Hali ya Kibinadamu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Warumi 1:18-3:20)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Umewahi kutafakari kiasi ambacho ni kwa jinsi gani suala la haki kwa imani linaongoza mtazamo wako mzima wa Mungu? Chukulia kwamba haki kwa imani (neema) inamaanisa kuwa juhudi zote za mwanadamu zina dosari. Mungu pekee ndiye mkamilifu. Hii haisemi tu jinsi ambavyo ninaokolewa, bali inasema jinsi ninavyopaswa kuwaangalia watu wengine. Inasema jinsi ninavyopaswa kuangalia wajibu wa Mungu ulimwenguni. Somo letu juma hili kuhusu “hali ya kibinadamu” inatuanzishia safari yetu ya kuangalia mtazamo mpana wa neema. Hebu tuzame kwenye somo letu na tujifunze kile Biblia inachotufundisha!

 

  1. Hakuna Kisingizio

 

    1. Soma Warumi 1:18-20.  Paulo anaelezea mambo mawili. Kwanza, anaelezea wakandamizao ukweli. Pili, anaelezea kwa nini ukweli hauwezi kukandamizwa. Wanadamu wanajaribuje kuukandamiza ukweli? (Kwa wao kutokuwa na Mungu na kuwa waovu.)

 

      1. Je, unaliona jambo hili katika jamii leo? (Nina wasiwasi kwamba uovu unashika kasi. Sio tu kwamba kanuni za Kibiblia zinazoshughulika na mahusiano ya kingono zinabezwa, bali pia kuna vuguvugu linalokua kwa kasi linalokandamiza maneno ya watu wanaoamini katika kanuni za Kibiblia.)

 

        1. Je, unaona kukua kwa hali ya “kutokuwa na Mungu?” (Hili limefanyiwa utafiti. Idadi ya watu wasiomwamini Mungu inakua.)

 

      1. Vifungu hivi vinazungumzia jambo gani linalotupatia tumaini? (Ukweli juu ya Mungu hauwezi kukandamizwa kwa mafanikio. Uwepo wa Mungu na asili yake ya Uungu viko wazi katika uumbaji wake. Wazo la kwamba mbingu na nchi vilitokea kwa bahati na kutokana na mambo ya asili ni kichekesho. Kwa sehemu kubwa, wanadamu wanaweza tu kuchunguza na kuelezea kanuni za asili, hawawezi kuelezea jinsi zinavyotenda kazi. Mantiki inakataa kata kata kudhani kuwa kanuni hizo za ajabu zilizo ngumu sana kueleweka zilitokea kwa bahati. Ikiwa zilitokea kwa bahati, ni kwa jinsi gani sisi kundi la wanadamu tulivyo wapumbavu ikiwa hatuwezi kubaini jinsi zinavyotenda kazi.)

 

      1. Je, mwanadamu yeyote anacho kisingizio cha kutokumwamini Mungu? (Hapana. Biblia inasema kuwa hakuna visingizio.)

 

    1. Soma Warumi 1:21-23. Wanadamu wasio na mantiki wamekataa kufanya nini? (Hawakumshukuru Mungu wala kumpa utukufu.)

 

      1. Matokeo ya kutokumkiri Mungu kama Muumba wa Ulimwengu ni yapi? (Hii inavuruga na kutatanisha akili ya mtu anayemkana Mungu. Watu werevu wanatenda mambo ya kipumbavu kama vile kutengeneza sanamu zinazofanana na wanadamu au wanyama kisha wanaziabudu.)

 

        1. Katika maeneo ninayoishi, sijamwona mtu yeyote akisujudia sanamu. Je, wanadamu wamekuwa werevu kiasi cha angalao kutokufanya hivyo? (Anguko la mkana Mungu la mantiki ni kutokumtambua Mungu. Nadhani mantiki ya kibinadamu, nadharia za wanadamu, zimekuwa sanamu mpya. Hatutengenezi sanamu inayofanana na mtu au mnyama, tunatengeneza sanamu kwenye karatasi au kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa kujenga hoja dhidi ya Mungu.)

 

      1. Angalia jinsi wazo la neema linavyokubaliana na dhana hii hapa. Ikiwa tunadhani matendo yetu yanahusiana na wokovu wetu, je, tunafanana na wale wanaotengeneza sanamu kwa mikono yao?

 

    1. Soma Warumi 1:24-25. Matokeo ya kumkataa Mungu Muumba ni yapi? (Mungu “aliwaacha” katika hali yao ya kutokuwa na hofu na tamaa za ngono.)

 

    1. Soma Warumi 1:26-27. Dhambi gani mahsusi ya ngono inabainishwa inayotokana na kumkataa Mungu? (Ubasha/usenge.)

 

      1. Unadhani ni kwa nini Paulo anabainisha ngono baina ya wasenge kama matokeo ya asili ya kumkataa Mungu? Kwa nini inafuatia dhambi ya kuabudu sanamu zinazofanana na wanyama na wanadamu? (Paulo anajenga hoja kwenye suala la mantiki. Unawezaje kuuangalia uumbaji na usiamini kwamba Mungu yupo? Mwanadamu anawezaje kuabudu kitu alichokitengeneza? Wanadamu wanawezaje kuangalia jinsi wanawake na wanaume walivyoumbwa na kuhitimisha kwamba ubasha/usenge ni jambo la kawaida?

 

      1. Unadhani Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa wale wanaojihusisha na usenge “wanapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao?” Je, kuna adhabu ya moja kwa moja ambayo ni ya asili kwenye hii dhambi?

 

    1. Soma Warumi 1:28. Hii inatuambia kuwa jambo gani lipo katikati ya “akili iliyopotoka?” (Akili “isiyofikiri kwamba kuna thamani kuwa na uelewa wa Mungu.” Ikiwa humjui Mungu, ikiwa hutaki kujua na kuelewa mapenzi ya Mungu kwa ajili yako, basi akili yako inakengeuka na kupotoka.)

 

    1. Soma Warumi 1:29-31. Unapoangalia orodha hii, je, unaona dhambi yako yoyote imetajwa?

 

      1. Paulo anaonekana kuelezea suala la kuteleza dhambini. Kwanza, kumkataa Mungu na kumbadilisha na sanamu. Pili, ngono baina ya wasenge. Tatu, orodha hii ndefu ya dhambi. Je, hii inamaanisha dhambi zilizopo kwenye orodha ndefu ni mbaya zaidi ya usenge? (Kuna mjadala unaoendea ulimwenguni kote wa kufanya ngono baina ya wasenge kuwa ya kawaida katika sheria za kilimwengu. Ikiwa Paulo anatuambia kuwa ngono baina ya wasenge si mbaya zaidi kuliko kuwa “fidhuli, kuwa na kiburi na kujigamba,” basi suala la kile ambacho sheria inapaswa kukizuia inakuwa ngumu zaidi, isiyoelezeka kwa urahisi (complex).)

 

    1. Soma Warumi 1:32. Dhambi gani inaelezewa hapa? (Pia ni dhambi ya “kukubaliana nao watendao” dhambi. Hatuwezi kuwa kwenye nafasi ya kuidhinisha vitendo vya dhambi.)

 

  1. Hakuna Hukumu

 

    1. Soma Warumi 2:1. Nilipokuuliza endapo unatambua mojawapo ya dhambi zako kwenye ile orodha ndefu ya dhambi, Paulo angetarajia ujibuje? (Paulo anasema tunazo baadhi ya zile dhambi maishani mwetu.)

 

      1. Tunaweza kuitaja dhambi kwa jina lake sahihi?  Au, hiyo ni sawa na “kuhukumu?” (Tunaweza kuitaja dhambi kwa jina lake sahihi. Kwa hakika, Paulo amefanya hivyo. Tusichoweza kukifanya ni “kumhukumu mtu mwingine.”)

 

        1. Kwa nini? (Kwa sababu tunafanya mambo hayo hayo.)

 

      1. Unakumbuka kwenye utangulizi tulizungumzia mtazamo mpana wa neema? Uelewa wa kweli wa neema unatusaidiaje katika kukabiliana na dhambi kwa watu wengine? (Tunapoelewa kwa wazi utukufu wa Mungu, na asili ya mwanadamu ya kusikitisha, hatuna “kisingizio” cha kuwahukumu watu wengine kwa sababu kwa kufanya hivyo “tunajihukumu” dhambi zetu wenyewe!)

 

    1. Soma Warumi 2:2-3. Wale wanaowahukumu watu wengine wanapaswa kutarajia nini? (Kwamba Mungu atawahukumu kwa dhambi zao. Tunapaswa kukiri kwamba sisi ni wanadamu wadhambi.)

 

    1. Soma Warumi 2:4. Kwa muda mrefu sana nimekuwa sehemu ya uongozi wa kanisa langu mahalia. Katika “siku za kale” tulikuwa tunawaadabisha wale waliojihusisha na uzinzi. Nakumbuka kusoma kitabu cha mwongozo wa kanisa kilichosema kuwa lengo la adhabu ni kumshtua mdhambi ili aweze kutubu na kurudi kwenye msitari sahihi wa tabia njema. Kifungu hiki kinasema kuwa njia ya Mungu ni ipi? (Kinaonekana kusema kinyume chake tu: “wema wa Mungu unakuelekeza kwenye toba.”)

 

      1. Angalia msitari mgumu hapa: ikiwa hatuelewi kuwa neema inaakisi “wema, ustahimilivu na subira” ya Mungu kwetu, tunaonesha “dharau” kwa Mungu!

 

    1. Soma Warumi 2:5. Paulo anarejea mtazamo gani wa kikaidi na usio wa toba? (Vifungu vichache vya mwisho vinazungumzia juu ya kuwahukumu watu wengine. Je, umewahi kufikiri kuwa kuwahukumu watu wengine wakati wewe ni mdhambi inakufanya kuwa “mtu usiye na toba” na mtu ambaye “unahifadhi hasira?”)

 

      1. Baadhi ya watu wanaweza kujibu kwamba hapo awali aliandika kuhusu wale wanaokana uwepo wa Mungu. Je, Paulo anaandika kuwahusu anapoahidi ghadhabu inayokuja? (Angalia jambo la kawaida hapa. Wale wanaokataa kumkiri Mungu wanafanana na wale wanaokataa kukiri neema ya Mungu. Nafasi zote mbili zinaonesha dharau kwa uwezo wake.)

 

  1. Neema ni Kubwa Kiasi Gani?

 

    1. Soma Warumi 2:6-11. Sasa soma Warumi 3:21-24. Je, Paulo amesahau katika sura ya 3 alichokiandika katika sura ya 2? Je, hizi si kauli mbili zinazokinzana na kupingana kabisa? Je, sasa Paulo anaonesha dharau kwa uwezo wa Mungu?

 

      1. Hebu tuone kama tunaweza kulinganisha kauli za Paulo. Chukulia kwamba huna mtazamo wa “neema” na unadhani kuwa wewe ni bora kuliko watu wengine. Je, utajisikia kuwa na hitaji la toba? (Hapana.)

 

      1. Badala yake, ukitambua kwamba umekwama dhambini kama hawa watu wengine, je, utatubu? (Nadhani. Neema inatusukuma magotini na kutusababisha tutake kumpa Mungu utukufu.)

 

    1. Soma Warumi 3:10-12. Ikiwa hukumu ya Mungu imejengwa kwenye matendo mema, tunasimama wapi? (Hii inathibitisha kwamba Paulo hawezi kuwa anahoji suala la haki kwa imani katika Warumi 2:6-10.)

 

    1. Soma Warumi 3:19-20. Hili linaingilianaje na kipengele cha “usihukumu” katika sura iliyotangulia? (Hii inatuonesha kuwa neema sio tu njia ya wokovu, bali ni mtazamo unaopenya kila jambo tunalolitenda. Neema inatufundisha kutokuwahukumu watu wengine kwa kuwa hatuwezi kustahimili hukumu ya kweli.)

 

    1. Soma Warumi 3:27-28. Kuna nafasi gani kwa mtazamo wa kujiona watu wa hadhi kubwa kwa maisha yetu ya haki? Kuna nafasi gani kwa ajili ya mtazamo wa hukumu? (Hakuna nafasi kwa ajili ya hili. Tunahesabiwa haki kwa neema pekee. Sisi sote ni watu wa ovyo. Neema inatufundisha kuwa na shukrani kwa kile ambacho Yesu ametutendea.)

 

    1. Rafiki, je, utauchunguza moyo wako kwa ajili ya mtazamo wa kuhukumu? Ninakiri kwamba nilipokuwa ninaandika somo hili, ilinipasa kusimama na kuomba msamaha nilipokumbuka nyakati nilipokuwa mtu wa kuwahukumu watu wengine.

 

  1. Juma lijalo: Haki kwa Imani