria baa la njaa.)

 

    1.     Soma Matendo 11:28. Tunaona nini hapa? (Njaa kubwa katika ufalme wote wa Rumi!)

 

    1.     Soma Mathayo 24:1-7. Njaa inajitokezaje katika nyakati za mwisho? (Nimesoma maelezo kadhaa ya jinsi hali ilivyokuwa ya kutisha kule Yerusalemu wakati Rumi ilipoivamia na hatimaye kuiangamiza. Watu walikufa kwa njaa. Kwa kuongezea, njaa ni mojawapo ya ishara za mwisho wa dunia.)

 

  1.     Mhuri wa Nne

 

    1.     Soma Ufunuo 6:7-8. Rangi ya “kijivujivu” inatuambia nini? (Hii iko dhahiri, inamaanisha kifo.)

 

      1.     Nini kinatokea mhuri huu unapofunguliwa? (Robo za watu duniani ziko kwenye taabu!)

 

      1.     Mojawapo ya maoni niliyoyasoma kutoka kwa mtoa maoni mmoja yaliashiria kwamba watu hawa ni robo ya idadi ya watu wa nyakati za utawala wa Rumi, na si idadi ya watu duniani leo. Unalionaje wazo hilo? (Soma Ufunuo 9:14-16. Taarifa ya kwamba idadi ya askari wa Kalvari ni askari milioni mia mbili haionekani kuwa rejea ya sehemu ya idadi ya watu duniani katika kipindi cha utawala wa ufalme wa Rumi.)

 

    1.     Angalia kwa umahsusi katika Ufunuo 6:8. Nani anayefanya mauaji? (Mauti na Kuzimu.)

 

      1.     Soma Ufunuo 20:14. Je, Yesu yuko nyuma ya haya mauaji? (Yesu ni adui wa Mauti na Kuzimu kwa sababu anaviangamiza. Lakini, inaonekana kwamba Yesu anaruhusu jambo hili: “wakapewa mamlaka juu ya ....)

 

      1.     Tunapoangalia rejea ya Ufunuo 9, inasema kuwa theluthi ya watu walikufa. Je, Ufunuo 6:8 inasema kuwa robo ya watu wanakufa? (Hapana. Inasema kuwa Mauti na Kuzimu vilipewa mamlaka juu ya robo ya nchi.)

 

        1.     Kwa kutambua kile unachokifanya kuhusu asili ya Yesu, unadhani kwamba alianzisha jambo hili? (Kama ambavyo Adamu na Eva walivyochagua kubadili na kumpatia Shetani dunia, vivyo hivyo ninaamini kwamba watu katika sehemu hii ya dunia waliigeuzia kwa Mauti na Kuzimu. Yesu aliruhusu tu uchaguzi wao.)

 

  1.   Mhuri wa Tano

 

    1.     Soma Ufunuo 6:9-11. Je, mashahidi (wafia dini) hawa wapo mbinguni? Au, je, hii ni ishara?

 

      1.     Baadhi ya watu wanajenga hoja kwa nguvu sana kwamba kifungu hiki hakizungumzii chochote kuhusu hali ya wafu. Una maoni gani? (Soma Luka 9:30-32. Hatutajiingiza kwenye mjadala mrefu wa jambo hili, lakini Biblia inabainisha kwamba baadhi ya wanadamu walichukuliwa mbinguni moja kwa moja (Eliya) na baadhi walifufuliwa na kuchukuliwa mbinguni (Musa). Kwa kuwa Musa na Eliya ni mashujaa wa imani, sidhani kama jambo hili ni la kawaida, lakini hii inaonesha kile alichokifanya Mungu siku za nyuma. Mashahidi hawa wanaweza kuwa mbinguni.)

 

    1.     Soma tena Ufunuo 6:11. Hii inatuambia kuwa jambo gani linaendelea katika kipindi hiki cha mhuri? (Wakristo wanauawa kutokana na imani yao kama suala linaloendelea kutokea!)

 

  1. Mhuri wa Sita

 

    1.     Soma Ufunuo 6:12-14. Je, hili ni tukio la kikanda? Je, usomaji wa kutosha wa jambo hili utatimizwa kwa jambo lililotokea katika sehemu ndogo tu ya Marekani? (Rejea ya “tetemeko kuu la nchi” inaweza kuwa ni tukio la kikanda. Kwa upande mwingine, “kila mlima na kisiwa vikahamishwa” ni tukio la kiulimwengu.)

 

      1.     Je, tetemeko la ardhi linahusiana na kuhamishwa kwa visiwa? (Ikiwa ndivyo, basi hakuna hata moja kati ya mambo haya ambayo ni tukio la kikanda.)

 

      1.     Inamaanisha nini kwamba “mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa?” (Fizikia inaonesha kwamba tunaweza kuziona siku zilizopita na siku zijazo kwenye nyota. Kama vile tunavyoweza kuisikia na kuiona treni inavyotujia, vivyo hivyo tunaweza kuyaona matukio angani yakitujia. Hili ni tukio litokealo ulimwenguni kote.)

 

    1.     Soma Ufunuo 6:15-17. Ni kwa jinsi gani wafalme hawa wana muda wa kujificha? Ikiwa ujio wa Yesu Mara ya Pili ni tukio linalotokea ndani ya muda mfupi sana na ni tukio la kiulimwengu, je, waovu hawasimamishwi pale pale walipo? (Hii inaunga mkono zaidi hitimisho kwamba ulimwengu wote utayaona mambo yakitokea kwenye sayari na anga yatakayowaonesha kwamba ulimwengu unaangamia.)

 

    1.     Rafiki, je, uko tayari? Je, unataka kujificha au kushangilia Yesu atakapokuja tena? Kwa nini usikiri kwamba Yesu ni Bwana na upokee vazi lake jeupe la haki – maisha, kifo na ufufuo wake kwa ajili yako? Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

 

  1.       Juma lijalo: Watu wa Mungu Waliotiwa Muhuri.