Petro Azungumzia Pambano Kuu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(1 Petro 2-4, 2 Petro 1)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
1
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Juma hili tunaangalia jambo ambalo tumejifunza mara nyingi, suala la neema na matendo. Kwa mtazamo wangu, hatuwezi kujifunza jambo hili kupita kiasi. Sio kwamba suala la neema ni gumu sana, bali maisha yetu yanakuwa magumu tunapokabiliana na masuala halisi kivitendo katika maisha yetu. Matendo ni ya muhimu. Sio tu kwamba yana athari chanya kubwa kwenye ubora wa maisha yetu, bali jambo la muhimu zaidi ni kwamba matendo ni ya msingi maishani mwetu katika kumpa Mungu utukufu. Hebu tuzame kwenye somo letu ili tuone masuala tunayoweza kujifunza kivitendo!

 

I.                              Ishi kwa Uhuru, Ishi kwa Usahihi

 

A.                         Soma 1 Petro 2:1-3. Je, inawezekana “ukajiweka mbali” na hila, unafiki, husuda na masingizio? Je, unaweza “kuyatamani” maziwa safi ya kiroho? (Baadhi ya haya ni matendo – kwa mfano maneno tunayoyazungumza. Lakini, baadhi yake ni mitazamo. Ni vigumu kuyabadili yote kwa kutamka tu kwamba unajiweka nayo mbali.)

 

1.                           Petro anamaanisha nini anaposema kuwa ili kwa hayo “mpate kuukulia wokovu?” (Habari njema ni kwamba tunaokolewa kwa neema. Kuyalenga macho yetu kwenye haya matendo na mitazamo isiyotakiwa huja baada ya wokovu wetu. Hayatupatii wokovu wetu.)

 

2.                           Ishara gani ya jinsi tunavyopaswa kusonga mbele inapatikana kwenye kauli ya Petro, “ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili?” (Sidhani kama kujikita kwenye dhambi ndio njia ya kutibu dhambi. Petro anaposema kuwa “tumeonja” mambo mema ya Mungu, anatuelekeza kwenye uelekeo tunaopaswa kuufuata. Jikite kwenye mambo yaliyo mema, na kilicho kibaya kitaanguka pembeni. Bado ni muhimu kuwa macho kwa jambo ambalo ni dhambi, na hiyo ndio sababu, kama tulivyojifunza siku za hivi karibuni, tulipewa Amri Kumi.)

 

B.                         Soma 1 Petro 2:4-5. Juma lililopita tulijadili kuhusu umuhimu wa kanisa. Petro anasema nini kuhusu umuhimu wa kuabudu pamoja na waumini wenzetu? (Sisi ni “mawe yaliyo hai” katika “nyumba ya Roho” ambapo tunaingia kwenye ukuhani kutoa dhabihu za Roho.)

 

1.                           Tofauti na kufanya kazi pamoja, jambo hilo linaonekana kuwa na mashaka. Unadhani inamaanisha nini kutoa dhabihu za Roho? (Nadhani ni kuishi maisha matakatifu, kuutangaza Ufalme wa Mungu kwa kile unachokitenda na kile unachokisema.)

 

C.                         Soma 1 Petro 2:6. Hii inaashiria kuwa sisi “mawe yaliyo hai” tunapaswa kuhusianaje na “jiwe kuu la pembeni, teule lenye heshima?” (Tunatakiwa kumtumaini Mungu.)

 

 

1.                           Sasa unganisha mambo yote haya pamoja. Tunatoaje dhabihu za Roho zitakazoongeza tamaa yetu kwa mambo yaliyo mema na kupunguza tamaa yetu kwa mambo yaliyo maovu? (Kwa kumtumaini Mungu!)

 

D.                         Soma 1 Petro 2:7-8. Jiwe la “pembeni” linafanya nini? (Linalinda sehemu ya juu. Yesu sio tu msingi wetu (jiwe la pembeni), bali yeye pia ni jiwe linalotufunika (jiwe linalolinda ukuta usianguke). Tunazungukwa na uangalifu wake.)

 

1.                           Petro anamaanisha nini anaposema jiwe liletalo kikwazo na jiwe linalolinda ukuta? Ama tunaweza kuweka tumaini letu kwa Yesu, au tunaweza kumkataa na anakuwa tatizo linalosababisha tujikwae na kuanguka.)

 

2.                           Inamaanisha nini kusema kwamba “hatima” ya mwovu ni kutokutii? Je, inamaanisha kuwa hawana uchaguzi, Mungu amewachagulia? (Hapana. Sote uelekeo wetu ni kutokutii. Hicho ndicho kinachofanya tatizo la dhambi liwe gumu sana kwetu sote. Suluhisho la tatizo la dhambi ni kuelewa, kutumaini, kwamba tunaokolewa kwa neema. Hiyo ndio sababu Yesu ndiye jiwe la sakafuni na ndiye dari letu, na jiwe lenye kikwazo kwa waliopotea.)

 

E.                          Soma 1 Petro 2:9-10. Kazi yetu ni ipi? (“Kuzitangaza fadhili” za Mungu wetu aliyetuonesha rehema kwa kutuokoa kwa neema.)

 

II.                           Matamanio [Tamaa za Mwili]

 

A.                         Soma 1 Petro 2:11-12. Nimekuwa nikielezea kipengele cha neema ambacho Petro anakizungumzia. Petro anasema kuwa umuhimu wa matendo sahihi ni upi? (Yanampa Mungu utukufu. Yanaonesha kuwa mashambulizi ya ulimwengu kwa Ukristo ni ya uongo.)

 

1.                           Petro anaamini kuwa jambo gani ni la muhimu kwenye matendo mema? (“Kuepukana na tamaa mbaya za mwili.” Tunapojikita dhambini, badala ya kujikita kwenye matendo mema, tunajiweka katikati ya matamanio ya dhambi. Matamanio hayo yanatuingiza kwenye matendo ya dhambi. Tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu ili kuwa na matamanio sahihi.)

 

B.                         Soma 1 Petro 4:1. Mtazamo wa Yesu ni upi kuhusu dhambi na mateso? (Yesu aliteseka sana ili kuimaliza hii dhambi.)

 

1.                           Tunawezaje “kujivika” mtazamo huo huo? (Tunatakiwa kuichukulia dhambi kwa dhati. Tunatakiwa kukumbuka mateso iliyomsababishia Yesu, na kutambua mateso inayoweza kutusababishia.)

 

C.                         Soma 1 Petro 4:2. Tunapaswa kuwa na lengo gani maishani mwetu? (Kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.)

 

D.                         Soma 1 Petro 4:3-6. Waovu wanahukumiwa kutokana na nini? (Matendo yao maovu.)

 

1.                           Sababu ya injili kuhubiriwa kwao ni ipi? (Ili waweze kufanya uamuzi wa kuokolewa kwa njia ya neema. Ili waweze kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu.)

 

E.                          Soma 1 Petro 4:7. Je, umewahi kupitia uzoefu huu? Kwamba unapata ugumu wa kuomba unapokuwa umeburuzwa dhambini?

 

 

F.                           Soma 1 Petro 4:8. Upendo unasitirije dhambi? (Tunapofahamu kuwa mtu fulani anatupenda, kitendo hiki kinatusaidia kutoangalia zaidi upungufu wa mtu huyo. Ama kwa hakika, taswira pana ni kwamba kafara ya upendo wa Yesu husitiri dhambi zetu!)

 

III.                        Ujasiri wa Mustakabali Wetu [wa Siku Zijazo]

 

A.                         Soma 2 Petro 1:16-18. Kumbuka kwamba jambo la msingi katika maisha ya Mkristo ni kumtumaini Mungu. Ikiwa unamwamini Yesu, je, jambo lenye changamoto kubwa kuliko yote kuhusu kumtumaini Mungu ni lipi? (Endapo Yesu alishuka chini kutoka mbinguni, akaishi kama mwanadamu, akaishi maisha yasiyo na dhambi, akafa kwa ajili ya dhambi zetu, na akafufuka na kurejea kwenye mahali pake sahihi kule mbinguni.)

 

1.                           Kwa nini Petro anasema kuwa tunapaswa kuamini jambo hili? Kwa nini tunapaswa kutumaini jambo hili? (Kwa sababu Petro anasema kuwa alikuwepo. Aliona. Alisikia. Alishuhudia muungano wa kimbingu.)

 

a.                            Mashahidi wanaoshuhudia juu ya tukio halisi huwa sio wa kuaminika sana. Kwa nini tunapaswa kuamini ushuhuda huu? (Tunapaswa kuuamini kwa sababu moja tu, hakuwepo shahidi mmoja pekee. Walikuwepo mashuhuda wengi. Lakini, unapoangalia kwamba wanafunzi wa Yesu waliacha njia ya maisha yao ili kushiriki injili na watu wengine, kazi ambayo iligharimu maisha ya wengi wao, basi tunaweza kuwa na ujasiri kwamba wanasema ukweli.)

 

B.                         Soma 2 Petro 1:19. Tuna msingi gani mwingine wa kutufanya tuamini habari za maisha ya Yesu? (Petro anasema kuwa ikiwa utasoma habari za manabii wa Agano la Kale, walitabiri kuwa Yesu atakuja. Tunao ushuhuda wa manabii wa Biblia.)

 

C.                         Soma 2 Petro 1:20-21. Tuna msingi gani mwingine tena wa kutufanya tuamini habari za Yesu? (Petro anarejea juu ya matendo yasiyo ya kawaida. Anasema kuwa manabii walivuviwa na Mungu. Nadhani pia tunaweza kuelewa jambo hili likimaanisha kuwa maandiko ya Petro yamevuviwa na Mungu.)

 

1.                           Je, matendo ya Roho Mtakatifu maishani mwako yanaishuhudia injili? (Ikiwa umepitia uzoefu wa uwezo na mibaraka ya Roho Mtakatifu maishani mwako, basi hapo pia una shuhuda mwingine!)

 

D.                         Soma 2 Petro 3:3-4. Ni wakati gani ambapo watu watahoji kuwa Yesu harudi tena kwa sababu hadi sasa bado tu hajarejea? (“Katika siku za mwisho.”)

 

E.                          Soma 2 Petro 3:5-7. Kwa nini tuanapaswa kuamini kuwa Yesu anakuja tena? (Historia! Yesu aliumba ulimwengu. Yesu alitangaza hukumu duniani katika kipindi cha gharika. Kama Muumba wetu, Yesu ana nia njema endelevu kwetu na kukomesha kabisa tatizo la dhambi.)

 

F.                           Rafiki, je, unamtumaini Mungu? Suala hili linaendelea kwenye vipengele vyote kimatendo maishani mwetu. Suala hili ndilo msingi wa neema – kwamba tunamtumaini Mungu kwa ajili ya wokovu wetu na wala hatuyatumaini matendo yetu wenyewe. Ni msingi wa jinsi tunavyoishi, je, tunamtumaini katika kuyaongoza matamanio yetu na matendo yetu? Je, tunajikita kwenye mambo yaliyo mema, badala ya kujikita kwenye juhudi zetu wenyewe katika kukomesha kabisa dhambi maishani mwetu? Je, unaamini kuwa Yesu alikuja duniani na kupita kwenye mapito tunayoyapitia? Je, unaamini kuwa anakuja tena kukomesha tatizo la dhambi na kutuchukua ili kukaa naye milele? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu sasa hivi ili akusaidie umtumaini Mungu katika mambo yote?

 

 

IV.                      Juma lijalo: Kanisa Lililo Katika Mapambano.