Bwana wa Wayahudi na Mataifa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 14 & 15)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
2
Lesson Number: 
7

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Watu wanaamini kwamba wanaume hawawaelewi wanawake kwa undani. Inawezekana wazo hili lilianzishwa na wanawake! Je, kuna watu ambao huwaelewi? Kwa wale unaowaelewa, je, huwa unawaelewa mara zote? Mojawapo ya sababu za kujifunza Biblia ni kumwelewa Mungu vizuri zaidi. Nadhani sababu mojawapo iliyomfanya Mathayo aandike waraka tunaojifunza katika somo la juma hili ni kutufundisha kumtumaini Mungu, hata pale ambapo hatuelewi maamuzi yake. Hebu tuzame kwenye somo letu ili tujifunze zaidi!

 

1)      Kifo cha Yohana Mbatizaji

 

a)      Soma Mathayo 14:6-11. Jambo gani lilisababisha kifo cha Yohana? (Herode kutaka kuonekana shujaa, kutokupevuka (uchanga) kwa Herode, na wasiwasi wake wa kupata aibu. Hila ya Herodia, hasira kutokana na kukemewa (na Yohana kwa ndoa yake isiyo halali – angalia Mathayo 14:3-5). Yote haya yanafungamanishwa na binti wa Herodia kucheza dansi ya kifisadi.)

 

i)        Ikiwa unampenda Yohana, endapo ungekuwa mwanafunzi wake, kifo chake kilikuwa cha kutisha sana na kuacha pengo kubwa. Mazingira yanaongezea nini kwenye mwitiko (reaction) wako?

 

b)      Soma Mathayo 14:12. Kwa nini wanafunzi wa Yohana walimwendea Yesu?

 

i)        Je, walidhani kwamba Yesu alipaswa kumwokoa Yohana? (Majuma mawili yaliyopita tulijadili kwamba huenda Yohana Mbatizaji alikuwa anashangaa kwa nini Yesu hakumwokoa.)

 

c)      Soma Mathayo 14:13. Kwa nini Yesu alitafuta muda kuwa faraghani baada ya kusikia habari za kifo cha Yohana? (Aliathiriwa sana na habari hizo. Yumkini alikuwa anatafakari kwamba tukio hili lilithibitisha kuwa atakuwa mikononi mwa Warumi. Huenda alikuwa tu na masikitiko kwamba binamu yake alikuwa amefariki.)

 

d)     Soma Mathayo 14:14. Je, ungefanya hivi endapo ungekuwa Yesu? (Nahisi ningekuwa ninajiliwaza huzuni yangu na kujiponya hisia zangu. Lakini, tunaona kwamba Yesu anajali zaidi kuhusu kuwasaidia watu wengine.)

 

2)      Kuwalisha Watu

 

a)      Soma Mathayo 14:15-17. Je, hili ndilo jibu ambalo ungelitoa?

 

i)        Soma tena Mathayo 14:14. Katika muktadha huu, je, hilo ndilo jibu ambalo wanafunzi walipaswa kulitoa? (Walikuwa hawaangalii taswira pana. Walikuwa hawautegemei uwezo wa Yesu. Walikuwa wanategemea kile wanachokimiliki.)

 


b)      Soma Mathayo 14:18-21. Wanafunzi ni wa muhimu kiasi gani katika huu muujiza?

 

i)        Je, unahitajika kuwa na imani kamilifu ili kushirikishwa kwenye muujiza? (Kwa dhahiri hapana. Ama kwa hakika hii ni habari njema.)

 

ii)      Soma tena Mathayo 14:16-17. Je, Yesu alitarajia wanafunzi watende huu muujiza?

 

iii)    Yesu alitendaje huu muujiza – kuwalisha watu 15,000 kutokana na mikate mitano na samaki wawili? (Angalia tena Mathayo 14:19. Alitazama mbinguni, akashukuru na kuanza kuimega ile mikate.)

 

c)      Soma Mathayo 14:22. Hii inashangaza – “Yesu aliwalazimisha wanafunzi kupanda chomboni.” Kwa nini hawakutaka kuondoka? (Soma Yohana 6:14-16. Hii inatupatia jibu. Mtiririko wa matukio uliobainishwa na Yohana unabainisha kuwa watu, baada ya kuona huu muujiza mkuu, waliamua kumfanya Yesu kuwa mfalme wao. Bila shaka wanafunzi walisema, “Naam, hebu tufanye hivi! Tutakuwa wasaidizi wa Yesu katika ufalme mpya!”)

 

3)      Upepo

 

a)      Soma Mathayo 14:23-24. Je, tatizo la wanafunzi kukabiliana na upepo liliakisi mtazamo wao – kwamba walikuwa tu hawaendelei maishani?

 

b)      Soma Mathayo 14:25. “Zamu ya nne” ni kitu gani? (Hii ni kati ya saa 9 na 12 za asubuhi kwa mujibu wa maoni ya Adam Clarke.)

 

i)        Hiyo inakuambia nini kuhusu kiwango cha ugumu ambao wanafunzi walikabiliana na upepo? (Walikuwa wakienda pole pole sana tangu walipopata chakula cha usiku.)

 

ii)      Una maoni gani kuhusu usununu (hali) wa wanafunzi? (Hawakufurahia kitendo cha kushindwa kumfanya Yesu kuwa mfalme. Walikuwa wamekatishwa tamaa na upepo.)

 

iii)    Kwa nini Yesu alitembea juu ya maji kwenda kuwaona?

 

c)      Soma Mathayo 14:26. Unadhani Yesu alitarajia mwitiko (reaction) huu? (Sidhani. Alikwenda kuwafariji, sio kuwatisha.)

 

d)     Soma Mathayo 14:27-31. Je, unaweza kusema kuwa Petro alikuwa na “imani ndogo?”

 

i)        Kwa kumlinganisha na nani? Wanafunzi chomboni?

 

ii)      Kwa nini Mathayo anajumuisha kisa hiki kwenye mfululizo wa hivi visa? (Kifo cha Yohana kinaonekana kama kushindwa kwa watu wa nje. Wanafunzi wa Yesu wamekata tamaa. Mathayo anaelezea visa hivi ili kujenga hoja dhidi ya kukatishwa tamaa. Anatuonesha kwamba Yesu ana uwezo wa kutenda miujiza, uwezo wa kuwashawishi watu wengine kumfanya yeye kuwa mfalme, na mamlaka juu ya nguvu za mvutano na vitu vingine. Nadhani jambo la muhimu ni kwamba Yesu anachagua muda wa kuingilia kati, hapungukiwi mamlaka ya kuingilia kati.)


 

e)      Soma Mathayo 14:32. Kwa nini asitembee ufukweni? (Yesu amejikita zaidi kwa wale waliopo chomboni.)

 

f)       Soma Mathayo 14:33. Sasa wanafunzi wanaonesha imani. Yesu amewaendea na kubadilisha kabisa usununu (hali) wao. Je, Yesu atakutendea hivyo? Je, atakuja nyakati ambazo umekata tamaa na kuvunjika moyo na kukudhihirishia uwezo wake?

 

i)        Watu wengi wanakana kwamba Yesu si Mungu. Wanasema kuwa Yesu ni “mtu mwema tu.” Hii inasema nini kuwahusu watu hao? (Hawajui chochote kuhusu Biblia. Biblia inabainisha wazi kabisa kwamba Yesu ni Mungu.)

 

g)      Soma Mathayo 14:34-36. Je, Yesu alikuwa anaamua juu ya watu watakaoponywa na wale ambao hawataponywa? (Hapana.)

 

i)        Kwa nini hafanyi hivyo? (Tulianza sura hii ya kitabu cha Mathayo kwa Yesu kufanya uamuzi wa ama kumwokoa Yohana au la. Tumeishia na uponyaji mkuu (wa watu wengi) kwa wote waliomwendea Yesu.)

 

4)      Utamaduni

 

a)      Soma Mathayo 15:1-6. Huu ni mfano mwingine ambapo inaonekana Yesu anajibu mashtaka ya kutenda kosa kwa kusema “Nanyi pia mnatenda makosa!” Je, kweli hicho ndicho anachokisema Yesu? (Viongozi wa dini wanadai ukiukwaji wa “utamaduni” wao. Yesu anajibu kwa kusema kuwa utamaduni wao ni jambo lenye mashaka. Linabatilisha neno la Mungu angalao kwenye baadhi ya vipengele.)

 

b)      Soma Mathayo 15:7-9. Isaya anatabiri nini kuhusu matatizo waliyonayo watu wa Mungu? (Kwamba wanafuata sheria za mwanadamu badala ya kufuata sheria za Mungu. Hawana ibada ya “kweli kutoka moyoni.”)

 

i)        Kusema kweli, nadhani wanafunzi wanapaswa kunawa mikono yao kabla ya kula. Kwa nini kuna pingamizi la aina hiyo kutoka kwa Yesu? (Hili ni jambo la muhimu. Kuna mawazo mazuri mengi sana. Suala lililopo ni endapo tunajikita kwenye “mawazo mazuri” au kwenye matakwa ya Mungu.)

 

c)      Soma Mathayo 15:10-11. Je, Yesu amebadili mada? (Hapana. Anatoa wito kwa makutano ili waweze kuelewa ujumbe wake kuhusu mjadala juu ya kunawa mikono.)

 

i)        Ujumbe wa Yesu ni upi? (Kilichotoka kinywani mwa viongozi wa dini kilikuwa ni ukosoaji. Kitendo hiki ni kibaya zaidi kuliko kunawa mikono yako.)

 

d)     Soma Mathayo 15:12. Je, unachukizwa na wazo hili kwamba kiingiacho kinywani hakikutii unajisi?

 

e)      Soma Mathayo 15:13-20. Unauelewaje ujumbe wa Yesu – je, anazungumzia tu kuhusu unawaji wa mikono? (Inaonekana ujumbe wake ni mpana zaidi. Vitu tuvilavyo na tunywavyo, kama ilivyo kwa unawaji wa mikono, vinaendana na suala la kuishi maisha bora. Vinaakisi mawazo mazuri. Hata hivyo, tunayoyasema yanaakisi tunayoyafikiria, na kwenye mawazo ndipo tunapopata pambano la kweli dhidi ya dhambi.)

 


5)      Mataifa

 

a)      Soma Mathayo 15:22-27. Unaelezeaje kitendo cha Yesu kumwita huyu mwanamke masikini “mbwa?” (Soma Mathayo 15:28. Yesu alikuwa anamjaribu.)

 

b)      Soma tena Mathayo 14:36. Je, hii ni haki? Wote wanaomgusa Yesu wanaponywa. Mwanamke huyu ilimpasa kustahimili matusi na fedheha ili mwanaye aweze kuponywa. Jambo gani linaendelea hapa? (Nadhani hii ni kwa faida ya wanafunzi (angalia Mathayo 15:23). Yesu anataka kuwaonesha kuwa watu wa mataifa wanaweza kuwa na imani kubwa. Jifunze kutokana na fundisho hili kwa ajili ya nyakati ambazo Mungu anaonekana kukataa/kujizuia kukusaidia.)

 

c)      Rafiki, tunaona kwamba Yesu anafanya maamuzi ya kusaidia na kuponya, maamuzi ambayo mara nyingine ni magumu sana kuyaelewa. Je, utadhamiria leo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuamua tu kumtumaini Mungu?

 

Juma lijalo: Petro na Mwamba.