Uasi Ulimwenguni na Wazee

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mwanzo 4, 6, 22 & 45)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
1
Lesson Number: 
3

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kwenye somo letu la kwanza katika mfululizo wa masomo haya tulijifunza jinsi dhambi ilivyoanza mbinguni. Kisha tukajifunza jinsi mchochezi wa dhambi mbinguni, ambaye alitupwa kutoka mbinguni, alivyoeneza tatizo la dhambi duniani kwa viumbe wakamilifu walioumbwa na Mungu: Adamu na Hawa. Juma hili tunachunguza jinsi dhambi ilivyoendelea kupenyeza madhara yake hapa duniani. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

  1. Wana
    1. Soma Mwanzo 4:1-2. Je, unakumbuka jinsi ulivyojisikia ulipompata mtoto wako wa kwanza? Mimi nilikuwa ninadhani kwamba mwanangu (wa kiume) alikuwa anafanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa na mtoto mwingine yeyote yule katika historia ya ulimwengu huu! Unadhani ilikuwaje kwa mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa, kwa kuwa ilikuwa ni ukweli kwamba matendo ya Kaini wakati akiwa mtoto yalikuwa hayajawahi kutokea (yalikuwa ya pekee)?
      1. Angalia mgawanyo wa kazi kati ya hawa wana wawili. Unadhani kwa nini walichagua kazi hizi? (Soma Mwanzo 3:17. Kaini anatekeleza haswaa kile ambacho Mungu alisema kuwa anapaswa kukifanya. Huenda Habili alitaka kuwa tofauti kidogo na kudhani kwamba kazi yake ilikuwa ya kiroho zaidi.)
    2. Soma Mwanzo 4:3-5. Unaweza kuelewa sababu ya ghadhabu ya Kaini? (Bila shaka alidhani kwamba alikuwa anatekeleza kazi iliyoamriwa na Mungu. Kwa nini matokeo ya kazi hiyo hayastahili kutolewa sadaka?)
    3. Soma Mwanzo 4:6-7. Tunajifunza nini kuhusu kama ghadhabu ya Kaini ina sababu za msingi? (Tukisoma kwa makini tunajifunza kwamba ghadhabu ya Kaini haina uthibitisho. Mungu alipozungumza naye kuhusu kutenda “kilicho sahihi,” hii inabainisha kuwa Mungu alimpa maelekezo juu ya utoaji wa sadaka sahihi.)
      1. Asili ya anguko la Kaini katika hatua hii ni ipi? Unailinganishaje na dhambi ya mama yake? (Ilikuwa inafanana na dhambi ya Hawa kwa maana ya kwamba kwa dhahiri hakuamini alichokisema Mungu kuhusu sadaka sahihi inayopaswa kutolewa. Kaini aliamua kufuata mantiki yake binafsi kuhusu kile anachopaswa kukitoa sadaka, kwa mujibu wa mazingira ya kazi yake.)
    4. Soma Mwanzo 4:8-12. Mungu anatoa adhabu ya namna gani? (Katika Mwanzo 3:17-19 tulijifunza kuwa adhabu mojawapo kwa dhambi ya asili ilikuwa ni kwamba kutakuwa na ugumu katika ukulima wa mazao ya chakula. Adhabu ya Kaini ni kali zaidi, ardhi haitamzalia mazao yoyote ya chakula.)
      1. Jiweke kwenye nafasi ya Adamu na Hawa. Mtoto wao wa kwanza amemuua mtoto wao wa pili, na kisha mtoto wa kwanza kuzaliwa anapelekwa uhamishoni. Wanawapoteza watoto wao wote wawili kwa siku moja. Una maoni gani kuhusu jambo hili?
      2. Unaifikiriaje adhabu aliyoitoa Mungu kwa Kaini? (Soma Mwanzo 9:5-6. Ni mauaji ya kudhamiria, na hayajawahi kutokea. Pamoja na hayo, Mungu alimpunguzia Kaini adhabu.)
      3. Unadhani nani alimhamasisha Kaini kufanya mauaji?
        1. Unadhani maisha yangekuwaje endapo Shetani angekuwa na udhibiti kamili wa hii dubia?
  2. Nuhu
    1. Soma Mwanzo 6:1-4. Maana ya “wana wa Mungu” na “binti za wanadamu” haiko wazi. Kilicho dhahiri ni kwamba walizaa watu wenye miili mikubwa, na Mungu hakufurahia hali hii na matokeo yake ni kwamba alipunguza urefu wa maisha yao. Unadhani kwa nini Mungu alidhani kuwa hili lilikuwa suluhisho zuri? (Ikiwa una watu wanaoishi mamia ya miaka, na wanatetea ushawishi wa dhambi, kitendo hicho kingeingilia kazi ya Mungu hapa duniani.)
    2. Soma Mwanzo 6:5-7. Je, tuliumbwa kwa isivyo bahati (kwa bahati mbaya)?
      1. Mungu aliwaumba wanadamu na kuwapa uhuru wa kuchagua. Je, Mungu anajuta kwa kutupatia uhuru wa kufanya uchaguzi?
      2. Kwa kuwa tunaangalia historia ya uasi na ukombozi katika mfululizo wa masomo haya (pambano kati ya wema na uovu), je, nani anashinda?
        1. Endapo ungekuwa Shetani, je, ungelalamika kwamba Mungu amebadili sheria?
        2. Je, Mungu amebadili sheria? (Soma Mwanzo 2:15-17. Adhabu ya dhambi ni mauti. Mungu hajabadili sheria. Mara watu wanapomkataa Mungu, wanakuwa wanastahili kupata hii adhabu.)
    3. Soma Mwanzo 6:8-13 na Mwanzo 6:17-21. Hebu tuone kama tunaweza kuelewa mawazo ya Mungu. Je, anajuta kuwaumba wanadamu? (Hapana. Mungu anataka kuendelea kuwafanyia wanadamu majaribio. Hata hivyo, Mungu hataki kuendelea kuiendeleza dhambi.)
      1. Je, hii inatufundisha nini kuhusu kuishi maisha makamilifu? Je, Mungu atamfurahia mtu mwenye haki? (Ndiyo!)
      2. Kwa nini Mungu hakumwangamiza Shetani na malaika zake wapotovu kwa wakati mmoja? Kwa nini asiondoe uongozi uliokuwa unaupigia debe uovu? (Jibu langu bora ni kwamba muda sahihi ulikuwa bado haujafika. Mungu alikuwa hajaja duniani kuwaokoa wanadamu na Shetani alikuwa hajadhihirisha ukubwa kamili wa mpango wake wa uovu.)
  3. Ibrahimu
    1. Soma Mwanzo 22:1-2. Hebu niambie kinachoendelea akilini mwako endapo wewe ndio ungekuwa Ibrahimu?
      1. Soma Yeremia 32:35 na 2 Wafalme 16:3. Kila kitu si sahihi katika jambo hili. Mungu anaiita kafara ya mtoto kwa kumpitisha motoni kuwa ni “machukizo” na anasema mawazo kama hayo “hayakuingia moyoni mwangu.” Kafara itafanyikia mlimani, mahali pa asili pa ibada ya sanamu. Je, wewe ungeamini kuwa ujumbe huu umetoka kwa Mungu? (Lazima Ibrahimu alikuwa anaifahamu sauti ya Mungu. Vinginevyo, amri hii haiaminiki.)
      2.  
      3. Soma Mwanzo 17:19-21. Unalinganishaje hii ahadi ya Mungu na maelekezo ya Mungu ya kumtoa Isaka sadaka ya kuteketezwa?
      4. Muda mfupi uliopita tumejadili jinsi Mungu anavyowafurahia (anavyowapendelea) wale wanaomfuata. Unaelezeaje maelekezo haya ya kutisha kwa mmojawapo wa watu waaminifu?
    2. Soma Mwanzo 22:3-5. Ibrahimu anatumia muda gani kufuata maelekezo ya Mungu?
      1. Angalia sehemu ya mwisho ya fungu la 5: “tutaabudu na kuwarudia tena.” Je, Ibrahimu anasema uongo ili watumishi wasiingilie kati? Ikiwa sivyo (na ninachukulia kwamba sivyo), je, Ibrahimu anafikiria nini? (Anaamini ahadi ya Mungu kuhusu mustakabali wa Isaka. Kwa namna fulani hivi Mungu atashughulika na jambo hili.)
    3. Soma Mwanzo 22:9-12. Kwa nini Mungu alimfanyia Ibrahimu kitendo hiki (na Isaka pia)? Kwa nini Mungu aliweka kumbukumbu ya tukio hilo kwenye Biblia? (Ikiwa hiki ni mojawapo ya visa vibaya kabisa ulivyowahi kuvisikia, anachokimaanisha Mungu kwa Ibrahimu na kwetu ni kwamba hiki ndicho ambacho Mungu alikitenda kwa ajili yetu alipomtuma Mwanaye, Yesu, kufa badala yetu. Hapakuwepo na mtu yeyote wa kuzuia kifo cha kutisha kabisa cha Yesu.)
    4. Hebu turejee nyuma kidogo. Kisa cha Ibrahimu kinaleta hisia kali sana (hususani kwa wazazi walio na ukaribu na watoto wao). Wakati huo huo, kisa cha Nuhu kinamweka Mungu kwenye nafasi ya chini. Je, ujumbe wa jumla wa Mungu kwetu ni upi kutokana na hivi visa viwili? (Mungu anatupenda mno kwa kiasi kisichoweza kufikirika katika akili ya kawaida. Mungu alitoa kafara ya pekee kwa ajili yetu, hata kama katika kipindi cha Nuhu Mungu alisema kuwa anajuta kutuumba. Wakati huo huo, Mungu ni Mungu wa hukumu. Atauangamiza uovu.)
  4. Yakobo na Yusufu
    1. Yakobo na Yusufu wana visa vigumu sana kueleweka kirahisi kiasi tusichoweza kuelezea kwa undani hapa. Kila mmoja alipitia kwenye hisia kali na chungu dhidi ya nduguze. Yakobo na Yusufu walikuwa watu “wema,” lakini kwa kiasi fulani walikuwa wanawajibika kutokana na ghadhabu ya ndugu zao dhidi yao. Hebu tuangalie jinsi hii ilivyotokea kwa Yusufu. Soma Mwanzo 45:1-4. Wale mnaofahamu kisa hiki vizuri niambieni jinsi Yusufu alivyo na “watumishi,” nyumba ya Farao na watu wake wanatamani masuala yanayomhusu Yusufu, na hapo awali Yusufu “aliuzwa?” (Ndugu zake Yusufu walimuuza utumwani kwa sababu walimchukia (Mwanzo 37), na kupitia kwenye mfululizo wa matukio mbalimbali, sasa Yusufu ni Waziri Mkuu wa Misri (Mwanzo 41).)
      1. Je, nduguze Yusufu wanahesabiwa haki kwa kitendo chao cha “kuogopa?”
        1. Je, Yusufu anawasaidia kwa kuwakumbusha kuwa walimuuza (Mwanzo 45:4)?
    2. Soma Mwanzo 45:5-7. Hii inatufundisha nini kuhusu mambo mabaya yanayowatokea watu wema? (Soma Mwanzo 50:19-20. Mungu aliyatumia mambo mabaya katika maisha ya Yusufu kufanya mambo mema.)
      1. Ikiwa unakifahamu kisa cha Yusufu na Waebrania, unafahamu kuwa hatimaye walifanywa na Wamisri kuwa watumwa (Kutoka 1). Kuna uhusiano, ikiwa upo, uliokuwepo kwa nduguze Yusufu kumuuza Yusufu utumwani?
    3. Rafiki, dhambi imesababisha hali ya kutisha kwa wanadamu. Mungu wetu yu hai katika mapambano dhidi ya dhambi. Anaikandamiza dhambi bila kuingilia uhuru wa wanadamu wa kufanya uchaguzi, na anabadilisha majanga ya dhambi kuwa mambo mema. Alitoa kafara ya pekee ili kuishinda dhambi na kutupatia uzima wa milele ulio huru dhidi ya dhambi. Kwa nini usifanye uchaguzi sasa hivi kuwa mtiifu kwa Mungu badala ya kuwa mtiifu kwa yule aliyehamasisha kifo cha Habili?
  5. Juma lijalo: Mapambano (Ugomvi) na Mtafaruku: Waamuzi.