Fundisho Mlimani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 5)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
2
Lesson Number: 
3

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Fundisho Mlimani ni wasilisho la kushangaza sana. Hata hivyo, kuna mitazamo tofauti kuhusiana na fundisho hilo. Wengine wanadhani kuwa ni “orodha ya kanuni” zitakazotumika tutakapokuwa mbinguni – na hivyo fundisho hilo halituhusu kwa sasa. Wengine wanadhani kuwa fundisho hilo limedhamiria kutufanya tuhitimishe kuwa haiwezekani kufikia viwango vya Mungu, na hivyo tunasukumwa kuitegemea neema. Wengine wanalichukulia fundisho hilo kama changamoto kwao ili kuboresha matendo yao ya haki kwa kiwango cha juu. Mtazamo wangu ni kwamba Fundisho Mlimani linatuonesha kwamba neema sio tu suala la wokovu, bali pia ni suala la mtindo wa maisha. Mungu anatupatia wito wa kutegemea uwezo wake katika mambo yote, na hiyo inajumuisha namna tunavyoishi. Hebu tuzame kwenye somo hili linalotafakarisha ili tujifunze zaidi!

 

I.                   Mustakabali Chanya

 

A.                Soma Mathayo 5:3-6. Je, unataka kuwa kwenye kundi lolote kati ya makundi yafuatayo: umaskini, huzuni, upole (unyenyekevu), njaa au kiu? (Hakuna anayetaka kuwa kwenye kundi lolote.)

 

1.                  Yesu anasema nini kuhusu watu waliopo kwenye makundi haya? (Watabarikiwa na Mungu na hali yao itabadilika na kuwa nzuri.)

 

2.                  Je, kuna mtu amewahi kukuambia kwamba udhamirie kuwa kwenye mojawapo ya makundi haya? (Nimewahi kuambiwa kuwa nijitahidi kuwa kwenye makundi haya kwa sababu makundi haya yamebarikiwa na mwisho wake ni mzuri, yaani kupata vitu vizuri. Nina mashaka kama haya ni malengo – tofauti na kutamani kuhesabiwa haki. Hivi karibuni tulijifunza kuwa tunapaswa kuwa na malengo ya kufufuliwa katika “ufufuo wa kwanza” – ambao ni wafu wenye haki. Hiyo haimaanishi kuwa ninapaswa kutamani kufa! Badala yake, huu unaonekana kuwa ujumbe wa rehema kwa wale wanaojikuta kwenye hali ngumu.)

 

B.                 Soma Mathayo 5:7-9. Je, ungependa kuwa mmojawapo kati ya hawa? (Naam, mie ningependa. Ni jambo la maadili mema kuwa mtu mwenye rehema, moyo safi, au mpatanishi.)

 

1.                  Tunajifunza mambo gani chanya kuhusu mustakabali wao? (Mambo mazuri/mema yatawatokea.)

 

2.                  Hebu jiweke kando kidogo. Tumepitia orodha ya mambo ambayo kwa ujumla tusingependa kuwa hivyo na orodha ya mambo ambayo tungependa kuwa hivyo. Kuna habari gani njema kuhusu orodha zote mbili? (Kwamba mambo mazuri yanawangoja.)

 

C.                 Soma Mathayo 5:10-12. Kwa mara nyingine tuna orodha ya mambo ambayo tusingependa yatutokee. Yesu anazungumzia jambo gani chanya kuhusu sisi kujikuta katika hali hii? (Kwa mara nyingine, Yesu anaahidi matokeo chanya. Anaongezea kuwa hatuko peke yetu. Watu maalum walio na uhusiano wa pekee na Mungu (manabii) wanajikuta kwenye hali hiyo hiyo. Suala la msingi ni kwamba hatuko peke yetu ikiwa mambo haya yatatutokea.)


 

II.                Sheria Chanya

 

A.                Soma Mathayo 5:13-16. Mungu anatutaka tufanye nini? (Anatutaka tumpe sifa na utukufu kwa kutenda matendo mema.)

 

1.                  Rejea ya chumvi iliyoharibika na isiyofaa kabisa inatuelezea jambo gani? (Ikiwa hatumpi Mungu sifa na utukufu, basi hatutendi jukumu tulilopewa.)

 

B.                 Soma Mathayo 5:17. Utume wa Yesu ni upi kwa kuizingatia torati? (Kuitimiliza!)

 

1.                  Je, huu ni ujumbe wa neema? (Ndiyo! Yesu aliishi, akafa na kufufuka ili tuweze kuikiri kazi aliyoikamilisha kwa ajili yetu.)

 

2.                  Je, Yesu anamaanisha nini anaposema kwamba hatangui torati? (Kimantiki neema haihafifishi torati. Badala yake, inaonesha jinsi torati ilivyo na umuhimu. Ikiwa utawala wa sheria haukuwa na maana, Mungu angeweza tu kuifutilia mbali torati na hivyo kujiepusha na maumivu mengi.)

 

C.                 Soma Mathayo 5:18-19. Kwa nini watu ambao sio tu kwamba wanavunja sheria, bali pia wanawafundisha watu wengine kuvunja sheria, wawepo kwenye Ufalme wa Mbinguni? (Neema! Lakini, rafiki, je, unataka kuwa na hadhi mbaya katika umilele wote? Hii inaonesha kwamba wale wanaopingana na utunzaji wa sheria hawaelewi taswira kamili ya neema. Hawaelewi umuhimu wa kumpa Mungu sifa na utukufu kutokana na jinsi tunavyoishi.)

 

D.                Soma Mathayo 5:20. Hawa ndio viongozi wa juu wa kipindi hicho. Haki yetu inawezaje kuzidi haki yao? Kwa nini hata hilo liwe lengo? (Mtu anayekiri na kuipokea haki ya Yesu kwa neema, mara zote atakuwa na haki zaidi kuliko mshika dini anayeng’ang’ania matendo kwa ajili ya kuhesabiwa haki. Kujibidiisha kwenye matendo ni madhumuni ya mpumbavu. Ni kujitumainia mwenyewe (kama ilivyo kwa watu wanaoabudu miungu), badala ya kumtumaini Mungu.)

 

III.             Sheria (Kanuni) Kuhusu Msisimko wa Mwili

 

A.                Soma Mathayo 5:21-22 na Mathayo 5:27-28. Tafakari mafungu haya kwa dakika chache. Mungu anatuonya dhidi ya jambo gani linaloonekana kuvuka mipaka ya kile kinachotakiwa kutendwa na Amri Kumi? (Yesu anazungumzia mawazo yetu, mtazamo wetu. Hasira, maneno ya hasira, chuki, na tamaa vyote vimo akilini.)

 

1.                  Soma Warumi 8:5-8. Je, hii inaleta mantiki kwako – kwamba namna unavyoyaweka mawazo yako inaelezea jinsi utakavyoenenda? (Nadhani hiki ndicho Yesu anachokimaanisha. Kuwa mwangalifu na mawazo yako ikiwa unataka kuepuka kujiingiza kwenye matatizo na dhambi.)

 

a.                   Ikiwa niko sahihi, je, jambo hili linazungumzia nini kuhusu asili ya hasira, tamaa na maneno makali na ya kuchukiza? (Nina mashaka kama kupendezwa (kufurahia) na wanawake wazuri au kufadhaika ni sawa na uzinzi na kutenda mauaji. Badala yake, nadhani Yesu anatufundisha kwamba dhambi hutokea baada ya kukasirika kiasi cha kufikia hatua ya kuwa tayari kuua, na kuwa na mawazo yenye dhamira ya kufanya uzinzi. Ikiwa tuko radhi kutenda dhambi, lakini hatuna fursa, basi hatuvuki mpaka na kuingia kwenye dhambi.)

 


B.                 Hebu turejee nyuma ili tuendelee na mafungu tuliyoyaruka. Soma Mathayo 5:23-26. Hapa ushauri wa jumla ni upi? Unaweza kuandikaje kwa ufupi jambo hili kwenye msitari mmoja? (Jitahidi kuishi kwa amani na watu wengine.)

 

1.                  Ni mara ngapi umewasikia Wakristo wakisema kuwa wana wakati mgumu na watu wengine, wao ni waathirika, kutokana na imani zao za dini? (Bila shaka kuna nyakati wapagani huwasababishia Wakristo matatizo. Hata hivyo, watu wengi ninaowasikia wakisema hivyo hawafanyi jitihada za kuishi kwa amani na watu wengine.)

 

C.                 Soma Mathayo 5:29-30. Je, kitendo hiki kinaleta mantiki yoyote kwako? Hivi punde tu Yesu ametuambia kuwa kufikiria jambo fulani ni sawa na kutenda dhambi. Kung’oa jicho lako au kukata mkono wako kunawezaje kufanya akili yako isitende dhambi? (Kitendo hicho hakiwezi kuzuia. Niliwahi kuwa na mwanadarasa mmoja ambaye alikuwa anapoteza uwezo wake wa kuona. Akaniambia kuwa kitendo hicho hakikumwepusha na matatizo ya kutamani. Nadhani Yesu anataka apate usikivu wetu kuhusu umuhimu wa mafundisho yake. Bila shaka ndio maana sote tunakubaliana kwamba kupoteza sehemu ya kiungo cha mwili ni bora kuliko kuikosa mbingu.)

 

IV.             Sheria (Kanuni) ya Kulipiza Kisasi

 

A.                Soma Mathayo 5:38-41. Yesu anamaanisha nini anaposema “Mmesikia kwamba imenenwa?” (Sheria kuhusu ulipizaji kisasi imeandikwa mara tatu ikiwa ni maelekezo ya dhahiri kutoka kwa Mungu. Angalia Kutoka 20:22 na Kutoka 21:23-25; Mambo ya Walawi 24:17-20; na, Kumbukumbu la Torati 19:21.)

 

B.                 Soma tena Mathayo 5:39 na Yohana 18:22-23. Kwa nini Yesu hakuufuata ushauri wake mwenyewe? Badala ya kugeuza shavu lake jingine, aliibua changamoto ya kisheria kutokana na kupigwa kwake kofi!

 

C.                 Pitia kwa haraka haraka Mathayo 18:23-35 na usome Mathayo 18:32-34. Je, sheria ya ulipizaji kisasi ni kanuni ya Kibiblia? (Ndiyo! Bwana alibadili uamuzi na kumfanya mtumwa asiyesamehe ateswe. Lakini, malipo sio kwa ajili yetu. Yesu hakujibu kwa kurudishia kofi baada ya yeye kupigwa kofi. Tunatakiwa kuacha malipizi kwa Mungu. Mungu ametusamehe mara nyingi sana, tunawezaje kushindwa kuwasamehe wale waliotudhuru?

 

1.                  Soma Zaburi 84:5. Yesu anatufundisha habari za neema kuwa mtindo wetu wa maisha. Kama ambavyo tunamtegemea Yesu kwa ajili ya wokovu wetu, vivyo hivyo tunapaswa kumtegemea Mungu kuwalipizia kisasi wale waliotudhuru.)

 

2.                  Soma Warumi 12:19. Paulo anashiriki nasi ahadi gani kuhusu kanuni ya ulipizaji kisasi?

 

3.                  Umewahi kulipiza kisasi katika siku za nyuma? Ulipata matokeo gani? (Ubashiri wangu ni kwamba mambo hayakwenda vizuri. Kitendo hicho hakikukufanya ujisikie vizuri na kiliendeleza mtafaruku. Kama jinsi neema inavyokupatia amani kuhusu wokovu wako, vivyo hivyo neema kama mtindo wa maisha hukupatia amani maishani.)

 

D.                Rafiki, nadhani Fundisho Mlimani ni wito kwetu wa kumtumaini Mungu kututunza na kututatulia matatigo magumu maishani. Je, utafanya uamuzi, sasa hivi, kuutegemea uwezo wa Mungu na kuifanya neema kuwa mtindo wako wa maisha?

 

V.                Juma lijalo: “Inuka Uende Zako!” Imani na Uponyaji.