Vielelezo vya Umoja
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mara ngapi unasema “piga picha ya jambo hili akilini?” Au, “hebu ngoja nipige picha akilini ya jambo linalotokea?” Hii si michoro wala picha, bali ni taswira za kimaneno zinazotusaidia kuelewa dhana fulani. Hilo ndilo somo letu juma hili. Taswira gani ndani ya Biblia zinatusaidia kuelewa vizuri zaidi umoja ndani ya kanisa? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!
- Taifa
-
- Soma 1 Petro 2:9. Unadhani Petro anamaanisha nini anaposema “taifa takatifu?” (Halielezei tu taifa, anaelezea muungano wa kanisa na taifa.)
-
-
- Jambo gani lisilo la kawaida kwa wananchi wa nchi yenye mfumo wa utawala/serikali ya makasisi? (Sisi sote ni makuhani wa “kifalme” tulio wa Mungu.)
-
-
-
-
- Kwa kawaida dhana gani zinakujia akilini unapomfikiria kuhani? (Yule aongozaye masuala ya kidini. Picha hii inatuambia kuwa sisi sote ni viongozi wa kidini.)
-
-
-
-
- Kazi yetu ni ipi? (Kumpa Mungu sifa!)
-
-
-
- Tulikuwa tukiishi wapi? (Tulikuwa tukiishi gizani na sasa tunaishi nuruni.)
-
-
-
- Unapoyatafakari maneno “takatifu,” “taifa,” “kuhani,” na “nuru,” je, hii inaashiria mgawanyiko wa watu? (Ndiyo. Taifa linabainisha eneo mahsusi kiutawala, ukuhani ni kundi maalumu la kazi, kitu kitakatifu ni kitu kilichotengwa kwa kusudi maalumu, na kuielekea nuru kunaashiria kuviweka vitu pamoja. Vyote hivi vinatoa picha ya mgawanyo dhidi ya mambo mengine ulimwenguni.)
-
-
- Soma 1 Petro 2:10. Hali yetu ya awali ilikuwaje? (Hatukuwa watu wa Mungu na hatukuifurahia rehema.)
-
-
- Hilo linawezekanaje? Kwani Mungu hakutupenda mara zote na kutuonesha rehema? (Muktadha ni wa muhimu. Tutachambua hilo katika sehemu inayofuata.)
-
- Hekalu
-
- Soma 1 Petro 2:4-5. Makuhani walifanya nini katika kipindi cha Petro? (Walitoa dhabihu kwa Mungu.)
-
-
- Kitu gani kinafanya dhabihu zetu zikubalike? (Tunazitoa kwa njia ya Yesu Kristo.)
-
-
-
- Tafakari jambo hili kidogo. Sababu ya dhabihu kutolewa katika Agano la Kale ilikuwa ipi? (Kuwaondolea watu dhambi zao.)
-
-
-
- Hivi ni vifungu vinavyotangulia kifungu kinachotuambia kwamba hatukuwa watu wa Mungu na hatukufurahia rehema. Utajibuje swali kuhusu endapo mara zote Mungu ametupenda na kutuonesha rehema? (Mungu alikuja kukaa nasi, kutufia na kufufuka kwa ajili yetu. Hii ilituokoa na uamuzi wetu wa kutisha wa kuugeuzia utiifu wetu kwa Shetani. Mungu alitupatia fursa ya uzima wa milele. Ni fursa yetu ya kuwa na uhusiano sahihi na Mungu!)
-
-
- Soma tena 1 Petro 2:5. Ni kwa jinsi gani tunafanana na Yesu? (Sasa sisi nasi ni “mawe yaliyo hai.”)
-
-
- Kwa nini tunaelezewa kuwa sisi ni mawe? Sina uhakika kama hivi ndivyo ambavyo ningependa kusifiwa – “Cameron, hufanani na huu mwamba: mwenye sura ya duara, mkubwa, mzito, na huyumbi.” (Sisi ni “mawe” yaliyo hai kwa ajili ya kujenga “nyumba ya Roho na kuwa na ukuhani mtakatifu.”)
-
-
-
- Kwa mara nyingine, tunaambiwa kuwa sisi sote ni “makuhani,” sehemu ya mpango mkubwa wa makuhani. Hiyo inazungumzia nini kuhusu kama sisi sote ni watendakazi wa Mungu? (Katika sehemu inayofuata tutakuwa tunajifunza picha (taswira) ya kanisa linalofanana na mwili. Hii inatuambia kuwa sote hatuna kazi moja. Lakini, sote tu wamoja kama utendakazi.)
-
-
- Soma 1 Petro 2:6. Hekalu letu lililo hai limebuniwaje? (Yesu ni jiwe letu kuu la pembeni. Tukiwa na ujasiri naye, “kamwe hatutatahayarika.”)
-
- Soma 1 Petro 2:7-8. Ikiwa mtu hayajengi maisha yake kwa Yesu, nini kinatokea? (Yesu ni mwamba tu unaotupiga ngwala, kutufanya tujikwae na kuanguka.)
-
-
- Jambo gani linasababisha kujikwaa huku? (Kutokutii.)
-
-
-
- Unaweza kulielezea jambo hili? Kwa nini kumkataa Yesu kunatufanya tusiwe watiifu? (Kwa asili sisi ni waovu. Asili yetu ya dhambi inatufanya “tusiwe watu” wa Mungu. Yesu anayabadilisha yote hayo endapo tutamkiri na kumkubali.)
-
-
- Soma 1 Petro 2:11-12. Hapo awali tulijifunza kwamba kazi yetu kama makuhani ni kumpa Mungu utukufu. Hapa tunaona kipengele gani katika kazi yetu ya kumpa Mungu utukufu? (Sisi ni makuhani, katika “taifa takatifu” kwa lengo la kuwaonesha wapagani matendo yetu mema. Hii humpa Mungu utukufu.)
-
-
- Jambo gani linatokea kwenye haya matendo mema? (“Tamaa za mwili.” Unatamani nini? Unatumia muda wako kutafakari nini? Kama hicho ni dhambi, kinasababisha “vita dhidi ya roho yako.”)
-
-
-
- Yatafakari maisha yako. Unamtukuza nani kwa matendo yako? (Sifahamu kukuhusu wewe, lakini hili ni kemeo la mara kwa mara kwangu na ukumbusho wa kuziweka tamaa zangu kwenye lengo la kweli.)
-
- Mwili
-
- Soma 1 Wakorintho 12:7-11. Nguvu gani inaunganisha uwezo huu wa aina mbalimbali? (Roho Mtakatifu. Anaongoza nani apate uwezo gani na majukumu yapi.)
-
- Soma 1 Wakorintho 12:12-13. Washiriki wa kanisa wanafananishwa na nini? (Mwili wa mwanadamu.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 3:16-17. Sasa Paulo anatuambia kuwa mwili wetu ni hekalu na Mungu anakaa ndani yake. Tunawezaje kusema kuwa mwili wetu ni hekalu na kwamba sisi ni mawe kwa ajili ya hekalu kuu lililo hai? (Kila mmoja wetu ni wa muhimu, na sote kwa pamoja ni wa muhimu kama kanisa lililo na umoja. Kipengele cha jumla ni kwamba Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, anakaa ndani yetu. Pia anaelekeza ujenzi wa hekalu kuu.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:14-20. Tunaonywa dhidi ya nini? Wivu wa mkono? (Tunapaswa kutambua umuhimu wa nafasi yetu kanisani. Kila nafasi ni muhimu kwa mwili kuweza kufanya kazi vizuri.)
-
-
- Je, tunapaswa kuridhika na nafasi yetu? (Soma 1 Wakorintho 12:29-31. Hii inatuambia “tutamani sana karama zilizo kuu.”)
-
-
-
- Kuna tofauti gani kati ya husuda na kutamani karama zilizo kuu? Je, umewaona washiriki wa kanisa waliotamani jukumu la mshiriki mwingine wa kanisa? (Miongo kadhaa iliyopita nilikuwa na mshiriki wa darasa la kujifunza Biblia ambaye alikuwa anaanza kuuliza maswali ya wanadarasa wengine. Kama mwalimu ningeweza tu kukaa chini, kwa sababu sasa alikuwa anauliza maswali. Hili halikuwa wazo langu kwa kile ilivyomaanisha kwangu kufundisha darasa, hivyo kanisa likampa mtu huyo (mwanamke) nafasi ya kufundisha darasa lake mwenyewe. Ndani ya majuma kadhaa, watu waliacha kuhudhuria kwenye darasa lake, naye akaondoka na kuliacha kanisa. Naamini hii inaelezea tatizo la kusema “kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili.”)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:21-24. Paulo anatuonya kuwa makini na nini? (Sio tu kwamba kila jukumu kanisani ni la muhimu, bali pia hakuna mtu anayepaswa kudharau wajibu/jukumu la mtu mwingine.)
-
-
- Je, hii ni silaha nyingine dhidi ya wivu? (Ndiyo. Wivu unaweza kuanza kwa sababu washiriki wa kanisa wanahisi kwamba baadhi ya majukumu ni ya muhimu zaidi ya mengine.)
-
-
-
- Paulo anatoa ushauri gani mahsusi kwa kanisa katika kupambana na tatizo la kudhani kuwa majukumu fulani hayana maana sana? (Tunatakiwa kuzitendea kazi hizo kwa “heshima ya pekee.” Tunatakiwa kuwasifia na kuwashukuru hadharani wale wanaofanya kazi hizo. Kuwa “msitari wa mbele” kumejijenga kwenye karama. Tunatakiwa kuwazawadia wale wanaotenda kazi ambazo kwa asili hazina thawabu.)
-
- Wazamiaji
-
- Soma Yohana 10:1-6. Biblia inatuambia kuwa watu hawakuelewa kile alichokuwa anakisema Yesu. Je, unaona fundisho lolote la umoja katika jambo hili?
-
-
- Unadhani Yesu anamaanisha nini anapozungumzia kuzitambua sauti? (Tunatakiwa kuitambua sauti ya Mungu.)
-
-
-
- Unapoyafikiria masuala ya umoja kanisani, mambo gani kati ya hayo yanaibuka kutokana na kutoyaelewa mapenzi ya Mungu, kuielewa “sauti” yake [Mungu]? (Mwizi na mnyang’anyi wanaweza tu kufanikiwa kwa wale kondoo wasiomjua mchungaji wao.)
-
-
-
-
- Tunawezaje kuijua sauti ya Mungu? (Kwa kufanya kile unachokifanya sasa hivi, kujifunza neno la Mungu. Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie uelewa unapoisoma Biblia na ujaribu kuuelewa ujumbe wake.)
-
-
-
- Rafiki, je, hizi picha za Biblia za taifa, hekalu, jiwe, mwili na kondoo zinakusaidia kuelewa vizuri zaidi anachokifikiria Mungu kwa ajili ya umoja wetu? Je, utatimiza sehemu yako, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuleta umoja zaidi kanisani kwako?
Juma lijalo: Migogoro Inapoibuka.