Petro na Mwamba

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 16 & 17)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
2
Lesson Number: 
8

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, umewahi kupitia hali ambayo suluhisho la tatizo lipo mbele yako kabisa, lakini kwa namna fulani hivi unashindwa kuliona suluhisho hilo? Mtu mwingine anakujia, anakuonesha suluhisho hilo, na unashindwa kuamini kwamba umeshindwa kuliona suluhisho hilo la dhahiri kabisa! Katika somo letu juma hili, Mathayo anaelezea hali ya namna hii kwa watu waliopishana kimawazo na Yesu. Hebu tuchimbue somo letu na tujifunze zaidi ili tusijeshindwa kutambua na hivyo kuyakosa masuala ya kiroho yaliyo dhahiri!

 

I.                    Ishara

 

A.                  Soma Mathayo 16:1. Yesu ametenda miujiza ya aina mbalimbali. Je, anapaswa kutenda muujiza mwingine sasa hivi? (Ingawa ninadhani miujiza ya Yesu ina athari chanya za kuthibitisha kwamba yeye ni nani, mafungu kama lile la Mathayo 14:14 yanatuambia kuwa miujiza ya Yesu inahamasishwa na huruma. Hawa Viongozi wa dini “wanamjaribu” tu Yesu.)

 

B.                  Soma Mathayo 16:2-3. Viongozi wa dini wana tatizo gani? (Wanapuuzia jambo la dhahiri kabisa: kwamba Yesu anatimiza unabii.)

 

1.                   Je, nasi tunafanana na hao viongozi wa dini? Je, tunapuuzia yale yanayosemwa na Biblia na jinsi mambo hayo yanavyohusika katika maisha yetu, na badala yake tunamwomba Yesu atuoneshe ishara maalum?

 

C.                   Soma Mathayo 16:4. Yesu anasema kuwa watapewa “ishara ya Yona.” Unadhani kauli hiyo inamaanisha nini? (Jibu la kistaarabu kabisa na lisiloeleweka vizuri ni kwamba Yona alikwenda chini ya maji na akafufuka pale samaki mkubwa alipomtapika (Yona 2). Yesu atakwenda chini ya dunia (chini ya ardhi) na kufufuka katika uzima wa milele. Jibu la dhahiri zaidi ni kwamba Mungu alitia mkono wake (alibariki) kwenye matukio yote ambayo Yona aliyapitia. Matukio yaliyopitishwa na Mungu yatawapita hawa viongozi wa dini. Kitendo cha kumkataa Yesu kinasababisha kuangamizwa kwa Yerusalemu.)

 

II.                  Mkate

 

A.                  Soma Mathayo 16:5-11. Kwa nini Yesu analalamika kuhusu wanafunzi kuwa na imani chache, badala ya wao kutokuwa na akili (maarifa)? (Hakuna tatizo walilokabiliana nalo lililosababishwa na kutokuwa na mkate – tayari walikuwa wamekwishaona ile miujiza. Pamoja na hayo walichukulia kwamba alichokimaanisha Yesu kilihusiana na wao kutokuwa na mkate.)

 

1.                   Tunapokabiliana na chaguzi ngumu – je, tunapaswa kufikiria uwezekano wa kwamba Yesu hatatusaidia?

 


B.                  Soma Mathayo 16:12. Kwa nini Yesu anatumia “chachu ya mkate” kuwakilisha mafundisho ya viongozi wa dini? (Mambo ya Walawi 2:11 inakataza matumizi ya chachu (hamira) katika kumtolea Mungu sadaka. Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger inabainisha kuwa chachu inasababisha “uchangukaji na upotovu, jambo ambalo ni ishara ya uovu na nguvu ya dhambi.” Naamini usingependa fundisho lako lifafanuliwe kwa namna hiyo!)

 

III.               Mwamba

 

A.                  Soma Mathayo 16:13-14. Je, majibu hayo yangekukatisha tamaa endapo ungekuwa Yesu?

 

B.                  Soma Mathayo 16:15-18. Hili ndilo fungu linaloleta mjadala mkubwa sana. Yesu atajenga kanisa lake juu ya nini? (Yesu anasema kwamba atalijenga juu ya Petro.)

 

1.                   Je, una mashaka kidogo na jibu hili ikiwa nitakuambia kuwa Petro humaanisha “mwamba?” Ikiwa Petro inamaanisha “mwamba,” je, Yesu anarejea jambo gani anapozungumzia kujenga kanisa juu ya mwamba? (Inaonekana kuwa vigumu sana kutoa sifa nyingi kupindukia kwenye jibu kwamba ni “Petro,” kwa sababu Yesu anasema kuwa jibu sahihi lilitolewa na “Baba yangu aliye mbinguni” – na sio Petro. Huenda tunapaswa kuhitimisha kwamba mwamba ambao kanisa linajengwa juu yake ni watu (kama Petro) ambao wananena kile ambacho Mungu amewafunulia.)

 

2.                   Jambo gani limefunuliwa kwa Petro? (Kwamba Yesu ni “Mwana wa Mungu aliye hai.”)

 

3.                   Hebu subiri kidogo! Je, hilo linabadilisha kile unachodhani Yesu anakimaanisha kwa “mwamba” ambao juu yake atalijenga kanisa? (“Mwamba” sio tu wale ambao kupitia kwao Roho Mtakatifu anatupatia ufahamu, badala yake, ni kuelewa jambo la muhimu zaidi kiroho – kwamba Yesu ni Mungu. Yesu ni Masihi. Yesu ni “Mwana wa Mungu aliye hai.” Kanisa la Yesu litajengwa juu ya watu waliojawa na Roho ambao wanaelewa kuwa Yesu ni Mungu.)

 

4.                   Unafahamu kwamba mara kwa mara huwa ninakutaka uangalie muktadha unapojaribu kuelewa maana ya fungu katika Biblia. Je, Mathayo amekuwa akifanya nini katika injili yake yote? (Kuthibitisha kwamba Yesu ni Masihi, Yesu ni Mungu.)

 

a)                  Hiyo “inaashiria” nini kwenye uelewa wetu wa mwamba? (Mathayo hamtangazi Petro, amekuwa akitangaza uungu wa Yesu. Hicho ni kipengele kingine cha uthibitisho kuhusu kile ambacho Yesu anakimaanisha hapa.)

 

C.                   Soma Mathayo 16:19. Je, Yesu anawageuzia hukumu wanafunzi, ambao dakika chache zilizopita hata hawakuweza kutambua kama alikuwa anazungumzia mkate? (Sidhani! Ikiwa “mwamba” ni kumwelewa Yesu kunakotokana na kujawa Roho, basi tunaweza kuona kwamba kila mtu anayeukubali ufahamu huu makinifu anafunguliwa njia ya kuupata uzima wa milele, na wale wanaoukataa huu uelewa makinifu wanaanza kuelekea mauti ya milele.)

 

D.                  Soma Mathayo 16:20. Kwa nini wasiwaambie watu hizi habari njema kupindukia? (Haukuwa muda muafaka. Katika shughuli zetu za kiinjilisti tunatakiwa kumsikiliza Roho Mtakatifu kuhusu muda muafaka wa kupeleka injili kwa wengine.)

 

IV.               Karipio

 


A.                  Soma Mathayo 16:21-23. Kwa wakati mmoja Mungu anazungumza kupitia kwa Petro na muda unaofuata Petro anazungumza kwa niaba ya Shetani. Je, hiyo ni sahihi? (Soma Yakobo 3:10-12. Zamani nilikuwa ninaelewa kwamba Yakobo alikuwa akisema kuwa jambo hili haliwezekani. Petro anaonesha kuwa hii inawezekana – na kusema kweli, ninashukuru sana maelezo ya Mathayo yanayoonesha kuwa mara kwa mara tunapeleka ujumbe unaopingana wenyewe kwa wenyewe. Lakini, Yakobo yuko sahihi kwamba hii “haipaswi kuwa hivyo.”)

 

1.                   Soma tena Mathayo 16:23. Yesu anapomwambia Petro kwamba mawazoni mwake anawaza “mawazo ya wanadamu,” je, ni mambo gani hayo?

 

2.                   Je, inaonekana ni makosa kuhitimisha kwamba “Mwana wa Mungu aliye hai” hawezi kuuawa? (Petro alitaka Yesu awe Masihi ambaye atatawala, na Yesu alifahamu kuwa lazima awe Masihi atakayekufa kwa ajili ya watu wake.)

 

B.                  Soma Mathayo 16:24. Je, jambo hili linaonekana kukuogofya? Nani anayetaka kufanya hivi? (Kumbuka kwamba muktadha ni wa muhimu. Hapa kauli ya Yesu ni kali (ina nguvu sana) kwa sababu anataka kuwaelimisha (kuwasahihisha) wanafunzi juu ya ndoto yao ya mamlaka ya kidunia.)

 

C.                   Soma Yohana 15:10-13. Huu ni mjadala mwingine kuhusu “kuyaacha mambo mengine,” lakini katika muktadha wa “furaha.” Unaweza kuelezeaje jambo hili? (Utii kwa Mungu unahusisha kuziacha njia zetu zilizojaa ubinafsi. Kwa kuwa Mungu anafahamu kilicho bora kwa ajili yetu, kitendo hicho kinaleta furaha.)

 

V.                  Thawabu

 

A.                  Soma Mathayo 16:25-27. Je, unakubaliana na mambo haya? (Ishara ya ukomavu ni kujitoa sasa hivi kwa ajili ya kupata thawabu kubwa hapo baadaye. Kile tunachojitoa na kukiacha sasa hivi hakiwezi kulinganishwa na utukufu wa milele tutakaoufurahia.)

 

B.                  Soma Mathayo 16:28. Je, Yesu anawapotosha wanafunzi? Sasa ni maeluf ya miaka imeshapita baada ya Yesu kusema kauli hiyo, na bado Yesu hajarudi! (Watu wengi wanajaribu kusema kuwa Yesu hazungumzii ujio wake wa Mara ya Pili, lakini mafungu yaliyotangulia yanatuambia kuwa hicho ndicho ambacho Yesu anakizungumzia.)

 

C.                   Soma Mathayo 17:1-5. Ungeliitaje tukio hili? (Je, hiki si kionjo cha ujio wa Yesu Mara ya Pili? Je, huu sio uwezo wa mbinguni ukionekana na baadhi ya wanafunzi? Muktadha unaonesha kwamba hiki ndicho alichokimaanisha Yesu aliposema kuwa baadhi ya wanafunzi wake “watamwona Mwana wa Adamu akija” wangali wakiwa hai.)

 

VI.               Kuudhi

 

A.                  Soma Matthayo 17:24. Unadhani Petro alizingatia mambo gani katika kujibu swali hili? (Endapo Yesu anatimiza (analipa) wajibu wake wa kidini.)

 

B.                  Soma Mathayo 17:25. Yesu anaashiria kuwa suala gani ni kiini cha swali? (Ikiwa Yesu ni Mwana wa Mungu – kwa kuwa hii ni kodi ya hekalu.)

 

C.                   Soma Mathayo 17:26-27. Je, Yesu anapaswa kulegeza msimamo (compromise) kwenye suala linalobainisha kuwa yeye ni nani? Je, hapo kabla hatukufikia uamuzi kuwa hilo ni suala la muhimu sana kwa wanadamu?

 


1.                   Kwa nini “kuchukiza/kukasirisha/kuudhi” kunahusika tunapojadili suala la msingi la Ukristo? Je, si vibaya kulegeza masharti? (Yesu halegezi masharti kwenye suala la msingi. Nani awezaye kuvua samaki aliye na “chenji” kamili mdomoni mwake? Wakati huo huo, Yesu anaelezea jambo la msingi kwamba hatupaswi kuwaudhi watu wanaoshughulika na kazi zao.)

 

D.                  Rafiki, mara kwa mara wanafunzi wanaonekana kushindwa kuelewa jambo la dhahiri. Viongozi wa dini walishindwa kuelewa jambo la dhahiri. Yesu anatuambia kuwa Roho Mtakatifu atatufunulia mambo ya dhahiri. Je, utamwomba Roho Mtakatifu, sasa hivi, ili akupatie uelewa wa kiroho?

 

VII.  Juma lijalo: Miungu ya Roho (Pamoja na Mafunzo Mengine Kutoka kwa Yesu).