Urejeshwaji wa Mamlaka

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mwanzo 1 - 3, 6 – 7 & 9; Wathesalonike 3)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
3
Lesson Number: 
2

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Nini maana ya “Utawala?” Mji wa Virginia, mahali ambapo ninaishi, unaitwa “Utawala/Mamlaka ya Kale.” Nilipoangalia kwenye “Encyclopedia Virginia,” niligundua kwamba Virginia ulikuwa mji wa kwanza wa “utawala wa ng’ambo wa wafalme na malkia wa Uingereza.” Nilidhani kwamba “Utawala wa Kale” ulimaanisha jambo kubwa. Badala yake, inamaanisha kuwa ninaishi mahali palipomilikiwa/tawaliwa na nchi nyingine. Tafsiri ya Biblia ya Mfalme Yakobo (KJV) inasema kuwa wanadamu wana “mamlaka” juu ya uumbaji. Hebu tuzame kwenye Biblia zetu ili tujifunze kinachomaanishwa!

 

1)      Uumbaji na Utawala

 

a)      Soma Mwanzo 1:26-27. Mungu anawapa wanadamu mamlaka juu ya nini? (“Juu ya dunia yote.” Kisha Biblia inataja wanyama, wa kufugwa na wa porini. Inaonekana tuna mamlaka juu ya uumbaji wote.)

 

i)       Utaona kwamba kisha Mungu anasema kuwa anatuumba kwa sura yake. Kwa nini? (Kwa kuwa Mungu ndiye mtawala mkuu, alitufanya tufanane naye. Nadhani ni vyema kwa watawala kufanana sura.)

 

ii)     Yumkini umegundua kwamba Tafsiri ya Biblia ya “New International” inatumia neno “utawala” badala ya “mamlaka.” Je, hiyo haifanyi “mamlaka” kueleweka kiurahisi?

 

(1)   Ikiwa umesema, “ndiyo,” niambie jinsi unavyowatawala wanyama?

 

b)      Soma Mwanzo 1:28. Tunaona neno jipya, “kuitiisha.” Je, “kuitiisha” inaongezea nini kwenye uelewa wetu wa jinsi tunavyopaswa “kuutawala” uumbaji? (Kwa dhahiri, wanadamu wanatawala.)

 

c)      Soma Mwanzo 1:29-30. Ikiwa hivi punde tu umeambiwa kuwa wewe ni mtawala wa wanyama, je, hii inaongezea mamlaka yako au inapunguza mamlaka yako? (Kutokana na utamaduni wetu leo, huu ni udhaifu mkubwa kwenye mamlaka yetu. Haturuhusiwi kula wanyama. Badala yake, wanyama na wanadamu kimsingi wana chakula cha aina moja – majani (mimea ya kijani).)

 

i)       Udhaifu huu unatufundisha nini? (Mamlaka yetu yana mipaka.)

 

d)      Soma Mwanzo 2:15-17. Tunaona ukomo gani mwingine kwenye mamlaka yetu? (Adamu na Eva wanaambiwa wasile matunda ya mti mmoja. Na kwa kuongezea, wanapewa wajibu kuhusiana na uumbaji. Wanaambiwa “wailime” na “kuitunza.” Huu ni ukomo mwingine kwenye mamlaka yetu.)

 

i)       Kutokana na huu ukomo kwenye mamlaka yetu kamili, unawezaje kuelezea kwa ukamilifu kabisa kuhusu asili ya mamlaka yetu? (Ukarimu au kutegemeana. Tunautunza uumbaji na uumbaji unatutunza.)

 

 

2)      Anguko na Utawala

 

a)      Soma Mwanzo 3:17-19. Adamu na Eva walitenda dhambi, je, uhusiano wao na uumbaji umebadilikaje? (Hakuna chochote kwenye mafungu haya kinachosema kuwa wanadamu hawana mamlaka tena, badala yake, hali ya asili ipo kwenye uasi. Hali ya asili haitoi ushirikiano kama ilivyokuwa ikitoa ushirikiano hapo awali.)

 

b)      Soma Mwanzo 3:16. Unaona mantiki gani kwenye adhabu ya dhambi? (Unakumbuka kwamba tuliumbwa kuwa watawala kama Mungu? Sasa tutapitia uzoefu kama ule ambao Mungu anaupitia pamoja nasi. Mungu ni Muumba wetu. Kama ambavyo sasa hivvi tunavyowaumba wanadamu wengi zaidi, uzoefu huo ni mchungu – kama ambavyo tunavyosababisha maumivu/uchungu kwa Mungu. Sasa uumbaji wa Mungu unasababisha magumu, machungu na matatizo kwake. Sasa mimea inasababisha ugumu kwa Adamu. Mungu anatupatia uzoefu unaofanana kutokana na kile anachokipitia na kuteseka sasa hivi.)

 

c)      Soma Yohana 12:31-33. Yesu anamwita Shetani “mkuu wa ulimwengu huu.” Kwa kiasi gani utawala ulihamishiwa kwa Shetani wakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi? (Kwa dhahiri Yesu anamwita Shetani “mkuu,” na kuhusisha sehemu ya mamlaka duniani kwake. Lakini, mamlaka ya Shetani yamepunguzwa kwa sababu Mungu ndiye aliyemwambia Adamu na Eva (baada ya kutenda dhambi) kuhusu uhusiano wao na uumbaji. Inabainisha kuwa Yesu anamwita Shetani “mkuu” badala ya kumwita “mfalme.”)

 

d)      Soma Mwanzo 6:5-7. Kutokana na fungu hili, unawezaje kuelezea mamlaka ya Shetani baada ya dhambi ya wanadamu? (Mungu alichukua mamlaka yote. Mungu anapendekeza kuuangamiza uumbaji. Endapo Shetani alikuwa na mamlaka kamili duniani, angeweza kuzuia jambo hili, au angalao angekuwa na malalamiko halali kwamba Mungu alikuwa anaangamiza mali yake, ufalme wake.)

 

e)      Soma Mwanzo 7:1-4 na Mwanzo 7:20-23. Nani mwenye mamlaka hapa? (Mungu!)

 

f)       Soma Mwanzo 9:1-5. Nani ana mamlaka hapa? (Mungu na wanadamu.)

 

i)       Baada ya gharika, Mungu anasema nini kuhusu mamlaka ya wanadamu juu ya uumbaji? (Mungu anasema mambo kadhaa. Kwanza, anatangaza kwamba wanadamu wanaweza kula wanyama. Pili, Mungu anatangaza kuwa wanyama “wametiwa mikononi mwenu,” lakini Mungu anakataza ulaji wa damu ya wanyama. Mungu ana udhibiti na mamlaka kamili. Kwa mara nyingine, Mungu anagawa sehemu ya udhibiti huo kwa wanadamu.)

 

g)      Unapoendelea kutafakari mafungu tuliyoyasoma, je, unaona kuwa sisi wanadamu tunafanya kazi chini ya udhibiti wa Shetani, au kwamba Mungu amebaki na udhibiti na kwamba bado tunatenda kazi “katika sura yake (Mungu) kwa maana ya kwamba matatizo tuliyomsababishia Mungu sasa hivi ndio matatizo tunayotakiwa kukabiliana nayo? (Kamwe wanadamu hawakuwahi kuwa na mamlaka ya kuhamisha mamlaka kutoka kwa Mungu kwenda kwa Shetani. Walichokifanya wanadamu ni kuyafanya mamlaka yao kuwa magumu kwa kushiriki kwenye uasi dhidi ya mamlaka ya Mungu.)

 

h)      Soma tena Mwanzo 9:2 na uone kile inachokisema kuhusu mabadiliko zaidi kwenye uhusiano kati ya wanadamu na wanyama. Mabadiliko hayo ni yapi? (Sasa wanyama watawaogopa na kuwahofu wanadamu. Watataka kukaa mbali na wanadamu.)

 

 

i)       Kwa nini Mungu anafanya hivyo? (Kuhifadhi maisha ya wanyama kwa sababu sasa wanadamu wanawala!)

 

ii)     Je, kuna uhusiano, kwa mara nyingine, kati ya mamlaka ya Mungu na mamlaka yetu katika “sura yake?” (Sasa wanadamu wanaelewa kuwa Mungu ana uwezo wa kuangamiza uumbaji wake. Wanyama wanaelewa kuwa wanadamu wanaweza kuwangamiza.)

 

3)      Kuelekea Kwenye Utawala Kamili Zaidi

 

a)      Soma 2 Wathesalonike 3:1-5. Tunawezaje kushughulika na ukweli kwamba dhambi yetu na kazi ya Shetani vinasababisha matatizo halisi kwetu? (Tuombe ili kwamba tuokolewe kutoka uovuni na wanadamu waovu.)

 

b)      Soma 2 Wathesalonike 3:6-10 na Kumbukumbu la Torati 15:7-8. Je, mafungu haya mawili yanakinzana?

 

i)       Soma tena 2 Wathesalonike 3:6. Paulo anaandika kuhusu “fundisho” gani? (Muktadha unatuambia kuwa fundisho ni mfano wao wa kazi. Hivyo, maskini wanaosaidiwa katika Kumbukumbu la Torati 15 ni maskini wanaofanya kazi. Hawa si watu wasiotii fundisho la kazi.)

 

c)      Soma Mambo ya Walawi 19:9-10. Maskini wanatakiwa kufanya nini kama sehemu ya kupata chakula chao? (Wafanye kazi. Wanafanya kazi ya “kuvuna” masalio yaliyosazwa shambani.)

 

d)      Soma 1 Timotheo 5:3-4. Kanuni ni ipi kwa wajane ambao “kweli ni wahitaji?” (Kwamba chanzo cha kwanza cha msaada kinapaswa kuwa familia.)

 

e)      Soma 1 Timotheo 5:9-10. Kanuni ya kuwasaidia wajane wazee ni ipi? (Wanaweza tu kuwekwa kwenye “orodha” (orodha rasmi ya kanisa kwa wanaohitaji msaada) ikiwa wametenda matendo mema siku za nyuma.)

 

f)       Soma tena Mwanzo 3:17-19. Hapo awali tulikubaliana kwamba bidii ya kazi ilihitajika katika kutafuta chakula kutokana na asili mpya ya uasi, iliakisi ugumu mkubwa ambao Mungu anaupitia sasa hivi kwa sababu ya dhambi zetu. Hii inaashiria nini kuhusu kazi? (Inaboresha tabia. Kazi inatufundisha kuhusu umiliki na utawala.)

 

i)       Kwa nini kwa ujumla Mungu anatutaka tuwasaidie maskini, wale wanaofanya kazi pekee? (Ukiangalia tena 2 Wathesalonike 3:9, Paulo anatuambia kuwa yeye ni kielelezo cha kufundisha umuhimu wa kazi. Tunafundisha umuhimu wa kazi tunapofanya kazi na tunapovumbua njia za kuwasaidia maskini zinazowataka wafanye kazi.)

 

g)      Mjadala wa kuwasaidia wajane, na onyo la “kukaa mbali” na “ndugu” asiye na kazi ya kufanya (2 Wathesalonike 3:6), unawarejea miongoni mwa walio kwenye kundi la waumini. Je, unadhani kanuni hizi pia zinawahusu wale walio nje ya kanisa?

 

h)      Taarifa ya habari ya CNS inataarifu kuwa kwa mujibu wa Serikali ya Marekani, asilimia 62.8 pekee ya watu wa Marekani (wenye umri wa miaka 16 au zaidi na wasiopo kwenye taasisi) wapo kwenye kundi la watu wenye uwezo wa kufanya kazi. Idadi hii inawajumuisha wale ambao hawajaajiriwa, lakini wanatafuta kazi. Je, jambo hili linazungumzia nini kuhusu mustakabali wa mpango wa kazi ya Mungu?

 

 

i)       Rafiki, wanadamu walimwasi Mungu katika bustani ya Edeni na akatoa adhabu zinazotufanya kwa kiwango fulani kupitia uzoefu wa mateso yake tunapoboresha na kurekebisha tabia zetu. Je, hii leo wanadamu wapo kwenye uasi kwa kutenganisha msaada kwa maskini na matakwa ya kufanya kazi? Ikiwa unakubaliana, je, utaangalia upya jinsi unavyoweza kurejesha upya somo la Edeni kuhusu utawala wa Mungu?

 

4)      Juma lijalo: Haki na Rehema Katika Agano la Kale: Sehemu ya 1.