Somo la 6: Adamu na Yesu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, ungependa kuwa na amani zaidi maishani mwako? Wasiwasi, hofu, na dukuduku ni vipengele vikubwa katika maisha ya watu wengi. Injili inatoa ahadi ya amani. Lakini, kwa nini inatoa ahadi hiyo? Sababu moja kubwa ni kwamba Mungu anatupenda. Mtawala wa Ulimwengu anakupenda! Hilo lilitokeaje? Hebu tuzame kwenye somo letu la Warumi ili tujifunze zaidi!
- Amani
-
- Soma Warumi 5:1-2. Jambo gani linatupatia amani kwa Mungu? (Neema – kuhesabiwa haki kwa njia ya imani.)
-
-
- Warumi 5:2 inasema “tumepata.” Tumepata kuifikia nini au kumfikia nani? (Kuifikia neema, kumfikia Mungu! Kama kuna mtu unayetakiwa kumtii, basi ni Mungu. Paulo anaandika kuwa neema inatupatia amani ya jinsi ya kumfikia Mungu.)
-
-
-
- Warumi 5:2 pia inasema kuwa “kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.” Ninapenda amani. Lakini, ninapendelea kufurahi. Unadhani tumaini la utukufu wa Mungu ni kitu gani? (Nadhani hii ni ahadi yetu ya mbingu mpya na nchi mpya. Ukichukulia kwa “mtazamo mpana” matatizo yako ya sasa, unaweza kuwa na amani, lakini zaidi ya hapo unaweza kufurahi katika hatima ya mambo yote.)
-
-
- Soma Warumi 5:3-4. Paulo anaandika juu ya kufurahi wakati wa mateso. Hiyo ni dhana ngumu kuielewa. Paulo anatuambia kuwa hili linawezekanaje? (Paulo anatuambia kuwa mateso yanatuingiza kwenye mfululizo wa kuboresha mtazamo unaotuongoza kwenye “tumaini.”)
-
-
- Ninaona tatizo tunalotakiwa kulitatua. Warumi 5:1-2 inatuambia kuwa kuipokea neema hutuongoza kufurahi “katika tumaini la utukufu.” Kwa nini tusichukue njia hiyo ya tumaini badala ya kutumia njia ya mateso, ustahimilivu, na tabia kulifikia tumaini?
-
-
-
- Je, kuna njia ngumu na rahisi ya kulifikia tumaini? Kwa nini tusitumie njia rahisi? (Paulo hakutuambia kwamba haki kwa imani inatuepusha na mateso. Alituambia kuwa inatuongoza kwenye amani na tumaini. Tunapopata mateso, tunaweza kufurahi kwa kuwa tunafahamu kwamba mateso hayaharibu tumaini letu, badala yake yanatuelekeza kwenye tumaini.)
-
-
- Soma Warumi 5:5. Je, umewahi kutimiza lengo na kubaini kuwa haliridhishi kuliko vile ulivyotarajia? Je, tutasikitika tutakapofikia hatua ya tumaini? (Hapana.)
-
-
- Kwa nini? (“Kwa sababu pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu.” Sina uhakika ni kwa jinsi gani hili linahusiana na tumaini, lakini hebu tuangalie kile tunachoweza kujifunza Paulo anapoendelea kuzungumzia suala hili.)
-
- Upendo
-
- Soma Warumi 5:6-8. Jambo gani linakifanya kitendo cha Yesu kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu kuwa kitu kisichokuwa cha kawaida? (Paulo anaashiria kwamba kwa kawaida huu ni uamuzi unaotokana na mantiki ya kawaida – tunayatoa maisha yetu kwa ajili ya mtu atakayefanya kujitoa huko kuwe na maana. Lakini, Yesu alikufa kwa ajili ya wadhambi. Alikufa kwa wale ambao hata hivyo hatima yao ni kifo.)
-
-
- Utaona kwamba Warumi 5:6 inasema kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu “hapo tulipokuwa hatuna nguvu.” Hiyo inaongezea nini kwenye kafara ya Yesu isiyo ya kawaida kwa ajili yetu?
-
-
- Sasa turejee kwenye ile kauli iliyopo katika Warumi 5:5 inayozungumzia jinsi ambavyo tumaini halitatusikitisha kwa kuwa “pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu.” Kwa kuzingatia kile kilichoelezwa kwenye Warumi 5:6-8, je, hili sasa linaonekana kueleweka kwa urahisi? (Mungu alitupenda na kufa kwa ajili yetu wakati ambapo hatukustahili, wakati ambapo uamuzi wake haukuonekana kuwa na mantiki. Hii inatufanya tuwe na furaha kwa sababu hatuna haja ya “kufanyia kazi” msingi wa tumaini letu la kwenda mbinguni. Kama ilivyo kwa wokovu, ni karama ya bure. Hivyo, tunaweza kufurahi kwa kuwa tuna uhakika nayo!)
-
-
- Hatutaki kukosa kipengele cha ahadi cha Roho Mtakatifu kilichoelezewa katika Warumi 5:5. Wajibu wa Roho Mtakatifi ni upi?
-
-
- Soma Warumi 5:9-11. Kifungu cha 11 kinatuambia kuwa “tumeupokea upatanisho.” “Upatanisho” ni kitu gani? (Ni urejeshaji wa urafiki. Kuwafanya watu wawili wawe marafiki tena.)
-
-
- Ninamwona Mungu wa upendo na ukarimu hata katika Agano la Kale. Kwa nini itokee Mungu asiwe na urafiki na sisi? (Warumi 5:9 inasema kuwa “tunaokolewa na ghadhabu ya Mungu.” Lazima hiyo inamaanisha ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi inayoibuka katika ulimwengu wetu. Lazima imaanishe kuwa Mungu mkamilifu na mtakatifu haendani (hafungamani) na dhambi. Hivyo, tulipokuwa wadhambi ambao hatujafunikwa na kafara ya Yesu, hakukufungamana na Mungu.)
-
-
- Soma Warumi 5:12. Nani ambaye ni chanzo cha tatizo letu la dhambi? (Lazima huyo “mtu mmoja” ni Adamu.)
-
-
- Je, kwako wewe hicho kinaonekana kutokuwa kitendo cha haki? Je, dhambi ya Adamu inapaswa kukufanya uukose uzima wa milele? (Kifungu cha 12 pia kinaongezea “kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Unastahili mauti ya milele kwa sababu ya dhambi yako.)
-
-
- Soma Warumi 5:13-14. Je, pamewahi kutokea muda wowote tangu dhambi ya Adamu ambapo hatukuwa na dhambi hapa duniani? (Hapana. Kabla sheria haijatolewa, dhambi ilikuwepo ulimwenguni.)
-
-
- Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa “dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria?”
-
-
-
-
- Ikiwa Paulo anamaanisha kuwa dhambi haikuadhibiwa, tunawezaje kumwelezea Kaini na Gharika? Kaini aliadhibiwa kwa mauaji na wale waliokataa kuingia kwenye safina waliadhibiwa. Hili linaweza kuelezewaje? (“Kuzingatia” jambo fulani ni kuliweka katika kumbukumbu na kuliweka kwenye mpangilio mzuri. Nadhani Paulo anasema tu kwamba hatukuwa na kauli ya mpangilio wa dhambi kabla ya Amri Kumi. Hata hivyo, bado dhambi ilikuwepo na wanadamu bado walikufa kama matokeo ya kuingia kwa dhambi katika ulimwengu wetu.)
-
-
-
- Soma Warumi 5:15 na usome tena mwishoni mwa Warumi 5:14. Nani huyo “atakayekuja” ambaye atakuja baada ya Adamu? (Yesu!)
-
-
- Ni kwa jinsi gani hii ni kweli? (Dhambi moja ya Adamu ilituingiza sisi wote dhambini. Maisha, kifo na ufufuo wa Yesu vilitutoa dhambini – ikiwa tutavikubali.)
-
-
- Soma Warumi 5:16. Warumi 5:15 inatuambia “karama haikuwa kama lile kosa,” na Warumi 5:16 inarudia kusema kuwa “karama ya Mungu” si sawa na “matokeo ya dhambi ya mtu mmoja.” Kauli hizi zinatofautianaje? (Kwa kiwango cha kawaida kabisa, moja huleta mauti na nyingine huleta uzima. Endapo hii ilikuwa inahusu ubora wa taulo ya karatasi, au ufanisi wa sponji, dhambi moja ya Adamu ilisababisha jinamizi. Lakini, matendo ya Yesu kwa ajili (niaba) yetu yalitusafisha (yalitufuta) dhambi zetu zote. Ni dhambi moja dhidi ya utanguaji wa dhambi nyingi.)
-
-
- Hebu tuangalie sehemu ya mwisho ya Warumi 5:16. Matendo ya Yesu yalituletea nini maishani mwetu? (Haki.)
-
-
-
-
- Hivi karibuni nilisoma kauli iliyosema kuwa Yesu aliondoa tu dhambi zetu. Hivyo, tunatakiwa kufanya jambo la ziada ili kuwa na uhusiano sahihi na Mungu. Kifungu hiki kinazungumzia nini kuhusu wazo hilo? (Yesu huleta haki. Kujaribu kuongezea matendo yetu ni sawa na kubandika mapambo ya bei chee kwenye vazi kamilifu la haki tulilopewa na Yesu.)
-
-
-
- Soma Warumi 5:17. Tunapokea nini kutoka kwenye karama ya Yesu? (Uzima!)
-
-
- Kifungu hiki kinaongezea nini kwenye mjadala wetu wa kifo cha Yesu kutangua dhambi zetu? (Kinasema Yesu anatupatia “kipawa cha haki.” Yesu hakutangua tu dhambi zetu. Anatupatia kipawa chanya cha haki.)
-
-
- Soma Warumi 5:18-19. Tunaposoma mwanzoni hii inaonekana kusema kuwa moja kwa moja Adamu alitufanya sisi wote kuwa wadhambi, na moja kwa moja Yesu alituokoa sisi wote. Je, ni kweli kwamba kila mtu anaokolewa?
-
-
- Utaona kwamba tafsiri ya NIV inasema “watu wote kuhukumiwa,” na baadaye, “wote (wengi) wahesabiwe haki.” Hii inaonekana kama si wote wanaokolewa, bali “wengi” wanaokolewa. Tatizo ni kwamba neno la Kiyunani lililotumika kwa “wote” ni neno lile lile lililotumika kwa “wengi.” Hiyo inaathirije mtazamo wetu wa jambo hili? (Soma Warumi 3:22. Paulo anasema tu kwamba wokovu kwa njia ya imani inapatikana kwa watu wote. Hasemi kwamba wokovu huwajia wale wanaoyakiri maisha, kifo na ufufuo wa Yesu.)
-
-
- Soma Warumi 5:20-21. Kwa nini Mungu atake dhambi (“kosa”) iongezeke? (Nadhani hii inamaanisha kuwa uelewa wetu wa dhambi umeongezeka. Tulielewa vizuri zaidi jinsi Mungu anavyotutaka tuishi.)
-
-
- Je, ni jambo baya kwamba dhambi imeongezeka? (Hapana, kwa sababu hata neema imeongezeka zaidi.)
-
-
-
- Kuna matokeo gani kwa wale wanaoamini kuwa Yesu ni Mungu na kukiri kile alichokifanya kwa ajili yetu? (Tunao uzima wa milele!)
-
-
- Rafiki, uzima wa milele ndilo tumaini tunalolifurahia. Hicho ndicho kinachotupatia amani maishani. Dhambi inaweza kuleta furaha, bali utii, kumtumaini Mungu, kuiamini neema, hutupatia amani. Kwa nini usichague amani leo?
- Juma lijalo: Kuishinda Dhambi.