Somo la 11: Wateule

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Warumi 10 - 11)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
4
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Kwa namna nyingi Injili ya Yesu ni tofauti kabisa na utamaduni wa kawaida. Bidii ya kazi, kujitegemea kupita kiasi, kutaka kutenda mambo kwa usahihi hata kama unakosea – yote haya yanakinzana na somo letu la leo tunapozungumzia suala la wokovu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Warumi ili tuone kama tunaweza kuelewa vizuri zaidi ujumbe wa Mungu kwetu kuhusu wokovu!

 

  1. Injili ya Kweli

 

    1. Soma Warumi 10:1-4. Unaweza kuwa na ari (kufanya kazi kwa bidii) ya Mungu na bado usiokolewe? (Naam.)

 

      1. Jambo gani jingine linahitajika, ukiongezea kufanya kazi kwa bidii? (Maarifa. Hii ni habari mbaya kwa wale wasiojali kuielewa injili kwa usahihi.)

 

      1. Hebu tuhakikishe kuwa tunaelewa jambo hili kwa usahihi. Paulo anatuambia kuwa imani katika kazi ya Yesu kwa ajili (niaba) yetu ndio ufunguo wa haki. Bidii ya kumtafuta Mungu, ikiambatana na kutoielewa injili ni njia ya kuelekea upotevuni. Je, hiyo ni kweli? Je, unawafahamu watu walio kwenye hiyo njia?

 

      1. Angalia tena Warumi 10:4. Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa Yesu ni “mwisho wa sheria?” (Yesu alikomesha hukumu ya sheria. Hiyo ndio sababu wale wanaoamini katika Yesu wanaokolewa, na wale wanaoamini kuwa lazima wazishike Amri Kumi (na sheria nyingine zote) kama njia yao ya kupata wokovu wamepotea. Kwa nini wamepotea? Hawajakiri kile alichowatendea Yesu na hivyo hukumu ya sheria inasalia kwa ajili yao.)

 

    1. Soma Warumi 10:5. Je, uliwahi kuamini hivyo? Kwamba wale walio Wakristo wa kweli wanaitii sheria na hivyo wanaonesha kuwa wana haki? Bado unaiamini?

 

    1. Soma Warumi 10:9-12. Kanuni ya kweli ya wokovu ni ipi? (Kukiri kwamba Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Mungu alimfufua Yesu kutoka katika wafu.)

 

      1. Ngoja nikuulize maswali mawili. Je, jambo hili linaweza kuwa la dhahiri zaidi ya hapo? Je, unaliamini?

 

      1. Hebu tuangalie tena Warumi 10:11. Je, bado unazingatia upande wa utii katika suala la kuwa Mkristo? Ikiwa ndivyo, unadhani hii inamaanisha nini? (Tukimtumaini Yesu, tutamtii. Hii inatufundisha kuwa utii wa sheria ya Mungu unatuepusha na fedheha. Uhusiano wetu na Mungu una kipengele cha wokovu (kuamini na kukiri) na kipengele cha uhalisia wa maisha (kutii na kuishi maisha mazuri).)                                                                                               
  1. Fursa Yetu

 

    1. Soma Warumi 10:14-15. Wajibu wetu ni upi kwa kuzingatia huu ujumbe wa injili? (Kuwaambia wengine ili wasikie na kuelewa!)

 

    1. Soma Warumi 10:16-18. Je, wote watakaoisikia injili wataipokea?

 

      1. Utaona kwamba Warumi 10:18 ni nukuu kutoka Zaburi 19:4. Unakumbuka “sauti” ni nini katika Zaburi 19? (Soma Zaburi 19:1-4. Mbingu zinatangaza sio tu utukufu wa Mungu, bali pia Paulo anatuambia kuwa zinamtangaza Yesu.)

 

        1. Unadhani kwa nini hii ni kweli?

 

    1. Soma Warumi 10:19-21. Je, Israeli, iliyosikia injili, haikuielewa injili? (Mwelekeo wa jibu ni kwamba Israeli iliielewa, na waliukataa ujumbe kwa sababu walichagua kuwa “watu wasiotii na wakaidi.”)

 

      1. Je, hii kauli ya “watu wasiotii na wakaidi” si kauli ya ajabu kwa watu waliokataa kuhesabiwa haki kwa imani? (Hawatii na ni wakaidi kwa sababu walimkataa Yesu pamoja na kazi yake kwa ajili yao.)

 

      1. Utaona kwamba vifungu hivi vinazungumzia Israeli kuwa na “wivu” na “hasira.” Kwa nini? (Wale ambao hawakuchaguliwa kuwa wajumbe wa Mungu walimwamini Yesu.)

 

        1. Je, hiyo bado ni kweli leo – kwamba wale wanaoukandamiza utii wa sheria kama njia ya kupata wokovu wana wivu na hasira kwa wale wanaookolewa kwa neema pekee?

 

  1. Wateule

 

    1. Soma Warumi 11:1-4. Je, tutajua watu wangapi wamesalia kuwa waaminifu kwa Mungu katikati ya mateso?

 

    1. Soma Warumi 11:5-6. Unadhani kwa nini Paulo anawalinganisha wale wanaoamini katika wokovu kwa njia ya neema na wale walioponea mateso?

 

      1. Kwa nini Paulo anawalinganisha wale wanaotangaza wokovu kwa njia ya matendo na wale “waliopiga goti mbele ya Baali?” (Inaleta mantiki kamili kwamba ibada ya sanamu ni kuabudu kile ulichokitengeneza – ambayo kimantiki ni sawa na “kuabudu” utii wako wa sheria.)

 

    1. Soma Warumi 11:7-10. Hapa “wateule” ni akina nani? (Sio wale ambao kwa asili waliteuliwa, Israeli, bali Mataifa ambao kwa asili hawakuteuliwa kuwa watu wa Mungu kupeleka injili yake.)

 

      1. Kwa nini Mungu amzuie mtu asiielewe injili? (Soma Warumi 11:11-12. Sielewi kwa usahihi anachokiandika Paulo, lakini kilicho wazi ni kwamba Israeli inaweza kuokolewa – ama kwa hakika, injili kupenyezwa kwa Mataifa ni njia ya kutenda jambo hili.)

 

 

    1. Soma Warumi 11:13-16. Matumaini ya Paulo kwa Wayahudi ni yapi? (Watakuwa na wivu kwa kile Mungu anachokitenda kupitia kwa Mataifa na wataipokea imani katika Yesu.)

 

      1. Hebu turejee nyuma kidogo kwenye mjadala wetu wa Mungu kutoa “roho ya usingizi” (Warumi 11:8) kwa Israeli. Je, Wayahudi walikuwa wanatimiza wajibu wao kupeleka habari za Mungu ulimwenguni kote? (Hapana. Kwa ujumla, walishindwa kuelewa uhusiano kati ya huduma ya patakatifu na utume na ujumbe wa Yesu.)

 

        1. Ikiwa Mungu hakutenda jambo lolote, matokeo yangekuwaje? (Kazi yake ingeshindw)

 

        1. Badala yake, wale “waliotiwa upofu” wasiuone ukweli waliwatesa wale waliomkiri Yesu. Mateso yaliyofuatia yaliwatawanya waumini wa Kiyahudi ulimwenguni kote. Je, hizi kauli za “usingizi” wa Paulo na “wasiweze kuona” zinaleta mantiki kwako?

 

    1. Soma Warumi 11:17-21. Paulo anaelezea dhambi gani tunayopaswa kuiepuka? (Kiburi.)

 

      1. Paulo anatuambia kuwa tunatakiwa kuogopa kile ambacho Mungu anaweza kukitenda. Kwa nini? Je, hatukuwa tukijadili upendo mkuu wa Mungu na rehema yake kwetu? (Huo ndio unaoonekana kuwa ujumbe, hatuwezi kujisifu kwa kuwa neema ni karama. Ikiwa tunafundisha kwamba lazima mambo fulani yatendeke ili kuipokea karama, basi tunaweza kukatiliwa mbali” kama Wayahudi walivyokatiliwa mbali kwa kujibidiisha dhidi ya karama ya Yesu.)

 

    1. Hebu turuke vifungu kadhaa. Soma Warumi 11:25-27. Paulo anatoa utabiri gani juu ya mustakabali wa Israeli? (Katika kipindi fulani Israeli itamkiri Yesu.)

 

    1. Soma Warumi 11:28-32. Mungu “amewafungaje wote pamoja katika kuasi?” (Sisi sote ni wadhambi. Baada ya uamuzi wa Adamu na Eva, tulizaliwa na asili ya dhambi. Mungu ameturehemu sisi sote.)

 

      1. Paulo anabainisha ujumbe gani mwingine kwenye hivi vifungu? (Ukweli kwamba taifa la Kiyahudi liligeuka na kuuacha wito wa Mungu inaakisi ukweli tu kwamba sisi sote ni wadhambi na Mungu anaendelea kutupatia rehema yake kwetu wote.)

 

    1. Soma Warumi 11:33-36. Tulipokuwa tunajadili Warumi 11, je, ulikuwa na tatizo kuelewa mambo yote aliyoyaandika Paulo? Nukuu hizi kutoka Isaya 40:13 na Ayubu 41:11 zinasaidiaje katika kuelezea ugumu wetu? (Ingawa Mungu anatutaka tujifunze neno lake ili kumjua zaidi, inafikia hatua ambapo tunasema tu kwamba “sina uhakika kama ninaelewa. Mungu ni Mungu na mimi si Mungu.” Katika hatua hiyo, jibu letu linapaswa tu kuwa kwamba tunamtumaini Mungu.)

 

  1. Rafiki, ujumbe wa Paulo juma hili ni kwamba ujumbe wa injili ni mwepesi. Wokovu hupatikana kwa kukiri kwamba Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Mungu alimfufua Yesu kutoka katika wafu. Tukilifanya jambo hili kuwa gumu, na kudai kwa kiburi kuwa juhudi za ziada zinahitajika, basi tuko kwenye hatari ya kukatiliwa mbali na kifo, kama ilivyokuwa kwa Israeli. Hata kama katika siku za nyuma uliifanya injili ionekane kuwa ngumu, habari njema kuu ni kwamba Mungu bado ananyoosha mkono wake kwa Israeli, na anaunyoosha mkono wake kwako. Je, utarejea kwenye ujumbe rahisi wa wokovu kwa imani pekee?

 

 

Juma lijalo: Kuushinda Uovu kwa Wema.