Somo la 3: Mungu au Mali?
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Katika somo letu la kwanza kwenye huu mfululizo wa masomo yetu tulijifunza kuwa ikiwa tutautafuta Ufalme wa Mungu, basi atatupatia vitu vyote ambavyo wapagani wanavisaka (Luka 12:30-31). Ikiwa hiyo ni kweli, basi je, kichwa cha somo hili kina upotoshaji? Je, kuwa mtumishi wa Mungu hakuendani na kuwa na fedha? Ikiwa hakuendani, tunawaelezeaje mashujaa wa Agano la Kale ambao kwa ujumla walikuwa watu matajiri? Kwa upande mwingine, kwa ujumla mashujaa wa Agano Jipya walikuwa maskini. Hivyo basi, je, huu ni mgongano kati ya haya maagano mawili ya Biblia? Au, je, kuna ujumbe mmoja katika Biblia unaohusu utajiri? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kama tunaweza kupata ujumbe wa Mungu kuhusu utajiri!
- Mtawala Kijana Tajiri
-
- Soma Mathayo 19:16. Je, unafurahia jibu la Yesu kwa swali hili? (Hili ni jibu la muhimu sana kupita majibu yote hapa duniani! Yesu anakaribia kutoa ufunguo wa kuingia kwenye uzima wa milele.)
-
- Soma Mathayo 19:17. Kwa nini Yesu anauliza swali hili? Yesu ni Mungu! Unaona mantiki yoyote kwa mwitiko wa awali wa Yesu kwenye hili swali la muhimu sana? (Hebu tuliweke tatizo hili akilini mwetu na tulijadili baadaye.)
-
- Angalia tena nusu ya mwisho ya Mathayo 17:17. Yesu anatoa jibu gani? (Zishike Amri Kumi.)
-
-
- Siku chache zilizopita tumemaliza kujfunza vitabu vya Wagalatia na Warumi. Je, Paulo atapata mshtuko wa moyo kwa jibu hili? (Soma Warumi 3:28. Hatuwezi kukitegemea kifungu kimoja pekee kujenga teolojia yetu, lakini huenda Paulo angesema kuwa, “Yesu, ninahitaji kuelewa vizuri zaidi kile unachokisema.”)
-
-
- Soma Mathayo 19:18-19. Unalichukuliaje swali la kijana huyu? Je, baadhi tu ya amri ndizo za muhimu? Swali hilo linaonekana kuwa la dhihaka!
-
-
- Ikiwa unadhani kuwa swali la kijana huyu lilikuwa linahangaisha akili, vipi kuhusu jibu la Yesu? Ananukuu amri nne tu kati ya Amri Kumi (anaacha amri inayohusu Sabato, amri inayohusu kutamani, na amri zote zinazohusu wajibu wetu kwa Mungu – angalia Kutoka 20:1-17), na kisha Yesu ananukuu kwa ufupi nusu ya pili ya Amri Kumi (Angalia Mathayo 22:36-40). Ikiwa tunaupata wokovu kwa kuzishika amri, kwa nini huu uchaguzi mahsusi wa amri?
-
-
- Soma Mathayo 19:20. Habari njema! Uchaguzi wa amri zilizonukuliwa na Yesu ndizo hasa ambazo kijana huyu amekuwa akizishika. Mpatie tiketi yake ya kuingia mbinguni, sawa?
-
- Soma Mathayo 19:21. Nani aliyesema jambo lolote kuhusu kuwa mkamilifu? Huyu kijana aliuliza tu kile anachotakiwa kukifanya ili kuupata uzima wa milele! Kwa nini Yesu anaongezea matakwa ya ukamilifu?
-
-
- Au, je, unatakiwa kuwa mkamilifu ili kumfuata Yesu?
-
-
-
- Na, kwa nini ni sahihi kwa Yesu kurekebisha swali lake la awali kwa kuongezea matakwa (ambayo hayakuelezewa mahali popote katika amri) kwamba kijana huyu lazima auze vyote alivyo navyo na kuwapa maskini?
-
-
-
- Soma Warumi 3:19-20 na Wagalatia 3:10-11. Je, mafundisho ya Yesu na Paulo yanakinzana moja kwa moja? Au, je, Yesu anauthibitisha ukweli wa kile anachokiandika Paulo – kwamba lengo la sheria ni kufumba kinywa cha vijana wadogo wanaodhani kuwa wanazishika sheria kikamilifu? (Soma Mathayo 19:22. Kura yangu ni kwamba Yesu na Paulo wanakubaliana. Yesu anathibitisha jambo kwamba alichokisadiki mtawala huyu mdogo tajiri kwenye swali lake (Mathayo 19:16) kuwa unaweza kutenda jambo ili kuingia mbinguni ni makosa. Kijana huyu hawezi kufanya anachokisema Yesu juu ya kinachotakiwa na sheria.)
-
-
- Hebu turejee kwenye swali tuliloliacha likielea. Soma tena Mathayo 19:17. Je, sasa swali la Yesu lina mantiki? Yesu alikuwa anajaribu kumfanya kijana huyu tajiri akiri jambo gani? (Soma Wagalatia 3:21-24. Yesu alitaka kijana huyu mdogo tajiri akiri kwamba Yesu ni Mungu.)
-
-
- Ikiwa kijana tajiri alitambua umuhimu wa swali la Yesu, na kulijibu kwa usahihi, unadhani Yesu angemwambia kuuza vyote alivyo navyo? (Sidhani. Jambo la muhimu katika mazungumzo kati ya Yesu na kijana tajiri hayakuhusu fedha (ingawa ninaamini hii ilionesha kijana huyu alizitegemea fedha zake badala ya kumtegemea Mungu), badala yake yalihusu jinsi wanadamu wasivyoweza kujiokoa wenyewe kwa kuzishika sheria.)
-
-
- Hebu tuangalie kichwa cha somo hili. Je, Mungu au mali ni suala la uchaguzi? (Naam, ikiwa unataka kuelewa jinsi ya kwenda mbinguni: amini kwamba Yesu ni Mungu, na kubali (kiri) kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zako, hivyo kukupatia tiketi ya uzima wa milele! Kutafuta fedha, kugawa (kutoa) fedha, hakuna chochote kinachohusiana na fedha kikupatiacho tiketi ya kwenda mbinguni. Matendo hayawezi kukuokoa.)
-
- Soma Mathayo 19:23-26. Je, hii inakinzana na kile tulichokihitimisha hivi punde? Kwamba hakuna kinachohusiana na fedha kikupatiacho tiketi ya kwenda mbinguni? (Kisa kinaonesha kuwa kijana huyu hakuwa tayari kuacha kuzitegemea fedha zake na kumtegemea Yesu. Hiyo ndio changamoto kwa wale walio matajiri – kwamba wasizitegemee fedha zao, bali wamtegemee Mungu. Kuzitegemea fedha ni mfumo mwingine tu wa kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo, mfumo mwingine wa kuabudu sanamu. Humtegemei Mungu, bali unakitegemea kile ulichokitengeneza kwa mikono yako miwili.)
- Karama (Zawadi) ya Mali
-
- Soma Luka 16:13. Hapa ndipo mahali kwenye Biblia ambapo kichwa cha habari cha somo letu kinapatikana. Tafsiri ya Biblia ya Mfalme Yakobo (King James Version) inaziita fedha “mali.” Je, kifungu hiki kinakusaidia kuelewa vizuri zaidi kisa cha mtawala kijana tajiri? (Alikuwa hautafuti Ufalme wa Yesu kwanza. Yesu alimwomba kijana amchague yeye, badala ya kuchagua fedha zake.)
-
-
- Mfano unaofuata ni maelezo ya Yesu kwenye msemo wa kwamba huwezi kumtumikia Mungu na fedha. Hebu tuone kama tunaweza kuona mantiki yoyote!
-
-
- Soma Luka 16:1-4. Mashtaka dhidi ya meneja ni yapi? (Hatunzi fedha kwa maslahi bora ya bwana wake tajiri.)
-
-
- Je, meneja ana wasiwasi juu ya mustakabali wake? (Ndiyo. Lakini, anao mpango.)
-
-
- Soma Luka 16:5-7. Unauchukuliaje mpango wa meneja? (Kwa hakika si jambo la uaminifu! Anajipendelea yeye mwenyewe dhidi ya bwana wake – hata kama ni fedha za bwana wake. Anapaswa kutimuliwa kazi, sawa?)
-
-
- Je, meneja anaweka fedha mbele kuliko Ufalme wa Mungu? (Bila shaka!)
-
-
- Soma Luka 16:8. Subiri, subiri, subiri! Ni nini hiki? Je, Yesu anasema kuwa wabadhirifu, kama huyu meneja, ni werevu kuliko Wakristo wanaomtii Mungu? (Wao ni “werevu.” Wanaonesha akili ya kawaida zaidi.)
-
- Soma Luka 16:9. Nani anayezungumza sasa? Je, bado hii ni sehemu ya kisa? (Hapana. Sasa Bwana wetu Yesu anakielezea kisa.)
-
-
- Lazima “makao ya milele” yatakuwa yanazungumzia mbingu. Je, tunapaswa kuwa wabadhirifu wa fedha kwa werevu kwa jina la Mungu ili kukaribishwa mbinguni? Na, hii inatusaidiaje katika suala la kumchagua Mungu au mali – suala linalotakiwa kuwa ujumbe mkuu wa kisa hiki? (Anachokimaanisha Mungu ni kwamba Wakristo wanapaswa kutumia akili ya kawaida kwenye suala la fedha. Wanapaswa kuzitumia “kuwapata marafiki” (kuwaongoa wapagani) ili kwamba wote waweze kukaribishwa mbinguni.)
-
-
-
- Hii inazungumzia nini kuhusu uchaguzi kati ya Mungu na fedha? (Lengo si fedha. Hata hivyo, fedha ni zana ya kawaida na ya muhimu katika kuutangaza Ufalme wa Mungu.)
-
-
- Soma Luka 16:10-12. Je, tusihitimishe kwamba meneja asiye mwaminifu na mbadhirifu kamwe hapaswi kuaminiwa kwa fedha nyingi? Licha ya yote hayo, Yesu anamsifia. Hapa Yesu anamaanisha nini? (Ikiwa hutumii akili ya kawaida kwenye fedha zako, ikiwa huzitumii “kutengeneza marafiki” kwa ajili ya Ufalme kwa njia ya werevu, Mungu hatakuamini kwa fedha nyingi!)
-
-
- Utaona kwamba kifungu cha 11 kinazungumzia “mali ya kweli.” Unadhani Yesu anamaanisha nini kwa mali ya kweli? (Huenda Yesu anamaanisha kwamba ikiwa hatutumii fedha zetu kuutangaza Ufalme wa Mungu, hatatuamini kwa karama za roho kwa ajili ya kuutangaza ufalme. Kwa hakika, Yesu anazungumzia mambo zaidi ya fedha.)
-
-
- Soma tena Luka 16:13. Kwa kuwa sasa tumeshajifunza kisa ambacho kifungu hiki kinakihitimisha kwa ufupi, unadhani kisa hiki tunapaswa kukielewaje?
-
- Rafiki, una mtazamo gani dhidi ya fedha na mali? Yesu anatutaka tuweke tumaini letu la uzima wa milele kwake, badala ya kuliweka kuliweka kwenye fedha zetu. Fedha si mbaya, bali kuzitumaini ni tatizo kubwa. Badala ya kuzitumaini fedha, tunatakiwa kutumia akili ya kawaida kwenye fedha kama zana za kuwavuna marafiki kwa ajili ya uzima wa milele! Kwa nini usijitoe kufanya hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Kuepuka Njia za Ulimwengu.