Somo la 13: Injili na Kanisa
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Sehemu kubwa ya somo letu la Wagalatia imejikita juu ya namna tunavyoishi katika Roho na kwa neema. Sasa Paulo anajikita kwenye suala la jinsi tunavyopaswa kuhusiana na washiriki wenzetu wa kanisa. Tunatakiwa kufanya nini juu ya dhambi kanisani? Je, aina ya dhambi inajalisha? Je, umaarufu wa mshiriki wa kanisa unahusika? Katika “retreat” moja ya kanisa iliyofanyika siku za mwisho wa juma hivi karibuni, mshiriki mmoja alihitaji kujadiliana nami kuhusu suala hili. Tulikubaliana kwamba kila mtu kanisani ni mdhambi. Sote tunahitaji neema. Hata hivyo, tofauti inajitokeza pale mshiriki wa kanisa anapokuwa mtetezi wa dhambi. Sio tu kwamba wanatenda dhambi, bali pia wanajenga hoja kwamba dhambi inapaswa kukubalika. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!
- Urejeshaji
-
- Soma Wagalatia 6:1. Unadhani inamaanisha nini “kumghafirisha” mshiriki wa kanisa dhambini? (Inaweza kumaanisha kumshtukiza au inaweza kumaanisha kwamba mtu huyo “amekamatika” dhambini.)
-
-
- Je, hiyo inaleta tofauti yoyote?
-
-
- Angalia tena Wagalatia 6:1. Lengo letu ni lipi mara baada ya kuitambua dhambi? (Kumrejesha mtu huyo.)
-
-
- Unadhani hiyo inamaanisha nini – kumrejesha mtu? (Kumsaidia kutoka dhambini.)
-
-
-
- Jambo hili linatendekaje ikizingatiwa kwamba sisi sote ni wadhambi? (Sisi sote ni wadhambi, lakini Paulo anatofautisha kati ya “ninyi ambao ni watu wa kiroho” na wale “waliokamatika dhambini.” Inaonekana hii ni dhambi inayotakiwa kushughulikiwa.)
-
-
-
- Tunatakiwa kushughulikiaje jambo hili? Kwa kumpayukia maneno au kujaribu kumfedhehesha mdhambi? (Biblia inatuambia kuwarejeza kwa “roho ya upole.” Sio kumbwatukia. Pasiwepo na jaribio la kumfedhehesha.)
-
-
- Hebu tujikite zaidi kwenye sehemu ya mwisho ya Wagalatia 6:1. Kuna hatari gani ya kumrejesha mtu kutoka dhambini mwao? (Tunaweza kujaribiwa.)
-
-
- Kujaribiwa na nini? (Kifungu hakisemi chochote, lakini jambo la kwanza nililolifikiria ni kwamba tunatakiwa kuepuka kujaribiwa na dhambi tunayojaribu kuishughulikia.)
-
-
-
-
- Je, umewahi kupitia uzoefu huu?
-
-
-
-
- Ikiwa tatizo ni kuiangalia dhambi kwa undani, hii inaashiria nini juu ya kutazama televisheni na sinema zinazoshughulika na dhambi? (Dhambi hiyo inakuwa wazi kwetu bila kunufaika na upande chanya wa kujaribu kumsaidia mtu kutoka kwenye dhambi hiyo.)
-
-
- Soma Wagalatia 6:2-3. Niliposoma Wagalatia 6:1, nilidhani kuwa jaribu ni kujihusisha kwenye dhambi ile ile kama ya mtu “aliyekamatika.” Hii inaashiria jibu tofauti. Ni lipi hilo? (Hapa tatizo la dhambi ni kwamba nitadhani kuwa hadhi yangu ni ya juu kuliko mtu ninayemsaidia kutoka dhambini.)
-
-
- Ikiwa ninamsaidia mtu kutoka dhambini, je, hiyo haimaanishi moja kwa moja kwamba mimi ni “bora zaidi” kwenye dhambi hii? (Ikiwa tunadhani hivyo, Paulo anatuambia kuwa tumedanganywa. Sisi sote ni wadhambi.)
-
-
-
- Mojawapo ya mambo anayotuambia Paulo ili tuyatende ni “kuchukuliana mizigo.” Ikiwa mara zote unadhani kuwa wewe ni bora kuliko mtu unayejaribu kumrejesha kutoka dhambini, je, lipo tatizo halisi? (Ikiwa unao mtazamo wa ukubwa, hilo litakujia. Ama kwa hakika, mtazamo wa aina hiyo unakufanya usiwe na moyo wa huruma. Hufanyi lolote katika kumsaidia mtu huyo mzigo wake.)
-
-
- Soma Wagalatia 6:4. Inamaanisha nini “kuzipima kazi zetu wenyewe?” (Ikiwa nawe uko kama mimi, kiukweli sijaribiwi katika mambo yote maishani mwangu. Kuiba fedha au kuua mtu si vitu vinavyonijaribu. Ikiwa ninamshauri mtu anayependa kuiba vitu, Mungu ananiambia niyafikirie maeneo ambayo nina matatizo nayo ili nisiweze kujisikia bora zaidi ya mwizi.)
-
-
- Hebu subiri kidogo! Hivi punde nimeandika kuwa tusijisikie kuwa bora zaidi ya mwizi, lakini kifungu hicho cha Biblia kinatuambia kuwa tunaweza “kujisifu” ndani ya nafsi zetu. Tunawezaje kuepuka kujisikia bora zaidi na wakati huo huo kujisifia? (Hatupaswi kujisifu kutokana na ukweli kwamba sisi ni bora zaidi ya mtu tunayemsaidia. Badala yake, tunatakiwa kujisifu kutokana na ukweli kwamba tunapiga hatua kwenye safari yetu ya kuielekea haki.)
-
-
-
-
- Je, kujisifu hakukinzani na uelewa wa kwamba Roho Mtakatifu atendaye kazi ndani yetu ndiye anayetuwezesha kupiga hatua kuielekea haki? (Nadhani mantiki iliyopo ni kwamba tunafurahia ushindi dhidi ya dhambi.)
-
-
-
- Soma Wagalatia 6:5. Kwa nini tunapaswa kubeba “furushi letu wenyewe?” (Paulo amekuwa akituandikia habari ya sisi kuchukuliana “mizigo.” Hapa anatuambia tuchukue mizigo yetu wenyewe. Kwa mara nyingine, nadhani ujumbe ni kwamba tunapozitambua dhambi zetu, inatufanya tusijisikie kuwa na hadhi ya juu kwa watu wengine wanaokabiliana na dhambi za aina nyingine.)
- Kumwinua Mkufunzi
-
- Soma Wagalatia 6:6. Inamaanisha nini “kumshirikisha mkufunzi wake katika mema yote?” (Inamaanisha kumsaidia mtu anayekufundisha.)
-
-
- Angalia aina ya maelekezo yanayostahili msaada – “maelekezo katika neno.” Hiyo inatuambia nini juu ya watu wanaofundisha falsafa ya maisha ambayo haijajengwa juu ya Biblia? (Mafundhisho hayo hayastahili msaada wetu.)
-
- Sheria ya Kurudisha
-
- Soma Wagalatia 6:7. Tunafahamu kwamba mkulima “anavuna alichokipanda.” Nadharia hii inatendaje kazi kwenye suala la dhambi na kuwasaidia watu wengine kutoka dhambini?
-
- Soma Mhubiri 8:14 na Mhubiri 9:1-2. Je, Mfalme Sulemani na Paulo wanapaswa kuwa na mjadala? Wanaonekana kutokukubaliana kabisa! (Mambo mawili yanaendelea. Kwanza, Sulemani anawezakuwa anasema kwamba kuna jambo la pekee kwenye kanuni ya jumla. Waebrania 11, hususani Waebrania 11:35-38, inakubaliana na ukweli kwamba mambo yasiyo ya haki yanatokea hapa duniani. Hata hivyo, hiyo si kanuni ya jumla. Na kwa kuongezea, Waebrania 11 inasema kuwa mambo yote yatatendwa kwa usahihi Yesu atakaporejea. Pili, kwa dhahiri Sulemani ana msongo wa mawazo. Wakristo wengi ninaowafahamu wananukuu Mhubiri 9:5 kuthibitisha hali ya wafu. Huo ni upuuzi. Kifungu hicho kikichukuliwa neno kwa neno, kinapingana na ahadi ya Waebrania 11 kwamba mambo yote yatafanyika kwa usahihi mbinguni. Sulemani ana msongo wa mawazo tu – na ukweli huu unawahamasisha wale wanaopambana na msongo wa mawazo.)
-
- Soma Wagalatia 6:8. Paulo anaelezea kuwa mavuno anayoyazungumzia ni hatima yetu ya milele. Hiyo inasuluhisha baadhi ya ukinzani na Sulemani. Umegundua nini? Je, umegundua “malipo” hata wakati wa uhai hapa duniani?
-
- Soma Wagalatia 6:9. Tunapaswa kufanya nini tukijisikia “kuchoka” kutokana na matendo yetu mema? (Tunatakiwa kujikumbusha kwamba tutapokea thawabu endapo hatutakata tamaa!)
-
-
- Je, hii haikinzani na dhana ya neema? (Wagalatia 6:8 inafanya iwe vigumu kujenga hoja kwamba Paulo anazungumzia mambo mawili tofauti, uzima wa milele dhidi ya thawabu mbinguni. Badala yake, nadhani Paulo anatuambia kuwa wale wanaoipokea neema, wale wanaochagua kuishi kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu, wale wanaotembea kwenye uelekeo wa haki, wanaakisi matendo mema katika maisha yao.)
-
-
- Soma Wagalatia 6:10. “Nafasi” yetu imebadilikaje tangu kipindi cha Paulo? (Sasa tunayafahamu mahitaji ulimwenguni kote. Tunaweza kuyasikia na kuyafahamu mara moja mara tu yanapotokea. Paulo, kwa upande mwingine, alikuwa anazungumzia mambo yatakayovuta usikivu wa anayeamini.)
-
-
- Je, wakati mwingine “nafasi” yetu inaonekana kuwa kubwa kupita maelezo?
-
-
-
- Nilisoma makala ya utafiti inayohusu mapato ya kodi yanayopatikana eneo mahalia dhidi ya mapato ya kodi ya taifa. Makala ilibainisha kwamba watu wa maeneo mahalia walitumia kwa busara zaidi kodi yao kutatua matatizo yanayowakabili katika maeneo yao. Waliifahamu hali inayowakabili vizuri zaidi kuliko wale wanaoshughulikia mapato katika ngazi ya taifa. Je, dhana hiyo inaweza kutumika katika kuwasaidia watu wengine? Tunaweza kuwa na ufahamu wa matatizo yaliyopo ulimwenguni kote, lakini je, kuwasaidia watu wanaotuzunguka na tunaowafahamu hutusaidia kutoa msaada wenye matokeo mazuri?
-
-
-
- Paulo anasema nini kuhusu kuwapa kipaumbele waumini tunapotoa msaada? (Anasema tunapaswa kuwasaidia “hasa” jamaa ya waaminio.)
-
-
- Rafiki, je, umezingatia kwa umakini mkubwa jinsi unavyoweza kuwasaidia watu wanaokuzunguka? Je, umegundua kwamba Paulo anatoa maelekezo mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine? Hiyo inamaanisha kwamba tunatakiwa tukusudie kutoa msaada. Paulo anatuhamasisha tuwe watu wa kutoa msaada kwa kutuambia kuwa tutavuna thawabu kutokana ya msaada tulioutoa. Je, unaweza kutafakari juu ya kile unachoweza kukifanya ili kuwasaidia watu wengine?
Juma lijalo: Kuona Fahari Juu ya Msalaba.